Prezidah
JF-Expert Member
- Feb 1, 2013
- 750
- 182
Haeleweki!!
Inategemea uwezo wa kuelewa au kiwango cha uzushi kwenye bongo lako
Haeleweki!!
Huyu ndo anayedauwa kuwa hazina ya taifa! Huyu ni mshenzi kupita washenzi wote kwenye siasa. We umealikwa halafu na wewe unaalika wanachama wa chama ambacho unajifichaficha kuwa mwanachama wake! Shame on you! Ni kama mtu umealikwa kwenye sherehe kwa kadi ya single halafi wewe unabeba na mchepuko kwenda nao! Huu ni upumbavu! Nadhani lipumba aliyekuwa anataka chadema wasuluhishane na zzk ameona kumbe kunguru hafugiki na chadema wamevumilia sana kuwa na type ya kishenzi kama hiyo. Nadhan prof hata amejionea mwenyewe jinsi chadema walivyohangaika na mzigo huoProf. Lipumba akerwa na
Zitto Mtwara.
Prof. Lipumba ambaye ni
wenyekiti wa chama cha
wananchi Cuf amekerwa na
tabia isiyo ya kinidhamu
wala staha iliyofanywa na
mbunge wa kigoma
kasikazini Bwana Zitto
Kabwe,
Katika kikao cha dharula
alichokiitisha usiku ule wa
mkutano baada ya
kumaliza kuhutubia,
alitufokea viongozi wa
Mtwara kuhusu alichokiona
katika mkutano, alisema
aliwaona wanachama wa
ACT-Tanzania wakiwa na
mavazi yao na bendera zao
akahoji kwanini tuliwaalika
wakaja wakiwa na bendera
zao na kuzichomeka
hewani?
Mmoja wetu aliinuka na
kujibu vizuri kuwa wale
vijana tuliwakamata baada
ya kuwaona na bendera
hizo katika viwanja vyetu,
tulipotaka kuwapeleka
polisi mmoja wao
aliyejitambulisha kwa jina
la Kaila alisema yeye ni
afsa habari wa chama
chao taifa,
Akadai kuwa walialikwa na
zitto kuhudhuria mkutano
ule,na wamekuja kwa gari
lake alilowapatia waje
nalo, Mh Mwenyekiti
tunakuomba radhi sana
kwa uliyoyaona pale
uwanjani, wale vijana
hatukuwaita sie,
aliyewaleta toka dar es
salaam ni swahiba wako
uliyeongozana nae Zitto
Kabwe, hata gari
walilokuja nalo ni lake
kawapatia
Lakini pia prof. lipumba
alidai kuwa zitto hana
heshima hata kidogo kwa
sababu tumemwalika sisi
katika jukwaa la chama
chetu, amekosa jukwaa la
kuhutubia siku nyingi, leo
tumempa fadhila lakini
ametufanyia vitimbi,
amekodi mpaka waandishi
wa habri wake bila hata
kuniambia, kumbe hata
wafuasi wake
amewagharamikia waje
wakiwa na bendera na
mavazi ya chama kingine
katika mkutano wetu?
alihoji Prof. Lipumba
Mbona asitumie jukwaa la
hicho chama cha wapambe
wake? ikiwa ana unafiki wa
namana hii basi hafai
kupewa hifadhi kabisa
alimalizia Prof. Lipumba
Tarehe 31/12/2014 chama
cha wananchi cuf kilifanya
mkutano wake katika
viwanja vya mashujaa hapa
mjini Mtwara ambapo zitto
kabwe alikuwa mgeni
mwalikwa, pia watu
wanaodaiwa kuwa wafuasi
wa zitto walivamia
mkutano huo wakiwa na
bendera na mashati yenye
chama kingine ambacho
hakikuwa na makubaliano
ya kufanya mkutano
pamoja na cuf..
Huyu ndo anayedauwa kuwa hazina ya taifa! Huyu ni mshenzi kupita washenzi wote kwenye siasa. We umealikwa halafu na wewe unaalika wanachama wa chama ambacho unajifichaficha kuwa mwanachama wake! Shame on you! Ni kama mtu umealikwa kwenye sherehe kwa kadi ya single halafi wewe unabeba na mchepuko kwenda nao! Huu ni upumbavu! Nadhani lipumba aliyekuwa anataka chadema wasuluhishane na zzk ameona kumbe kunguru hafugiki na chadema wamevumilia sana kuwa na type ya kishenzi kama hiyo. Nadhan prof hata amejionea mwenyewe jinsi chadema walivyohangaika na mzigo huo
We jibu ACT waliamikwa na nani? Cuf waliaka ACT? Au pseudo chairman wa ACT? Jibu basi!Hivi hata kwenye maisha yako binafsi uko hivyo? ??? Taarifa yenyewe marire hajaweka hata chanzo umeshaamini na kufanya judgement. Jamaa kaandika "vijana wanaodaiwa" alafu wewe hata huulizi. Acha kuwa muumini wa mipasho tafuta facts.
We jibu ACT waliamikwa na nani? Cuf waliaka ACT? Au pseudo chairman wa ACT? Jibu basi!
Wewe sio size yangu ngoja niachane na wwNow u are coming to the point hayo maswali ulitakiwa umhoji mleta mada marire kabla hujatoa judgement yako mwambie aweke chanzo hapa. Hapa siyo fb ndo maana unatakiwa uhoji statement za kusadikika "inasemekana" inadaiwa" etc.
Nafahamu vizuri ukoo wao ndiyo jambo la msingi kwao hata pale kariakoo yupo baba yake mdogo ni balaa kwa uchawi ndiyo maana siku moja alijisahau akasema hakuna wa kumgusa kwa madai ya kuwa anatoka kigoma.
Kiukweli Zitto is a political genius, chini ya jua hakuna binadamu hata mmoja asiye na mapungufu, mapungufu ya Zitto ni machache sana kuliko mazuri yake. Tatizo ni kwamba watanzania wengi wamezoea siasa za kinafiki kama ni nyeusi wanataka waambiwe ni nyeupe. Kama kuna mtu mwenye hoja ya kumponda Zitto hapa amuweke mwanasiasa yeyote wa nchi hii na awafanyie comparative analysis kupima mazuri na mabaya ya Zitto na wanasiasa wengine tuone. Zitto ni muhanga tu wa siasa chafu za washindani wake kisiasa wanaoutambua uwezo, nguvu na ushawishi alionao. Zitto ni mfano bora wa kuigwa na wanasiasa wa vyama vyote kwa kuendesha siasa za kiungwana na kistaarabu.
msaliti ni afadhali mchawi upo mkuuAcha tuseme ukweli japo unauma,Mheshimiwa Zitto Kabwe ni hazina muhimu kwa taifa hili.Mheshimiwa huyu ana upeo wa kuona mambo kwa upana wake,Anajua kujenga hoja kwa hoja, Ana uvumilivu, Ni mtaalamu wa demokrasia, Hafanyi mambo kwa kukurupuka, Ana msimamo(Hayumbishwi juu ya kile anachokiamini hata kama kinaleta mgongano wa kimasilahi), Anachukia ukandamizaji na unyonyaji, Ni mwenye kusamehe, Ni muwajibikaji, Ni mzalendo anayeweka maslahi ya Taifa mbele.nk
NB:
Maadui wake kisiasa wanajaribu kila kukicha kuipoteza hazina hii.
- mchawi ..........anaamini katika nguvu za giza----panya panya , Wazee wa kigoma waliomba waende wakamzindike na mengine mengi
- ni mwansiasa ambaye ni msahulifu sana ...............usaulifu wake ni kama wale waadhirika hua anonge, hujichanganya sana katika kauli zake
- Mkanda sana
- Mdaku
- Msaliti--------------mtu anayeandika nyaraka za sirk kwa lengo la kuwapindua viongozi huyo kwako unamwit nani vile?, kwetu huwa twawaita #WASALITI
- Mpenda sifa
- Ndumi la kuwili
- Mla Rushwa
- Mbinafsi
Uzuri wa mshabiki ukifanya jambo zuri anasahau ya jana. Hivi Zitto akirudi chadema utafanya nini we ben. ndera?
Huyu anafaaa kwa maonesho kama twiga vile na simba porini, sio siasa tena. MSALITI WA UKOMBOZI hawezi kuwa hazina
Hilo halina tatizo ila sasa yeye tatizo lake anajiona anajua wakati hajui.Kwani mtu ukijiona unajua na ni kweli unajua kuna ubaya gani?
Unaandika ukiwa umevaa nguo au unataka kutuaminisha wabunge wrote waliochangia walikua wajinga au ndio team pr muongoZito ni mchochezi kama wachochezi wa uasi kwa Serikali kabisaa na ni kwa makusudi haya amekwenda kuyasemea Mtwara na Lindi ambako anajua ni rahisi kutibua nyongo zao na kuibua hasira dhidi ya Serikali wakati akijua anasema uongo. Inashangaza kabisa kwamba Serikali inaumacha aendelee kuichonganisha na wananchi.
Kudhihirisha kwamba Zito ni mchochezi, kwenye Ripoti yake ya PAC iliyopo kwenye tovuti ya Bunge la Tanzania, ukurasa wa 21 inakiri kwamba fedha waliyolipwa PAP ni Sh. 203.1billioni na kwamba fedha iliyokuwa kwenye Escrow Account ni Sh. 306,675,081,939/=
Lakini kwa makusudi kabisa na kwa kuongozwa na nia ya uchochezi ukurasa wa 47 Maoni na Mapendekezo ya Kamati, Ripoti ya PAC umetumia maneno makali ya uchochezi tofauti na ukweli waliouandika wenyewe ukurasa wa 21, ninanukuu "Mfumo mzima wa Serikali ulipata ganzi au uliganzishwa ili kuwezesha zaidi ya shilingi bilioni 306 kuporwa kutoka Benki Kuu ya Tanzania na kutakatishwa kupitia benki mbili hapa nchini"
Kwa mtu yeyote mwenye akili ya kawaida tu, atagundua kwamba kubadilisha matumizi ya neno "iliyolipwa" ukurasa wa 21 kuwa "kuporwa" ukurasa wa 47 na kuamua kutumia kiasi cha fedha ambazo hazikuwemo kwenye Escrow Account, ni mbinu ya kufanya propaganda ya uchochezi.
Zito, alitumia wadhifa wake kama M/Kiti wa PAC vibaya na haiyumkiniki kwa kuhongwa au kuingia kwenye dili chafu ya Standard Chartered Bank iliyotaka kinyemela kuiba fedha za IPTL kwenye Escrow Account kwa kutumiwa na Mkono.
PAC kutolea maamuzi ya uhalali wa SCB wakati kesi ziko mahakamani na kumuandama Mh. Masele, Naibu Waziri wa Nishati na Nadini kwa kumkemea Balozi wa Uingereza kutojiingiza kwenye mambo ya Wizara yake, ni ushahidi tosha kwamba Zito, alikuwa anaongozwa na dhamira ovu na maslahi binafsi, hakutumia hata chembe ya busara. PAC lini imekuwa juu ya Mahakama? Na je, Mh. Masele ni kosa lipi alilokuwa amelifanya kwa kumkumbusha Balozi wa Uingereza kuheshimu mipaka yake ya kazi?
Ni vyema kabisa Serikali ikamuangalia vizuri na kudhibiti hila zake chafu ambazo ziko dhahiri kabisa. Bunge linapaswa kuiangalia kwa makini Kamati ya PAC kwa ilichokifanya kuleta taharuki isiyokuwa na sababu kutokana na uzushi wa Zito. Huyu ni mtu hatari kama Hitla, asipodhibitiwa ataliangamiza taifa.
Tufikirie kwa makini, Zito leo hii ni Mbunge wa mahakama, kwa nini ametengwa na chama chake? Na kama siyo mahakama, basi leo Zito asingelikuwa mbunge CHADEMA waliishamvua nyadhifa zote, ilibaki tu afukuzwe. Hivi kweli huyu ni mtu anayestahili kuaminiwa? Tuache mzaha, Zito hafai katika jamii ya watu Wastaarabu ni mzushi, mchochezi na msaliti.