Mvaa Tai
JF-Expert Member
- Aug 11, 2009
- 6,157
- 4,456
Ana Makinda ni Mwanamke:smash:Jana huyu mama wakati akiliahirisha bunge ametoa kauli moja nzito sana ambayo nilitegemea palepale wabunge wote wangeng'aka lkn ikawa kimya.
Makinda alise" ndgugu zangu mawaziri mliosemwa hapa bungeni msichukie na kufika hatua ya kuumia bure, haya yaliyosemwa hapa ni maneno tu na yameishia hapahapa. Msiendelee kuyawaza sana wakati mwingine hata waliowasema wameshaondoka na hata hawayakumbuki"
Ndg. Zangu hii ni kauli inatolewa na spika tena mkuu wa bunge kwamba hawa wabunge wetu ni wapiga porojo tu, wakishatoka hapo yameisha na hata hawakumbuki nini walisema.
MY TAKE: kama wabunge hawataichukulia hatua kauli hii, natangaza rasimi mm sitakuwa na imani na mbunge yeyote tena.