The Assassin
JF-Expert Member
- Oct 30, 2018
- 4,289
- 16,973
Miaka 20 ijayo majina ya Asili Tanzania ya makabila kama Ngonyani, Mkude, Kimaro, Haule, Maduhu, Mwita, Wambura, Mabada, Sumari, Kiondo nk yatakua ni ya kuhesabu ana ni ya kutafuta ama yatakua yameisha kabisa.
Leo 95% ya watoto wanaozaliwa majini ni James, John, Abdalah, Mohamed, Abdrazak, Jayden, Johnson, Beatus, Julius, julieth, Jayna, Jasmine, Chris, nk nk.
Wazazi wa siku hizi unakuta kabisa wanauliza eti naomba jina zuri la mtoto wa kike, naomba jina zuri la mtoto wa kiume halafu mapendekezo yanayotolewa huwezi kukuta jina la asili hata moja.
Uzungu, ulimbukeni na ushamba utafuta kabisa majina ya asili ya wazee wetu wa zamani, watasahaulika kabisa.
Mimi binafsi sijawahi kuona ni wapi dini inalazimisha kwamba ni lazima mtu abatizwe kwa majina ya kizungu ama ya jamii nyingine, sasa sijui hii ya kwetu inatoka wapi.
Nashindwa kuelewa, kwamba nikibatizwa John ndio Mungu anapenda ila nikibatizwa Majura Mungu hapendi ama ni nini? Mungu anafanyia nini jina langu?