Mkuu hapa naona umeweka ubaguzi. mfanyakazi ni mfanyakazi bila kujali yupo serikalini au kampuni binafsi.
kwa ufahamu wangu mdogo,mliopo serikalini hasa hasa mamlaka(EWURA,PURA,LATRA,TRA,TCRA n.k) nao wamekutuma uombe msamaha?
Umechunguza wafanyakazi waliopo makampuni ya wahindi na wachina wanalipwaje ukilinganisha na mliopo serikalini ?
kwa ufupi sisi tuliopo makampuni binafsi tunawaonea wivu,sema tu nafasi za kuajiriwa serikalini ni kidogo tunalazimika kwenda makampuni binafsi. Suala la mfanya kazi kuwa na TIN nampongeza rais maana hata tulipokuwa hatuna TIN tulilipa pay as you earn wakati mamalaka hazikutambui kama mlipa kodi,utaratibu uliopo kwa sasa ni mzuri maana hata mimi natambulika kama mlipa kodi.
Ukienda dukani kkoo kwa kiasi fulani thamani ya fedha yako ndogo unaiona,ikilinganishwa na zamani ambapo fedha ndogo ya mshahara ilipambanishwa na fedha ya vigogo waliopiga mabilioni ya fedha na kwenda shopping ambapo wafanya biashara waliuza kwa faida zaidi ya mara mbili. Ni kweli kwa sasa mishahara haijaongezeka lakini kitu kinaitwa value for money kinaonekana.