Mhh! Maskini! Wanamuomba msamaha kwa kosa lipi?

Mhh! Maskini! Wanamuomba msamaha kwa kosa lipi?

Wewe kwa chuki zako ndo maana ulitumbuliwa mapema tu.
Mwache rais apambane kuweka uchumi wa hii nchi vyema, hata siku mishahara ikipandishwa thamani yake ionekane.

Bila kudhibiti mifumuko ya bei kwa bidhaa, mshahara hata upande bado mzigo utakuwa mkubwa tu kwa watumishi.

WAVUMILIE KIDOGO TU MAMBO YATAKUWA MSWANO.
Mfumuko upi wa bei unaodhibitiwa?
Udhibiti wa bei ya sukari alifeli vibaya,vifaa vya ujenzi enzi za JK na sasa ni sawa na mbingu na ardhi,mafuta ya kula hayo yanapaa kwa viwango vya dreamliner, ukweli unabaki kuwa ukweli tu,kwamba mzee amewanyongelea mbali wanyonge wake, gharama za maisha na vipato vya watumishi kwa uhalisia wao ni huruma sanaaa

Sent from my Z9 using JamiiForums mobile app
 
Mwambie yaache kazi KBS



Akajiajiri


Uprofesa anashindwa kubuni njia mbadala ya kutoka kimaisha.

Si ndo nyie mnasema vijana mjiajiri? Au mnamaanishaga ajira ni za wazee?
Ukibuni tu kesi ya uhujumu uchumi inakuhusu, "mtaishi Kama mashetani"
 
Kwa watumishi wa umma kwa Tz ni ngumu sana kutoka kupitia nje ya ajira yake, tatizo kubwa ni usimamizi wa shughuli,/miradi yao. Wengi wamejaribu,wamefanya ila wameishia kuumizwa na wasimamizi. Uaminifu ni changamoto kubwa ndio maana wengi wameshindwa kuzifanya. Unafikiri kwanini walimu wanakamatwa sana ktk UPATU? DESI, Q-NET n.k.sio kwamba wanapenda shortcut, NO.... wameumizwa vya kutosha na watu wasio waaminifu ktk kusimamia miradi yao, wakosa Muda wa kufanya shughuli zao binafsi.

Mfano shule za msingi na sekondari za serikali siku hizi ni kawaida walimu na wanafunzi kumaliza masomo saa 12 jioni. Uliza ni kwa muongozo upi? Kuna posho ya kufidia huo Muda ambao ilitakiwa ukakishw kuku, kulima mchicha? Ukifika nyumbani mda huo unafanya nini?

Unajua majukumu ya WAHADHIRI wa vyuo vyetu vikuu? Unajua athari za wao kuwaza au kujiingiza ktk shughuli binafsi nje ya elimu? Unajua muda wanaotoka maofisini? Unajua idadi ya wanachuo waliopo madarasani? Unajua idadi ya kazi anazotakiwa kusahisha huyu mhadhiri kwa semista/mhula mmoja na atoe matokeo kwa wakati!!? Unajua anatakiwa kwa lazima afanye TAFITI NA KUANDIKA? kwa uchache hayo yakufikirishe ujue athari za kumfanya mhadhiri kufikiria MIKUKUTA nje ya utaaluma.

Kipekee kabisa SECTA YA ELIMU tena elimu ya juu.......!!!! Kuruhusu wahadhiri kuwaza nje ya boxi la ajira yao ni Hatari kubwa. Kwamba nao waanze kukimbizana na ufugaji, maduka n.k. ni hatari na ni msiba kwa Taifa. Vile ni VIWANDA vya KITAALUMA, muda wote wanapaswa kufikiri na kutenda ndani ya taaluma/fani zao....ni hatari profesa/mhadhiri wa elimu ya juu ktk fani yoyote kutoka kazini saa 9:30 kwa mujibu wa muda wa serikali. Ili eti nae akafuge kuku, akalishe ng'ombe, akapige hesabu za duka lake la jumla na rejareja, akakague saluni zake za kisasa......!!

Wanapaswa kuandika, kufanya tafiti, kubuni, kushauri n.k.
Hao wanaofanya shuguli binafsi fuatilia utendaji wao kazini utaelewa namaanisha nini.

Nyakati hizi tumeshuhudia wahadhiri wajasiriamali ndio maana ELIMU YA VYUO VIKUU iko kama ilivyo kila mtu anaona, leo tumeruhusu walimu ktk ngazi zote kufanya mambo yao kujitafutia km kuku wa kienyeji ili waweze kujikimu na familia zao ndio maana elimu ktk ngazi zote iko km ilivyo hususani taasisi za umma. Sekta binafsi zinazosimamia elimu si wajinga kuwa na viposho vingi vingi vya kumfanya mwalimu akili, mwili, nafsi yake viweze tu matokeo chanya ya ufundishaji wake.

LAZIMA TUWEKEZE KWA WALIMU/WAHADHIRI WETU. sekta ya elimu ni sekta mama, ni kiwanda kinachotakiwa kufanya kazi saa 24 na mhusika ni huyu mwalimu/mhadhiri.lazima tumpe maslahi bora zaidi ili kufidia muda wake wa kuwaza ufugaji wa kuku, ng'ombe, duka, au kuvumisha km sio kuuza mitihani na matokeo.

Mchawi wa maendeleo ya TAIFA lolote ni ELIMU yake. Tunapozungumzia elimu tunamzungumzia MWALIMU... mwalimu wa ngazi zote... Ndiye Roho ya elimu na maendeleo ya Jamii/taifa kwa ujumla.

Kama taifa Lazima tuhakikishe tunamlinda mwalimu kwa Gharama yoyote aifanye kazi hii takatifu kwa weledi,moyo,uzalendo mkubwa. Tumuwezeahe kiasi kwamba tukimwona anakimbizana na mambo binafsi tuwe na haki hata ya kumshitaki kwa kulihujumu taifa.
I appreciate your facts mkuu, but wazo pia n kuwa Kuna baadhi ya watumish wana mda wa kutosha, but nao unakuta wanajoin kupiga majungu, mfano nilishawah fanya industrial practical training ( Field study) sehem flan tz, ilikuwa tukifika ss na wafanyakaz hao n kurelax mpaka itokee hitirafu , isipotokea basii ikifika saa 10 n kuondoka kazn, so kwa facts zako nimekuelewa but siyo ndo kila mfanyakaz abweteke wakat maybe kwa upande wake ana time la kutosha, unakuta afisa utamaduni wa wilaya, afisa mifugo, kilimo, na wengine ambao in other words tunashinda tunacheza nao bao kitaa 😂 sometimes
 
Hii nchi inavijana wengi wasomi wamezagaa mitaani, kama kunamfanyakazi anaona hatendewi haki, mara moja na haraka sana
bila shuruti aache kazi, ili kusudi waingie vijana wasomi na wachapakazi walokosa ajira, rizikeni na jiongezeni na mnachokipata.
Na watakaocheleweshewa mafao yao nao utawashauri waache nini?!?
 
nitawashauri waache kubweka, wangesave na kutumia mishahara yao vzr ktk kujiongeza na kujiendeleza wasingetegemea mafao.
Hivi una uwezo wa kuelewa kuwa hapo sio kwenye negotiation table ya malipo kabla ya ajira?!? Kusave? Sasa ile hifadhi ya jamii wewe unadhani ni nini kama sio savings zao?

Hapo watu wanaongelea malipo ya kazi ambayo tayari imefanyika.
Ebu, siku moja mpigishe mtu zege halafu jioni wakati kakutolea macho anataka chake, wewe mwambie huna na kama hakubali aache.
 
Kuna watu wana roho mbaya, ni wakatili, ni wabinafsi! Ila huyu mzee amezidi. Yaani kwa utashi wake na maamuzi yake, ameamua tu kuwafanya wafanyakazi waishi kama watumwa.

Unafanyishwa kazi kinguvu, unatishwa, unanyimwa haki zako za msingi, unanyanyaswa bila sababu!! Inashangaza sana kuona watu wema wanakufa mapema, halafu wale wabaya wanadunda tu mtaani!!

Yaani miaka zaidi ya sita hakuna kupandishwa daraja! Unaishi kwa mshahara ule ule tangu mwaka 2014! Bora tungetawaliwa na dikteta kamili kama ilivyokua kwa Gaddaf ila siyo dikteta uchwara.
Mkombozi aliwaasa muandamane mkasusa mkataka yeye na familia yake watangulie mbele. Kuliko kupigwa virungu bora maisha haya haya sada mnalalamika nini. Tulieni mkuu afanye majukumu yake
 
Mkombozi aliwaasa muandamane mkasusa mkataka yeye na familia yake watangulie mbele. Kuliko kupigwa virungu bora maisha haya haya sada mnalalamika nini. Tulieni mkuu afanye majukumu yake
Kwanini mkombozi asitangulie yeye?
 
Hii nchi inavijana wengi wasomi wamezagaa mitaani, kama kunamfanyakazi anaona hatendewi haki, mara moja na haraka sana
bila shuruti aache kazi, ili kusudi waingie vijana wasomi na wachapakazi walokosa ajira, rizikeni na jiongezeni na mnachokipata.
Sio suala la kuridhika ni suala la haki ya mhusika, nchi hii tungejifunza kuacha ubinafsi wa kila mtu kudai chake kwa wakati wake tungefika mbali, tungesaidiana katika kudai kwa makundi makundi, mathalani leo waalimu kesho madaktari, kesho mapolisi keshokutwa watendaji wa vijiji.

Uchumi hautaki ubinafsi, hawa walipwa mshahara wakiongezewa ni faida kwao directly, na ni faida kwa wengine indirectly, akiwa na ziada ataspend zaidi pesa yake itazunguka mpaka kumfikia muuza urojo pale chumbageni.

Hata wewe jobless utajiajiri na biashara yako itasimama sababu kuna mtu kule usiyemjua purchasing power yake ni kubwa!
 
Huu ni uongo hata pump operator Hawezi kula mihogo sababu ya mshahara wake. Kamuulize huyo prof mshahara wake anautumiaje?
 
Usibadili somo husika la huu uzi. Haijawahi kutokea tangu tupate uhuru miaka 60 iliyopita kwa Wafanyajazi wa Serikali kutopewa nyongeza ya mishahara kwa miaka 6 mfululizo, na huu uchumi unavyozidi kuyumba si ajabu hata miaka 10 itafika bila nyongeza. Gharama za maisha tangu 2015 zimepanda sana lakini mishahara imebaki ile ile hivyo kusababisha Wafanyakazi wengi wawe na madeni makubwa kutokana na mikopo wanayochukua sehemu mbali mbali ili kukidhi gharama zao za maisha za kila siku.
Weye ni mfanyakazi wa Serikali au unawasemea? Umefungwa pingu kuwa mfanyakazi wa serikali? unadhani ile migomo ya wafanyakazi wa umma, enzi za Mkapa na Kikwete, kupigania stahiki zao, imeishia wapi?
 
Wewe ni nani hadi uhoji kama mimi ni mfanyakazi wa Serikali au la? Mind your own biz especially if you have nothing important to write.
Weye ni mfanyakazi wa Serikali au unawasemea? Umefungwa pingu kuwa mfanyakazi wa serikali? unadhani ile migomo ya wafanyakazi wa umma, enzi za Mkapa na Kikwete, kupigania stahiki zao, imeishia wapi?
 
Wewe ni nani hadi uhoji kama mimi ni mfanyakazi wa Serikali au la? Mind your own biz especially if you have nothing important to write.
Usianzishe uzi kama haupo tayari kuutolea ufafanuzi!!
 

Hata MOD hawajawahi kunitaka nitolee ufafanuzi chochote ninachokiandika hapa, who are you to ask for clarification from this newspaper article?
Usianzishe uzi kama haupo tayari kuutolea ufafanuzi!!
 
Mwambie yaache kazi KBS



Akajiajiri


Uprofesa anashindwa kubuni njia mbadala ya kutoka kimaisha.

Si ndo nyie mnasema vijana mjiajiri? Au mnamaanishaga ajira ni za wazee?
Unafikiri kaandika kwa ajili ya yeye pekee yake au kwa ajili ya wafanyakazi wote
 
Back
Top Bottom