Mh. Zitto Kabwe ni hazina kwa Taifa hili

Mh. Zitto Kabwe ni hazina kwa Taifa hili

Handsome Boy 2014

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2014
Posts
605
Reaction score
152
Acha tuseme ukweli japo unauma,Mheshimiwa Zitto Kabwe ni hazina muhimu kwa taifa hili.Mheshimiwa huyu ana upeo wa kuona mambo kwa upana wake,Anajua kujenga hoja kwa hoja, Ana uvumilivu, Ni mtaalamu wa demokrasia, Hafanyi mambo kwa kukurupuka, Ana msimamo(Hayumbishwi juu ya kile anachokiamini hata kama kinaleta mgongano wa kimasilahi), Anachukia ukandamizaji na unyonyaji, Ni mwenye kusamehe, Ni muwajibikaji, Ni mzalendo anayeweka maslahi ya Taifa mbele.nk
NB:
Maadui wake kisiasa wanajaribu kila kukicha kuipoteza hazina hii.
 
Na kweli kwa sababu kaanzisha ACT kwa siri na kwa fedha ambazo hazijajulikana amezitoa wapi, kwa nia ya kupanua demokrasia. Lakini sasa ACT imekumbwa na mgogoro anatafuta suluhu ya kurudi chadema. Kweli Zitto ni mzalendo....
 
Hazina nzuri kwa wanafiki wenzake kina Kitila na Mwigamba.

Hazina kwa wapinga mageuzi.

Zitto wa Buzwagi si Zitto wa leo.
 
Dah kumbe ndio maana kila siku serekali inasema hazina haina pesa kumbe ni zzk yuko huko

mwaambieni aache roho mbaya atupe mikopo wanachuo
 
Hazina nzuri kwa wanafiki wenzake kina Kitila na Mwigamba.

Hazina kwa wapinga mageuzi.

Zitto wa Buzwagi si Zitto wa leo.

Unafiki huo ni mpango mkakati uliosukwa na wale wasioitakia mema nchi hii.Kama wameweza kuwawekea sumu wapenda maendeleo watashindwaje kusuka mpango mkakati wa kuangamiza hazina muhimu kwa ttaifa hili.
 
Acha tuseme ukweli japo unauma,Mheshimiwa Zitto Kabwe ni hazina muhimu kwa taifa hili.Mheshimiwa huyu ana upeo wa kuona mambo kwa upana wake,Anajua kujenga hoja kwa hoja, Ana uvumilivu, Ni mtaalamu wa demokrasia, Hafanyi mambo kwa kukurupuka, Ana msimamo(Hayumbishwi juu ya kile anachokiamini hata kama kinaleta mgongano wa kimasilahi), Anachukia ukandamizaji na unyonyaji, Ni mwenye kusamehe, Ni muwajibikaji, Ni mzalendo anayeweka maslahi ya Taifa mbele.nk
NB:
Maadui wake kisiasa wanajaribu kila kukicha kuipoteza hazina hii.

ni kichaa pekee ndo ataweza kukupinga,
 
Kwa hadhi aliyo nayo bin-adam, hastahili kuitwa "hazina" ya taifa au "nyara" ya taifa.
 
Na kweli kwa sababu kaanzisha ACT kwa siri na kwa fedha ambazo hazijajulikana amezitoa wapi, kwa nia ya kupanua demokrasia. Lakini sasa ACT imekumbwa na mgogoro anatafuta suluhu ya kurudi chadema. Kweli Zitto ni mzalendo....

Ukijadili hoja hii kwa misimamo au tetesi za vyama hutapata ukweli.
 
Ninachojua zitto anacho ni uchawi tu ambao kaachiwa na wazazi wake hiyo ndiyo hazina pekee aliyonayo lakii siyo vinginevyo.
 
hoja ni kwamba jamaa ni hazina ya taifa. tuache propaganda juu ya tuhuma ambazo hata hazijawahi kuthibitishwa kwa njia inayoeleweka. jamaa anaweza na anaijua kweli siasa, mpeni moyo lakini pia mumshauri pale inpobidi ili kuipalilia hazina hii

kweli kabisa mkuu, pale penye mapungufu panatakiwa kurekebishwa.Kwasababu sote ni binadamu na kila mmoja ana mapungufu yake.
 
Back
Top Bottom