Majibu ya utafiti: Miaka 10 ijayo Tanzania itakuwa imesimama wapi?

Mama Amon

JF-Expert Member
Mar 30, 2018
2,021
2,478
Samia-Suluhu.jpg


1672604948051.png

Rais Samia pamoja na marais waliomtangulia: Nyerere, Mwinyi, Mkapa na Kikwete

MIAKA 10 ijayo, hadi kufikia mwaka 2033, Tanzania itakuwepo. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan hatakuwa madarakani, huku idadi ya watu ikikadiriwa kuwa zaidi ya milioni 75.

Je, uchumi wake utaimarika na maisha ya watu kuwa bora zaidi? Swali hilo linajibiwa na Watanzania walioko ndani na nje ya nchi kwa kutoa maoni yao kupitia gazeti hili la Pambazuko.

Idadi kubwa ya Watanzania ‘wamejenga’ matumaini na imani kwa nchi yao kwamba katika kipindi cha miaka 10 ijayo, nchi itakuwa na maendeleo makubwa.

Maendeleo wanayoyazungumza hapa ni kuwa na uchumi imara wenye kuakisiwa kwenye miundombinu bora na ya kisasa; ikiwamo barabara, shule, hospitali zenye huduma bora za afya na mazingira mazuri ya kufanya biashara.

Hata hivyo, wapo wanaoeleza wasiwasi kuhusu maendeleo hayo huku wakieleza kwamba huenda yakatingwa na baadhi ya tabia ambazo sasa zinaonekana kukomaa na kuwa za kawaida; rushwa na ubadhirifu.

Pambazuko limefanya tathmini ya utendaji wa serikali inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na kubaini kwamba asilimia 57 ya watu waliohojiwa wamejenga imani ya “mambo mazuri kuendelea kutokea,” huku wakieleza kwamba ndani ya miaka 10, Tanzania itakuwa na ustawi wenye “heri kwa idadi kubwa ya watu wake.”

Imani yao inajengwa na mtazamo wa mwenendo wa utendaji wa serikali ya sasa, huku wakieleza kwamba Rais Dkt. Samia “anakwenda vizuri.”

Hata hivyo, wapo watu asilimia 43 ambao wamehojiwa, ambao wameonyesha wasiwasi wao kuhusu ujio wa maendeleo makubwa katika miaka 10 ijayo, wakieleza kwamba, “matumizi ya serikali ni makubwa kupita kiasi, hivyo kuwa tishio kwa matumaini ya maisha bora kwa watu wengi zaidi.”

Tathmini ya utendaji wa serikali kwa kipindi cha mwaka mmoja na maoni yao kuhusu miaka 10 ijayo, ilifanywa kwa kuwahoji wachangiaji na wasomaji wa gazeti la Pambazuko, ambao waliulizwa maswali matano makubwa, mengine yakiwa ni maswali madogo.

Maswali hayo yaliyotumwa kwa njia ya dodoso pepetevu (soft questionnaire) kupitia WhatsApp, yalikuwa haya: je, serikali imefanya kazi zake vyema kuhudumia wananchi kwa mwaka mmoja uliopita? Nini kifanyike ili maisha ya watu yawe bora zaidi?

Je, serikali imegusa vipi maisha ya Mtanzania mmoja mmoja? Kama serikali imekwama, shida iko wapi na nini kifanyike?

Na, unaiona Tanzania ikisimama wapi katika kipindi cha miaka 10 kutoka sasa? Watu 412 walirudisha majibu yao na baadaye kufanyiwa uchambuzi wa kina.

Watu walioshiriki zoezi ni wanaume 367, sawa na asilimia 89, wakati wanawake walikuwa 45, sawa na asilimia 11. Asilimia 92 (sawa na watu 379) ya walioulizwa wamebainika kutoka Dar es Salaam.

Waliobaki, yaani asilimia 8, sawa na watu 33, wako mikoa mbalimbali, na wachache walitoka nje ya Tanzania. Dodoso hilo halikuuliza umri wala elimu.

Watu 177, sawa na asilimia 43, wamekuwa na shaka kuhusu Tanzania kuwa na uchumi wa juu ndani ya miaka 10 ijayo.

Wanaeleza wasiwasi wao kwa kuangalia zaidi matumizi ya serikali waliyoita “makubwa mno.”

Hawa wanaeleza kwamba serikali kununua magari ya kifahari kila mwaka kwa mawaziri, manaibu, wakurugenzi, wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya, wakuu wa idara na taasisi, ni “kufuru” kwa walipa kodi.

Mmoja wa wajibu dodoso, ambaye ni kiongozi mstaafu alipiga simu kwa Pambazuko na kutoa dukuduku lake kwamba kwa nini magari makubwa na aghali zaidi yanunuliwe wakati kuna barabara nzuri zaidi kwa sasa?

“Zamani wakati wa Mwalimu (Nyerere - rais wa kwanza- 1961 hadi 1985) wakubwa waliokuwepo walitumia magari ya kawaida sana, wakati hakukuwa na barabara nzuri, iweje hawa wa leo wajione ni bora zaidi na kujinunulia magari ya bei mbaya,” amelalamika na kuongeza; ‘hivi hawajua kuwa walipa kodi wanaumia.”

Pambazuko halitamtaja jina lake. Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Mwigulu Nchemba amebainisha kuwa serikali kwa mwaka huu wa fedha itatumia Sh. bilioni 558 kununua magari.

Kiasi hiki, endapo nusu yake ingetumika kuagiza magari ambayo ni nafuu kidogo – hasa Prado, na inayobaki kujenga miundombinu ya barabara, kungepatikana barabara ya kiwango cha lami yenye urefu wa kilomita 233.

Kilomita moja ya barabara hujengwa kwa Sh. bilioni 1.2. Urefu huo ni sawa na umbali wa kutoka Mwanza hadi Bariadi (kilomita 230) au kutoka Njombe hadi Songea (kilomita 237).

Viongozi wakubwa serikalini hutumia magari yanayouzwa kuanzia Sh. milioni 250 hadi 330 na sheria hulazimisha magari kununuliwa mapya kutoka kwa mtengenezaji. Aina ya magari hayo ni Toyota LandCruise V8 na VX.

Toyota Prado huuzwa nusu ya bei hizo. Zaidi sana, hawa wenye matumaini finyu, wanaeleza kwamba rushwa na ubadhirifu vimeongezeka kiasi cha kutishia hayo matumaini ya kuwa na uchumi imara na maisha bora baada ya miaka 10 kuanzia sasa.

Wenye matumaini ya kuwa na maisha bora zaidi katika kipindi cha miaka 10 ijayo wanaeleza kuboreshwa kwa huduma za afya ni chahu, kwamba huenda bajeti kubwa ya fedha inayotengwa kwenye afya, ikasaidia kuimarisha afya, hivyo kuwa na nguvu kazi imara.

Kwamba endapo serikali itaendelea kuongeza bajeti ya afya, kuwa na madaktari wa kutosha, dawa na vifaa tiba, pamoja na vile vya uchunguzi, idadi ya watenda kazi wenye siha njema itaongezeka, hivyo kuwa na uhakika wa ongezeko la uzalishaji wa viwandani, ofisini na hata mashambani.

Katika bajeti ya 2022/23, serikali ilitenga jumla ya Sh. 1,109,421,722,000 ikiwa ni ongezeko la asilimia saba (sawa na Sh. 75,287,427,000) kutoka bajeti ya mwaka 2021/22 iliyokuwa Sh. 1,034,134,295,000, huku Rais Dkt. Samia akieleza mara kadhaa kwamba serikali itaendelea kuongeza bajeti hiyo.

Utawala bora

Katika kipindi cha miaka 10, Rais Samia atakuwa amestaafu utumishi wake wa umma – kwa nafasi ya urais kwani anatarajiwa kustaafu baada ya kutimiza awamu mbili za uongozi kikatiba.

Atastaafu Novemba 2030 ikiwa atachaguliwa kuongoza kwenye uchaguzi mkuu wa 2025.

Katiba ya Tanzania inaharamisha rais yeyote kuzidisha awamu mbili za miaka mitano mitano, hata kama amefanya vizuri zaidi katika uongozi wake.

Kwa Rais Dkt. Samia, Watanzania hawatarajii kusikia mapambio ya wapambe kwamba “atake- asitake” – aendelee kuongoza hata baada ya awamu mbili kumalizika - kwani kufanya hivyo itakuwa ni kuvunja katiba ya nchi.

Bado Dar au Dodoma?

Mbali na kuwa dodoso pepetevu, Pambazuko pia lilifanya hojaji iliyohusisha sampuli ya kinasibu (random sampling) kutaka kujua Watanzania wanaiona wapi nchi yao kwa miaka 10 ijayo.

Hili lilifanyika Wilaya ya Kinondoni, Dar es Salaam, pekee. Miongoni mwa waliohojiwa ni Khamis Hamza, ambaye alieleza kuwa na elimu ya chuo kikuu.

Alisema ana imani kuwa Tanzania ndani ya miaka 10 itakuwa mbali zaidi kiuchumi, kwamba mapato ya vijana wengi yataongezeka kutokana na kukua kwa sekta ya viwanda.

Hata hivyo, kuhusu matumizi, akadai “serikali ina matumizi makubwa sana kwa sasa,” na kuweka mfano mmoja kwa njia ya swali; “hivi ofisi za mawaziri na hata wakubwa wengine ziko wapi – Dar au Dodoma, wewe huwaoni wakipishana angani au barabarani kila wiki kuja Dar es Salaam?”

Anasema kupishana huko ni “pesa inateketea,” hivyo akaongeza kwamba ni heri matumizi hayo ya safari za kila mara kwa viongozi wakuu zikapunguzwa – kwa wao kuishi zaidi Dodoma na fedha zaidi kuelekezwa kwenye maeneo mengine yanayogusa maisha ya Watanzania moja kwa moja.

Uraia pacha

Msomaji wa Pambazuko, Mtanzania anayeishi Kitongoji cha Coppell, Texas, Marekani anaandika kuwa Tanzania kuwa na uchumi imara zaidi na maisha bora kwa wengi ni kujidanganya kwani inaonekana kuwa na ubaguzi kwa raia wake, hasa wanaoishi na kufanya kazi nje ya nchi.

Anasema serikali inaendelea kupoteza fedha nyingi na fursa zinazoweza kupatikana kwa Watanzania walioko nje ya Afrika, hasa Marekani, kwani kuwanyima uraia ni “kujifunga kitanzi wenyewe.”

Matamanio yake ni kwamba serikali ingeruhusu uraia pacha kama Kenya, Uganda, Afrika Kusini na nchi zingine jirani, ingekuwa na uhakika wa kuvuna, kile anachokiita “dhahabu kutoka Ulaya na Marekani.”

Anafafanua kwa kusema ni ujuzi na mitaji. Mtanzania huyo, anaungana na wengine walioshiriki na kutamani serikali kuacha kile wanachoita “woga usiokuwa na sababu” na kuamua kuwa na uraia pacha.

Uchumi utaimarika?

Pambazuko limefanya mapitio ya taarifa mbalimbali za taasisi za kimataifa, Benki ya Dunia (WB), Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) na Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kwa kipindi cha mwaka mmoja uliopita na kujiridhisha kwamba jitihada kubwa zinafanyika ili kuelekea kwenye uchumi imara.

Katika Fahirisi ya Ufanisi wa Kibiashara ya Benki ya Dunia (2021), nchi tano kati ya kumi zilizofanikiwa zaidi kukuza uchumi wake ziko barani Afrika, na theluthi moja ya mageuzi yote yaliyorekodiwa yalifanyika katika Afrika - kusini mwa Jangwa la Sahara. Tanzania inatajwa kuwemo.

Imebainika kwamba kuna ongezeko kubwa la uwekezaji wa nje ya nchi na kukomaa kwa wawekezaji wa ndani.

Zaidi ya kampuni 100 ama zimeanza kazi au zimeomba leseni ya kuwekeza na tayari zimebanisha maeneo ya kuleta mitaji yao – Kampuni zote hizo zinaleta mtaji wa zaidi ya dola za Marekani trilioni moja.

Benki ya Maendeleo ya Afrika (ADB) inaeleza kuwa Tanzania ikiweka nguvu na utashi zaidi kwa kufanya maboresho ya kibajeti na kitaaluma, hasa katika sekta za nishati, kilimo, maji na madini, uchumi wake utapaa zaidi na wananchi wake kuwa na maisha bora.

Dkt. Lenny Kasoga, mchumi na mhadhiri mwandamizi mstaafu anaeleza kwamba Tanzania itakuwa na uchumi imara endapo tu, uchumi hautaingiliwa na misimamo ya kisiasa.

Anasema Tanzania inaongoza kuwa na rasilimali nyingi kuliko mataifa mengi ya Afrika na Ulaya, lakini watu wake wengi masikini na ustawi wao unakwamishwa na siasa kuingilia kila kitu na hata uchumi.

“Bahati mbaya hata wasomi wa uchumi nao wameingiliwa na siasa, wamekuwa wauza siasa badala ya kuuza mizania ya uchumi; mchumi akiwa na mawazo ya siasa zaidi, basi ujue hakuna kitu,” anasema msomi huyo aliyewahi kufundisha vyuo vikuu Marekani, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na maeneo mengine.

Chanzo: Gazeti la Pambazuko, Toleo la Jumatatu, Januari 2-7, 2023, ukurasa wa 10-12.
 
Samia-Suluhu.png

View attachment 2466108
Rais Samia pamoja na marais waliomtangulia: Nyerere, Mwinyi, Mkapa na Kikwete

Chanzo: Gazeti la Pambazuko, Toleo la Jumatatu, Januari 2-7, 2023, ukurasa wa 10-12.
Mkuu Mama Amon , thanks for this.
Wewe ni hazina kubwa hapa jukwaani, wakati wengi wetu concentration yetu ni 2025 kama twende na Mwanamke Watanzania, tuunge mkono 2025 ni zamu ya Mwanamke, ila sio lazima awe yeye bali yule aliyepangiwa na 'YEYE', kama ni yeye aliyepangiwa, then ni yeye!
Au Voices From Within: Japo 2025 Tumepanga Twende na Mwanamke, 2025 Mama Akabidhi Kwanza Mwanamume, Kisha 2030 Ndipo Aje Mwanamke
Wewe uko 10 years ahead!.
Vitu vikubwa hivi sijui vitachangiwa na wangapi humu!.
Thanks again
P
 
Samia-Suluhu.png

Chanzo: Gazeti la Pambazuko, Toleo la Jumatatu, Januari 2-7, 2023, ukurasa wa 10-12.
Mkuu Mama Amon , japo bandiko lako ni la kuhusu miaka 10 ijayo, usiweke potrait photo kama ya miaka 10 ijayo, please change hiyo potrait Mama anaonekana kama amenanii sana, chagua hapa portraits bomba za kumwaga.
download.jpeg
images.jpeg
images (3).jpeg
images (1).jpeg
images (4).jpeg

P
 
Kwanza utafiti wako ninja hovyo hausemi benchmark ya maendeleo kiuchumi ni kipato kiasi gani!? GDP kiasi gani?

Export Vs import trade-offs. Rudi tena field uje na kitu trustworthy otherwise fungia tu maandazi
 
Back
Top Bottom