Mheshimiwa Zitto, kwa hili umekosea | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mheshimiwa Zitto, kwa hili umekosea

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mchambuzi, May 9, 2011.

 1. Mchambuzi

  Mchambuzi JF-Expert Member

  #1
  May 9, 2011
  Joined: Aug 24, 2007
  Messages: 4,819
  Likes Received: 1,140
  Trophy Points: 280
  [FONT=&quot]Mheshimiwa Zitto, kwanza mimi ni mwana CCM, lakini kwanza ni Mtanzania kama wewe kwani mtazamo na msimamo wangu kwanza kabla ya itikadi yoyote ni Tanzania Kwanza, Siasa Baadae! Lakini pili, lazima nikiri kwamba kuingia kwako katika medani za siasa ya nchi yetu kuliamsha sana moyo, udadisi na mvuto wangu juu za siasa za Tanzania. Nina uhakika vijana wengi hawatofautiani nami katika hili. Tangia mwaka 2005, umekuwa tumaini letu vijana wengi bila kujali vyama vyetu vya siasa kwamba – Vijana Tukiamua, Tunaweza!

  Ni katika hali hii ndipo mimi pia nikaamua kujitosa katika kinyan'ganyiro cha kura za maoni CCM kwa nafasi ya ubunge jimbo la Kinondoni kwa uchaguzi uliopita na kuambulia nafasi ya nne kwani kura hazikutosha. Matarajio yangu yalikuwa, pamoja na mengine, iwapo wana CCM kinondoni wangeniamini na kunipa dhamana ya kuwa mgombea wao katika uchaguzi wa October 2010 na hivyo kupata nafasi ya kupambana na wewe jukwaani, ningejifunza mengi toka kwako kwani tetesi ni kwamba ulifikiria kugombea majimbo kadhaa kinondoni likiwa ni jimbo moja wapo. Niliamini kabisa kwamba kama mshindi angekuwa mimi au wengine wa CCM ili kukutana na wewe October 2010, wana kinondoni wangepata fursa nzuri ya kusikia hoja zako kwani wakati wote huwa zinagusa sana jamii, hususan vijana. Nisewe wazi kwamba bila Zitto, bunge letu la jamhuri ni butu.
  [/FONT]

  [FONT=&quot]Napenda kuchukua nafasi hii kukupongeza kwa kurejea bungeni kwa kishindo lakini pia kwa kupata vijana wenzako wengine wapiganaji kama kaka yangu tundu lissu, na wadogo zangu Mnyika, Mdee, Shilinde na wengineo. Tunawategemea sana kama vijana, napenda kusititiza tena - Tanzania Kwanza, Siasa Baadae - na tunaomba msituangushe na Mungu awaongoze katika hilo.[/FONT]

  [FONT=&quot]Nimekuwa mfuatiliaji mzuri wa kazi zako za ndani na nje ya bunge kwa kipindi cha miaka mitano na ushee sasa. Mara nyingi, hoja zako zimekuwa na msisimko, mvuto na mashiko kwani, haukurupuki, ukiachilia mbali suala la Richmond/Dowans ambalo ulijaribu kufafanua msimamo wako lakini ukiweli unabakia kwamba hoja yako juu ya Richmond/Dowans was a double edged sword. Lakini lengo langu leo sio juu ya Richmond/dowans bali ni juu ya ziara yenu Chadema huko nyanda za juu kusini wiki iliyopita. Mengi tumeyasikia. Kwanza na awali ya yote, poleni sana waheshimiwa wabunge wa vyama vyote kwa kutolipwa misharaha na posho kwa wakati. Ila cha kustaajabisha ni kwamba hali halisi ya uchumi sasa imewafikia hata waheshimiwa kwani ilikuwa ni wananchi pekee waliokuwa wanaonja machungu ya maisha. Ama kweli Mheshimiwa Zitto, hata wabunge sasa mkuki wa nguruwe sasa mmeusikia uchungu wake na kuamua kuamka.[/FONT]

  [FONT=&quot]Mimi kama wewe nina background ya uchumi. Mheshimiwa, hoja yako kwamba watanzania tupo katika hali ngumu kutokana na imbalance between government's revenue and expenditure nakubaliana na wewe mia kwa mia. Nakubaliana nawe pia kwamba kielelezo kikuu juu ya kwanini mtanzania leo hii anaishi HOI ni kutokana na ufisadi na uendeshaji na usimamizi mbovu wa muundo wa uchumi kwa ujumla. Ila ninachotofautiana nawe ni the means towards ufumbuzi wa tatizo hili kama ulivyoainisha huko Mbeya juzi. Awali ya yote, ngoja niseme kwamba nakubaliana nawe katika hili – kwamba kodi ya mafuta na petrol inachangia sana kwa hali tete ya uchumi nchini.

  Kwa mtazamo wangu, ni sahihi kabisa kulipeleka suala hili bungeni mwezi ujao kama ulivyoelezea kwa kirefu kwani kama serikali yetu haina ubunifu juu ya kutafuta au kuimarisha vyanzo vya mapato, ni kosa kubwa kukimbilia kiholela kwenda toza kodi za ajabu kwenye sekta ambazo ni life blood ya maisha ya mtanzania kiuchumi. Bei ya mafuta na petrol isipodhibitiwa, hali itakuwa mbaya sana ndani ya miezi tisa ijayo. Mafuta na petroli ni injini ya uzalishaji viwandani, usafirishaji wa bidhaa toka mashambani n.k. Kama ulivyoainisha, maeneo haya ya uzalishaji kama yatakuwa yanalemewa kutokana na gharama za mafuta na petroli kuwa juu,itaendelea leta matatizo makubwa ya kiuchumi nchini. Waziri mkullo katika taarifa yake ya hali ya uchumi na mikakati kwa mwaka 2008-2012 aliainisha kwamba mkakati ni kuwa na mfumuko wa bei in single digits yani usiofikia asilimia kumi. Kuna taarifa kwamba atatolea maelezo hoja zenu za Mbeya, lakini natumai atajibu pia in the context of alichotueleza katika taarifa yake ya hali ya uchumi (see above), wewe ukiwa ndani ya bunge lile.
  [/FONT]

  [FONT=&quot]Mfumuko wa bei utaendelea kuwa tatizo kwani mchango mkubwa wa bei kufumuka unatokana na bei ya vyakula kuwa juu sana kutokana na tatizo la bei kali za mafuta na petroli ambazo ni key input kufanikisha chakula kifike sokoni. Na hapa hatujafikia mwezi wa ramadhani, tunaweza jikuta katika hali mbaya sana kwani kwa mazoea, ni kawaida kwa bei ya vyakula kuwa juu sana wakati wa mfungo. Sasa ramadhan ikichanganyikana bei kali za mafuta na petrol na vile vile speculation za wazalishaji utaopelekea creation of shortage, hapatakalika.[/FONT]

  [FONT=&quot]Katika hoja zako huko Mbeya, ni eneo moja tu ambalo limenitatizo kidogo na ndio kiini cha mimi kuja na waraka huu. Nina kunukuu Mheshimiwa: "tunaitaka serikali iuze hisa zake zilizoko kwenye benki ya NBC na Kampuni ya simu ya Zain kwani zitaipatia fedha za kutosha ya kuweza kufidia kodi tunayotaka ipunguzwe kwa asilimia 50 katika mafuta. Hiyo ndiyo moja ya ajenda ambayo chadema tunakwenda nayo bungeni Juni 7". [/FONT]

  [FONT=&quot]Mheshimiwa, hoja hii ukiipeleka bungeni itakuangusha hivyo nakushauri ufikirie mara mbili. Nasema hayo nikiwa mmoja wa vijana wanaopenda siasa zako hususan pale unapokuwa na hoja zenye mashiko, msisimko na ushawishi unaoiweka serikali sawa. Tunakuhitaji, hatutaki uteleze tena kama Richmond/Dowans. Sielewi mantiki yako ya Mbeya juzi ilikuwa nini, je ni ukata wa kutolipwa mishahara na posho za ubunge kwa mwezi Aprili? [/FONT]

  [FONT=&quot]Unajua mheshimiwa wewe ni mwenyekiti wa kamati muhimu sana ya bunge letu – je, hoja yako imetokana na uelewa wako ukiwa mwenyekiti wa kamati hii? NBC na Airtel zina mamatizo gani ili tuiokoe serikali yetu?unatoa tafisiri nyingi na zitatuchanganya kama hautoi maelezo, na ni tatizo kubwa sana sababu wewe ni mwenyekiti wa kamati muhimu ya mashirika ya umma na ningependa pia kusema, pale ambapo sio mashirika ya umma moja kwa moja basi ya ushiriki wa umma (hisa za serikali kwa niaba yetu walipa kodi). Je baadhi ya wanakamati wako wanakubaliana nawe katika hili au ni asilimia mia moja chadema? Haiingii akilini kijana makini kama wewe kutofafanua hili badala yake kutumia nafasi hiyo pia kuwaambia wananchi kwa mfano nyinyi Chadema mtaibana serikali ipunguze by half mishahara na posho za wabunge kwani zinachangia sana kuumia kwa wananchi hivi sasa.[/FONT]

  [FONT=&quot]Mheshimiwa, kama wewe ni mfuatiliaji mzuri wa mwenendo wa uchumi wetu, bado tupo kwenye msiba mkubwa kitaifa wa kupoteza mashirika ya umma mengi yao ikiwa ambayo yalikuwa yanajiendesha kwa ufanisi na kutoa ajira nyingi kwa watanzania na pia kuchangia pato la taifa kupitia kodi. Mfano mzuri ni TBL na TCC. Mashirika mengi ya umma yalibinaifsishwa kiholela, jambo ambalo hata vingozi wetu wakuu wastaafu walishakiri huko nyuma kwamba waliteleza katika hilo. Katika mfumo wa uchumi wa karne hii, hususan katika nchi maskini kama Tanzania, umuhimu wa Public-Private-Partnership unasisitizwa sana.

  Vilevile kuna msisitizo wa kuwa na mfumo wa uchumi ambao serikali inapata nafasi ya kushiriki ili kurekebisha market failures. Kwa mantiki hiyo, sio ajabu kwa serikali kuendelea kushika hisa NBC na Airtel. Ikiwezekana, serikali iendelee na mfumo huo ufikie hata aslimia 50 katika sekta muhimu nchini, sana sana sekta kama ya madini kama wenzetu wanavyofanya Botswana. Kufanya hivyo ni kwamba serikali inashikilia hisa kwa niaba ya watanzania, sio CCM kwani hata Chadema ikishinda uchaguzi mkuu, suala hilo litahamia katika serikali yenu. Jambo la msingi hapa juu ya Airtel na NBC iwe usimamizi wa mapato na matumizi, sio kuuza hisa.
  [/FONT]

  [FONT=&quot]Pengine nikukumbushe kidogo – wiki tatu zilizopita, Katibu Mkuu wako Dr. Wilbrod Slaa aliulizwa swali na Makwaia Kuhenga katika kipindi cha Je Tutafika kwamba kwenye luninga Channel Ten– Je, Chadema ina sera gani mbadala za uchumi, mbona hazipo wazi sana? Dr. Slaa akajibu kwa ufasaha swali hilo kwa kuziweka bayana moja wapo ikiwa juu ya umuhimu wa serikali kuwa na mkono katika uchumi wa nchi. Mheshimiwa Zitto, hivi huwa mna consulat each other kabla ya kutoa matamko hadharani?

  Nilivutiwa sana na sera za Chadema alizozitoa Dr. Slaa, nikabaki kuduwaa mbona CHADEMA haitumii muda mwingi kuzinadi na badala yake ni juu ya ufisafi tu. Suala la ufisadi ni tatizo kubwa sana kwa taifa letu lakini hata miaka ya nyuma niliwahi kuuliza, je, Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya muungano akifanikisha kulivalia njuga suala hili, chadema watakuwa na sera au agenda gani ya kuleta ushindani? Kama muelewa wa umuhimu wa siasa za ushindani, napenda sana ushindani wa hoja toka vya upinzani kwani hiyo ndio njia pekee ya kuiweka serikali sawa katika kuwahudumia na kuwatumikia wananchi, na kuifanya serikali yetu ya CCM ijue ni wapi inakosea ili ijisahihishe. Ni dhana ile ile uliyoitoa Mbeya ya "mbwa wa tajiri".
  [/FONT]

  [FONT=&quot]Mheshimiwa, kauli yako ya Mbeya kwamba serikali iuze hisa zake za NBC na Airtel ipo katika msimamo gani wa chadema kisera? Au ni hati ya dharura? Hivi unafahamu kwamba pakiwa na referendum leo hii juu ya kuamua serikali iwe au isiwe na hisa katika makampuni kwenye umma, asilimia kubwa itasema serikali ikamate hisa kwa niaba ya wananchi? Suala hili haliitaji kuwa a rocket scientist mheshimiwa. Kikubwa hapa ni serikali kuendelea na mtindo huu lakini usimamzi wa mapato na matumizi uwe mzuri. Katika hili Mheshimiwa uliteleza kwani mkakati wako ni short term, unsustainable and contradictory to msimamo wa chama chako (rejea kauli za Dr. Slaa juu ya sera za CHADEMA kiuchumi).

  Pengine nikuulize, je, hali ikizidi kuwa tete, serikali iuze hisa zake zote za ATCL kwa mwekezaji yeyote atakayekuwa tayari kununua? Je hisa za Mwadui (kama bado zipo) nazo ziuzwe? Hisa za Mchuchuma nazo ziuzwe ili serikali iweze pata fedha za kutosha kuweza fidia kodi mnayotaka ipunguzwe kwa asilimia 50 katika mafuta? Naomba ufafanuzi Mheshimiwa kwani haingii akilini.
  [/FONT]

  [FONT=&quot]Kwa kumalizia Mheshimiwa – kama mwenyekiti wa kamati ya umma ya mahesabu ya mashirika ya umma, unatambua kwamba mashirika ya umma Tanzania katika miaka themanini, zaidi ya nusu ya mashirika zaidi ya 300 yalikuwa yakiendeshwa kwa hasara. Kubinaifsishwa ilikuwa ndio njia pekee, tatizo limebakia sio uamuzi wa kubinaifsishwa bali utaratibu wake. Vinginevyo, katika nchi nyingi, mashirika ya umma bado yapo na yanajiendesha kwa ufanisi, yanatoa ajira na yanachangia sana katika pato la taifa. Umelisemea sana hili bungeni mheshimiwa. Nikupe mfano wa wenzetu - shirika la umeme la ufaransa, kiwanda kikuu cha chuma south korea, shirika la ndege la Ethiopia, shirika la ndege ya Afrika ya kusini, kiwanda kikuu cha mbolea Indonesia na mengine mengi huko Singapore – hizi ni nchi za Asia ambazo zilikuwa na Maendeleo sawa ya kiuchumi na sisi Tanzania miaka ya sitini lakini sasa ni nchi tajiri. [/FONT]

  [FONT=&quot]Ushauri wangu[/FONT]
  [FONT=&quot]1. [/FONT][FONT=&quot]Hoja ya kuuza hisa za NBC na Airtel usiipeleke bungeni, haina mashiko. Nakushauri kama kijana mwenzako ninayependa siasa zako na kutaka kuwa kama wewe siku moja.[/FONT]
  [FONT=&quot]2. [/FONT][FONT=&quot]Ukiwa mwenyekiti wa kamati ya bunge ya mahesabu ya mashirika ya umma, jaribu kujifunza wenzetu wanafanyeje kuendesha mashirika yao kifanisi wakati yakiwa ya umma au serikali husika zikiwa na hisa. Fanya a cost benefit analysis kabla ya kuja na kauli kubwa kama hizi, sanasana kwa mtu kama wewe ambae taifa wakati wote linategea sikio kusikia unasema nini.[/FONT]
  [FONT=&quot]3. [/FONT][FONT=&quot]Endelea kuibana serikali juu ya mapato na matumizi katika mashirika yote ya umma, mifuko ya pensheni, na pia katika kampuni ambazo serikali ina hisa kama vile NBC na Airtel. Ni bora kuboresha usimamizi wa mapato na matumizi kuliko kuuza hisa. Umekuwa unafanya vizuri katika hili Mheshimiwa.[/FONT]
  [FONT=&quot]4. [/FONT][FONT=&quot]TIB – benki ya rasilimali Tanzania – tulielezwa kuna fedha zilienda huko, zifuatilie hizo kwani zinaweza changia sana katika hali tete ya sasa kiuchumi.[/FONT]
  [FONT=&quot]5. [/FONT][FONT=&quot]Endelea na kazi nzuri ya kutuelimisha juu ya upungufu katika mikataba mbali mbali ambayo inajaa mianya ya rushwa au kupotea kwa mapato ya serikali. Suala la kuziba mianya ya kodi katika mauzo ya Zain kwa Airtel ambapo tulipoteza zaidi ya dollar million 300 kwa kweli ni la kusikitisha. Asante sana kwa kutuelimisha.[/FONT]
  [FONT=&quot]6. [/FONT][FONT=&quot]Jaribu kujenga hoja ya kitaasisi kwamba Benki Kuu ina nafasi muhimu katika kuendeleza uchumi kuliko inavyofanya hivi sasa. Nchi za wenzetu central banks zao zilikuwa na majukumu tofauti na haya tunayoamrishwa na IMF.[/FONT]

  [FONT=&quot]Vinginevyo, nikikunukuu Mbeya hivi karibuni juu yenu chadema, ni kweli kwamba:[/FONT]

  [FONT=&quot]"Sisi ni sawa na mbwa wa tajiri, jukumu letu ni kunusa na kubweka.Pale tunapoona kodi yenu imeliwa sisi tunakuja kuwaeleza, ili mchukue hatua za kuwawajibisha viongozi wenu na hatimaye mtupe ridhaa ya kuwaongoza…maana wenzetu wameshindwa kazi"[/FONT]


  [FONT=&quot]Lakini Mheshimiwa zitto, mkiwa kama Mbwa, msimbwekee tajiri kisa kikiwa tu ni alirudi akiwa amelewa. Nakutakia kila la kheri katika shuguli zako za ujenzo wa Taifa.[/FONT]

  [FONT=&quot]Tanzania Kwanza, Siasa Baadae.[/FONT]
   
 2. k

  kilombero yetu JF-Expert Member

  #2
  May 9, 2011
  Joined: May 6, 2011
  Messages: 1,007
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Safi sana kaka hope CDM na Zitto watasikia ushauri wako
   
 3. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #3
  May 9, 2011
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0

  Nimeipaenda analysis yako lakini kama mwana CCM na wewe unatumiaje position na kadi yako kusahihisha na kushauri CCM iliyopo madarakani juu ya haya mambo ua Uchumi ???? Sometime uhasuri ukitoka kwao unaweza kupokelwa kwa mikono miwili kuliko wa Zitto.

  Nyie vijana mlioko CCM Taifa kwanza kama ulivyosema mnafanya nini maana hawa kina Zitto na Slaa inabidi watumie effort kubwa sana. Tanzania kwanza siasa baadae. Na nyie huko mliko mnatakiwa ku press button......
   
 4. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #4
  May 9, 2011
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,634
  Trophy Points: 280
  Mabango ya aina hii siku hizi adimu sana jamvini.

  Asante kaka nimekusoma na kukuelewa vyema.
   
 5. Z

  Zion Train JF-Expert Member

  #5
  May 9, 2011
  Joined: Jun 5, 2008
  Messages: 503
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  ulipaswa kuwa mbunge wangu kinondoni, lakini wakina mama ndiyo wametuangusha
   
 6. Ehud

  Ehud JF-Expert Member

  #6
  May 9, 2011
  Joined: Feb 12, 2008
  Messages: 2,696
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  CCM kumbe na nyie mna mawazo mazuri hivi? Sasa huwa inakuwaje mkipewa madaraka?
   
 7. Butola

  Butola JF-Expert Member

  #7
  May 9, 2011
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 2,221
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145


  Ushauri makini, kama Zitto kweli alisema hivyo apige break haraka, sio wazo zuri kwa nchi yetu na pia litamharibia image yake kisiasa.
   
 8. L

  LAT JF-Expert Member

  #8
  May 9, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  mpoki mwambulukutu .... habari za siku mkuu
   
 9. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #9
  May 9, 2011
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,927
  Likes Received: 2,080
  Trophy Points: 280
  Mchambuzi, hebu kamuone Dr Slaa akupe kadi....hiyo ya kijani na manjano itie moto haikufai!
   
 10. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #10
  May 9, 2011
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Ningechangia ila hilo kamba la kijani napata kichefuchefu
   
 11. Gamba la Nyoka

  Gamba la Nyoka JF-Expert Member

  #11
  May 9, 2011
  Joined: May 1, 2007
  Messages: 6,600
  Likes Received: 6,766
  Trophy Points: 280
  Ukisikia kumkoma Nyani Giladi ndio kama hivi, bravo haya ndiyo mambo tunayoyataka hapa JF.
   
 12. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #12
  May 9, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  habari ndefu sana c.v na ishu zakujinadi tu hakuna ishu hapo tired...
   
 13. Zitto

  Zitto MP Kigoma Urban

  #13
  May 9, 2011
  Joined: Mar 2, 2007
  Messages: 1,197
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  Nashukuru sana. Nipo Sumbawanga. Hujanielewa. Ninashauri kufanya IPO ya Airtel na NBC ili kwanza kupata mapato kwa serikali lakini pili kwa kumilikisha uchumi kwa umma. IPO ni kwa wananchi kupitia soko la hisa.

  Hukunielewa vema na ninaomba unielewe. Siku zote nimekuwa mstari wa mbele kuhakikisha DSE inakuwa more liquid. Nataka tuwe na kampuni nyingi sana DSE. Hii itawezesha uwazi.
   
 14. J

  Joblube JF-Expert Member

  #14
  May 9, 2011
  Joined: Mar 4, 2011
  Messages: 367
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Niuchambuzi mzuri sana hauna magamba kama chama chako cha magamba
   
 15. K

  Kidatu JF-Expert Member

  #15
  May 9, 2011
  Joined: Jun 11, 2008
  Messages: 1,491
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Ndaga fijo nyambala ujobile kanunu fijo. CCM ingekuwa na watu kama wewe 30 bila shaka mambo mengi yangekuwa shwari. Na ninakushauri usitoke CCM, baki huko huko ili upigane nao ukiwa ndani.
   
 16. Kitila Mkumbo

  Kitila Mkumbo Verified User

  #16
  May 9, 2011
  Joined: Feb 25, 2006
  Messages: 3,347
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  Very good Mchambuzi. Pamoja na kwamba sikubaliani na baadhi ya hoja zako, nimependa sana approach yako. Siasa zetu zinatakiwa ziende huko. Tuanze kujadili juu ya hoja za kisera, kuangalia sera gani itatuvusha na ipi itatuangamiza.

  Angalizo: Serikali kuuza hisa katika NBC na mashirika mengine kama hayo hakuifanyi serikali kutokuwa na mkono katika uchumi wa nchi. Aidha, serikali kuwa na hisa 50% au zaidi katika mashirika kama hayo ya Airtel haitoshi kuonyesha kwamba serikali ina mkono katika uchumi wa nchi. Ni zaidi ya hayo. Ukisoma Ilani ya CHADEMA ya uchaguzi 2010 Sura ya Tano inafafanua vizuri sana namna ya serikali kushiriki katika kujenga uchumi shirikishi bila kuibughudhi sekta binafsi.

  Nakupongeza tena kwa uchambuzi na approach yako. Ndio maana ulishika namba nne maana watu kama wewe katika CCM ni odd out!
   
 17. J

  Joblube JF-Expert Member

  #17
  May 9, 2011
  Joined: Mar 4, 2011
  Messages: 367
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA, Bw. Kabwe Zitto, aliwaambia wananchi katika mikutano yake kuwa chama hicho kimepanda chati kwa asilimia 400, kati ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2005 na 2010, kwani kabla ya uchaguzi wa mwaka jana kilikuwa na madiwani 101 sasa wameongezeka kufikia 466, huku wabunge wakiongezeka kutoka 11 mpaka 48.

  Huku akiwataka wananchi kuendelea kujipanga kwa ajili ya uchaguzi mkuu ujao, kuhakikisha chama hicho kinashinda na kuchukua dola, Bw. Zitto alisema kuwa mgombea urais wa CHADEMA uchaguzi mkuu mwaka jana, Dkt. Willibrod Slaa alishinda lakini matokeo yake 'yakachakachuliwa'.
   
 18. Titans

  Titans JF-Expert Member

  #18
  May 9, 2011
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 867
  Likes Received: 1,073
  Trophy Points: 180
  good analysis bro
   
 19. m

  mwana wa africa JF-Expert Member

  #19
  May 9, 2011
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 490
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  ile speech yako ya mbozi imenivutia sn na ilikuwa inagusa maisha ya kila siku ya mtanzania wa kawaida. kweli taaluma yako ya uchumi unaitendea haki. BIG UP br!
   
 20. D

  DAR si LAMU JF-Expert Member

  #20
  May 9, 2011
  Joined: Mar 31, 2007
  Messages: 2,942
  Likes Received: 286
  Trophy Points: 180
  ...Zitto, sahihisho hili limekaa vizuri kiasi, maana hata mimi nilipoona hilo pendekezo la kuuza hisa, kama lilivyonukuliwa, nilishtuka kidogo.

  ...Ila, nadhani hizo hisa zinaweza kuuzwa, si kwa kufidia kodi itakayopotezwa kwenye punguzo la kodi ya mafuta, kwani si endelevu, bali kuondokana na umiliki usio na tija. Sidhani kama hizo hisa zinasimamiwa vya kutosha na kuna uwezekano tunadanganywa sana. Nadhani wewe uko katika nafasi nzuri zaidi ya kufahamu hili.

  ...Katika suala la kulist hayo makampuni huko DSE, je, wanahisa wengine (airtel, absa, barclays, etc) watakubali au mikataba inasemaje?
   
Loading...