Waafrika ni wamoja ushahidi majina ya wachezaji wa Afrika magharibi AFCON

Steven Joel Ntamusano

JF-Expert Member
Jun 17, 2023
2,948
1,988
Nilianza kumsikia Ibrahim Bakayoko akiwa mchezaji wa Ivory Coast akitamba Ulaya miaka kama 18 iliyopita. Nikamsikia Camara akitamba pale Liverpool miaka zaidi ya 22 iliyopita, alikuwa akirudi afrika anachezea timu ya Taifa ya Guinea.

Nikamsikia Souleymane Sane akichezea Ivory Coast miaka 30 iliyopita huyu akaacha mtoto wake akaja kuwa nyota pale Man City na sasa ni nyota wa Bayern Munich.

Kuna majina ni utambulisho mpana wa raia wa Afrika ya Magharibi Camara, Diarra, Bakayoko, Diakhite, Diawara, Konate, Kanoute. Ukiyasikia tu unajua ni raia wa nchi mojawapo ya afrika ya magharibi. asipokuwa raia wa Mali atakuwa wa Guinea asipokuwa wa Guinea atakuwa ni Ivory Coast, Nigeria, Gambia, Senegal na hata Nigeria wapo kina Keita, Koita.

Wazungu walipokuja afrika waliona cha muhimu kwanza ni kuwagawa hawa waafrika ili wapoteane kabisa kwa kuwawekea mipaka ya Berlin. Walituanzisha uhasama wa asili kwa kutuchorea mipaka wakati ukichunguza maana ya hayo majina ya magharibi unakuta yana maana moja ile ile.

Camara wa Guinea hana tofauti na yule wa Chad au Mauritania na jina linaweza kuwa lilitolewa kwa sababu ile ile kwa nchi zote tatu.

Tambwe wapo Tabora na wapo Kinshasa DRC. Kasambula wapo Mtwara na pia wapo DRC. Mwanza wapo Rukwa na pia wametapakaa Zimbabwe, Zambia na Malawi. Mwenda wapo Singida na pia wapo Afrika ya Kusini na Namibia.

Sisi ni wabantu ni watu wamoja ambao tulidanganywa tuna tofauti kwa kuwekewa mipaka ili utajiri wetu usitutajirishe na uwe na neema kwa wazungu peke yao, kuweza kuutambua ukweli huo ni mwanzo mzuri wa mwafrika kuweza kuitambua asili yake kwa mapana ili aweze kupigania fahari ya miaka na miaka inayokwenda pamoja na utu wake.

Nilisikitishwa na kauli ya hivi karibuni kutoka kwa mtu mwenye cheo cha juu kabisa anayevaa magwanda, ilikosa kuona mbali na busara ya kina. Kuna kushambuliwa kwa watu wenye asili ya Burundi na Rwanda kama vile hao wanaotokea mipaka ya kusini mwa Tanzania hawawezi kuwa na nia mbaya dhidi ya Tanzania!.

Mwalimu Nyerere alikuwa ni bingwa wa masuala ya ubinadamu na akapewa shahada nyingi za heshima na vyuo mbalimbali vya dunia, sababu mojawapo ni namna alivyowakaribisha wanyasa hapa nchini na kuwapa uraia wa asili wakajiona kama vile wapo kwao Malawi, kina Kanyama Chiume miaka yote walikuwa wakiandika makala kwenye magazeti yetu huku wengi wetu tukidhani ni watanzania wenzetu!. Huo ni upendo wa Mwalimu Nyerere.

Hakuongozwa na roho za chuki zinapandikizwa hivi sasa, kana kwamba asili yetu ni kitu cha kujivunia sana, ni asili nyepesi kuilinganisha na upendo wa kibinadamu kwani ni asili inayoongozwa na mipaka iliyowekwa kwa nia za kifedhuli za wakoloni.

Mungu Ibariki Tanzania, Mungu ubariki mshikamano wetu unaopitia msukosuko mwingine wa kitaifa.
 
Back
Top Bottom