The dream
JF-Expert Member
- May 10, 2015
- 999
- 997
Sio kweli mkuu hata kidogo, kwani kutoa mimba ndio ujanja kuonesha kwamba una uwezo wa kuzaa?Kama wewe ni mwanaume au mwanamke na umetimiza miaka 27 lakini huna hata mtoto wa kusingiziwa na hata kutoa mimba hujawahi basi unapaswa kujichunguza huenda una matatizo ya kizazi.
Haiwezekani mtu anaefanya ngono hadi kufikisha umri huo hana mtoto, hilo ni tatizo maana maisha ya sasa ni mafupi sana! Sasa kama hutaacha legacy basi ni hatari sana kwako au subiri tu kuitwa babu au bibi na watoto wako.
Wenzako wanaacha kuzaa wewe ndio unaanza![]()
![]()
![]()
Wanafunzi wengi wa vyuo Tanzania wanamaliza wakiwa na 24-26 yrs, so kwa bandiko lako ulipenda wazae wakiwa vyuoni huko au wazae baada tu ya kumaliza chuo wakiwa hawana hata ramani ya maisha?
Mi nafikiri suala la kuzaa na kua na familia ni personal sana na kila mtu anafanya kwa muda wake baada ya kujiandaa(hasa kwa wanaume)
Moja ya sababu ambazo zinatufanya sisi waafrica kua masikini ni kua na kundi kubwa katika jamii ambalo halizalishi(sio productive kiuchumi) ambalo ni watoto wadogo na kua na kundi dogo sana la watu wanaofanya kazi kuhudumia kundi hilo kubwa(watoto na wazee).Ukiangalia graph za population za nchi zilizoendelea utakua watu wazima ni wengi kuliko watoto wadogo.
Tukiiendelea na mitizamo kama hii kwamba ukiwa huna mtoto na una miaka zaidi ya 27 umaskini hautatuacha kamwe.
