SEHEMU YA 17
Theresa alimwangalia mume wake, aligundua kwamba kulikuwa na tatizo, hakuwa sawa, alionekana kuwa kwenye lindi la mawazo kupita kawaida. Hakutaka kumuacha hivyo, alimuuliza tatizo lilikuwa nini lakini hakujibu zaidi ya kumwambia kwamba alikuwa kawaida.
“Haiwezekani! Niambie kuna nini mpenzi,” alimwambia mumewe.
“Hakuna kitu!”
“Kweli?”
“Ndiyo!”
“Dili bado lipo mezani au wamelifuta?”
“Yote yapo mezani mke wangu!”
Hawakukaa mahali hapo, wakaondoka. Muda wote alikuwa akiangalia simu yake, alitaka kuona mwanaume huyo akimpigia na kumwambia mahali alipokuwa akipatikana kwani alijua kabisa kwamba asingelala, asingekula kwa sababu yake.
Kama ambavyo mwanaume anayependa wanawake anapokutana na msichana mzuri, akampa namba na kutaka kupigiwa, jinsi alivyokuwa akisubiri kwa presha ndivyo ambavyo alivyokuwa akisubiri kwa presha kubwa.
“Mbona hanipigii zaidi ya kunitamanisha tu! Mtoto ameumbika sana, ana miguu membamba lakini hapa kiunoni amekaa poa sana. Naomba anipigie tu! Ila namba yangu anayo kweli au aliniambia vile kama kunitega?” alijiuliza Godfrey, hakupata jibu.
Aliendelea kusubiri, aliisubiria simu ya mwanaume huyo zaidi ya alivyokuwa akisubiri dili za kuanza kufanya biashara zake. Siku ya kwanza ikakatika, ya pili, ya tatu mpaka wiki hakuwa amepigiwa simu kitu kilichomfanya kuukosa amani, hata safari zake za kwenda Marekani na Uarabuni hazikuwa na furaha tena, muda wote moyo wake ulikuwa ukimuwaza mwanaume huyo tu aliyekuwa na muonekano kama wa kike, alikuwa shoga.
**** Godfrey aliendelea kusubiri mpaka akakata tamaa. Miezi mitatu ilipita lakini hakuwa amepigiwa simu na mwanaume huyo hivyo kuona kwamba ilishindikana hivyo kuendelea na maisha yake.
Maisha yake hayakubadilika, kila siku aliwatamani wanaume wenzake, hakuwa na muda na wanawake, kwake, maisha yalionekana kuwa tofauti, wakati wanaume wenzake wakiwatamani wanawake, kwake, aliwatamani sana wanaume kuliko wanawake.
Alikwenda nchini Marekani, huko, kazi yake kubwa ilikuwa ni kulala na wanaume na kufanya nao mapenzi. Alijua kwamba ilikuwa dhambi kubwa lakini hakutaka kuacha, yalikuwa ni maisha ambayo aliyazoea, ikawa tabia yake na kumganda kama ruba.