Mhe. Pinda aahirisha Bunge hadi Juni 12, 2012

Mhe. Pinda aahirisha Bunge hadi Juni 12, 2012

bunge lilikuwa so hot bt hyu mizengo anavolimaliza, daah me hoi! "irresponsible wazir mkuu"
 
Maamuzi ya kik@*@
serikali ya kik@*@
watendaji wakik@*@
Ila tutafika tu....
 
Hivi Kurugenzi ya Ikulu ilikuwa inakanusha kitu gani ? Tunayoyashuhudia ni ushahidi kwamba JK aliingilia mchakato wa mawaziri kujiuzulu hata kama Rweyemamu anakataa lakini huo ndo ukweli.
Pia nimuuliza Pinda na Jenista Mhagama walichosema tusubiri leo jumatatu ni kitu gani wakati bunge limeshaahirishwa bila kuona cha ajabu?
 
Waziri Mkuu katoa hotuba ya kufunga bunge (Hotuba nzima ipo post ya pili chini).

Hakuna Waziri hata mmoja aliyejiuzulu wala kuwajibishwa kama wengi walivyotarajia.

Spika kahitimisha kwa kuwataka wabunge wasichukiane nje ya Bunge kwakuwa yaliyojadiliwa bungeni ni sehemu ya kazi.

hiyo ndio imetoka hiyoo...kweli tanzania daima walikua wa kweli kua Rais kasema hakuna kujiuzulu mtu hii kitu itakwisha taratibu kama upepo....mheshimiwa anajua baada ya muda kila kitu kitakua kimetulia....its up to akina zitto na wapinzani wengine ku make sure kua hii kitu haishi.....i wonder what the foreigners, sponsors, donors, embassies make of this..its a disgrace to not only society but to the world....
 
He did not even mentioned the issue na hatua gani serikali itachukua!kweli usanii.com
 
Hotuba iliyotolewa na Mh M.Pinda Waziri mkuu wa Tanzania inatufundisha Watanzania tuwe na mioyo ya kuvumiliana na kustahimiliana katika kuelekea katika maamuzi magumu kwa mustakabali wa amani na utulivu wa taifa letu.

Kwa Watanzania wapenda amani hutuba ya Pinda ya kuhairisha bunge ni hutuba ya kishujaa na ya kizalendo.
 
Received with thanks,

Nakubaliana na wewe mkuu Kiongozi makini hakurupuki katika kufanya maamuzi.
 
Hotuba iliyotolewa na Mh M.Pinda Waziri mkuu wa Tanzania inatufundisha Watanzania tuwe na mioyo ya kuvumiliana na kustahimiliana katika kuelekea katika maamuzi magumu kwa mustakabali wa amani na utulivu wa taifa letu. Kwa Watanzania wapenda amani hutuba ya Pinda ya kuhairisha bunge ni hutuba ya kishujaa na ya kizalendo.

ushujaa upo wapi sasa hapo?labda we ni mmoje wenye akili za kimagamba ambao ni wabadhilifu na wasio wawajibikaji kwa wananchi wao.
 
pinda kwa nini usiingie humu na id yako ya kweli kama slaa na zitto kuliko kujifichaficha kama digidigi!
 
<STRONG>Yaani ungekua karibu yangu wakaki unaandika hii post ningekuwasha vibao vingi? ushujaa au uwoga? Kiongozi mwenye akili timamu hawezi kutozungumzia hoja muhimu kama ufisadi wa serikali yake? ushujaa gani wakati ameshindwa kuwawajibisha walio chini yake? shujaa gani kashindwa kuwajibika? Shujaa siku zote yuko radhi afe ili watu wake wakombolewe. Ushujaa wa Pinda hapa uko wapi? Na sasa ameingia mtoni kukwepa mvua. Sijui huo mto ukijaa hali yake itakuaje humo ndani? Emmy umenibore sana</STRONG>
 
Tuvumilie nini ?? wezi, mafisadi na wanasiasa matapeli?? tuvulimiliane ktk nini?? big no wachukuliwe hatua km wengine.

kustahimili nini?? ukosefu wa maji salama, umeme na barabara ?? tustahimili nini hakuna kitu kama hicho wakati mamilioni
ya watanzania wanateseka wewe jawabu lako wavumilie na wawe wastahimiivu. you must be out of mind.

unajua hata maana ya rule of law wewe ?? tunayoambiwa nchi inaongozwa nayo wakati ukiangalia hiyo ni nadharia tu.
 
watanzania wote hatuna akili upepo umeshatusafisha
hivi waziri mkuu hajaona tuhuma zote za wizi wa mawaziri wake?
I wish ningekuwa na mabawa ningemzungusha tanzania nzima wananchi wamwone asivo na huruma
 
Anazungumza pumba nyingiiii, wakati sisi tunasubiri atoe maamuzi aliyoahidi kuyatoa J3

Gonjwa la kushindwa au kuogopa kufanya maamuzi ya maana ndiyo linaiua nchi hii! Pinda kama Mkubwa wake wa kazi; KAAMUA KUTOAMUA!
 
Shujaa anayedharauliwa?

Skendo ya Jairo ilimdhalilisha sana, na bado JK na Ikulu kwa kiburi walicho nacho wamegoma kutekeleza maazimio ya Bunge na ndo maana Spika wa Bunge alijua kwamba swala hilo lingejadiliwa lingewapandisha hasira wabunge.

Serikali yenu sio ya kubembelezana, ukiwabembeleza hakuna watakachotekeleza, na ndio maana mawaziri wanajibu mbovu na kujifanyia wanayotaka.

Wakati wa skendo ya Jairo, alisikika akisema kwamba hata wachonge sana hatatoka, na mpaka leo kweli bado yuko na hakuna walichomfanya.

Mbaya zaidi IKULU kupitia Luhanjo ikamsafisha na kumrudisha kwa mbwembwe na kupokelewa akisukumwa kwenye gari. Hayo kama sio matusi kwa Waziri Mkuu ni nini? Pinda alitutangazia watanzania kwamba kama angekuwa yeye ndo mwenye final say, angemfuta kazi Jairo. Juzi amekaa kwenye kikao mpaka usiku, wakakubaliana kwamba mawaziri 8 waondoke, nini kimetokea? Huyo ndo shujaaa? Angekuwa shujaa kweli angesema anajiuzulu, hapo ningemuona ni shujaa anayelinda heshima yake baada ya kudhalilishwa mara 2 tena mbele ya watanzania wote. Kwa kuwa kilichotokea sio kwamba ni vikao vya siri, bali ni maamuzi ya wazi yaliyotangazwa.

He is the weakest PM ambaye hajapata kutokea hapa Tanzania. JK anambuluza apendavyo na bado yuko tu amekomaa na u-PM! Halafu unakuja kusema eti ni shujaa!
 
Hata kuwa muoga unaweza kuwa shujaa katika waoga, hata wajinga wana kipanga wao. Kwa hiyo Pinda ni shujaa katika waoga, shujaa katika group la wajinga.

Na huo ndiyo ushujaa ambao kama taifa hatuwezi kumuhesabu kama shujaa.
 
Maskini Wakereketwa..

Mnajitahidi sana kutengeneza sred, ila sasa tatizo hamjui hata cha kuongea, mnajitahidi sana kukitetea chama chetu cha magamba ila bahati mbaya hakuna hata pa kusemea jema.. chama kinawaangusha na kila sred mnayoipeleka hewani ukiisoma unawaza huyu mtu ameandika akiwa admitted mirembe mental hospital au kavaa nguo ya ndani kichwani..

Kiongozi wenu mwenyewe naye keshakunjika kama jina lake, maamuzi yamemshinda, kabanwa nkotekote, pumzi kaishiwa anaomba fadhila.. angekuwa mwerevu asingeongelea lolote lenye upepo wa vuguvugu linaloendelea bungeni.. yeye angewashukuru wabunge kwa kazi kubwa na ngumu ya kusimamia matakwa ya wananchi kazi ambayo wameifanya vema na kuliahirisha Bunge .. bas.. mambo ya kuvumiliana.. sijui maamuzi mazito au magumu.. yanatoka wapi.. yalishamshinda toka kwa jairo atayaweza leo?.. nani avumili e.. mwizi umeshamgundua unaambiwa vumilia? mbona tusi hilo..

 
pinda kwa nini usiingie humu na id yako ya kweli kama slaa na zitto kuliko kujifichaficha kama digidigi!

Wewe ni kama kipofu aliyeona Punda. Unaona kuwa kila kitu ni JF tu.

Pinda ana mambo ya kumpindisha zaidi ya JF.

Fikiri!
 
Hotuba iliyotolewa na Mh M.Pinda Waziri mkuu wa Tanzania inatufundisha Watanzania tuwe na mioyo ya kuvumiliana na kustahimiliana katika kuelekea katika maamuzi magumu kwa mustakabali wa amani na utulivu wa taifa letu. Kwa Watanzania wapenda amani hutuba ya Pinda ya kuhairisha bunge ni hutuba ya kishujaa na ya kizalendo.

As the saying goes,
It's so simple to be wise,
Just think of something stupid to say
And then don't say it...
like OMG, the rain's wet!

images
 
Hon. mwanaJF kuchangia hoja kwa matured thinkers needs directed mind to the agenda. mara nyingi watu wanatoa majibu na conclusions rahisi kwa maswali au issues nzito, hatutafika. Tujielekeze katika wajibu wa PM. Hata kumuwajibisha Jairo alishindwa na publicly tulimsikia akilalama na JK akampuuza. Wakati wa Richmond likewise na baadae akamruka Lowasa. Sasa wana Jamii tungejikita kufikiria tufanye nini sisi kama Watanzania? sisi kama jamii tuliomchagua JK anatupuuza,wabunge anawapuuza hata PM anampuuza,aah
 
Back
Top Bottom