Mheshimiwa Zitto, kwa hili umekosea

Mkuu,

Mchambuzi nadhani jibu lako ni moja Ondokana na siasa za kijamaa. Kwa mujibu wa maandishi yako hicho unachokipendekeza ni vigumu sana kutokea na kitakuwa vigumu kutekelezwa. Hata huko marekani walipoanzisha stock markets kuna wengine waliingia darasani kujifunza stock market inafanyakazi vp kuna wengine walijifunzia mtaani mfano mzuri ni Rockefeller, Phillip Fisher, Jesse Livermore na wengineo wengi walikuwa hawana a formal education but they manage to penetrate into the industry and emerged themselves as top investors.

Sikubaliani na ushauri wako wa groups in ownership of public corporations. Hilo litasababisha wafanyakazi wafanye kazi mategemeo ya kupata stock options. Hii ni hatari kwani itachangia kukua kwa risk taking behavior among staff of the company. Vile vile itajenga kingdoms kwenye kampuni kitakachochangia kuongezeka kwa ufisadi. Ni vema waruhusu umma umiliki kampuni kupunguza uwezo wa mtu mmoja kutawala maamuzi ya kampuni.
Jibu lako ni moja vile vile,ACHA KUIGA MFUMO USIOUWEZA! unazungumzia mfumo tofauti kabisa wa maisha,kabla ya kuupa umma stock options ni lazima uhakikishe kuwa umma huo una uwezo wa kununua hizo shares.Sio kujifunza tu,uwezo wa kununua shares watanzania wengi hawana,hivyo basi kwanini makampuni ya binafsi hayauzi shares zao hapa tanzania?
Na asikudanganye mtu kuna makampuni hata marekani ambayo shares zake zinamilikiwa na wafanyakazi,mfano ni HYVEE FOOD STORES na makampuni mengi tu yanakupa stock options as a benefit!
Unajua wenzetu wamepata mali nyingi sana kwa kutumia migongo yetu,lakini mtu kama wewe unaona ni stories tu!....haya mataifa pamoja na kuwa na rasilimali nyingi nchini mwao,wamekuwa na mirija mingi ya kiuchumi na wametawala nchi nyingi tu kwa kutumia makampuni yao nadhani umeshasikia hiyo,pia hawakutosheka wakaja kununua watu ili wakawafanyie kazi kwao(slavery) kwa hiyo wewe na waziri wako kivuli wa fedha msitake kutufanya sisi ni wajinga!...mwambie apiganie kuondolewa kwa posho za wabunge na mawaziri kama ilani ya chama chake inavyoisema la sivyo come 2015 we gonna spend all of our time making sure they don't get any decision-making spots......shame on yall! pseudocapitalists,stop copying what you cant do!!
 
Bwana Mchambuzi nashukuru kwa kuweza kutoa mchango wako wa mawazo kwa hilo ndo dhumuni halisi la jamii forum. Ila naomba nikueleweshe kidogo hasa kuhusa Botswana na madini.....Botswana mwekezaji si adui wa maendeleo kama wanavyochukuliwa na Watanzania wengi kuwa wanaiba mali zrtu. Serikali ya botswana ni share holder wa The Debeers ikiwa na hisa za asilimia 15, kwahiyo serikali inapata faida kutokana na shughuli za utendaji za kampuni hiyo dunia kote. Serikali ya Botswana ina haki ya kupata hisa za asilimia 15 katika kila mgodi unaoanzishwa nchini mwao na dhamani ya hizo hisa zina fanywa na mtu mwingine ' third part' na serikali inazilipia hizo hisa soma Botswana Metals Limited - Botswana - The Economy. Watanzania wengi wanataka free carried interest ya mpaka asilimia 50....je hii inawezekana??

Tatizo la sekta ya madini limeanzishwa na ccm yenyewe kwani wao ndo waliweka hii system inayowanufaisha wao. KWANZA... Asilimia 90 ya leseni zote za utafutaji wa madini hapa nchini zinamilikiwa na watanzania kwa majina na kampuni mbalimbali. Hivyo wao ndo wanaingia ubia wa utafutaji na wawekezaji kazi iliyotakiwa kufanywa na serikali yenyewe hivyo ili free carried interest ya asilimia 10 iko mikononi mwa watanzania wachache wasio lipa kodi.....nafahamu Buzwagi,Goldern Pride,Tulawaka na North Mara zote kunawatanzania wanaokusanya zaidi ya dola milioni moja kwa mwaka kwa kila mgodi...je hawa wana submit annual returns zao TRA?? GOD KNOWS. Bulynhulu na Geita zenyewe zilikuwa chini ya serikali na serikali iliuza hisa zake zote hivyo haina hisa pale

TATIZO LA KAMPUNI...Migodi mingi ilizinduliwa wakati wa bei ya dhahabu iko chini miaka ya 1998 na 2003 na katika biashara hii kuna aina mbili za uuzaji wa dhahabu moja ni spot market price na nyingine ni hedge system.... kila njia ina faida na hasara zake Hedge system unauza mali kabla ya kuchimba hivyo buyer anafanya mahesa akitarajia kupata faida kutokana na kumuuzia dhahabu yako.. Buly na Geita wali hedge kwa kiasi kikubwa tu hivyo hata bei ikipanda kwenye soko wewe hunufaiki na pando hilo kwani halikuhusu...ila ikiteremka wewe unanufaika... Hivyo ndo maana Buly na Geita wamekuwa hawatengenezi faida kwa sababu hiyo ...We are punished because of their bad business model..... ...Sio vyema kulaumu wawekezaji wakati wanalipa kodi kuliko watanzania asilia......Asilimia 70 eneo la uzalishaji Tanzanite linamilikiwa na Watanzania jingine linamilikiwa na mwekezaji....Kodi wazawa wanachangia asilimia 30 mwekezaji asilimia 70.....je wazawa kwanini mchango wao unapungua?.......Kuna habari ya kuwa kisima cha gesi kilichogunduliwa pale mkuranga kimo kwenye eneo la mkuu wa majeshi mstaafu je kwa maana siku ya kusaini production agreement serikali itakuwa third part wala sio owner......

MAFISADI ndo wanao haribu uchumi wetu....Mining act ya 1998 tulikopy kutoka Australia kule ina fanya kazi na serikali na watu wako happy hapa ilishindikana.......uchakachuaji kwani sheria zinawekwa pembeni
 
Nashukuru kwa makala yako yenye changamoto, nabaki na wasi wasi kuwa watu wenye mtazamo kama wako wa 'Tanzania kwanza, siasa baadae' wana nafasi hapo ulipo. Pengine ungefikiria kuungana na wengine kusukuma gurudumu. Sipendi kupandikiza siasa kwa kuwa ni mfuasi wa Tanzania kwanza siasa baadae siku nyingi, ila ikibidi tuwapongeze wahusika na hapa ni Chadema. CDM kilipojizatiti kimetoa changamoto sana na hakika Tanzania kwanza ni sehemu ya sera zao. Nadhani unaweza kuona mfano mzuri tu bungeni ambako wabunge wenye nguo kama zako wamebaki kupiga makofi na hata kura hawajui inahusu sera gani. Hata wewe ungekuwa mbunge wa Kigamboni sidhani ungejinasua kwenye mfumo huo wa miaka 47, ndio maana nakusihi uangalie, je upo upande sahihi wa barabara?

Mchambuzi: 'mashirika ya umma yemefanya vibaya miaka ya 80 nahakukuwa na njia ila kuyabinafsisha'. Sikubaliani na hoja hii kwasababu mashirika ni kitu na yanaendeshwa na watu. Tatizo ni uongozi na siasa katika uchumi. Wakuu wa mashirika na bodi zao walichaguliwa kufuata utiifu na si elimu wala uzooefu. Jiulize Tanganyika packers iliyokuwa inatengeneza nyama na kuuza kwa askari wa ukombozi na Uarabuni ilikufa kwanini ili hali ng'ombe wapo na hawana soko. Mtu aliyeua kiwanda anachaguliwa kuwa bodi member wa kiwanda kingine. Mifano ipo mingi sana, nachosema hapa uzembe huo bado tunauona katika sekta za madini n.k hadi leo
Iweje CRDB na NMB, au Brewerie na sigara viendelee kufanya vema urafiki, UFI, Bora vife.

'Rais akishika bango Ufisadi CDM watakuwa na sera gani za ushindani' Mchambuzi hakuna taifa lolote lililopiga hatua bila kupambana na kushinda ufisadi. Ushindi si 100% ni kupita kiwango cha ufaulu ambacho sisi tupo chini sana. Unapo mwambia Zitto aendelee kuelemisha kuhusu rushwa ni kumtwisha kazi ambayo kama viongozi wa serikali yako wangekuwa makini na wabunge wao leo ufisadi ungekuwa maktaba, si hivyo asilani. Zitto akipambana na wewe wanyooshe kidole serikali ya chama chako hadharani kama tunavyofanya.

Mukandara: Naungana nawe kuwa uchumi wetu ni mdogo sana na haujafungamana kiasi cha kuathirika sana na masoko ya dunia. Suala la kupanda bei za mafuta linatumika tu kuhalalisha kushindwa. Tatizo lipo kuanzia miaka ya 70 lakini serikali ilikuwa na jinsi ya kulishughulikia.
Marekani majuzi kidogo wafungue 'strategic reserve' kupunguza makali, sijui pamoja na sera za IMF nini kiliua TPDC ambayo ingesadia sana kukabiliana na hali hii. Serikali makini ilitakiwa iwe imejipanga kwa kujua kuwa nishati tunayotegemea ni ya kuagiza.

MMKJ: Nakubaliana kuwa hakuna serikali isiyokopa jambo la muhimu ni kuwa na 'fiscal balance'. Marekani sasa wanafikiri kuweka 'debt ceiling'. Tatizo letu ni kuwa bajeti yetu haiendani na matumizi. Pesa zilizopotea kwa malipo hewa, kazi hewa, mishahara hewa, misamaha ya kodi, mikataba mibovu kama taarifa za CAG, Zitto na Mrema tusingekuwa na nakisi katika bajeti yetu wala kutegemea wafadhili.
Tatizo ni nidhamu ya uongozi inayozaa uzembe, kutowajibika na ufisadi kutoka ngazi za juu za serikali, na hapa ndipo nawaunga mkono CDM kuwa huwezi kuwa na mipango ukiwa umezungukwa na rushwa na ufisadi =( kutia maji ndani ya pakacha)

Kobello: Ni kweli matumizi ya serikali ni makubwa sana, naongezea kuwa hivi nchi masikini kama yetu tunapata wapi Billion 20 kwa ajili ya vitumbua ofisini? Hivi kwanini kuwe na ofisi za bunge Dar/Dodoma, ofisi ya Waziri mkuu Dar/Dodoma, serikali ilipe wabunge wakiwa katika kituo chao cha kazi n.k

Hitimisho: Mh Zitto pamoja na kuweka uwazi wa mashirika ya umma kuuza hisa, bado ni muhimu serikali kuwa na hisa kulinda maslahi ya taifa tusijefika kwa mama Thatcher aliyegomewa na waingereza ambao ni champs wa ubinafsishaji. Sidhani ni vema tukitafuta njia za zimamoto kukabili tatizo. Pongezi kwa jitihada zako za kupambana kwa ajili ya taifa.

Kwani tusifikirie haya:
Nidhamu ya kazi, mapato na matumizi irudishwe kwa nguvu. matumizi= mapato
Futa misamaha ya kodi, rejea mikataba, ongeza wigo wa kodi( tafuta vyanzo kama bandari, madini, utalii)
Punguza ukubwa wa serikali, wingi wa viongozi ( Mkoa mmoja =RC, RAO,DCs,DAO,DED,Wabunge wengi kuliko wilaya zilizopo)
Punguza idadi ya mawaziri na wizara zisizofaa( mfano akina mama na watoto, utawala bora), vikao vya bunge 2 tu.Futa wabunge wa kupendelewa, punguza majimbo ya wabunge
Punguza semina na safari za viongozi, dhibiti matumizi ya anasa ununuzi wa fenicha, magari na vitafunio vya chai
Taarifa za CAG zifanyiwe kazi kisheria.
Kilimo kiwe mikononi mwa wataalamu sio wanasiasa.

Huko ulaya wenzetu wanaita 'austerity measures'
Mkuu ungepata siku hata moja tu bungeni ukayamwaga manyanga haya...Nimekukubali mkuu wangu.
 
DeBeers Botswana ni tofauti na DeBeers,sometimes watu huwa wanaiita DEBTSWANA na miaka kama ishirini ijayo deposits za almasi botswana zitakuwa depleted.
pili botswana inazalisha almost 30mil carats compared to 300,000 za tanzania,almost 100 times,hata mauzo yetu ya dhahabu na almasi ni negligible kulinganisha na almasi ya botswana.Ukiwa na deposits nyingi unakuwa na say kubwa kwenye mikataba na sisi hatuna madini mengi kama tunavyohadithiwa bearing in mind ratio ya maliasili/population/area.
Kwa hiyo ningeomba upunguze kamba...Botswana haihodhi 15% ya DeBeers thats misleading!
 
Jibu lako ni moja vile vile,ACHA KUIGA MFUMO USIOUWEZA! unazungumzia mfumo tofauti kabisa wa maisha,kabla ya kuupa umma stock options ni lazima uhakikishe kuwa umma huo una uwezo wa kununua hizo shares.Sio kujifunza tu,uwezo wa kununua shares watanzania wengi hawana,hivyo basi kwanini makampuni ya binafsi hayauzi shares zao hapa tanzania?
Na asikudanganye mtu kuna makampuni hata marekani ambayo shares zake zinamilikiwa na wafanyakazi,mfano ni HYVEE FOOD STORES na makampuni mengi tu yanakupa stock options as a benefit!
Unajua wenzetu wamepata mali nyingi sana kwa kutumia migongo yetu,lakini mtu kama wewe unaona ni stories tu!....haya mataifa pamoja na kuwa na rasilimali nyingi nchini mwao,wamekuwa na mirija mingi ya kiuchumi na wametawala nchi nyingi tu kwa kutumia makampuni yao nadhani umeshasikia hiyo,pia hawakutosheka wakaja kununua watu ili wakawafanyie kazi kwao(slavery) kwa hiyo wewe na waziri wako kivuli wa fedha msitake kutufanya sisi ni wajinga!...mwambie apiganie kuondolewa kwa posho za wabunge na mawaziri kama ilani ya chama chake inavyoisema la sivyo come 2015 we gonna spend all of our time making sure they don't get any decision-making spots......shame on yall! pseudocapitalists,stop copying what you cant do!!

Mfumo gani wa kiuchumi tuliouanzisha wenyewe zaidi ya kuiga mifumo iliyotoka nchi zengine si ujamaa wala ubepari tuliouanzisha sisi. Tumeufata ujamaa angalia umetufikisha wapi sasa viongozi wetu wenyewe wamekuwa mabilionea. Ndio maana nasema acheni fikra zenu za ujamaa ndio zimetufikisha hapa leo. Time to change the direction of the boat.
 
Ushaanza ku sound kama rais wako kikwete! Ujamaa haujatufikisha hapa,tushaliongelea hili,unajua mnampinga ****** wakati mna mawazo sawa tu,kila kitu kuwavutia investors...and you think capitalism is the thing nowadays while it's actually the opposite...ndio maana nikawa nawaambia marafiki zako kuwa wamarekani ni wajamaa kuliko watanzania..........TAFAKURI
 
Nchi kama Botwsana , China, India n.k mafanikio yayanatokana na nidhamu. Aliyetengeneza maziwa ya watoto fake China alikula risasi kwasababu ya kudhuru nchi yake. Japan ukipatikana na rushwa ni afadhali ule kitanzi mwenyewe. Marekani ma-tycoon waliosababisha crisis wote wako mbele ya sheria, Botswana rushwa utaozea jea.
Ulaya wanabana matumizi (austerity measures) ili kukidhi haja ya bajeti zao ikiwa ni pamoja na misaada tunayoomba.

Mipango ya kuendeleza uchumi ipo mingi na mizuri tu. Tatizo ni nidhamu ya kufikia ndoto hizo. Tunaongelaje investment na stocks ili hali hatujaweza ku-balance bajeti yetu miaka 47 iliyopita. Sio umasikini bali ni nidhamu yetu iliyojengwa katika ubinafsi, ulafi na ukosefu wa maadili. Kodi zetu zinaweza kukidhi bajeti yetu kama kuna umakini, tatizo hakuna wa kusimamia na anayeona aibu kuomba omba. Rejea taarifa ya CAG/Zitto/Mrema uone mamilioni yanavyopotea na hakuna anayeshtuka si magogoni au Dodoma,zaidi akina Zitto wanaonekana wakorofi tu,wakati huo huo mkuu anazindua Airtel iliyokwapua bilioni 340 kijanja ujanja tu!!!!

Tuanze na mipango inayofanana na sisi kama wachina, Brazil na India wanavyofanya. Tuige kwa kuzingatia hali yetu na sio copy and paste. Mwananchi leo hii anapigania mkate wa siku, ukimwambia stock markets ni rocket science kwake. Kwanini tusianze kuinua hali yake ya maisha kwa kumpunguzi mizigo isiyo ya lazima kama kodi asizoona matokeo yake?
Tunaweza! kwanza kuangalia nidhamu yetu kwa kuanzia na bajeti. Matumizi yalingane na bajeti kwanza. Tuangalie vyanzo vya kodi na sio sigara, Bia na mafuta. Hakuna anayejiuliza kwanini bandari zetu zilizopo katika strategic positions zisichangie robo ya bajeti na badala yake watanzania wakimbilie kutoa mizigo Mombosa na Beira!! Tunafaidika nini na madini yetu, kwanini tusizalishe chakula kwa EA na SADC tukiwa nchi yenye arable land na nzuri kwa irrigation schemes.

Tujiulize, hivi mwekezaji gani atakayekuja mahali pasipo na maji wala umeme, yaani aje na jenerata na katapila kuchimba visima, imetokea wapi dunia! na kwanini asiende mahali palipo tayari. leo miaka 47 bado tunapata maji kutoka bomba la mjerumani alilojenga mwaka 1930.
Tujiulize, hivi kwanini hatuwezi kuendesha Tazara, TRC, ATC n.k.
kwanini Mjapan aweze kulima mpunga moshi akiondoka mradi umekufa. Kwanini Norway watujengee miundo mbinu na kutuachia DSSD walipoondoka imekufa n.k. Je tutawezaje kuendesha soko la mitaji kwa mafanikio!!
Tujiulize, kwanini Seneta Obama(wakati huo) apange chumba Washngton, na serikali ya Tanzania itumie billion 26 kujenga nyumba za Wabunge Dodoma! Kwanini marekani yenye watu milioni 300 na uingereza yenye watu milioni 50 iwe na ukubwa sawa wa bunge na Tanzania yenye watu milioni 40. Iweje marekani na ulaya wasiwe na wabunge wa kuteliwa kama 106 wa TZ.
Kwa uchumi gani tuna baraza la mawaziri kubwa kuliko Ufaransa, Norway na Uingereza. Misamaha ya trilion1 imemsaidiaje mtanzania.

Yote hapo juu majibu yake ni Ukosefu wa nidhamu, Rushwa na Uongozi usiojua wapi tuelekee. Bila kukabiliana na haya kwanza ,hata tuwe na stocks au capital investment za ajabu kiasi gani hatutafanikiwa. Bajeti yetu ya trilion 11 kwa kuzingatia ukubwa wa serikali, matumizi ya hovyo,misamaha ya kodi, rushwa, ukubwa wa bunge inaweza kurudi hadi trilion 6 tena kwa ufanisi bila ya kuachia watoto wetu madeni yatakanayo na ununuzi wa fenicha, VX n.k
Hakuna mipango inayofanikiwa kukiwepo na rushwa au ukosefu wa nidhamu. Mimi naona hili ndilo tatizo letu kubwa.
 
Matumizi yetu makubwa zaidi ni kulipa mishahara ya watumishi ambayo kama 60% (naomba mnikosoe kama nimekosea) .

Tatizo linakuja watumishi wengi waliajiriwa miaka ya nyuma hata kutumia teknolojia za kisasa hawawezi unakuta kazi ya mtu mmoja inafanywa na watu 3 au 4. Ushauri wangu serikali kuna wanavyuo wengi mtaani wana ujuzi wa kufanya kazi yoyote iwe wizarani, wilayani etc tafadhali ondoeni hao wazee wavaa miwani na suspender.

Wekeni vijana wachache hili zoezi liende taratibu taratibu ili ikifika baada ya 5 years wengi wao wawe wameondoka waingie vijana wenye nguvu na ari ya kufanya kazi , lakini maslahi yaboreshwe kidogo.

Swala la nishati mbadala nalo la kuzingatia maana mafuta sasa yamekuwa hayashikiki huko Brazil wenzetu wanatumia mahindi kutengeneza mafuta ya kuendesha magari yao na sisi tuanze na gesi yetu.
 
Nikirudi kwenye ishu yenyewe ya msingi namuunga mkono mtoa hoja.

Waswahili wanasema huwezi kuchenji buku kwa njaa ya mtoto.

Hii kuuza hisa kupata pesa za kutumia ni short term fix ya hii tatizo lakini in the long run tunarudi kule kule bei za mafuta zitaendelea kupanda na hatutakuwa na hisa nyingine za kuuza in the future.

Mimi nahauri ifanyike study ndogo tu ya ki Finance kuona Present Value ya cash flows tunazopata kutoka kwenye hizo hisa kwa miaka infinity tufanye comparison na pesa tutakazopata kwa mkupuo mmoja wa kuuza hisa.Hapo tunaweza kufanya informed decision.
 
Zitto hana tofauti na Profesa Muhongo kwenye swala la communication, ndio maana hakuna pendekezo la kamati yake linatekelezwa na serikali.

kuropoka ropoka tu, ohoo tunapoteza trilioni ngapi sijui kwenye misamaha ya kodi, umewahi kumsikia anasema ni misamaha ipi?
 
Back
Top Bottom