Miaka 20 ijayo, majina ya Asili Tanzania yatakuwa yamefutika kabisa

Mnajazana ujinga kuitana majina ya kilugha kana kwamba ndo mmeepukana na utumwa.

Hakuna mwafrika ambaye si mtumwa. Mifumo ya dunia hii imetengenezwa kutegemea wazungu.
 
Mimi ni wakwanza sitak kumpa mtoto wangu jina la kurithi kabisa ntampa hayohayo yanayoonekana yakizungu, mimi nina jina la kurithi linanitesa balaaa mizimu hainishi nipo napambana na maombez kanisani kwasabu sitaki uganga na wenzangu wenye hilo jina karibu wanne wamekua waganga kisa ni hilohilo jina lol
Naunga mkono hoja..

Haya majina ya kurithi ( mengine tusiyojua maana yake) yametusumbua Sana na kukwamisha mengi maishani.
YEHODAYA Blood of Jesus Mshana Jr
 
Miaka 20 ijayo majina ya Asili Tanzania ya makabila kama Ngonyani, Mkude, Kimaro, Haule, Maduhu, Mwita, Wambura, Mabada, Sumari, Kiondo nk yatakua ni ya kuhesabu ana ni ya kutafuta ama yatakua yameisha kabisa.

Leo 95% ya watoto wanaozaliwa majini ni James, John, Abdalah, Mohamed, Abdrazak, Jayden, Johnson, Beatus, Julius, julieth, Jayna, Jasmine, Chris, nk nk.

Wazazi wa siku hizi unakuta kabisa wanauliza eti naomba jina zuri la mtoto wa kike, naomba jina zuri la mtoto wa kiume halafu mapendekezo yanayotolewa huwezi kukuta jina la asili hata moja.

Uzungu, ulimbukeni na ushamba utafuta kabisa majina ya asili ya wazee wetu wa zamani, watasahaulika kabisa.

Mimi binafsi sijawahi kuona ni wapi dini inalazimisha kwamba ni lazima mtu abatizwe kwa majina ya kizungu ama ya jamii nyingine, sasa sijui hii ya kwetu inatoka wapi.

Nashindwa kuelewa, kwamba nikibatizwa John ndio Mungu anapenda ila nikibatizwa Majura Mungu hapendi ama ni nini? Mungu anafanyia nini jina langu?
Nilikuwa Kilimanjaro wiki iliyopita kwenye ubatizo wa mtoto wa mshikaji. Mtoto anaitwa 'Pandemic Covid Lyimo'.
 
Siyataki ya kifala sana yanaleta ukabila ukitaja tu unajulika unatokea kabila gani siji kumpa mwanangu hayo majina sijui kindamba ndo nn Sasa masumbuko ona na hili

Nimetaja jina somewhere HR enzi izo anakaniambia we ni kabila fulani unatokea sehemu fulani na ni kweli yeye ni mchaga hpo nikakosa job akapewa mwenye jina la macha niliomba nae pamoja pia tulikuwa marafiki tulimaliza wote
 
Wanangu nitakuwa kuwapa majina yenye utata hujui kabila gani Wala dini gani kama ibrahimu ,mussa ,Sophia,adam
 
We amini unavyoamini na mie niache! Siwezi kuabudu mtu aliyekufa ambaye anataka kila mwaka nimwage dam sijui niague mtu! Niache ustarabu wa kuvaa sut na baibui nivae kaniki?
Sawa ioa ukifa unaungana na ndugu zako uliowakana na wao wanakukana ni bora kua kat kat hapa usinielewe vibaya maana maandiko yenu yanasema usiwe moto wala barid kua upande mmoja ila unaweza kua kwa mungu wa kweli ambae anaitambua uwepo wa roho hizo ndio maana katika sala ya marehem wanatamka usikumbuke roho zilizo toharan tohara ni roho zilizo kat kat ya mungu na dunia ambayo bado zipo hai ni kama eneo la kusafishwa kuelekea mahala patakatifu kwa mungu hapa ndipo ilipo mizimu na kua kat kat kwenye dini zenu maana ukijitenga watakutenga kikubwa wanachoitaji ni sadaka yako tu haijalish wewe nan unafanya dhamb au lah
 
Atuganile tuntufye mwakifulefule...kwanza refu balaa😅
Kuna siku nilikuwa napita pale soko matola kwenye ile round about kuna sehemu wameorodhesha majina ya wanajeshi waliokufa na kuzikwa eneo hilo

Aise nilijikuta nashindwa kujizuia yani nilicheka yale majina yalikuwa mapya kwangu.

Yale majina yanachekesha aisee asikuambie mtu, kuna moja liliamdikwa antutusuigwege mwakilongwa.
 
Mmh kwa kweli sijui wahenga walifikiri Nini kutunga hayo majina.
 
Miaka 20 ijayo majina ya Asili Tanzania ya makabila kama Ngonyani, Mkude, Kimaro, Haule, Maduhu, Mwita, Wambura, Mabada, Sumari, Kiondo nk yatakua ni ya kuhesabu ana ni ya kutafuta ama yatakua yameisha kabisa.

Leo 95% ya watoto wanaozaliwa majini ni James, John, Abdalah, Mohamed, Abdrazak, Jayden, Johnson, Beatus, Julius, julieth, Jayna, Jasmine, Chris, nk nk.

Wazazi wa siku hizi unakuta kabisa wanauliza eti naomba jina zuri la mtoto wa kike, naomba jina zuri la mtoto wa kiume halafu mapendekezo yanayotolewa huwezi kukuta jina la asili hata moja.

Uzungu, ulimbukeni na ushamba utafuta kabisa majina ya asili ya wazee wetu wa zamani, watasahaulika kabisa.

Mimi binafsi sijawahi kuona ni wapi dini inalazimisha kwamba ni lazima mtu abatizwe kwa majina ya kizungu ama ya jamii nyingine, sasa sijui hii ya kwetu inatoka wapi.

Nashindwa kuelewa, kwamba nikibatizwa John ndio Mungu anapenda ila nikibatizwa Majura Mungu hapendi ama ni nini? Mungu anafanyia nini jina langu?
Avatar yako ni kabila gani tuanzie hapo
 
Vizuri lazima vipendwe na vilivyo vibaya lazima visemwe

Ungependa kutunza misingi ya kiafrika basi leo hii kama we ni mwanamke hukupaswa kuvaa nguo

Ulitakiwa uwe umevaa magome ya miti na ukiyaacha matiti wazi
Sasa hizo nguo zimekusaidia nini kama bikra zote umepotezea? Hao waliokua wanaacha matiti nje mbona hawakupoteza bikra zao
 
Mimi ni wakwanza sitak kumpa mtoto wangu jina la kurithi kabisa ntampa hayohayo yanayoonekana yakizungu, mimi nina jina la kurithi linanitesa balaaa mizimu hainishi nipo napambana na maombez kanisani kwasabu sitaki uganga na wenzangu wenye hilo jina karibu wanne wamekua waganga kisa ni hilohilo jina lol
Sasa subiri kizazi chako kutakavyoteseka unampa mtt jina la john kumbe mzimu wa john ulikuwa shoga huko ulaya
 
Watu wasichokijua majina ya afrika yananguvu sana ww angalia mfano mtu aitwa julius mwantika...automatic jina la mwantika ndio linakuwa na nguvu! Kingine wakoloni hawakuwa wapumbavu kutaka kufata majina ya afrika walijua yananguvu na yanatenda
 
Hayo kama yapo kwenu hata wote mkija kujiita majina ya kizungu yatakuja tu......huwezi kimbia asili yako
Ndugu hz dini zinawaaribu sana watu. Watu hawataki asili yao hawataki kuridhi mila zao, ndio maana kwenye familia zetu mtu akichewa kidogo mambo yanaharibika kwasabb watu wanakosa kinga za koo zao km hzi... mtu anakwambia hataki mikoba, mwingine anaitia moto mara anaenda kwenye maombi hajui wale ni ancestors wake wamekuja na wanataka kutunza asili ya koo yake kupita yy na mda mwingine ni kwa ajili ya ulinzi wake mafanikio yake na kizazi chake. Kwanza ile kitu huja kwa bahati sana ndio maana sio kila mtu inamtokea na ikikutokea ujue ww una kitu chaziada kwenye damu yako!!

Nasio lzm uzima uwe mganga wa kutibia watu ile unakuwa nayo kuwatuliza ancestors. Ile kitu ukiwa nayo watakuonyesha vitu vingi na kukupa nguvu
 
Back
Top Bottom