Napenda nifafanue zaidi. Kwanza napenda mjadala huu. JF inapaswa kuwa hivi. Kujadiliana masuala ya kisera. Pili, kwanza sote tunakubaliana kwamba gharama za maisha zimepanda sana. Mwananchi wa kawaida ndiye anayeathirika zaidi na kupanda huku kwa gharama za maisha kuliko mwananchi mwenye kipato kikubwa. Hii inatokana na sababu kwamba bei zinapanda haraka zaidi kuliko kipato cha mwananchi wa kijijini ambacho ni cha msimu.
Kumekuwa na pengo kubwa sana kati ya matajiri na masikini. Sababu kubwa ni kwamba sekta za uchumi zinazokua zinafanya matajiri wawe matajiri zaidi. Sekta ya Kilimo inayoajiri watanzania takribani asilimia 65 haikui inavyotakiwa na hivyo masikini wanakua masikini zaidi.
Kwa kuwa watu masikini wanauza bidhaa zao kwa bei za vijijini, lakini wananua mahitaji yao kama sukari, mafuta nk kwa bei za mijini, basi mfumuko wa bei husukuma watu masikini kwenye lindi la umasikini. Policy intervention inapaswa kuokoa hawa masikini wasiwe masikini zaidi. Tunafanyaje -
Mosi, katika 'basket of goods and services' ambayo mtanzania hutumia kwa siku, chakula ni asilimia 47, umeme na mafuta 11 na usafiri 3. Kwa hiyo NBS wanapokokotoa inflation, asilimia 61 ni masuala hayo. Food inflation inapaswa, narudia, inapaswa kudhibitiwa kwa kuongeza uzalishaji wa chakula na kuhakikisha kinaingia sokoni. Hili ni suala la msimu maana kilimo chetu ni cha mvua. Hivyo inabidi kudhibiti bei ya mafuta.
Sisi hatuna visima vya mafuta ( kuna 1bn barrels of oil in mtwara yet to be officially declared). Bei ya mafuta hatuna mamlaka nayo. Sisi tuna mamlaka na kodi tunazotoza kwenye mafuta. CHADEMA inapendekeza tupunguze kodi hizi kwa asilimia 50.
Sasa tunazibaje pengo hilo la kodi? Ndio tunapendekeza mambo 3- kupunguza misamaha ya kodi kutoka 2.5% ya GDP sawa na 630bn tshs kwa mwaka mpaka 1% ya GDP sawa na kuokoa takribani 400bn tshs. Pili, tunataka kumilikisha umma uchumi. Tunauza hisa za serikali katika Airtel kwa njia ya IPO. Serikali ina hisa 40%, tutauza 25% na kupata takribani 324bn ths. Tutauzakwa IPO hisa za NBC 15% na kupata takribani 200bn.
Hizi ni njia za muda mfupi. Njia za muda mrefu ni kuongeza uzalishaji wa chakula na kuboresha miundombinu chakula kifike sokoni.
Tunapaswa kukuza uchumi na kuweka usawa ie growth with equity.
Ngoja niwahi kikao cha tathmini
Mkuu nadhani hakuna mtu hapa anayepinga mtazano wa CDM kuhusiana na hali halisi ya kiuchumi lakini binafsi nachosema hizi sera zinauzwa kwa wananchi ndivyo kisiasa inavyotakiwa sio kuziuza CCM. Mwisho wa siku kila CCM wanapotekeleza sera za Chadema sifa huwafuata waliwezesha (CCM) na mwaka 2015, wataingia tena madarakani kwa sababu hapatakuwa na sababu ya kuwaondoa.
Hizi ndizo gharama za demokrasia ya vyama vingi yaani mawazo, falsafa, itikadi hadi sera za wale wanaokubaliana hukaa kundi moja, wengine hukaa kundi jingine na huja na zao pia kisha wananchi huchagua mawazo na njia zipi zinaonekana bora zaidi. sasa inapotokea hali kama hii sera za CCM zinashindwa kufanya kazi, ndio huwa nafasi ya Chadema na vyama vya upinzani kuwaonyesha wananchi sera bora ni zipi kwa maelezo na hotuba ili kudhibiti hali iliyopo na sii jukumu la chama pinzani kuuza sera zao kwa chama kinachotawala, ila CDM wanaweza kupinga maamuzi ya CCM kama itataka kuuza share za NCB na Airtel kinyume cha mtazamo wao na kutoa ushauri kama huu pinzani na huo wa CCM.
Binafsi mkuu wangu siamini kabisa kwamba maisha yanapanda tanzania kwa sababu za mfumko wabei isipokuwa Tanzania ni nchi tegemezi na walionacho ndio walioshika mpini kiasi kwamba wananchi (Consumers) ni wahitaji.. Kuna kitu tunaita reverse economy mahala ambapo supplier sii mhitaji wa soko kutokana na dhiki iliyopo. Leo hii Tanzania hakuna swala la Demand and supply kama wataalam wengi mnavyolitazama bali tupo ktk hatua za mwanzo kabisa yaani - Necessity against invention, hivyo msemo ule wa 'Necessity is the mother of invention' ndio unatakiwa zaidi kutazamwa..kuondokana na SHIDA hizi kwani demand ya mtu mwenye njaa na yupo at critical condition ni tofauti kabisa na mtu mwenye njaa inayotokana na tabia ya milo mara tatu kwa siku..
Kifupi leo hii mwananchi nyumbani wananyanyaswa kila mahala kutokana na shida waliyokuwa nayo na mfumo mzima wa CCM unamwezesha Mlanguzi ambao ndio matajiri wetu kuchukua nafasi kubwa ya ku dictate hali ya uchumi wa nchi yetu. Kila unapotazama nchini ni walanguzi watupu aidha wanauza mali ya nje au hata yetu nchini hakuna utaratibu mzuri baina ya mkulima na consumer pasipo kupitia kwa mlanguzi anayeongoza uchumi wa nchi na mafanikio madogo tunayojivunia...
Pili, kutokana na kuwa taifa tegemezi tunajaribu sana kurekebisha mambo mengi ktk mfumo huo huo wa kutegemea pasipo kuboresha uzalishaji wa kitu kile kile. Ama tutafikiria kuboresha pasipo kujali mahitaji yetu wakati huo huo. I mean mkuu wangu kuna sababu gani Tanzania leo haijitoshelezi kwa umeme, maji, kilimo na maghala ya chakula..
Kwa nini vitu hivi sio vipaumbele kwa zaidi ya miaka 20 toka tumeingia Ubepari hali population imeongezeka mara mbili..Kisha tunashangaa kwa nini maji ya chupa yanauzwa Tsh 1000 wakati kiafya tunaambiwa mtu mmoja anatakiwa kunywa lita nne za maji kwa siku... That is Tsh 4,000 ni watu wangapi wanaweza ku afford?..Lakini kama serikali ingeweza kuhakikisha maji yapo sidhani kama hii biashara ya maji ya kuchemsha na kuwa distilled ingekuwa big deal...Ufisadi tunautengeneza wenyewe kwa fikra mbaya za kiuchumi..
Kwa ushauri wangu Zitto, nakuomba sana jaribu kusimamia sera za Chadema na kuziuza kwa wananchi ili kesho mpewe nafasi ya kuongoza lakini kuwauzia CCM, waswahili hawataona tofauti ila CCM ndiye kawawezesha na maadam siasa hizi ni mpya kwetu wadanganyika hawataona umuhimu wa kuwaondoa CCM madarakani.