Michirizi ya Damu

Michirizi ya Damu

SEHEMU YA 16

Akarudi kwa nyuma kidogo na kumpisha mwanaume huyo ambaye naye alipita upandeupande huku akimpa mgongo Godfrey, kilichomshangaza, bila aibu yoyote ile mwanaume huyo akamgusa eneo la zipu na kumtekenya kidogo.
“Wewe vipi?” aliuliza Godfrey lakini mwanaume huyo hakuzungumza kitu zaidi ya kutoa tabasamu na kuelekea alipokuwa akielekea.

Godfrey alibaki pale alipokuwa, alisimama huku akimwangalia mwanaume yule. Kwa kumwangalia, alionekana kama mtu aliyekamilika lakini alipomwangalia vizuri, akagundua kwamba hakuwa sawa, alikuwa mwanaume aliyekuwa na tabia za kikekike.

Kichwa chake kilichanganyikiwa. Katika maisha yake yote, Godfrey hakuwa mtu wa wanawake, hata kumuoa Theresa ni kwa sababu tu alitakiwa kufanya hivyo.
Katika utajiri mkubwa aliokuwa nao, hakuwa akitembea na wanawake, wengi walijigonga kwake na kumwambia kuhusu hisia zao lakini hakuwa akishughulika nao hata kidogo.

Ugonjwa wake mkubwa ulikuwa ni wa kutembea na wanaume wenzake, alipenda mambo ya mapenzi ya jinsia moja, kila alipokuwa akimuona mwanaume aliyekuwa kwenye hali ya uanawake, alichanganyikiwa na wakati mwingine alikuwa tayari kufanya kitu chochote kile kumpata.

“Haiwezekani! Huyu simuachi,” alijisemea huku akimwangalia mwanaume yule aliyevalia kipensi kifupi, nywele zake alizipaka kalikiti na macho yake alikuwa akiyarembua mithili ya mwanamke aliyekula kungu.

“Call me my sweetie,” (nipigie mpenzi) alisema mwanaume yule kwa sauti nyembemba zaidi huku akiweka kidole cha gumba karibu na sikio na kidogo karibu na mdomo wake kumaanisha kwamba alitaka kupigiwa simu.
“I ain’t got your number,” (sina namba yako!) alisema Godfrey huku akimwangalia mwanaume huyo aliyeingia ndani ya gari.

“I will call you,” (nitakupigia) alisema mwanaume huyo, akawasha gari na kuondoka mahali hapo.
Godfrey akarudi kwenye kiti chake huku akionekana kuchanganyikiwa mno, kichwa chake kilikuwa kikimuwaza mwanaume tata aliyekutana naye.

Alikuwa kwenye mawazo tele, huo ndiyo ulikuwa ugonjwa wake, hakuwa na hamu na wanawake hata mara moja. Kitendo cha kukutana na mwanaume huyo mwenye sura nzuri kilimpagawisha kupita kawaida.
Story imeanza vizuri... naona inataka kuharibika sasa... inasikitisha sana...


Cc: mahondaw
 
SEHEMU YA 17

Theresa alimwangalia mume wake, aligundua kwamba kulikuwa na tatizo, hakuwa sawa, alionekana kuwa kwenye lindi la mawazo kupita kawaida. Hakutaka kumuacha hivyo, alimuuliza tatizo lilikuwa nini lakini hakujibu zaidi ya kumwambia kwamba alikuwa kawaida.

“Haiwezekani! Niambie kuna nini mpenzi,” alimwambia mumewe.
“Hakuna kitu!”
“Kweli?”
“Ndiyo!”
“Dili bado lipo mezani au wamelifuta?”
“Yote yapo mezani mke wangu!”

Hawakukaa mahali hapo, wakaondoka. Muda wote alikuwa akiangalia simu yake, alitaka kuona mwanaume huyo akimpigia na kumwambia mahali alipokuwa akipatikana kwani alijua kabisa kwamba asingelala, asingekula kwa sababu yake.
Kama ambavyo mwanaume anayependa wanawake anapokutana na msichana mzuri, akampa namba na kutaka kupigiwa, jinsi alivyokuwa akisubiri kwa presha ndivyo ambavyo alivyokuwa akisubiri kwa presha kubwa.

“Mbona hanipigii zaidi ya kunitamanisha tu! Mtoto ameumbika sana, ana miguu membamba lakini hapa kiunoni amekaa poa sana. Naomba anipigie tu! Ila namba yangu anayo kweli au aliniambia vile kama kunitega?” alijiuliza Godfrey, hakupata jibu.

Aliendelea kusubiri, aliisubiria simu ya mwanaume huyo zaidi ya alivyokuwa akisubiri dili za kuanza kufanya biashara zake. Siku ya kwanza ikakatika, ya pili, ya tatu mpaka wiki hakuwa amepigiwa simu kitu kilichomfanya kuukosa amani, hata safari zake za kwenda Marekani na Uarabuni hazikuwa na furaha tena, muda wote moyo wake ulikuwa ukimuwaza mwanaume huyo tu aliyekuwa na muonekano kama wa kike, alikuwa shoga.

**** Godfrey aliendelea kusubiri mpaka akakata tamaa. Miezi mitatu ilipita lakini hakuwa amepigiwa simu na mwanaume huyo hivyo kuona kwamba ilishindikana hivyo kuendelea na maisha yake.
Maisha yake hayakubadilika, kila siku aliwatamani wanaume wenzake, hakuwa na muda na wanawake, kwake, maisha yalionekana kuwa tofauti, wakati wanaume wenzake wakiwatamani wanawake, kwake, aliwatamani sana wanaume kuliko wanawake.

Alikwenda nchini Marekani, huko, kazi yake kubwa ilikuwa ni kulala na wanaume na kufanya nao mapenzi. Alijua kwamba ilikuwa dhambi kubwa lakini hakutaka kuacha, yalikuwa ni maisha ambayo aliyazoea, ikawa tabia yake na kumganda kama ruba.
Dhambi kubwa sana...

Vyote vingaavyo siyo dhahabu...


Cc: mahondaw
 
SEHEMU YA 18

Baada ya kupita miezi sita tena huku akiwa barani Asia ndipo akatumiwa meseji katika akaunti yake ya WhatsApp, harakaharaka akaifungua na kuisoma, alitumiwa kupitia namba ngeni na ujumbe aliotumiwa ulikuwa mfupi tu uliosomeka ‘Miladiva’.

Kitu cha kwanza kabisa kumjia kichwani mwake kilikuwa ni kukumbuka kitu kilichotokea kwenye ufukwe huo. Alikumbuka kwamba mara ya mwisho kwenda katika ufukwe huo ni miezi kadhaa iliyopita ambapo alikwenda pamoja na familia yake.

Hakujua ujumbe huo ulimaanisha nini lakini alipouliza, akatumiwa ujumbe mwingine mfupi uliosomeka ‘Nipigie’, hapo ndipo akakumbuka, picha ya mwanaume tata yule aliyemwambia ampigie ikamjia kichwani mwake, hakutaka kuchelewa, akamtumia meseji ya kulalamika kwamba ilichukua muda mrefu mpaka kumtafuta.

“Nilikuwa bize sana. Ila nimekumiss baba watoto,” aliusoma ujumbe huo, mwili ukamsisimka.
“Kweli?” aliuliza.
“Ndiyo! Naomba nikuone jamani!” aliusoma ujumbe huo ambao uliambatanishwa na sauti iliyorekodiwa, alipoifungua, ilikuwa sauti ya mwanaume huyo iliyokuwa ikilalamika kimahaba, tena mbali na hiyo, alimwambia kwamba alihitaji mpenzi wa kudumu kwani wapenzi wote aliokuwa nao waliishia kumtenda tu, hawakuwa na mapenzi ya dhati.

“Nipo kwa ajili yako! Nitakulinda mpenzi! Naomba kuonana nawe nikifika Tanzania,” alimwambia.
“Kwani upo wapi?”
“Nipo Kuwait, kuna kitu nimefuata.”
“Basi sawa baba watoto! Nakupenda!”
“Nakupenda pia. Mwaaaaah!”
“Mwaaaah!”

Wakaagana, Godfrey hakuamini kama aliwasiliana na mwanaume tata huyo, alibaki hotelini huku akiwa amechanganyikiwa kwa furaha, aliinuka na kuanza kurukaruka, alikuwa na hamu ya kupata mawasiliano na mwanaume huyo na mwisho wa siku alipigiwa na hivyo kuwa na namba yake.

Wakati akiwa anafurahia akasikia simu yake ikilia na alipoifungua akakutana na picha za kihasarahasara alizotumiwa katika akaunti yake ya WhatsApp ambazo zilimuonyesha mwanaume huyo akiwa katika mikao ya hatarihatari.

Japokuwa alikwenda Kuwait kukaa kwa wiki moja na kutakiwa kwenda nchini Uingereza lakini wiki moja akaiona kuwa kama mwaka, kila siku kazi yake ilikuwa ni kuangalia kalenda, hakukuwa na kipindi alichokiona siku kwenda taratibu kama kipindi hicho.
Wanasikitisha sana...


Cc: mahondaw
 
MICHIRIZI YA DAMU-31

Asteria akakata simu na kisha kufanya kama alivyoambiwa. Hakuamini macho yake baada ya kugundua kwamba alikuwa akiwasiliana na bilionea mkubwa nchini Marekani. Kwanza akaanza kutetemeka, yeye mwenyewe alihofu, hakujiamini kwani miongoni mwa watu waliokuwa mabilionea, Keith alikuwa balaa.
“Umeona sasa?” aliuliza Keith baada ya kumpigia simu.

“Ndiyo! Unahitaji wanawake wangapi?”
“Tuanze na mmoja.”
“Nitakupa aitwaye Penny?”
“Anajua?”
“Usiwe na shaka na watu wangu. Wewe niachie anuani yako!” alisema Asteria na kukata simu.
Huo ndiyo ulikuwa mwanzo wa kufahamiana na bilionea huyo, mara kwa mara walikuwa wakiwasiliana huku akimwambia kwamba alikuwa akihitaji wanawake zaidi. Alipenda kufanya ngono na wanawake weusi, maishani mwake, japokuwa alikuwa Mzungu lakini hakuwapenda Wazungu.

Wakatengeneza uswahiba mkubwa na kujikuta ndani ya miezi sita wakiwa marafiki wakubwa. Wakati mwingine Asteria alikuwa akisafiri mpaka nchini Marekani ambapo huko alikutana na mwanaume huyo na kuzungumza mambo mengi.

Biashara yake iliendelea kukua. Alizidi kuwasafirisha wanawake kwenda huko kwa ajili ya kufanya nao mapenzi na bilionea huyo.
Baada ya mwaka mmoja kupita huku urafiki wao ukiwa mkubwa ndipo siku moja bilionea huyo akamualika Asteria katika shere yake ya kuzaliwa ambayo angeifanya Jijini Los Angeles, alimuomba sana ahudhurie kwani ilikuwa ni sherehe kubwa ambayo ingekutanisha mastaa wengi kutoka sehemu mbalimbali hapo Marekani.

“Nitakuja!”
“Njoo na marafiki zangu basi!”
“Haina shida. Wangapi?”
“Wawili!” “Sawa.”
Asteria akafurahia, moyo wake ukajua kwamba hiyo ndiyo ilikuwa nafasi ya kutengeneza fedha zaidi. Hakutaka kuiacha nafasi hiyo, alitaka kuhakikisha anaitumia vizuri kuhakikisha kwa mwaka huo anakuwa na kiasi kikubwa cha fedha.

Akawachukua wasichana wawili, Ester na Queen lakini pia akamuongeza na Fareed kwa kuamini kwamba ndani ya sehemu ambayo wangeonana kwa ajili ya sherehe hiyo ingewezekana kabisa kupata mteja mwingine kupitia Fareed.
“Marekani?”
“Ndiyo! Kuna mabwana wa Kizungu, wenye hela zao,” alisema Asteria.
“Basi sawa. Nitakwenda!”
Penny... hahahaha....


Cc: mahondaw
 
Back
Top Bottom