GE2025 Zitto Kabwe ameyakanyaga kwa Baba Levo huko Kigoma Mjini

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Soka Ndio Maisha Yangu

Senior Member
Joined
Nov 27, 2024
Posts
110
Reaction score
377
KWa mdomo aliokuwa nao Baba Levo ambaye hachagui cha kuongea, Zitto Kabwe kazi unayo.

Wapiga kura wa Tanzania wamebadilika, hawaangalii usomi tena ndio maana wako tayari kumpa ubunge Mr Two a.k.a Sugu au kama walivyompa Ramadhan Kihiyo mwaka 1995 akatenguliwa na mahakama.

Zitto ni msomi sana, hana siasa za majitaka ndio maana wengi wanamtafsiri Kama mamluki, siasa zake zinafanana sana na mwalimu wake Prof Lipumba, hawaamini kuwa ili upendwe na wananchi basi uwe radical Kama Heche au Lissu, wao wamesema no reforms no election cjui 2030 wataendelea na msimamo huo huo maana reforms zilishafanyika, au watavunja chama chao.

Babalevo ana mdomo kama chuchunge, uwezo wa kuongea kuanzia saa 1.00 asbh hadi saa 1.00 jioni utamweka katika wakati mgumu sana Zitto ambaye amepania lazima aende bungeni safari hii.

Ni mpambano wa Simba vs Yanga huu sio mchezo.

Mpambano baina ya Msomi na Asiyesoma, Zito anajua kupanga hoja huku Baba Levo anatifua tifua akiwa na akina Mbosso, Diamond, Zuchu na wasanii wanaofika 300, aisee kazi ipo, saa 5 tu asbuhi Babalevo anasema matokeo yatakuwa yameshatangazwa maana atampiga kipigo cha mbwa koko.
 
Ninachojua mimi Zito chaguo LA watu wa Kigoma.
 
Hilo jimbo ccm watalichukua na act kuachiwa baadhi ya sehem nyingine
 
Makubaliano lazma zzzk aende bungeni Ili kuongoza kambi ya upinzani, pia kuonesha dunia uchaguzi una demokkrasia
 
Back
Top Bottom