Mhh! Maskini! Wanamuomba msamaha kwa kosa lipi?

Kuna watu wana roho mbaya, ni wakatili, ni wabinafsi! Ila huyu mzee amezidi. Yaani kwa utashi wake na maamuzi yake, ameamua tu kuwafanya wafanyakazi waishi kama watumwa.

Unafanyishwa kazi kinguvu, unatishwa, unanyimwa haki zako za msingi, unanyanyaswa bila sababu!! Inashangaza sana kuona watu wema wanakufa mapema, halafu wale wabaya wanadunda tu mtaani!!

Yaani miaka zaidi ya sita hakuna kupandishwa daraja! Unaishi kwa mshahara ule ule tangu mwaka 2014! Bora tungetawaliwa na dikteta kamili kama ilivyokua kwa Gaddaf ila siyo dikteta uchwara.
Wewe kwa chuki zako ndo maana ulitumbuliwa mapema tu.
Mwache rais apambane kuweka uchumi wa hii nchi vyema, hata siku mishahara ikipandishwa thamani yake ionekane.

Bila kudhibiti mifumuko ya bei kwa bidhaa, mshahara hata upande bado mzigo utakuwa mkubwa tu kwa watumishi.

WAVUMILIE KIDOGO TU MAMBO YATAKUWA MSWANO.
 
Kwani lazima afanye kazi? Mwambieni aache kazi
Mawazo haya ni ya kitoto sana ukute ndoo wale mlioteuliwa mnakula kuku kwa mlija ungejuwa watumishi wanavyohangaika mitaani na familia zao usingeongea hivi! Raisi ajue anaowaongoza wanafamilia na wanamajukumu ya kusomesha kula na kufanya mambo mengine ya maendeleo swala la mishahara aliangalie sana huku kada za ualimu manes madakitari wamenyanganywa Hadi kadi zao za benki wameziweka kwenye taasisi ndogo za fedha kwa ajir ya kukopeshwa mbaya zaidi wametoa namba za siri
 
Ndo wajiongeze wafanye na shughur nyingine,Kuna sst angu n mwalm wa primary ana ki biashara cha kukopesha na kuuza vitenge, hategemei mshahara na mambo yake yanaenda poa, tatizo Watz uvivu mwingii, angalia mfano nchi Kama China, mtu kaajiliwa sehem 2, au kaajiliwa sehem but kajiajil, ukifika hm saa 11, one hour unaweza fanya kitu ukapata pesa ya kula, weekends, sasa Kama unapenda fuatilia movie na tamthilia YOU WILL DIE POOR
 
Wafanyakazi wenzangu walioko Serikalini wameniomba nije kukuomba radhi, kama wakati wowote tangu ukiwa waziri hadi Rais kuna mahali tulikukosea, tunaomba msamaha. Maisha yetu huku mtaani ni magumu, hatuna furaha, baadhi yetu tuna sura za uzee kumbe bado vijana.
Mkuu hapa naona umeweka ubaguzi. mfanyakazi ni mfanyakazi bila kujali yupo serikalini au kampuni binafsi.
kwa ufahamu wangu mdogo,mliopo serikalini hasa hasa mamlaka(EWURA,PURA,LATRA,TRA,TCRA n.k) nao wamekutuma uombe msamaha?
Umechunguza wafanyakazi waliopo makampuni ya wahindi na wachina wanalipwaje ukilinganisha na mliopo serikalini ?

kwa ufupi sisi tuliopo makampuni binafsi tunawaonea wivu,sema tu nafasi za kuajiriwa serikalini ni kidogo tunalazimika kwenda makampuni binafsi. Suala la mfanya kazi kuwa na TIN nampongeza rais maana hata tulipokuwa hatuna TIN tulilipa pay as you earn wakati mamalaka hazikutambui kama mlipa kodi,utaratibu uliopo kwa sasa ni mzuri maana hata mimi natambulika kama mlipa kodi.

Ukienda dukani kkoo kwa kiasi fulani thamani ya fedha yako ndogo unaiona,ikilinganishwa na zamani ambapo fedha ndogo ya mshahara ilipambanishwa na fedha ya vigogo waliopiga mabilioni ya fedha na kwenda shopping ambapo wafanya biashara waliuza kwa faida zaidi ya mara mbili. Ni kweli kwa sasa mishahara haijaongezeka lakini kitu kinaitwa value for money kinaonekana.
 
Watumishi wa umma wamwache Rais wetu kipenzi atekeleze miradi yake ya kimkakati. Sasa akianza kuwalipa mapunjo atatoa wapi pesa ya kujenga hiyo miradi? John, shikilia hapo hapo tu na ukaze sana baba, sisi wanyonge tuko nyuma yako! Siyapendi matumishi ya umma kwa sababu hayajitambui! Na mimi nilikuwa huko nikabwaga manyanga! Wacha yakome!!
 
Usibadili somo husika la huu uzi. Haijawahi kutokea tangu tupate uhuru miaka 60 iliyopita kwa Wafanyajazi wa Serikali kutopewa nyongeza ya mishahara kwa miaka 6 mfululizo, na huu uchumi unavyozidi kuyumba si ajabu hata miaka 10 itafika bila nyongeza. Gharama za maisha tangu 2015 zimepanda sana lakini mishahara imebaki ile ile hivyo kusababisha Wafanyakazi wengi wawe na madeni makubwa kutokana na mikopo wanayochukua sehemu mbali mbali ili kukidhi gharama zao za maisha za kila siku.
nadhani sasa ni wakati muafaka wafanyakazi wote, wapunguziwe mishahara yao ilikusudi ielekezwe kwenye shughuli za maendeleo ya nchi, twataka nchi hii itoke uchumi wa kati na kwenda uchumi wa juu zaidi.
 
hii nchi inavijana wengi wasomi wamezagaa mitaani, kama kunamfanyakazi anaona hatendewi haki, mara moja na haraka sana
bila shuruti aache kazi, ili kusudi waingie vijana wasomi na wachapakazi walokosa ajira, rizikeni na jiongezeni na mnachokipata.
Hata ikitokea hivyo unavyosema ww baada ya muda na wao wapya wataanza kulalamika na kudai nyongeza ya mishahara....miaka sita unalipwa mshahara uleule wakat gharama za maisha zinapanda inakatisha tamaa kwa kweli.
 
Sent from my CAM-L21 using JamiiForums mobile app
watulie bado minne tu, au wakipenda wamuongezee kumi mingine ili awaweke sawa wajue kujiongeza na kujitegemea kama watu wengine bila kutegemea mshahara.
 
Poleni kwa hii shubiri manayoinywa wafanyakazi hasa wa serikalini.

Bado minne tu, asipoongeza muda madarakani.!
 
hii nchi inavijana wengi wasomi wamezagaa mitaani, kama kunamfanyakazi anaona hatendewi haki, mara moja na haraka sana
bila shuruti aache kazi, ili kusudi waingie vijana wasomi na wachapakazi walokosa ajira, rizikeni na jiongezeni na mnachokipata.

Nao wakiingia wakafanya kazi kidogo kwa staili hii ya malipo kiduchu lazima nao waanze kulalamika,kumbuka wakipata kazi matumizi yanaongezeka.
 
Back
Top Bottom