Miaka 28 sijawahi kumiliki hata milioni moja

Miaka 28 sijawahi kumiliki hata milioni moja

nimeshajaribu kufungua acc na nikawa naweka 50,000 tu, ilipofika 350,000 huyo wa f6 akawa ndo amemaliza f4, nikadraw zote akaenda f5...nakwambia maisha yananipeleka mbio ndo maana nikamweleza mleta uzi kwamba hata mimi m 1 haijawahi kukaa kwenye kibubu

ni hatari
Duuuhh
 
Ama kweli msiba wa wengi furaha.
Mimi mwaka 2013 nilifilisika biashara yangu hadi nikawa nakula maandazi ya Bakhresa mawili na na maji ya Kandoro ili yakavimbiane tumboni.
Huo ulikuwa mlo wa usiku, asubuhi nilikuwa sigusi kitu natafuta michongo tu.
Kuna watu bado nilikuwa nawadai, kwa hiyo akilipa deni nakula ugali dagaa wa 1200 katikati ya usiku na mchana yaani mida ya saa 11 jioni then naunga hadi kesho.
VIP kwa sasa
 
Sasa wewe kila siku uko kwenye MAANDAMANO YA KINA LISSU NA MBOWE,Wanakutumia kuingiza MAMILIONI YA KULA WAO NA WAKE ZAO,Then unategemea upate MILIONI Lini.
"If you must change the way YOU PERCEIVE THINGS"
Sijawahi kwenda huko mkuu
 
bundle,simu ya kuchat na mabwana wa JF ,shopping,dining out ...all these leave me penyless....🙂🙂🙂🙂🙂🙂🙂🙂🙂🙂🙂🙂🙂🙂🙂🙂🙂🙂🙂🙂
Poleee
1470424884570.jpg
 
Jiunge na wazee wa Kubet, utaingiza milion na zaid
 
Weka akiba, acha starehe panga mambo yako vizuri SIKU ukipata fedha yawe ya kwanza kuyashughulikia. Mwisho chagua marafiki sahihi wa kuwa nao. Kwa hapo ulipo penda kuwa na aina ya marafiki walio kutangulia ili wakupe changamoto mpya
 
Nidhamu ya matumizi ni muhimu sana ukitaka kuweka akiba na kuanzisha mradi wa kibiashara utakaokuingizia hela. Ningependa utunze kumbukumbu za matumizi yako na mwisho wa mwezi uorodheshe matumizi yako. Hapo utagundua mahali ambapo hela yako inatumika zaidi. Ukishagundua jinyime. Utashangaa jinsi utavyoweka mamilioni ya akiba. Btw: kama upo single yafaa uoe au uolewe. Mkiwa wawili ndani mnafunguana macho. Mipango mnayoiweka inawafanya kuweka akiba.
 
Kila mwezi jitahidi kujitafakari katika pesa yako ya mshahara umefanya nini cha maendelea au umeserve kiasi gani. Mwisho wa mwaka jitathmini kuna kitu gani cha maendeleo umefanya, ukiona unaishi hand to mouth ujue kabisa utakuwa masikini na mwisho wako sio mzuri, jaribu kutafuta chochote cha kufanya uingize pesa, kuna jamaa nafahamu amejenga nyumba na ipo kwenye viwanja viwili in one na kaweka bati za mgongo mpana kwa ajili ya kusuka watu nywele aina za rasta. Ondoa mawazo kichwani haiwezekani haya mawazo yatakufanya uone haiwezekani daima
 
mwaka2013 nilikuwa nafanya kazi fulani ambayo mwisho wa mwaka tulikaa na mhasibu wa kampuni tukapiga hesabu tumeingiza dola laki1 na ushee na tukapiga hesabu za matumizi yangu tukakuta ni kama dola elfu8 nikakaa chini nikatafakari saana saana hivi hii pesa niliyoiingizia kampuni ni nyingi sana na mimi hii pesa niliyoipata laiti kama ningekuwa na usimamiz mzuri wa matumizi yangu ingewezekana kila mwaka nikawa na akiba ata ya dola4000 au 3000
ila kwa sababu yakutokua na nidhamu ya pesa ndio
ivyo unajikuta pesa unapata ila inapoishia hauoni na kuona kama kuna mazingira tata ya pesa inapokwenda

Kikubwa ni kuwa na nidhamu ya pesa unayoipata na kusimamia vizuri bajeti yako na malengo uliyoyaweka achana na kuhonga mkuu na kuwa na mwanamke mmoja kama utaweza maana hawa nao wanahusika sana na màtumizi yako ya msingi ambayo hauwezi kuyakwepa
Kama hela yako ulikuwa unaikanyaga sa utamshaurije mwenzako?
 
Afadhali yako wewe unawaza milioni, mimi nawaza jinsi ya kupata mlo mmoja wa siku, nikipata mia tano naenda kwa mama ntilie ananikwangulia ukoko na maharage au mchuzi siku imepita
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] pamoja na kukwepa kulipa kodi bado hujaji make tu mkuu?
 
Hapo kuwa na mwanamke mmoja ni jambo jema, nilijitia kiherehere nikawa nao watatu, pesa zilinitoka balaa nikajikuta sijafanya cha maana.

Ss hv mmoja nimemtua, amebakia mwengine natafuta namna ya kumalizana nae ,ili nibakize mmoja ambay ananikumbusha kila siku Maendeleo na matumiz ya pesa. Hawa wengn wanawaza kudhurura tu
ha ha ha,,huyo uliemtua umempa haki yake?,nusu ya mali mliyochuma au ndo umemdhulumu?
 
Wengi tunapokea m na kitu wengi tu mpaka hata m 2 au na nusu ukijumlisha na vimiradi unapata hata m 3 ila hatuwezi kuwa nazo mkononi kwa sababu ya majukumu kwa hiyo unaposema hujawahi kukamata m ina maana kwamba hupati mshahara huo au unapokea nyingi ila hazikai na kama hujakamata m jiulize umefanya mambo mangapi maana tatizo sio kushika m tatizo n umefanya mambo gani? Kama hujawahi kushika m na umegegeda dada zetu wa kutosha basi wewe tambua tu kwamba hutashika mpaka unakufa ila wadada wai wanazishika sana tu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom