Miaka 4 ya mahusiano akaambulia patupu

Miaka 4 ya mahusiano akaambulia patupu

Asante rafiki umenisaidia kuelewa unajua nilikua napata shida kuelewa hili kumbe kuna watu wanakua kwenye relationship kwa sababu ya company tu according to @ mafinyofinyo. Lkn hebu tujiulize unampaje mtu company for 4 yrs hapa mdada kuna mahala alikosea nafikiri.

kwa uelewa wangu wanasema we meet for a reason ur either a blessing or a lesson.
alikuwa kwenye mahusiano akiamin yata yield positive results lakin haijawa hivyo. kwa hiyo hili litakua funzo tosha kwake. kumbe hizo 4 years mwenzake alichukulia kama company tu. haya mambo ni magum muda mwingine.
 
Isije ikawa jamaa yake ndio huyo kafunga ndoa leo du
 
Uko sahihi kwani kila binadamu yupo sahihi ktk mtazamo wake lkn naamini huwezi kaa miaka 4 kibubu bubu .

hii story nahs ina mengi yamejificha. pengine huyu shosti alimkuta jamaa tayar ana mtu wake na bibie akataka kuovertake hivyo jamaa kukosa msimamo na kuamua kwenda kibubububu. nway, kuna kuwin au kuloose. akubali tu matokeo na maisha yasonge mbele. binafs siamini miaka yote hiyo minne halaf muachane tu bila sabb ya kueleweka.
tukumbuke pia kuna wanawake wagumu kujirekebisha makosa, pengne jamaa alikuwa anamvumilia bidada vitabia flani flani na imeshindkana kuvirekebisha. tusilaumu tu upande mmoja, tujifanyie assesment na sie tuone wapi tunakosea.
 
kwa uelewa wangu wanasema we meet for a reason ur either a blessing or a lesson.
alikuwa kwenye mahusiano akiamin yata yield positive results lakin haijawa hivyo. kwa hiyo hili litakua funzo tosha kwake. kumbe hizo 4 years mwenzake alichukulia kama company tu. haya mambo ni magum muda mwingine.
Kweli kabisa ni magumu ila rai yangu kwa wadada usikubali kukaa na mtu muda wote huo bila kujua hatma yenu ingawa bado waweza achwa kwani kuna vitu viko nje ya uwezo wetu ni kumuomba Mungu tu.
 
Kweli kabisa ni magumu ila rai yangu kwa wadada usikubali kukaa na mtu muda wote huo bila kujua hatma yenu ingawa bado waweza achwa kwani kuna vitu viko nje ya uwezo wetu ni kumuomba Mungu tu.

nzuri zaidi ni kuulizana toka mnatongozana, kabla hamjaamua kuonjeshana mnajua kabisa mpango wenu ni nini, siyo mtu alikutongoza na wewe ukamkubali kama company tu then moyoni mwako we unawaza ndoa!
 
  • Thanks
Reactions: EMT
hii story nahs ina mengi yamejificha. pengine huyu shosti alimkuta jamaa tayar ana mtu wake na bibie akataka kuovertake hivyo jamaa kukosa msimamo na kuamua kwenda kibubububu. nway, kuna kuwin au kuloose. akubali tu matokeo na maisha yasonge mbele. binafs siamini miaka yote hiyo minne halaf muachane tu bila sabb ya kueleweka.
tukumbuke pia kuna wanawake wagumu kujirekebisha makosa, pengne jamaa alikuwa anamvumilia bidada vitabia flani flani na imeshindkana kuvirekebisha. tusilaumu tu upande mmoja, tujifanyie assesment na sie tuone wapi tunakosea.
Hicho ndicho nilichokua nasema yawezekana na dada kuna pahala ana makosa ingawa ni vigumu kujifahamu kama unakosea bila kuambiwa. Halafu miaka 4 mingi sana kwenye mahusiano inaweza kueleweka tu iwapo kuna masuala ya shule vinginevyo haiko njema. Binadamu tuna kasoro nyingi mno hivyo tukaapo muda wote huo waweza leta matokeo mabaya kwa mmoja wenu. Kumjua sana mtu kuna faida na hasara iwapo bado hamjaanza kuishi pamoja kama wengine wasemavyo ukimchunguza sana kuku huwezi kula kitoweo chake. Kama ulivyosema akubali matokeo na amove on maisha ndivyo yalivyo yana rafu nyingi kuna kuvunjwa mbavu kama ilivyo kwenye mpira.
 
nzuri zaidi ni kuulizana toka mnatongozana, kabla hamjaamua kuonjeshana mnajua kabisa mpango wenu ni nini, siyo mtu alikutongoza na wewe ukamkubali kama company tu then moyoni mwako we unawaza ndoa!
Kweli kabisa usemayo yaani wewe unawaza ndoa mwenzako anawaza company hapo lazima mtofautiane. Ingawa wengi hawapendi kukaa kiaminifu kwenye mahusiano yao lkn ni vema kutoonjeshana kabisa manake mtu akiishaonja haoni tena anachopungukiwa manake kwanini atangaze ndoa iwapo unaweza kumpa kila kitu hata kabla ya kuoana. Hapo lazima ufanywe pozeo mpaka atakapochoka mmoja wenu ndo anakudump unabaki umebutwaa tu usiamini macho yako kwani hata ukirudi nyuma hukumbuki kama palikua na commitment yoyote.
 
Je, walikuwa wanakulana?
Je, walipanga kuoana ama ndiyo kulana which automatically she tought ndio ndoa anafuata.
Kungwi @lara1 njoo ufanye assessment kama ilikuwa free p au lah
 
huwa ni wepesi wa kusahau.
Lakn yawezekana ndivyo walivyoumbwa na Mungu.
Mbona hata wakat wa kuzaa kuna baadhi wanasema hawata zaa tena. Lakn baada ya siku tu kasahau uchungu wote
Acha kusahau..kuna wasichana huwa wanazugwa na vitu vidogo vidogo...wanasahau kuuliza na kujua mambo ya msingi kwenye mahusiano..
 
Je, walikuwa wanakulana?
Je, walipanga kuoana ama ndiyo kulana which automatically she tought ndio ndoa anafuata.
Kungwi @lara1 njoo ufanye assessment kama ilikuwa free p au lah

Hiyo automatically ni free P
 
Duuu pole yake, mi ilikua miak mitatu, na nimate wa chuo bt mwisho wa siku alizaa na mtu kwa siri mi nikazawadiwa mitusi.
 
Kweli kabisa ni magumu ila rai yangu kwa wadada usikubali kukaa na mtu muda wote huo bila kujua hatma yenu ingawa bado waweza achwa kwani kuna vitu viko nje ya uwezo wetu ni kumuomba Mungu tu.

nimekusoma mama... ngoja nianze kuulizana na huyu wangu mapemaaaa
 
Uko sahihi mkuu hapa ni vema tukaangalia kosa la huyu dada iweje udate na mtu 4 yrs bila kujua mwelekeo wenu manake toka mnaanza mahusiano kila mmoja anaonyesha nia yake ili kama zinamatch then mnaendelea na mahusiano huku mkiyaangalia malengo yenu. Hapa inabidi wadada wabadilike wajue kuwa hakunaga muda wa kupoteza yafaa ufanye maamuzi mapena kama utaishi single au unataka kuwa married otherwise utadate na mtu bila kujua hatma yake.

Miaka minne naona kama ni mingi. Of course, kunaweza kuwa na sababu ambazo zinamfanya mwanaume aku-date miaka minne. Inawezekana labda anapatwa na matizo yaliyo juu ya uwezo wake kama kufiwa na watu wa karibu sana, kufukuzwa kazi, au kuuguza mgonjwa, n.k.

Lakini zile execuse za sijui ngoja kwanza nimalize kujenga nyumba I don't but them. Au anakuwambia ana "mambo mengi hivyo, anashindwa kutoa msimamo kwa sasa". Mambo gani hayo ambayo hakushirikishi even after dating for four years? Mwanaume ambaye yuko serious na wewe atakushirikisha kwenye masuala yake. Hayo "mambo mengi yanayomfanya ashindwe kutoa msimamo kwa sasa" yatakuwa pia ni mammbo yako. Lazima mtakaa pamoja na kujadiliana jinsi ya kudeal na hayo mambo bila kuharibu uhusiano wenu. If after four years, bado hana uhakika, then he will never be sure about your relationship and you.

Tofauti na watu wengi wanavyoamini, wanaume wengi wanaweza kuji-commit kwenye mahusiano. Wapo wanaojua moja kwa moja wajicommit kivipi kwenye mahusiano kwa ku-reflect on their lives, how comfortable they are in themselves, attraction waliyonayo kwako plus mazagazaga mengine. Lakini miaka minne ni mingi kwa mwanaume kuwa na uhakika hasa kama amepevuka and is not in his earlier twenties.

This has more to do with the woman than the man. Inabidi huyu mwanamke ajiulize anataka nini hasa? Asahau muda ambao ali-invest kwa huyo mwanaume. This was not a job or some sort of a financial venture between the two. This was all about a relationship. Anaweza kuitumia hiyo miaka minne kujifunza badala ya kudhani kuwa it was a waste of time. Miaka minne atakuwa amekua kiali sasa. Atakuwa amefigure out maisha yake na kujifunza for future relationship(s).
 
Duuu pole yake, mi ilikua miak mitatu, na nimate wa chuo bt mwisho wa siku alizaa na mtu kwa siri mi nikazawadiwa mitusi.

hahahaha story ka ya rafiki yangu imenifanya nicheke ye ilikua kama 6 years baadae akamuacha akampa mimba msichana mwingine wazazi wakachachamaa aoe akaoa. rafiki yangu had I sasa hajatulia kwenye stable relationship tangu aachane na W.
 
6 years and still counting? Kweli mna moyo.
 
Achape lapa hana chake hapo....kwa kifupi tu hamuhitaji.

miss strong;
B/up sana. 4 yrs hata iliyochoropoka hamna??? Naoa wa kuja kujaza choo?? Chapa lapa nilete mchuma mwingine. Ati anajutia midume iliyo mjia akaivimbia, leo wamekuwa wazuri?? Huenda nao walitamani kuona kulikoni mbona jamaa anavumilia tuuu?? Kaushauri; Hama mtaa au mji nenda ugenini huenda akaja mwingine kipofu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom