Mhh! Maskini! Wanamuomba msamaha kwa kosa lipi?

Mhh! Maskini! Wanamuomba msamaha kwa kosa lipi?

Kuna watu wana roho mbaya, ni wakatili, ni wabinafsi! Ila huyu mzee amezidi. Yaani kwa utashi wake na maamuzi yake, ameamua tu kuwafanya wafanyakazi waishi kama watumwa.

Unafanyishwa kazi kinguvu, unatishwa, unanyimwa haki zako za msingi, unanyanyaswa bila sababu!! Inashangaza sana kuona watu wema wanakufa mapema, halafu wale wabaya wanadunda tu mtaani!!

Yaani miaka zaidi ya sita hakuna kupandishwa daraja! Unaishi kwa mshahara ule ule tangu mwaka 2014! Bora tungetawaliwa na dikteta kamili kama ilivyokua kwa Gaddaf ila siyo dikteta uchwara.
nawaza fedha zinazoteketea pale chato kwa kuweka watu wote pale, achilia mbali wanaokwenda na kurudi!
 
Kuna watu wana roho mbaya, ni wakatili, ni wabinafsi! Ila huyu mzee amezidi. Yaani kwa utashi wake na maamuzi yake, ameamua tu kuwafanya wafanyakazi waishi kama watumwa.

Unafanyishwa kazi kinguvu, unatishwa, unanyimwa haki zako za msingi, unanyanyaswa bila sababu!! Inashangaza sana kuona watu wema wanakufa mapema, halafu wale wabaya wanadunda tu mtaani!!

Yaani miaka zaidi ya sita hakuna kupandishwa daraja! Unaishi kwa mshahara ule ule tangu mwaka 2014! Bora tungetawaliwa na dikteta kamili kama ilivyokua kwa Gaddaf ila siyo dikteta uchwara.
Si mnaambiwa muache kama maslahi ni madogo.
 
Wafanyakazi wa Tanzania wana tofauti gani na watumwa tuliowasoma kwenye vitabu vya historia ?
Ni kweli kabisa utakuta wazee wetu wamembeba mwarabu kwenye machela na wamemshikia bunduki yake na wana uwoga usiokifani,mwarabu mmoja wao wako zaidi ya kumi its modern Tanzania with Tanzanians
 
Kuna nn kwani Hadi mnaomba msamaha,vp kumehappen nn huko[emoji16][emoji16]
 
Ndo wajiongeze wafanye na shughur nyingine,Kuna sst angu n mwalm wa primary ana ki biashara cha kukopesha na kuuza vitenge, hategemei mshahara na mambo yake yanaenda poa, tatizo Watz uvivu mwingii, angalia mfano nchi Kama China, mtu kaajiliwa sehem 2, au kaajiliwa sehem but kajiajil, ukifika hm saa 11, one hour unaweza fanya kitu ukapata pesa ya kula, weekends, sasa Kama unapenda fuatilia movie na tamthilia YOU WILL DIE POOR
Eti uvivu mwingi..kua kwanza ndipo uzungumze.
 
Ndo wajiongeze wafanye na shughur nyingine,Kuna sst angu n mwalm wa primary ana ki biashara cha kukopesha na kuuza vitenge, hategemei mshahara na mambo yake yanaenda poa, tatizo Watz uvivu mwingii, angalia mfano nchi Kama China, mtu kaajiliwa sehem 2, au kaajiliwa sehem but kajiajil, ukifika hm saa 11, one hour unaweza fanya kitu ukapata pesa ya kula, weekends, sasa Kama unapenda fuatilia movie na tamthilia YOU WILL DIE POOR
Kwa watumishi wa umma kwa Tz ni ngumu sana kutoka kupitia nje ya ajira yake, tatizo kubwa ni usimamizi wa shughuli,/miradi yao. Wengi wamejaribu,wamefanya ila wameishia kuumizwa na wasimamizi. Uaminifu ni changamoto kubwa ndio maana wengi wameshindwa kuzifanya. Unafikiri kwanini walimu wanakamatwa sana ktk UPATU? DESI, Q-NET n.k.sio kwamba wanapenda shortcut, NO.... wameumizwa vya kutosha na watu wasio waaminifu ktk kusimamia miradi yao, wakosa Muda wa kufanya shughuli zao binafsi.

Mfano shule za msingi na sekondari za serikali siku hizi ni kawaida walimu na wanafunzi kumaliza masomo saa 12 jioni. Uliza ni kwa muongozo upi? Kuna posho ya kufidia huo Muda ambao ilitakiwa ukakishw kuku, kulima mchicha? Ukifika nyumbani mda huo unafanya nini?

Unajua majukumu ya WAHADHIRI wa vyuo vyetu vikuu? Unajua athari za wao kuwaza au kujiingiza ktk shughuli binafsi nje ya elimu? Unajua muda wanaotoka maofisini? Unajua idadi ya wanachuo waliopo madarasani? Unajua idadi ya kazi anazotakiwa kusahisha huyu mhadhiri kwa semista/mhula mmoja na atoe matokeo kwa wakati!!? Unajua anatakiwa kwa lazima afanye TAFITI NA KUANDIKA? kwa uchache hayo yakufikirishe ujue athari za kumfanya mhadhiri kufikiria MIKUKUTA nje ya utaaluma.

Kipekee kabisa SECTA YA ELIMU tena elimu ya juu.......!!!! Kuruhusu wahadhiri kuwaza nje ya boxi la ajira yao ni Hatari kubwa. Kwamba nao waanze kukimbizana na ufugaji, maduka n.k. ni hatari na ni msiba kwa Taifa. Vile ni VIWANDA vya KITAALUMA, muda wote wanapaswa kufikiri na kutenda ndani ya taaluma/fani zao....ni hatari profesa/mhadhiri wa elimu ya juu ktk fani yoyote kutoka kazini saa 9:30 kwa mujibu wa muda wa serikali. Ili eti nae akafuge kuku, akalishe ng'ombe, akapige hesabu za duka lake la jumla na rejareja, akakague saluni zake za kisasa......!!

Wanapaswa kuandika, kufanya tafiti, kubuni, kushauri n.k.
Hao wanaofanya shuguli binafsi fuatilia utendaji wao kazini utaelewa namaanisha nini.

Nyakati hizi tumeshuhudia wahadhiri wajasiriamali ndio maana ELIMU YA VYUO VIKUU iko kama ilivyo kila mtu anaona, leo tumeruhusu walimu ktk ngazi zote kufanya mambo yao kujitafutia km kuku wa kienyeji ili waweze kujikimu na familia zao ndio maana elimu ktk ngazi zote iko km ilivyo hususani taasisi za umma. Sekta binafsi zinazosimamia elimu si wajinga kuwa na viposho vingi vingi vya kumfanya mwalimu akili, mwili, nafsi yake viweze tu matokeo chanya ya ufundishaji wake.

LAZIMA TUWEKEZE KWA WALIMU/WAHADHIRI WETU. sekta ya elimu ni sekta mama, ni kiwanda kinachotakiwa kufanya kazi saa 24 na mhusika ni huyu mwalimu/mhadhiri.lazima tumpe maslahi bora zaidi ili kufidia muda wake wa kuwaza ufugaji wa kuku, ng'ombe, duka, au kuvumisha km sio kuuza mitihani na matokeo.

Mchawi wa maendeleo ya TAIFA lolote ni ELIMU yake. Tunapozungumzia elimu tunamzungumzia MWALIMU... mwalimu wa ngazi zote... Ndiye Roho ya elimu na maendeleo ya Jamii/taifa kwa ujumla.

Kama taifa Lazima tuhakikishe tunamlinda mwalimu kwa Gharama yoyote aifanye kazi hii takatifu kwa weledi,moyo,uzalendo mkubwa. Tumuwezeahe kiasi kwamba tukimwona anakimbizana na mambo binafsi tuwe na haki hata ya kumshitaki kwa kulihujumu taifa.
 

msamahapic

Mheshimiwa Rais, nakusalimia kwa heshima na taadhima, Mimi kijana wako naendelea kulitumikia taifa nikiwa kituo changu cha kazi hapa Mlimani, kuna jamaa wengine wanapaita Jalalani, ingawa silipendi kabisa hili jina.

Kilichonisukuma kukuandikia ni baada ya kukutana na Profesa mmoja akinunua mihogo kwa ajili ya chakula cha mchana, mitaa ya jirani na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM). Profesa huyo kapandishwa cheo mwaka jana, lakini bado hajaanza kulipwa mshahara wa uprofesa hadi sasa.

Nilipomuuliza kwanini ananunua mihogo ya Sh2,000 akadai kuwa ‘purchasing power’ yake ni kidogo na haijaongezeka tangu uingie madarakani. Nilimkemea kwa niaba yako kwa sababu anakuonea; umekuwa ukipambana kukuza uchumi wa nchi.

Ingawa kiukweli wako wafanyakazi wengi wa kundi lake ambao hadi sasa wanalilia kulipwa mishahara stahiki kwa muda mrefu, lakini hawaoni dalili zozote. Na wengine bado wanasubiri malimbikizo.

Ukiacha maprofesa, wapo manesi, walimu, waganga, mabwana na bibi shamba na mifugo, askari polisi, magereza, uhamiaji, makarani, makatibu muhtasi, wakunga, waganga wa maabara, mafundi umeme, wakufunzi na wahadhiri, na wengine wengine. Orodha ni ndefu, nao kilio chao ni hicho hicho.

Nimekusanya sahihi zao kutoka maeneo mbalimbali ya Tandahimba, Newala, Namtumbo, Madaba, Ludewa, Makete hadi Ileje, Nkasi, Mlele, Buhigwe, Kakonko, Karagwe, Ngara, Busega, Itilima, Mkalama, hadi Rorya. Nilitaka niwakatae jamaa wa kutoka Runzewe, Katoro na Bwanga nikiamini wanaweza kukufikishia wao wenyewe, lakini nikaona si vibaya ngoja niwawakilishe.


Ila mawaziri, makatibu wakuu, majaji, wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya hawahusiki na msamaha.

Wafanyakazi wengi uwezo wao wa kufanya manunuzi ni mdogo. Kiasi kilichokuwa kinaingia mwaka 2016 ndo hicho hicho hadi mwaka 2021, wanatamani waone nafuu fulani kwenye uwezo wao wa kuhimili manunuzi kwa ajili ya kuhudumia familia.

Naona kama wenzetu wa Bodi ya Mikopo walinusa hilo mapema . Wao wakaweka kipengele cha ‘value retention fee’ toka 2016 kulinda thamani yao ya hela. Walijua kila mwaka thamani ya hela inashuka kwa asilimia sita na ikifika 2021 hela waliyoweza kumpatia mwanafunzi 2016 itakuwa haitoshi 2021, hivyo wakapachika hicho kijamii kinaitwa ‘value retention fee’.

Ukiacha Bodi ya Mkopo kutukata asilimia 15 ya mkopo, kuna hawa jamaa wa TRA nao naona wameamua kutukomalia zaidi wafanyakazi tuwe na TIN. Wamesema bila TIN mwezi huu wa Januari tunatoka bila bila kwenye akaunti zetu.

Mheshimiwa Rais, naomba nichukue nafasi hii kuzishukuru benki tunazopitishia mishahara yetu. Ingawa wanatengeneza faida, lakini huwa wanatuokoa. Baada ya mshahara kuingia wakakata hela yao waliyonikopesha mwezi uliopita. Nilipochungulia kilichosalia kikawa hakitoshi kunifikisha wiki moja mbele, basi siku hiyo hiyo nikakopa tena ‘salary advance’. Sasa hivi ndo ‘salary advance’ ndio mkombozi wetu.

Mheshimiwa, siyo kwamba tunapenda kuishi hivi, ila majukumu ya kifamilia ni mengi na uwezo wa kuyamudu kwa hiki tunachopokea ni mdogo, maana wakataji ni wengi.

Sitaki kuingia nao ugomvi lakini mishahara yetu inachukuliwa na TRA, HESLB, NHIF, PSSF/NSSF kwa sehemu kubwa.

Mheshimiwa Rais, nisikuchoshe na maneno mengi. Wafanyakazi wenzangu walioko Serikalini wameniomba nije kukuomba radhi, kama wakati wowote tangu ukiwa waziri hadi Rais kuna mahali tulikukosea, tunaomba msamaha. Maisha yetu huku mtaani ni magumu, hatuna furaha, baadhi yetu tuna sura za uzee kumbe bado vijana.

Ndoa zetu sasa hivi ziko hatarini, wake zetu wanatudhania wote tuna tabia za wangoni kumbe shida yetu ni hela. Tuna changamoto nyingi za kifamilia, kijamii na binafsi.

Sasa hivi hata viongozi wa dini tunawaona kama wapiga dili kwa sababu nao hawajui tumesahauliwa kwenye ‘value retention’ ya mishahara yetu, utawasikia wakisema, ‘safari hii tegemeza jimbo ongezeko ni asilimia 40 ya mwaka jana’.

Wakiangalia vitambi vyetu wanajua tuna hela kumbe thamani ya mifuko yetu bado ni ile ile ya mwaka 2016.

Tuonee huruma Mheshimiwa Rais, usishangae asilimia kubwa ya wafanyakazi wa Serikali tukianza kukusanya chupa tupu mtaani na kuzigombania kwenda kuuza. Natumaini wewe ni baba mwenye huruma utasikiliza maombi yetu ya msamaha.



Imeandikwa na Faraja Kristomus, mwandishi anafundisha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na anapatikana kwa simu ya mkononi 0787525396
Nimefurahi sana hapo ulipoandika wakuu wa mikoa makatibu wakurugenzi na wakuu wa idara hili haliwahusu kabisa maana mshahara wao mmoja na marupu rupu unalipa mishahara ya watumishi 10
 
Yaani Wasomi wetu ni wabinafsi sana, badala waombe Mheshimiwa Rais adhibiti kwa nguvu zake zote mfumuko wa bei kwenye soko, ili hata wale tusiyokwenda shule tufaidike, wao wanajiombea tu mishahara mikubwa, hata ukipewa mshahara mkubwa bila kudhibiwa mfumuko wa bei hiyo itakua kazi bure!!
 
Takwimu za idadi ya watu Tanzania hadi mwaka 2020 58.5M na Kati ya hao watu, zaidi ya watu 30M wako kwenye kundi la wazalishaji mali.

0-14 years: 42.7% (male 12,632,772/female 12,369,115)
15-24 years: 20.39% (male 5,988,208/female 5,948,134)
25-54 years: 30.31% (male 8,903,629/female 8,844,180)
55-64 years: 3.52% (male 954,251/female 1,107,717)
65 years and over: 3.08% (male 747,934/female 1,056,905) (2020 est.)

Kwenye 30M people serikali imeajiri watu watu wasiozidi 1M ikiwa ni pamoja na serikali kuu, serikali za mitaa na agency za serikali.
Waliobaki wako kwenye ajira za sekta binafsi ikiwa ni pamoja na ajira za moja kwa moja toka kwa wawekezaji wazawa na wageni, kilimo na ufugaji kazi ambazo wengi wetu tunazidharau

Kuongeza mshahara ni jambo jema kwa ustawi wa wafanyakazi japo hakuna mshahara uliwahi mtosha mtu.
Nyongeza ya mshahara inategemea sana na uzalishaji mali, ongezeko la kudumu la mapato na vipaumbele katika uzalishaji mali.

Ofisi nyingi za serikali zinahusika na kutoa huduma zaidi ya kuzalisha mali na kutengeneza faida inayoonekana, kwa hiyo kuongeza mshahara sio zoezi la kuamka na kutamka tuu. Usishangae nyongeza ya mshahara kwa hawa watumishi wa umma ikailazimu serikali kutafta trilion2 au zaidi juu ya kile wanacholipwa sasa kila mwezi. Lazima kuwe na uhakika kwamba vyanzo vya mapato vya serikali vitaweza kulipa kiasi cha mshahara kwa wakati.

Serikali yetu ni serikali sikivu, sisi milioni moja tunaosupport wazalishaji mali tuendelee kupambana kwenye maofisi yetu katika kutoa huduma nzuri ili wateja wetu ambao wengi wao ndio wazalishaji mali waweze kuongeza
Halafu yule ded ananunua gari la milio 460 nasamehewaa .huku mkisema hamna hela
 
Kwenye kipengele cha kuwa na TIN ndio unapata mshahara wa January, labda January ya 1990 maana hii ya 2021 watu washaramba mishahara na TIN hawana!
 
Yote haya yanatokea vyama vya wafanyikazi vipo kimya. Kuna mtu aliwahi kusema adui mkuu wa mfanyikazi wa Tanzania ni vyama vya wafanyikazi. Hao wameamua kula sahani moja na watawala na kuwasahau wafanyikazi.
 
Mnafiki mkubwa wewe.Vitu vinapanda bei kila kukicha alafu unasema hii hela ina thamani! Kama unanufaika na huu utawala kaa kimya na si kuongea ujinga humu.Mbinafsi mkubwa wewe!
Kama nakuona vile,nani mbinafsi kati yangu mimi na wewe?
Vuta taswira yako nyuma kabla ya 2015 ulivyokuwa unatetea watawala, sasa umewekwa kando unatema cheche?
mimi nikiulizwa nimtaje mtu mwenye sura mbili siweziacha kukutaja wewe Salary Slip
 
erikali yetu ni serikali sikivu, sisi milioni moja tunaosupport wazalishaji mali tuendelee kupambana kwenye maofisi yetu katika kutoa huduma nzuri ili wateja wetu ambao wengi wao ndio wazalishaji mali waweze kuongeza
Nakuunga mkono mia kwa mia. Sio wengi wanaolijua hilo ulisemalo. Ni kawaida sana kwenda kwenye ofisi ya umma ukacheleweshwa pasipo sababu za msingi au mtu anakwambia njoo kesho ukikomaa kuwaona viongozi wa juu yake unahudumiwa mara moja,wengi wanasahau kuwa kadri anavyokuchelewesha ndivyo unavyokwamisha pato la taifa ambalo likikaa vizuri ni rahisi kuongezewa mishahara.
Natamani watu tubadilike kifikira mengine yatafuata.
 
Nakuunga mkono mia kwa mia. Sio wengi wanaolijua hilo ulisemalo. Ni kawaida sana kwenda kwenye ofisi ya umma ukacheleweshwa pasipo sababu za msingi au mtu anakwambia njoo kesho ukikomaa kuwaona viongozi wa juu yake unahudumiwa mara moja,wengi wanasahau kuwa kadri anavyokuchelewesha ndivyo unavyokwamisha pato la taifa ambalo likikaa vizuri ni rahisi kuongezewa mishahara.
Natamani watu tubadilike kifikira mengine yatafuata.
Hamna namna ingine, lazima kila mtu afanye kazi yake kwa ubora na kwa wakati ili tunufaike sote
 
watulie bado minne tu, au wakipenda wamuongezee kumi mingine ili awaweke sawa wajue kujiongeza na kujitegemea kama watu wengine bila kutegemea mshahara.
Na wao wanajitegemea kupitia kazi zao...sawasawa na wafanyabiashara wanavyolia na kodi za TRA halafu uwashauri waache hizo biashara watafute kaz za kuajiriwa mshahara mwisho wa mwez,kila mtu na angle yake ya kuendeshea maisha hatuwez kufanana

Sent from my CAM-L21 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom