Mhe. Pinda aahirisha Bunge hadi Juni 12, 2012

Mhe. Pinda aahirisha Bunge hadi Juni 12, 2012

Haya sasa, hayo ndiyo majibu ya waziri mkuu. Mko wapi mliotuletea uongo hapa mkidai mko jikoni? Kwanza mlianza na kikao cha wabunge wa CCM Kilichoongozwa na waziri mkuu, mkatuambia mawaziri nane wamejiuzulu.. Wajinga wakaamini. Leo mkaleta habari kutoka jikoni kuwa waziri mkuu anajiuzulu, tumesikia kilichotokea. Siku chache zilizopita niliweka bandiko hapa kuwa wananchi na wabunge wetu wazalendo, anayepaswa kuwajibishwa ni rais. Watu wakanipigia kelele hapa. Nchi za wenzetu wana akili kuliko sisi. Tunisia waliandamana moja kwa moja kwa ajili ya kumtoa rais, wakafanikiwa. Misri nako vilevile. Sisi tunalia na waziri mkuu, mtu anayopokea amri kutoka kwa mkuu wake. Nilitoa mfano pia kuwa, timu ya mpila ikifungwa tunalia na kocha? Au kapten wa timu. Nikaongeza pia, nyoka akikuingilia unapaswa kupiga kichwa au mkia? Bila kuchukua hatua zinazostahili. Tutaishia kupiga kelele, lazima tujiulize. Mawaziri hawa kiburi wanapata wapi? Nadhani majibu tunayo..

Sasa tufanyaje? Toa muelekeo mkuu
 
Kumbe ile habari iliyokanushwa jana na Ikulu juu ya kilichoandikwa na Tanzania Daima ilikuwa ni ya kweli? Basi hii ni balaa. Hapo wabunge wa CCM waliosaini petition matumbo moto.



Mkuu Lukolo, Ile habari ya Tanzania daima ilikuwa sahihi 100%. Mimi nlishaa watu humu wanashabikia hilo kanusho la salvatory lisilokuwa na kichwa wala miguu. Chochote kinacho kanushwa na kurugenzi ya ikulu kwa haraka sana kuliko kawaida ujue kuna ukweli ndani yake.

Kwa kweli baada ya lile kanusho nlikuwa sitegemei kitu kipya kutoka kwa pinda na ndivo ilivyotokea.
 
Zitto kwenye twitter kasema hoja yake imepotezwa na spika.

Zittokabwe hoja naona kama imepotezewa vile...hii ndio serekali makini bana...am so dissapointed.hoja sasa mtaani then

tumewasilisha hoja kwa Spika leo na tumeomba Bunge la dharura kwa mujibu wa kanuni ya 27(4). Tutakaba mpaka kona,ikishindikana ni kwa wananchi.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu huko tunisia, misri hakuwezi kuwa model ya TZ,
huku ni ushabiki wa kisiasa na vyama. kule ilikuwa wananchi wote kwa ujumla dhidi ya Serikali.
kwa hiyo ni vitu viwili tofauti.

JK ni mwanajeshi wa kweli kimafunzo wakuu sio uamiri jeshi wa kupewa na katiba kama kina ben na mwinyi.
 
Mkuu huko tunisia, misri hakuwezi kuwa model ya TZ,
huku ni ushabiki wa kisiasa na vyama. kule ilikuwa wananchi wote kwa ujumla dhidi ya Serikali.
kwa hiyo ni vitu viwili tofauti.

JK ni mwanajeshi wa kweli kimafunzo wakuu sio uamiri jeshi wa kupewa na katiba kama kina ben na mwinyi.

mkuu hata Ghadafi alikuwa ninja, lakini alipigwa chini vile vile. Kwa hiyo unataka kuniambia kiburi cha mkuu kinatokana na ujeshi wa kweli?
 
Pengine anamsubiri mkuu wa kaya arejee mazikoni amkabidhi barua ya kujiuzulu.
That's my wish and only hope, at the moment.

Ni rahisi ardhi kupasuka na kummeza Pinda kuliko hicho unachotamani kitokee.
 
It is a shame for the Prime minister, he promised to talk the whole issue today, very unfortunitely he did nothing..
I think now it time for Zitto and others to take step ahead. Aibu tupu. Watanznia tuamke maana huu ni uhuni wanafanya, nimeamini maneno niliyosoma jana ya kuwa JK amesema upepo unpita, nafikiri sasa kinakuja kimbunga, sijui atasitahimili? Let us wake up.
 
asilimia 75 ya hotuba nzima ni viongozi kupongezana wakati na hakuna chochote kilichofanyika cha kubadilisha hali ya mwananchi mdogo kule vijijini.
 
Pinda heko mkuu hakuna kama wewe. leo umetoa bonge la show kwa wa TZ waota ndoto za mchana
 
Kila mtu mwenye kutoka jimbo linalowakilishwa na mbunge wa ccm ktk bunge hili anapaswa kuona haya. NI kama usaliti kwa uhai wa Taifa hili.

Mbwa koko, wanabweka lakini hawaumi na serikali yao inajua hivyo.
 
Waziri Mkuu katoa hotuba ya kufunga bunge (Hotuba nzima ipo post ya pili chini).

Hakuna Waziri hata mmoja aliyejiuzulu wala kuwajibishwa kama wengi walivyotarajia.

Spika kahitimisha kwa kuwataka wabunge wasichukiane nje ya Bunge kwakuwa yaliyojadiliwa bungeni ni sehemu ya kazi.

Tulitegemea lipi la ziada. Hivi kweli mlifikiri serikali ya kikwete kuna mtu wa kujiuzuru. Thubutu!!!!!. Mabadiliko yoyote huja kwa aridhi kushiba damu kwanza. Ndiyo kafara ya mabadiliko. Nilifikiri kwamba sisi tunaweza tukavuka stage hiyo bila kumwaga damu. Lakini ukweli ni kwamba tunaenda njia hiyo hiyo kwa sababu ya vibaka wachache wanaofikiri kuwa wameshinda leo, LAKINI KESHO HAWAJUI WATAAMUKAJE. Watanzania wengi wana hasira. Na kwa hakika waliowengi Mungu huwapa. Sisi watanzania si tofauti na wengine.
 
Sisi arusha 2nawasikiliza wakuu wa M4c kutangaza maandamano tutoke,LEMA KAMA VP TUANZIE ARUSHA.Nna hasira mungi
 
Back
Top Bottom