Miaka 20 ijayo, majina ya Asili Tanzania yatakuwa yamefutika kabisa

Siyataki ya kifala sana yanaleta ukabila ukitaja tu unajulika unatokea kabila gani siji kumpa mwanangu hayo majina sijui kindamba ndo nn Sasa masumbuko ona na hili

Nimetaja jina somewhere HR enzi izo anakaniambia we ni kabila fulani unatokea sehemu fulani na ni kweli yeye ni mchaga hpo nikakosa job akapewa mwenye jina la macha niliomba nae pamoja pia tulikuwa marafiki tulimaliza wote
Fikra finyu sana hz.. Hata hayo majina ya waarabu na wazungu bado nayo yana udini mwingi...!! Majina haya ya afrika kwanza yalikuwa yanasaidia mtu kujua ametokea wapi ili hata ukipata tatzo watu wanajua wapi watapata ndugu zako.

Sasa hv unaweza ukatoka dar mwanza utaenda dar na ww ni msukuma na usijue ndugu yako wala usipate mtu wa kukusaidia kwasbb kila mtu ana jina la slave master wake. Alafu kingine inabidi ujifunzr historia ktk mlengo wa waafrika pia na sio huo mlengo wa wazungu unakuaminisha eti waafrika wanaukabila ukabila uliletwa na wakoloni kwania kuintroduce pinciple ya divide and rule...mfno ni watusi na wahutu mfaransa ndio aliyeanzisha ukabila kwa kuwafanya kabila moja kuwapa hadhi na jingine kulishusha
 
Tuache utani jina lazima liwe na flavour unapolitamka na sio kufata kigezo cha maana ya jina.

Mi najiukiza kwanini majina yetu ya asili yote yawe yana sound vibaya, kwanini hatukuwa na ubunifu wa kufanya majina ya kiasili yawe na flolavojr nzuri kuwa attract hata wageni?

Nenda mbeya kule utakutana na kina Tuntufye, Mponjoli, Mwakitwange, asumwisye, Yalileni, Lipungo, Kibweja nk

Kama ni wazee hiyo inakuwa imekaa fresh kwao, ila kama ni vijana basi 85% hawafurahii majina yao

Kuna jamaa nilisoma naye alikuwa anaitwa "Tuombe" baada ya shuke tukapotezana siku nayokutana naye nikaskia washkaji zake wanamuita Jerady

Sikutaka kumuuliza ila alipoona nimrpigwa bumbuwazi akaniambia usishangae nishabadili jina nikasema freshi.
tuntufye au tuntu kama tumuitavyo yupo mtaani kwangu huwa nawaza wazazi wake walikuwa wanawaza nini sijui,ingawa ana jina jingine la mjini.

kuna mabaharia nimekutana nao waliitwa ndundu,kirundu,chililo,mponda dodo,cholo
yaani majina hayana hata ladha,kama wale jamaa wahadzabe wale mtu anaitwa khunkhu.
 
Mbona mimi bado natumia na nitaendelea kutumia jina la Kuku wa zabanga papa fololo, Kipeme biss ya mboka?
 
Ndugu hz dini zinawaaribu sana watu. Watu hawataki asili yao hawataki kuridhi mila zao, ndio maana kwenye familia zetu mtu akichewa kidogo mambo yanaharibika kwasabb watu wanakosa kinga za koo zao km hzi... mtu anakwambia hataki mikoba, mwingine anaitia moto mara anaenda kwenye maombi hajui wale ni ancestors wake wamekuja na wanataka kutunza asili ya koo yake kupita yy na mda mwingine ni kwa ajili ya ulinzi wake mafanikio yake na kizazi chake. Kwanza ile kitu huja kwa bahati sana ndio maana sio kila mtu inamtokea na ikikutokea ujue ww una kitu chaziada kwenye damu yako!!

Nasio lzm uzima uwe mganga wa kutibia watu ile unakuwa nayo kuwatuliza ancestors. Ile kitu ukiwa nayo watakuonyesha vitu vingi na kukupa nguvu
Ndo hivo tena wengi wameshapumbazwa
 
Chagua haya ya kienyeji: Shida, taabu, mateso, majuto, simanzi, chausiku, kisirani, kivuruge,n.k
 
Yanasaidia nini??

FB_IMG_16522075484108470.jpg
 
Mimi ni wakwanza sitak kumpa mtoto wangu jina la kurithi kabisa ntampa hayohayo yanayoonekana yakizungu, mimi nina jina la kurithi linanitesa balaaa mizimu hainishi nipo napambana na maombez kanisani kwasabu sitaki uganga na wenzangu wenye hilo jina karibu wanne wamekua waganga kisa ni hilohilo jina lol
Hayawatesi,,,,mnajitesa wenyewe kwa kukimbilia mambo ya wengine na kuacha ya kwenu
 
Leo 95% ya watoto wanaozaliwa majini ni James, John, Abdalah, Mohamed, Abdrazak, Jayden, Johnson, Beatus, Julius, julieth, Jayna, Jasmine, Chris, nk nk.kwenye intervi
Leo tumetoka kwenye kuinterview watu kwenye kada fulani nimeshituka interviewee mmoja wa kike anaitwa Loveson
 
Miaka 20 ijayo majina ya Asili Tanzania ya makabila kama Ngonyani, Mkude, Kimaro, Haule, Maduhu, Mwita, Wambura, Mabada, Sumari, Kiondo nk yatakua ni ya kuhesabu ana ni ya kutafuta ama yatakua yameisha kabisa.

Leo 95% ya watoto wanaozaliwa majini ni James, John, Abdalah, Mohamed, Abdrazak, Jayden, Johnson, Beatus, Julius, julieth, Jayna, Jasmine, Chris, nk nk.

Wazazi wa siku hizi unakuta kabisa wanauliza eti naomba jina zuri la mtoto wa kike, naomba jina zuri la mtoto wa kiume halafu mapendekezo yanayotolewa huwezi kukuta jina la asili hata moja.

Uzungu, ulimbukeni na ushamba utafuta kabisa majina ya asili ya wazee wetu wa zamani, watasahaulika kabisa.

Mimi binafsi sijawahi kuona ni wapi dini inalazimisha kwamba ni lazima mtu abatizwe kwa majina ya kizungu ama ya jamii nyingine, sasa sijui hii ya kwetu inatoka wapi.

Nashindwa kuelewa, kwamba nikibatizwa John ndio Mungu anapenda ila nikibatizwa Majura Mungu hapendi ama ni nini? Mungu anafanyia nini jina langu?
Mkuu hivi wazazi wako wangekupa jina la kisoda au kichuguu, ungefurahi?

Majina mengine ya kiafrika yana maana ya uchuro mtupu.
 
Sasa majina kama mateso, tabu kweli umwit mwanao, Mi wa kwanza kukataa majina ya mababu nilivopata ka akili kidogo
 
Mambo ya walimwengu waachie wenyewe...

Unaona hata magome ya miti hatuvai tena tunapiga pamba nyepesi...
 
Sisi wahaya tupo proud na majina yetu ya asili ujinga ni kutojua tu maana majina yote duniani yana fanana maana utofouti ni utamkwaji katika lugha Love Pendo glad furaha
 
Kazi kubwa ya kwanza aliyofanya mzungu ni kuhakikisha mtu mweusi anaikataa asili na ustaarabu wake na kufuata wa kigeni.......

Kitu ambacho hatujui ni kuwa hayo majina ya wazungu ndio majina yao ya asili........

Huu ni ulimbukeni na ulemavu wa akili aliotuachia wakoloni........
 
Back
Top Bottom