Nashukuru sana. Nipo Sumbawanga. Hujanielewa. Ninashauri kufanya IPO ya Airtel na NBC ili kwanza kupata mapato kwa serikali lakini pili kwa kumilikisha uchumi kwa umma. IPO ni kwa wananchi kupitia soko la hisa.
Hukunielewa vema na ninaomba unielewe. Siku zote nimekuwa mstari wa mbele kuhakikisha DSE inakuwa more liquid. Nataka tuwe na kampuni nyingi sana DSE. Hii itawezesha uwazi.
Kama hakukueewa, nashauri chukuna muda jibu kwa urefu kidiogo ili ulete uelewa si kwa huyu tu, bali na kwa sisi wengine ambao nao hatukukuelewa.
Kwangu mimi, kulazimisha serikali iuze hisa zake inaweza kuwa njia nzuri ya kuifamarisha liquidity ya stock markeyy lakini inaweza isiwe muafaka kwa kushughuklikia tatizo la kiuchumi loinalotukabili.
Nadhani unaelewa Zitto kwua tatizo lililopo ni zaidi ya kuifanya DSE iwe active sana. hata serikali ikiuza hisa zake hizo, bado hatuna uhakika na iwapo fedha hizo zitatumika ipasavyp. Tunaweza kukosa mwana na maji ya moto-hisa zikauzwa na fedha zikaliwa vilevile.
Kama hoja ni kuifanya DSE iwe active, tunaweza kuyahimiza na kuyawezesha makampuni katika sekta binafsi kuingia huko DSE na kuuza hisa zao. Hivi mpango wa barrick kuuza hisa umeishia wapi? Hao Zain nao si wana hisa zao ukiondoa zile za serikali, kwa nini nao wasiende, Vodacom na vipi? IPP, Mwananchi, bakhresa, METL na mengine kama hayo? nadhani hawa wakiingia huko DSE itachangamko kuliko kwa serikali peke yake kuuza hisa sake.
Najiuliza iwapo serikali ikimaliza kuusa hisa zake kwenye IPO, nini kitatokea (maana uzoefu unaonyesha kwua wanaonunua hisa wengi wanazinunua kwa lengo la kuzishikilia). Soko bado litaendelea kudumaa hata kama serikali itafanya IPO ya hisa zake.
La kufanya hapa, pamoja na kuyahimiza makamapuni kuuza, watanzania nao wachangamkie bishara hiyo. Uchangamfu wao unaonekana kwenye IPO tu kiasi kwamba nyingi zinakuwa oversubscribed, baada ya hapo, kila mtu anabaki na hisa zake kusubiri dividends.
Tafadhali rudi tena Zitto utupe ufafanuzi