Miaka 4 ya mahusiano akaambulia patupu

Miaka 4 ya mahusiano akaambulia patupu

kuchagua huko mwisho wa siku utakuja shtuka una miaka 35 lakn bado hajatokea unayemkubali hapo ndio taa nyekundu znaanza kumulika

Sio kisa ndoa basi ukubali yoyote kwa kivuli cha umri kunitupa mkono.Mbona wanaume hawaoi yeyote???
Mungu ni muaminifu
 
Habari zenyu bana....

"Gladdy najua unanipenda and of course na mimi nakupenda pia sana tu kama nitakosea naomba unisamehe... you are the woman na zaidi ya hayo una malengo yako hata kama nitakukosa haina shida kama utakuwa ktk mikono salama. mi nina mambo mengi nashindwa kutoa msimamo kwa sasa"

Ni maneno aliyoambiwa rafiki yangu usiku wa kuamkia leo. Anasema alihisi dunia imegeuka Up-side down. Moyo ulisimama kwa ghafla make hakuamini alichoambia na mwanaume ambaye amedumu naye miaka 4 akiamni ndiye mume wake mtarajiwa.

Aisee inauma sana..
anadai hakuna mkwaruzano wala ugomvi. Bali alitaka tu kujua mwanaume ana msimamo gani make walikuwa wanakwenda tu bila kujua hatma ya mahusiano yao.

Tumfariji na kujifunza pia kupitia relationship hii...

asikate tamaa,atapata tu mtu mwenye msimamo, huyo alikuwa hana msimamo.
 
Muda unakuja ambapo hata hao unaohisi moyo wako 'haujawaridhia' utawatafuta kwa tochi. Tunasubiri thread yako Love Connect :') #GodForbid

Mungu ni wa haki....anakupa sawa na maisha unayoyaishi.Sina papara coz wanaume wa gea ya kuoa ili wapate papuchi wapo pia.
 
Daaah unaweza ukahisi Mungu yupo likizo kwa upande wako. Na-imagine wanaume ambao huyo mdada aliwakataa probably akijua ashapata mume..... the sacrifices she made for the sake of love etc. Mwambie amshukuru tu Mungu kwa yote, pengine huyo mkaka hakuwa riziki yake. Najua ni ngumu sana kwake kumove on, but hiyo ndo only option aliyonayo kwa sasa. Mungu atampigania na atamfuta machozi yake

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums

Ndo hapoo ni bora mtu akuambie mapemaa ili wanakutaka kukuoaa usiwaacheee sasa kamtumiaa weeew miaka yote hiyo hii dunia banaaa unaweza ukaamuumba mtu upyaaa haki ya mamaa
 
Mwambie rafiki yako hajachelewa,bado mapema sana..anachotakiwa ni kuendelea na maisha yake na kufungua ukurasa mpya,for someone who really deserve her.mimi mwenyewe nilikaa na mtu for 4 years at the end akaniambia hana mpango wakuoa leo wala kesho niendelee tu na maisha yangu.Yes..i liuma bt nilijifunza kitu 'usikae na so called boyfriend for soo many years bila hata ya kumuuliza malengo ya mahusiano yenu'..wengine wanajitoa ufahamu na kujidai wanaogopa commitment...'eti,am nt ready'...mwanaume akikupenda anakuwa ready on the spot bt akitaka kukutumia he will never be ready.so as a woman u hv a right to ask abt ur future goals in a relationship.Thank God am happly married to the man who deserve me.
 
Ndio maana sitaki vijana wanaotaka kula ujana, nataka waliokwisha maliza kula ujana!! 4 good years aisee hapana....

Mhhhh wengine mpka 40yrz wanakula ujana hawataki stress za mapenzi,istoshe mapenz hayana guarantee kua nkiwa nawe ndio utakua mke wng.
Wanaume tunaangalia vigezo labda jamaa kuna vi2 aliona kua glady c wife material
 
Ndo hapoo ni bora mtu akuambie mapemaa ili wanakutaka kukuoaa usiwaacheee sasa kamtumiaa weeew miaka yote hiyo hii dunia banaaa unaweza ukaamuumba mtu upyaaa haki ya mamaa

Nanii wa hivyo akuambie pia 4yrz c kipimo kua ntaoana wanaume nasi kuna vi2 tunaangalia c kuoa 2,masharti na vigezo kuzingatiwa
 
Laiti angemwambia kuwa nivumilie mpaka hapo baadae nitakapokuwa nimejipanga hapo sawa. Lakini kuambiwa kuwa "Saivi nina mambo mengi nashindwa kuamua" ina maana hata hayumo kwenye plan zake...

Hakuna anayeyajua hayo mambo mengi aliyonayo huyo bwana so nadhani si sahihi kumhukumu! What if moja ya hayo mambo mengi ni kufunga ndoa au kuanzisha mradi ambao utamfanya aje kuishi safi na mkewe? Jibu lilikuwa ana mambo mengi anashindwa kuchagua lipe alipe kipaumbele... Ni mtazamo tu!
 
Wasichana wengi huwa tunaona kuwa huyu mwanaume hamna future ila tunajipa iman so tunakuwa tunacheza kamali
 
Mungu ni wa haki....anakupa sawa na maisha unayoyaishi.Sina papara coz wanaume wa gea ya kuoa ili wapate papuchi wapo pia.

Always GOD gives what you deserve and not what you need. Mwanaume mpaka anakufuata na kuwaacha wengine (kama alivyofanyiwa rafikiye mtoa mada) ni jambo la kulifikiria mara mbilimbili. Kumbuka kuwa lucky never come twice. May be utamdharau leo kwa kuwa hana pesa, sio smart (handsome) n.k..lakini hutojua kesho yake itakuwaje. Learn through examples and try to be optimistic.
 
Nanii wa hivyo akuambie pia 4yrz c kipimo kua ntaoana wanaume nasi kuna vi2 tunaangalia c kuoa 2,masharti na vigezo kuzingatiwa

Unaniangalia kwa miaka minne mi Tv! !!!!!!ni kusema tu ukwelii uniume ili nijimuvuzishe kwinginee kuolewa ni heshimaaa
 
Marketing kitu gani??

Hivi kwa akili yako humu kuna wanawake wa kuoa??

Kama ukiamua kupata wa kupiga wengi tu, tena nje ya JF mkuu.

JF is never the ultimate source of girls.

Welcome to the world

Amen Mkuu, niwie radhi kama nilikukwaza, Ila wa kuoa yupo, kwani wanawake wa humu wote vicheche mkuu?
 
haya ma'ushauri ya humu yananichoma, nadhani nina la kujifunza hapa
mmmh Mungu uniongoze kwa kweli inawezekana ya Glady yananikaribia
 
Marketing kitu gani??

Hivi kwa akili yako humu kuna wanawake wa kuoa??

Kama ukiamua kupata wa kupiga wengi tu, tena nje ya JF mkuu.

JF is never the ultimate source of girls.

Welcome to the world

Bulldog sorry to say if your comment is anything to go by......Man you are a shallow thinker.
 
Always GOD gives what you deserve and not what you need. Mwanaume mpaka anakufuata na kuwaacha wengine (kama alivyofanyiwa rafikiye mtoa mada) ni jambo la kulifikiria mara mbilimbili. Kumbuka kuwa lucky never come twice. May be utamdharau leo kwa kuwa hana pesa, sio smart (handsome) n.k..lakini hutojua kesho yake itakuwaje. Learn through examples and try to be optimistic.

Una uhakika gani kama kawaacha wengine.....wanaume hawatabiriki.La sivyo unaweza cheza pata potea.Wanaume wanaweza ahidi ndoa hata sehemu tano na kote asioe.Tena mwanamke ukijifanya unasaka ndoa sana basi inakula kwako ma zima coz wataingia na gea hizo hizo.
 
Majanga! Yaani sasa hivi inatakiwa mtu akikutokea unamuuliza unataka nini? Mke, mshkaji ama casual relationship?
Inashangaza sana wanawake hawa hawa kabla ya kupanda dala dala, au kusafiri lazima wajue na watauliza hilo gari linaenda wapi,sasa mbona wanapoanza mahusiano wanashindwa kumuuliza mwenzake hiyo relationship mwisho wake wapi. Ukiona mchizi anakidhi vigezo vyako hutaki hata kuongelea destination yenu, fasta unavua chupi mwenyewe baadae unakuja kulalamika playing the blame game na kujifanya we ndio victim, You are responsible for your own actions, stop being a cry baby and grow up.

Unaongopea Uma ndugu, Mfano mtoto kakidhi vigezo vyote, unahamu ya Papuchi, then anakuuliza una malengo gani nae, utamwambia u r only there for Sex?

Yaani ni sawa upande gari linaelekea mwenge tokae Tazara, halafu lifike Ubungo wanakuambia mwisho, break zimefeli au "klachi" inasumbua.... You have no choice than to drop and find how u will reach yo destination.

Kuongopa ama kuongopewa kupo, afu mnamuonea huruma huyu mdada, mnajua yy kawaumiza wangapi? Si ajabu kuna alieachwa ili dada atoke na huyo Jamaa soo, inakuwa what goes around, comes around.

Wengi wameumizwa na mapenzi, soo its part of Life, a topic you need to learn in the course of Life.

Kusanya vyako Mwanamke, anza safari, Pumzi ni bora kuliko chochote....

Always Learn how to pick up yo self everytime you Fall.

Mengine ni blaablaa tuu.
 
Mimi hua nawashangaa sana tena hasa kinadada,unakuta mnaanza mahusiano na mwanamme kiholela halafu baadaye unaanza kutaka kuolewa kwani wakati mnaanza mahusiano mlipatana kuwa mtaoana mnafikili kila mtu utakaye kuwa naye kimapenzi basi atakuoa:
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom