Miaka ya 60 tulikuwa tunalingana na Korea kimaendeleo, hawa jamaa walijikwaa wapi mpaka tukawaacha mbali kiasi hiki!

Sisi tulishaanza kuendeleaa anagalu kuanzia 1990s ndio tukaanza tena kurudi nyuma..

Kuna vitu vingi sana tulishakua navyo vikafa, viwanda vingi mno vimekufa.
Niliwahi kuwaambia watu ubunifu wetu umekwama mahali,hata ukiangalia shule za serikali zinazoanzishwa sasa hivi na za zamani,za zamani bado zinabaki kuwa shule bora. Viwanda vya zamani tumeua,tunaanzisha mambo kuendeleza hatuwezi mfano mradi wa mabasi ya mwendokasi.Naamini kuna tatizo kubwa kwenye mifumo yetu ya elimu,hatutoi products zenye tija katika maisha yetu ya kila siku.
 
China ni ya pili kwa uchumi mkubwa.
Tatizo sio ujamaa au upepari. Nchi nyingi sio wajamaa ila wanayumba.
Suluhu ni kuwa na viongozi wanaoyataka maendeleo, sio wanaotaka makofi jukwaani, sio wanaotaka sifa,sio wezi.
Mamiloni ya Watanzania yanapotelea mikononi mwa wachache.
Aliyekudanganya kwamba China iliendelea Kwa ujamaa ni nani?
 
Sasa kama miaka zaidi ya 60 sasa tunapeana vyeo/ajira kwa kutumia vigezo vya undugu, kujuana, urafiki, ukada, nk! Badala ya kuangalia maarifa ya mtu kichwani, unategemea nini!

Ufisadi unetamalaki, huku watu wakilindana yoyote ile! Wanasiasa wapiga midomo muda wote na wenye sifa ya kujua tu kusoma na kuandika; wanalipwa mishahara mikubwa kuliko wataalam wa fani mbalimbali! Bado tutegemee nchi hii kuendelea!!

Kuna wagunduzi kibao kwenye hii nchi! Lakini hawapewi kipaumbele. Badala yake watawala na wanasiasa wanaona bora wapige 10% kupitia bidhaa duni zinazo agizwa kutoka nje, huku zile za wazawa zikipuuzwa.
 
Mkuu usipotoshe watu, hatukuwa sawa na S.Korea kipind cha miaka ya 65, ujue kipindi hicho S.Korea kina Samsung tayari wanatengeza Computer, TV na vitu vingine, wakati huo sisi huku Tanzania tunauziana vitu kwa zamu kwenye maduka ya ushirika
 
Nimekuelewa mwandishi umetumia fasihi vizuri,hakika Korea wamechelewa sana
 
Hakuna maendeleo yeyeto Dunia kwa kuwatenga mabeberu.
Pote walipoendelea ni kwa mkono wa beberu, lazima uliwe ili uwe na maendeleo
 
Mkuu usipotoshe watu, hatukuwa sawa na S.Korea kipind cha miaka ya 65, ujue kipindi hicho S.Korea kina Samsung tayari wanatengeza Computer, TV na vitu vingine, wakati huo sisi huku Tanzania tunauziana vitu kwa zamu kwenye maduka ya ushirika
🤣🤣
 
Back
Top Bottom