Mhh! Maskini! Wanamuomba msamaha kwa kosa lipi?

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,792
287,994

msamahapic

Mheshimiwa Rais, nakusalimia kwa heshima na taadhima, Mimi kijana wako naendelea kulitumikia taifa nikiwa kituo changu cha kazi hapa Mlimani, kuna jamaa wengine wanapaita Jalalani, ingawa silipendi kabisa hili jina.

Kilichonisukuma kukuandikia ni baada ya kukutana na Profesa mmoja akinunua mihogo kwa ajili ya chakula cha mchana, mitaa ya jirani na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM). Profesa huyo kapandishwa cheo mwaka jana, lakini bado hajaanza kulipwa mshahara wa uprofesa hadi sasa.

Nilipomuuliza kwanini ananunua mihogo ya Sh2,000 akadai kuwa ‘purchasing power’ yake ni kidogo na haijaongezeka tangu uingie madarakani. Nilimkemea kwa niaba yako kwa sababu anakuonea; umekuwa ukipambana kukuza uchumi wa nchi.

Ingawa kiukweli wako wafanyakazi wengi wa kundi lake ambao hadi sasa wanalilia kulipwa mishahara stahiki kwa muda mrefu, lakini hawaoni dalili zozote. Na wengine bado wanasubiri malimbikizo.

Ukiacha maprofesa, wapo manesi, walimu, waganga, mabwana na bibi shamba na mifugo, askari polisi, magereza, uhamiaji, makarani, makatibu muhtasi, wakunga, waganga wa maabara, mafundi umeme, wakufunzi na wahadhiri, na wengine wengine. Orodha ni ndefu, nao kilio chao ni hicho hicho.

Nimekusanya sahihi zao kutoka maeneo mbalimbali ya Tandahimba, Newala, Namtumbo, Madaba, Ludewa, Makete hadi Ileje, Nkasi, Mlele, Buhigwe, Kakonko, Karagwe, Ngara, Busega, Itilima, Mkalama, hadi Rorya. Nilitaka niwakatae jamaa wa kutoka Runzewe, Katoro na Bwanga nikiamini wanaweza kukufikishia wao wenyewe, lakini nikaona si vibaya ngoja niwawakilishe.


Ila mawaziri, makatibu wakuu, majaji, wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya hawahusiki na msamaha.

Wafanyakazi wengi uwezo wao wa kufanya manunuzi ni mdogo. Kiasi kilichokuwa kinaingia mwaka 2016 ndo hicho hicho hadi mwaka 2021, wanatamani waone nafuu fulani kwenye uwezo wao wa kuhimili manunuzi kwa ajili ya kuhudumia familia.

Naona kama wenzetu wa Bodi ya Mikopo walinusa hilo mapema . Wao wakaweka kipengele cha ‘value retention fee’ toka 2016 kulinda thamani yao ya hela. Walijua kila mwaka thamani ya hela inashuka kwa asilimia sita na ikifika 2021 hela waliyoweza kumpatia mwanafunzi 2016 itakuwa haitoshi 2021, hivyo wakapachika hicho kijamii kinaitwa ‘value retention fee’.

Ukiacha Bodi ya Mkopo kutukata asilimia 15 ya mkopo, kuna hawa jamaa wa TRA nao naona wameamua kutukomalia zaidi wafanyakazi tuwe na TIN. Wamesema bila TIN mwezi huu wa Januari tunatoka bila bila kwenye akaunti zetu.

Mheshimiwa Rais, naomba nichukue nafasi hii kuzishukuru benki tunazopitishia mishahara yetu. Ingawa wanatengeneza faida, lakini huwa wanatuokoa. Baada ya mshahara kuingia wakakata hela yao waliyonikopesha mwezi uliopita. Nilipochungulia kilichosalia kikawa hakitoshi kunifikisha wiki moja mbele, basi siku hiyo hiyo nikakopa tena ‘salary advance’. Sasa hivi ndo ‘salary advance’ ndio mkombozi wetu.

Mheshimiwa, siyo kwamba tunapenda kuishi hivi, ila majukumu ya kifamilia ni mengi na uwezo wa kuyamudu kwa hiki tunachopokea ni mdogo, maana wakataji ni wengi.

Sitaki kuingia nao ugomvi lakini mishahara yetu inachukuliwa na TRA, HESLB, NHIF, PSSF/NSSF kwa sehemu kubwa.

Mheshimiwa Rais, nisikuchoshe na maneno mengi. Wafanyakazi wenzangu walioko Serikalini wameniomba nije kukuomba radhi, kama wakati wowote tangu ukiwa waziri hadi Rais kuna mahali tulikukosea, tunaomba msamaha. Maisha yetu huku mtaani ni magumu, hatuna furaha, baadhi yetu tuna sura za uzee kumbe bado vijana.

Ndoa zetu sasa hivi ziko hatarini, wake zetu wanatudhania wote tuna tabia za wangoni kumbe shida yetu ni hela. Tuna changamoto nyingi za kifamilia, kijamii na binafsi.

Sasa hivi hata viongozi wa dini tunawaona kama wapiga dili kwa sababu nao hawajui tumesahauliwa kwenye ‘value retention’ ya mishahara yetu, utawasikia wakisema, ‘safari hii tegemeza jimbo ongezeko ni asilimia 40 ya mwaka jana’.

Wakiangalia vitambi vyetu wanajua tuna hela kumbe thamani ya mifuko yetu bado ni ile ile ya mwaka 2016.

Tuonee huruma Mheshimiwa Rais, usishangae asilimia kubwa ya wafanyakazi wa Serikali tukianza kukusanya chupa tupu mtaani na kuzigombania kwenda kuuza. Natumaini wewe ni baba mwenye huruma utasikiliza maombi yetu ya msamaha.



Imeandikwa na Faraja Kristomus, mwandishi anafundisha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na anapatikana kwa simu ya mkononi 0787525396
 
Kuna watu wana roho mbaya, ni wakatili, ni wabinafsi! Ila huyu mzee amezidi. Yaani kwa utashi wake na maamuzi yake, ameamua tu kuwafanya wafanyakazi waishi kama watumwa.

Unafanyishwa kazi kinguvu, unatishwa, unanyimwa haki zako za msingi, unanyanyaswa bila sababu!! Inashangaza sana kuona watu wema wanakufa mapema, halafu wale wabaya wanadunda tu mtaani!!

Yaani miaka zaidi ya sita hakuna kupandishwa daraja! Unaishi kwa mshahara ule ule tangu mwaka 2014! Bora tungetawaliwa na dikteta kamili kama ilivyokua kwa Gaddaf ila siyo dikteta uchwara.
 
Hii nchi inavijana wengi wasomi wamezagaa mitaani, kama kunamfanyakazi anaona hatendewi haki, mara moja na haraka sana
bila shuruti aache kazi, ili kusudi waingie vijana wasomi na wachapakazi walokosa ajira, rizikeni na jiongezeni na mnachokipata.
 
Tofauti ni kwamba hawa wanatabasamu huku wanakufa...
Na kusifiwa kwamba alikuwa mchapakazi hodari.

Huu uzi unanifanya nijutie uzembe wangu wa kuwekeza tangu naanza kazi kiasi kwamba siku hizi ningekuwa namiliki uchumi mkubwa badala ya kumtegemea Baba Jesca.

Mnaoanza kazi siku hizi jipangeni kuwekeza badala ya kusubiri mwisho wa mwezi
 
hii nchi inavijana wengi wasomi wamezagaa mitaani, kama kunamfanyakazi anaona hatendewi haki, mara moja na haraka sana
bila shuruti aache kazi, ili kusudi waingie vijana wasomi na wachapakazi walokosa ajira, rizikeni na jiongezeni na mnachokipata.
Mawazo ya kukata tamaa hayo yaani utafikiri mtu katoka uzingizini kisa tu tamaa ya ajira,unapofanya kazi malipo ya halali ni haki yako wala siyo ombi kwa sababu ni jasho lako.
 
Usibadili somo husika la huu uzi. Haijawahi kutokea tangu tupate uhuru miaka 60 iliyopita kwa Wafanyajazi wa Serikali kutopewa nyongeza ya mishahara kwa miaka 6 mfululizo, na huu uchumi unavyozidi kuyumba si ajabu hata miaka 10 itafika bila nyongeza. Gharama za maisha tangu 2015 zimepanda sana lakini mishahara imebaki ile ile hivyo kusababisha Wafanyakazi wengi wawe na madeni makubwa kutokana na mikopo wanayochukua sehemu mbali mbali ili kukidhi gharama zao za maisha za kila siku.

hii nchi inavijana wengi wasomi wamezagaa mitaani, kama kunamfanyakazi anaona hatendewi haki, mara moja na haraka sana
bila shuruti aache kazi, ili kusudi waingie vijana wasomi na wachapakazi walokosa ajira, rizikeni na jiongezeni na mnachokipata.
 
Na kusifiwa kwamba alikuwa mchapakazi hodari.

Huu uzi unanifanya nijutie uzembe wangu wa kuwekeza tangu naanza kazi kiasi kwamba siku hizi ningekuwa namiliki uchumi mkubwa badala ya kumtegemea Baba Jesca.

Mnaoanza kazi siku hizi jipangeni kuwekeza badala ya kusubiri mwisho wa mwezi
Hakika
 
30 Reactions
Reply
Back
Top Bottom