Tatizo kubwa la kibongo Tunawaza sana namna ya kutumia Pesa kuliko Kutafuta Pesa, Yani hii ni pale mtu anawaza apate saa nzuri, gari nzuri, kuhonga! Sasa Muda Mwingi hatutumii kuwaza namna ya kuchange Ideas into Cash. Tunawaza Namna ya Kubadili Cash into Viatu na anasa. Siku zote ukipata Pesa, Usiwe na Presha, tulia kabisa, kama ukiweza achana nayo, we endelea na Maisha ya kawaida kabisa, Halafu baada ya Muda utagundua kuna kitu kizuri cha kuifanyia. Hata wale ambao wanatengeneza Video, ukiwa shooting Mtachukua scene nyingi sana, Lakini wale Maproducer na Madirector wa Video huwa wanahitaji sana muda ili watoe kitu kizuri. vivyo hivyo ukiwa kijana Jitahidi kuwa na Malengo, epuka gharama zisizo za lazima, kuwa na nidhamu ya pesa, Fanya kazi kwa bidii, tengeneza Networking na Watu wakupe Ideas na Market, ukipata pesa usiwe na pupa, just vumilia, Naamini hiyo 1million kuna siku utakuwa unawapa Ofa watu, kwa sababu utakuwa Billionea.