Mhe. Pinda aahirisha Bunge hadi Juni 12, 2012

*ALIPOULIZWA AKACHEKA, MKONO NAE AWEKA SAINIAONDOLEWE, UFISADI MALIASILI UNATISHA
WAKATI wabunge wakiendelea kusaini fomu ya majina ya kutokuwa na imani naWaziri Mkuu, Mizengo Pinda kiongozi huyo wa shughuli za Serikali bungeni janaalikwepa kuzungumzia hatua za kinidhamu dhidi ya mawaziri wanaokabiliwa natuhuma mbalimbali.

Akiahirisha Mkutano wa Saba bungeni Dodoma, Pinda hakugusia suala la kujiuzulukwa mawaziri wanane na badala yake alisema: “Siku zote Serikali imekuwa tayarikupokea ushauri wa Bunge baada ya kusikiliza mjadala na mapendekezo yawaheshimiwa wabunge.’’

Baada ya kuahirishwa kwa Bunge hadi Juni 12, mwaka huu. Pinda akiwa nje yaBunge alikwepa kuzungumzia suala hilo licha ya kubanwa na waandishi wa habarina badala yake alicheka: "Haahaa," kisha akaingia kwenye gari nakuondoka.

Kiongozi wa Kambi rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe alisema kitendo chaPinda kushindwa kuzungumzia chochote kuhusu agizo la wabunge kutaka mawaziriwanane wawajibishwe, kimewaacha wananchi katika hofu.

Alisema Waziri Mkuu ametoa hotuba nyepesi kama vile taifa haliko katika gizakutokana na Bunge kutaka kuwajibishwa kwa mawaziri hao na kuapa kulifikishasuala hilo kwa wananchi.

“Aliahirisha shughuli za Bunge kama hakuna kitu kikubwa kilichohitaji majibu yaSerikali, wananchi walitaka kusikia mawaziri waliotajwa kwa tuhuma za ufisadiwakiwajibishwa lakini, hakuna chochote kilichofanyika. Sasa sisi tutakwenda kwawananachi.

Jumamosi iliyopita, Pinda aliahidi kuwa jana Serikali ingeweka hadharanimsimamo wake kuhusu suala baadhi ya mawaziri kutakiwa kujiuzulu lakinihakutekeleza ahadi yake.

Jana, Waziri Mkuu alisema Serikali itachukua hatua stahiki kuimarisha usimamizina utendaji ndani ya wizara, Serikali za Mitaa na vyombo husika katikakuhakikisha watendaji wake wanafanya kazi kwa umakini.

MAWAZIRI WAZIDI KUBANWA:


Wakati Pinda akikwepa kuzungumzia suala hilo, joto la mawaziri kutakiwakujiuzulu linazidi kupanda baada ya vigogo zaidi kuendelea kusaini fomu yamajina ya wabunge wasiokuwa na imani naye huku viongozi wa dini wakisema sualala mawaziri kung’oka ni la lazima.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti jana, viongozi wa dini walisema kuwa suala lamawaziri hao kujiuzulu halina mjadala na kusisitiza kuwa kuwajibika kwakiongozi kunamjengea heshima katika jamii.

Askofu Msaidizi wa Jimbo Katoliki la Bukoba, Mhashamu Methodius Kilaini alisemakuwa kujiuzulu ni jambo la kawaida na kumtolea mfano Mzee Ali Hassan Mwinyikwamba aliwahi kujiuzulu uwaziri na baadaye akachaguliwa kuwa Rais wa Tanzania…“Kujiuzulu ni heshima siyo aibu… hili jambo mawaziri wote wanatakiwakulitambua.”

Alisema kama ndani ya wizara imeibuka tuhuma na ikathibitishwa kinachofuata niwatendaji wakuu wa wizara husika kuachia ngazi.

Akizungumzia kitendo cha kupishana kwa kauli kati ya Waziri wa Viwanda naBiashara na wa Uchukuzi dhidi ya manaibu wao alisema, “Walitakiwa kuzungumziatofauti zao katika vikao vya chama chao, siyo kujikosha katika vyombo vya habari.”



Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhadi Mussa Salum aliwataka mawaziri haokuacha kujitetea katika mambo ambayo yanaonekana wazi kuwa yanawahusu.

“Hakuna sababu ya waziri kuanza kujiteteta katika jambo ambalo anaonekana wazikuwa anahusika na ndiye mtendaji mkuu wa wizara yake,” alisema Sheikh Salum

Alisema mawaziri hao wanatakiwa kujiuzulu ili kulinda heshima zao hukuakiwataka Watanzania kuwa na utaratibu wa kuwajibika pale wanapoona mambohayako sawa.

Rais wa Baraza la Maaskofu Tanzania (Tec), Askofu Yuda Thadei Ruaichi alisema:“Kama mtu umefanya mabaya kwa nini uendelee kung’ang’ania? Sisitutakachokifanya ni kuwashauri watu kuhusu suala hili ila waondoke kama tuhumazao zipo wazi.”

Mchungaji wa Kanisa la Maombezi, Antony Lusekelo alisema taarifa za Mdhibiti naMkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), inaleza wazi hivyo hakuna haja yamawaziri hao kusita kuwajibika.

Alisema mawaziri hao wanatakiwa kuwajibika kabla ya Watanzania kuamua kuingiamtaani na kufanya maandamano… “Wakati ule wa Richmond kuna ambao waliwajibika.Sasa hawa wanasita kufanya hivyo kwa misingi ipi? Ukimya wao unaipa wakatimgumu CCM.”

KAMATI YAMSHUKIA MAIGE:

Katika hatua nyingine Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili naMazingira imependekeza kuwajibishwa kwa Waziri wa Maliasili na Utalii, EzekielMaige kwa madai ya kutengeneza mazingira ya rushwa katika ugawaji wa vitalu vyauwindaji.

Kamati hiyo chini ya Mwenyekiti wake, James Lembeli pia imependekeza Balozi waTanzania nchini Uganda, Ladislaus Komba achukuliwe hatua za kinidhamu kwa kutoavibali vya kusafirisha wanyama hai kwenda Pakistan kinyume cha sheria.

Wakati akitoa vibali vya kusafirisha twiga wawili, viboko wawili na swala wannekwenda Karachi, Pakistan mwaka 2010, Balozi Komba alikuwa Katibu Mkuu Wizara yaMaliasili na Utalii.

Akisoma taarifa ya kamati hiyo bungeni jana, Lembeli alisema kamati yake piainataka watumishi wote wa wizara hiyo waliohusika kwa namna moja au nyinginekatika kashfa hiyo nao washtakiwe.

Lembeli alisema ugawaji wa vitalu vya uwindaji ulitawaliwa na dosari nyingiikiwamo waziri mwenye dhamana kutangaza majina ya waliopata vitalu bilakuonyesha ni vitalu vipi walipewa na kampuni zisizo na sifa kupewa vitaluhivyo.
Mwenyekiti huyo alisema kampuni tatu, Mwanauta and Company Ltd, Kawawa HuntingSafaris Ltd na Malagarasi Hunting Safaris ziligawiwa vitalu kinyume namapendekezo ya kamati ya ushauri kwamba zisipewe vitalu kwa kuwa hazina sifa.

Katika tuhuma hizo, kamati hiyo imebainisha kuwa Waziri Maige ambaye pia niMbunge wa Msalala, Shinyanga azipatia vitalu kampuni 16 ambazo hazikuomba navingi vya hivyo vikiwa ni vya madaraja ya kwanza na pili.

Lembeli alisema dosari hizo ziliathiri dhana ya uwazi na misingi ya utawalabora na kuashiria kuwapo kwa rushwa hivyo kusababisha malalamiko kutoka kwakampuni nyingine zenye sifa ambazo zilinyimwa vitalu.

“Kamati inapendekeza Bunge liitake Serikali kumwajibisha Waziri wa Maliasili naUtalii, Mheshimiwa Ezekiel Maige kwa kutengeneza mazingira ya rushwa ikiwa nipomoja na kuyanyang’anya vitalu makampuni 16 yaliyogawiwa vitalu bila kuomba,”alisema Lembeli.



MPONDA ASUBIRI RUNGU:

Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Hadji Mponda alisema jana kwamba hatimayake ya kujiuzulu au kuendelea na uwaziri ipo kwa Waziri Mkuu.

Dk Mponda alitoa kauli hiyo alipokuwa akijibu maswali ya waandishi wa habarijuu ya taarifa za kuwa mmoja wa mawaziri wanaotakiwa kuachia ngazi. Alikuwaakizungumza nao kuhusu maadhimisho ya Wiki ya Chanjo na Malaria Duniani.

Alisema amepokea taarifa hizo za kuwa mmoja wa mawaziri wanaotakiwa kujiuzuluna lakini anasubiri uamuzi wa bosi wake.

MKONO ASAINI:

Juzi usiku Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (Nec) na Mbunge wa Musoma Vijijini,Nimrod Mkono, juzi usiku alisaini fomu ya majina ya wabunge wasiokuwa na imanina Waziri Mkuu yanayokusanywa na Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto kabwe.

Zitto alikuwa akikusanya saini za wabunge wasiopungua 70 ambao ni asilimia 20ya wabunge wote ili awasilishe hoja ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu kwaSpika wa Bunge.

Mkono alikuwa ni mbunge wa 74 na wa sita wa CCM kati ya 76 waliosaini fomu hiyohadi jana mchana. Juzi usiku, Mkono alimpigia simu Zitto na kumtaka ampelekeefomu hiyo ili aweke saini yake.

“Mimi ni mjumbe wa NEC na nimepata nafasi hiyo kwa kuchaguliwa na wabungewenzangu wa CCM, sasa ninapoona wabunge wenzangu wakiwemo wa CCM wanalalamikiautendaji wa mawaziri wetu kwa kuhusishwa na ufisadi wa fedha za umma naSerikali inakaa kimya ni lazima nichukue hatua,” alisema na kuongeza:

“Mawaziri wetu hata wafanye kosa gani sisi wabunge hatuwezi kuwawajibisha, nimmoja tu naye ni Waziri Mkuu ambaye tunaweza kufanya hivyo. Sasa tumeona kunamawaziri wamekutwa na kashfa mbalimbali na bado wanang’ang’ani kubaki kwenyenafasi zao hatuna jinsi, ili kuwang’oa nilazima tumuondoe Waziri Mkuu.”

“Sina tatizo na Pinda katika utendaji wake wa kazi lakini hatuwezi kuwaondoamawaziri wenye kasoro bila ya kumwondoa yeye kwa mujibu wa sheria zetu, ndiyomaana nimesaini fomu hii kwa maslahi ya taifa langu.”

WABUNGE CCM WANENA

Baadhi ya wabunge wa CCM wametaka mchakato wa kuwang’oa mawaziri uende mpakakwa watendaji wengine wa Serikali kwa kuwa ndiyo wahusika wakubwa wa matumizimabaya ya fedha za umma.

Wabunge hao walitoa kauli hiyo jana katika kipindi cha Jambo Tanzaniakinachorushwa na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC). Pia walipendekezakutungwa kwa sheria itakayowajumuisha mawaziri na watendaji wakuu wa wizara naidara zinazotuhumiwa katika makosa ya uhalifu.

Mbunge wa Kalenga, Dk William Mgimwa alisema: “Hii siyo njia pekee ya kupambanana vitendo vya ubadhirifu serikalini lakini lazima tuanze na hatua hii yakuwawajibisha mawaziri sababu ndiyo njia pekee ya kurejesha imani ya Serikalikwa wananchi.”

Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina alitaka hadi kufikia kipindi cha Bunge kupitishabajeti, watendaji wa Serikali wanaotumiwa na matumizi mabaya ya Serikali wawewamechukuliwa hatua.

Alitaka makatibu wakuu wa Wizara na idara za Serikali, wakurugenzi wa miji nahalmashauri za wilaya zinazotuhumiwa kwa ufisadi, kabla ya kikao cha Bunge laBajeti la Juni, mwaka huu wawe wamechukuliwa hatua.
 
Katika kuahirisha Bunge, Waziri Mkuu pia alitumia fursa hiyo kuwapongeza wabunge wawili wapya wa CDM. Kwa upande wangu alinigusa zaidi alipompongeza Joshua Nasari na kusema "Wananchi wa Arumeru Mashariki walitumia Demokrasia yao vizuri".

Je, Chaguzi zijazo CCM watasema kuchagua upinzani ni hasara? Je, Serikali imeanza kukubaliana na upepo unavyokwenda? Ama mtu anaweza kufikiri pia kuwa Pinda alipenda chama chake kiangukie pua kule ili kijifunze?
 
Kwa kweli moja ya watu ambao wameumizwa siku ya jana kwa hotuba ya majumuisho/kuhairisha bunge ni mimi,na madhui ya hotuba ile haikuzingatia mijadala/hoja zilizojadiliwa bunge la 7 kwa sababu kwa mfano waziri mkuu anazungumzia ukame ulioikumba baadhi ya wlaya za arusha mwaka 2008 kwenye bunge la 7,matokeo ya kidato cha nne na dalasa la saba,sensa na makazi n.k.ziko wapi hoja za wabunge na kamati mbalimbali za bunge?ina maana waziri mkuu alikuwa hasikii yanayojadiliwa bungeni?kwa nini anawalinda mawaziri ambao wameonekana dhahiri kushindwa kazi?je mh.pinda ataendelea kuwa dhaifu mpaka lini?kwa kweli nimesikiliza ile hutuba ya kuharisha bunge sikusikia jambo jipya hata moja zaidi ya kupata msongo wa mawazo lakini niligundua kitu kimoja haya yote yana baraka za ikulu.
Salva rweyemamu kurugenzi ya mawasiliano ikulu alikanusha juzi rais hajawakingia kifua mawaziri,kwa yaliyotokea jana kwa nini tusiamini ikulu imebariki wizi wa mawaziri?lakini pia kwa nini mkanushe vitu ambavyo viko peupe na kuufanya umma wa watanzania kama mataahira vile wakati watu wanaona na kuelewa mnachokifanya?kikwete kaonekana dodoma nyie mnakanusha,kasema yataisha na kweli ameyamaliza funika kombe mwanaharamu apite.mh.pinda umechoka kazi hivyo achia ngazi tu hakuna unachokifanya zaidi ya wewe kuwa mhimili wa matatizo hata yale ambayo yanaweza kupatiwa ufumbuzi ulio dhahili.
 
Nilisema haya siku zile posts za kuwa eti mawaziri 8 wa serikali ya CCM wamejizuru;nilijua mapema huu ni uzushi tu kwani mawaziri wengi wa sasa wa TZ HAWAWEZI JIUZURU labda wafukwe na Rais na siyo PM!

Kuwa waziri TZ ni dili kubwa ya kutengeneza hela;nani ajiuzuru akose milion 4 kwenye mikutano ya Wizara kwa siku?
 
Back
Top Bottom