Miaka ya 90 pale uwanja wa ndege mzee Mwinyi aliwahi kunipa hela, fulana kwa mkono wake mwenyewe kisha akanambia maneno haya...

Bibi aliacha na kuegemea zaidi kwenye maswala ya dini. Na huo ndio ukawa mwanzo wa kusambaratika kabisa kwa kundi hilo la ngoma zao za kitamaduni.

Ilikuwa wakienda kwenye show wanalipwa na bibi anamgawia kila mmoja sawa na mungine. Alivyojitoa hakupatikana mwenye uwezo wa kuongoza vizuri kama yeye. Wakawa wakienda kupiga sehem wakirudi wanadhulimiana. Hela za kutunzwa bibi alikuwa hata akitunzwa anawapa na wenzake, lkn hawa wengine mtu akitunza anaichimbia kwenye matiti na kuibana na sidiria.

Mwisho kikundi kikaanguka chali 😀😂
We jamaa umeamua kutuchekesha msibani😀
 
SIsi ni wanafiki sana, mtu akifa tunamsifia weee.

Mwinyi huyu aliyesababisha watumishi wa serikali waache kazi na kuingia kwenye biashara?

Mfumuko wa bei ulikuwa juu?

Nyerere kumlaumu kuwa aligeuza Ikuly kuwa nyumba ya walanguzi?

Akaiuza Loliondo?

Udini ukashamiri?

Mpeni mtu haki yake akiwa hai na akiwa mfu
Maisha ya mwanadamu ni hadithi tu....

Ishi utakavoishi hatimaye utaingia mavumbini...

....ukifa tutasimulia habari zako aidha kwa wema au ubaya wako....tujitahidi kuishi kwa wema ili watu wasimuliwe kuhusu wema tulioufanya kwa watu!

Hesabu ya mzee imekamilika naye yupo kwa Mola kupambana na hali yake, vipi wewe na mimi hesabu yetu ipoje?

Tuishi kwa wema....!
 
Maisha ya mwanadamu ni hadithi tu....

Ishi utakavoishi hatimaye utaingia mavumbini...

....ukifa tutasimulia habari zako aidha kwa wema au ubaya wako....tujitahidi kuishi kwa wema ili watu wasimuliwe kuhusu wema tulioufanya kwa watu!

Hesabu ya mzee imekamilika naye yupo kwa Mola kupambana na hali yake, vipi wewe na mimi hesabu yetu ipoje?

Tuishi kwa wema....!
Naam 🙏
 
Sipendi kuzungumzia udini maana hata kipindi cha hayati Magufuli serikali yake ilikuwa na mawaziri watatu tu waislam, huku waliobakia zaidi ya ishirini wakiwa wakristo. Kwako wewe hilo haukuliona maana huenda lilinufaisha upande wako.

Kumbuka raisi Mwinyi ndio raisi wa kwanza kumleta papa John Paul nchini Tanzania. Sasa huo udini wako unaosema hapa sijui ni udini upi?

Ngoja nijikite kwenye point za nje ya udini wako. Unasema Mwinyi alisabisha watumishi waache kazi, huo ulikuwa ni utashi wao. Lakini kwa vile katika taifa huwa kuna watu wengi huwa hawana kazi, basi walioacha kazi nafasi zao zilichukuliwa na watu waliokuwa hawana kazi tatizo liko wapi? Lakini umesahau kuwa wakati Mwinyi anaingia madarakani aliikuta hazina ya taifa ikiwa tupu, haina hela. Serikali nzima ilikuwa imefilisika na watumishi wengi walikuwa wanafanya kazi kizalendo tu bila kupata mshahara wowote. Alipoingia Mwinyi akaifungua nchi, wafanyakazi wakaanza kupokea, na wengine kuamua kuacha kazi ili kutoa fursa kwa wengine alaf wao wakajikita kwenye biashara, sasa kati ya mtu kufanya biashara bila kulipwa na yule anaelipwa na kuamua kujiongeza kufanya biashara ili kukidhi mahitahi ya maisha yake nani aliekosea?

Nyerere kamlaumu Mwinyi kuhusu loliondo, lakini Nyerere huyu huyu wakati wa utawala wake alizuia vyombo vya habari visiandike kuhusu matatizo wanayopitia wananchi kama vile kukosa mahitaji ya msingi madukani, watu wazima kuvaa midabwada na suruali za viraka, kuvaa chachacha, watoto kwenda shule bila viatu, kusababisha watu wenye maono makubwa kama kina Kambona kukimbia nchi nk. Nchi ilikuwa katika hali mbaya hadi kupelekea kuponea kupinduliwa mara mbili na baadhi ya wanajeshi, ambao walichoka na uozo wa serikali yake na kuamua kusimama upande wa wananchi.

Na bado mpaka leo hayati Nyerere tunamsifu kwa mema tu, hatujawahi kumsema kwa baya, ila haujaja kupinga sifa hizo alizopewa baada ya kufa. Wewe ndo mnafiki.
Kuhusu hazina kua tupu.......kwani hazina ni makabati ya kuifadhia pesa mkuu???
 
Back
Top Bottom