matunduizi
JF-Expert Member
- Aug 20, 2018
- 6,586
- 15,369
Niliwahi kukaa katika taasisi moja. Kulikuwa na mazali kila siku. Chuki kutuhumiana, kuviziana na kila namna ya fyokofyoko kati ya wahusika.
Nilipozama kutafiti nikagundua chazo ni nyumbani hawa jamaa wanapotokea. Hawana amani, familia zimejaa magomvi, kufumaniana, mivurugano na taabu za kila namna.
Nimegundua watu wenye kuleta migogoro, taflani, debate nyingi zisizojenga, taharuki na magomvi katika jamii (Ofisini, kanisani, nzengo, vyama, na taifa kwa ujumla) ukichimba mzizi wa hizo tabia ni namna ya wao kujifariji kutokana na matifu na mabifu wanayopitia kwenye ndoa na familia zao.
Tumia nguvu kubwa kusimamisha ndoa na familia yako. Haitakusaidia wewe tu bali na popote utakapokua utakuwa mtu wa faida.