Mh. Zitto Kabwe ni hazina kwa Taifa hili

Mh. Zitto Kabwe ni hazina kwa Taifa hili

Zitto angeomba msamaha CHADEMA iwe alifanya usaliti au la angejijengea heshma hata kimataifa.Pia kitendo cha kuipeleka CHADEMA mahakamani nimeonesha dhahili kwa yeye ni mjinga, kiburi na asiependa suruhu. Nafasi bado anayo kama ataomba msamaha bila kujali watu wamchukuliaje au watasema nini?

Ukisimamia tetesi au fikra binafsi za Mwenyekiti,hutatenda haki.Na ujue ktk kuomba msamaha, unaomba msamaha kwasababu umetenda kosa na msamaha huwa ni wa pande mbili.Au unaweza kuomba msamaha bila kosa?
 
Hakuna panya atakabaki.... hashafishiki hata kwa jiki.

Tokwa mapovu tu hapa, tunamjua. Muandalieni tena press conference na mapokezi makubwa kigoma.

Mkuu tusisimamie mpango mkakati,kwani hata kesho na keshokutwa unaweza kusukwa ili kuangamiza mwingine na tukajikuta tunazidi kupoteza viongozi muhimu kwa Taifa letu.
 
Huwezi kuishi kinafiki nafiki kama zitto then utegemee kufanikiwa kisiasa,haeleweki kama popo,cdm hayupo wala act hajulikani! Hivi tukikuuliza wewe mleta mada,huyo bwana wako zitto yupo ccm,cdm,cuf au act utajibu nini?

Kinachomfanya asieleweke kwasasa ni kwasababu ya mpango mkakati ambao umesukwa ili kumuangamiza kisiasa.
 
Okay nimejaribu kutoa taswira ya jumla then kwa sababu mada inamhusu nikamtolea mfano. Sasa kama unamjua vizuri weka hapa unachojua then niambie huyo ambae wewe unamjua ni msafi mi nikuwekee data zake hapa.
Hata kusoma lugha ya picha huwezi?

Utakuwa umekosea jukwaa mkuu,

Zitto wa buzwagi si Zitto wa leo.
 
Zito ni mwongo na mnafiki sana! ni hatari kumwamini. Na nashangaa anaendelea kuhubiri uongo kule lindi na mtwara. nimejua pia ni mwepesi kutumiwa na maadui wa nchi n kutuangamiza. Namuuliza standard chartered Bank wamempa ngapi?

Mkuu, madai haya yote yamekuwa yakirudiwa rudiwa bila uthibitisho.Zaidi ni mpango mkakati uliosukwa ili kumuangamiza.
 
Tatizo la zitto si mtu wa msimamo kiongozi mziri lazima aoneshe msimamo

Zitto ni mbunge kupitia chadema, amefanyiwa fitina ya kutaka kuvuliwa uanachama akaenda mahakamani kwenye haki. Lakini alishasema hadharani kwamba atakuwa wa mwisho kuondoka chadema. Ni muumini wa demokrasia ya kweli, ya ukweli na siasa safi. Unataka msimamo gani zaidi ya huo? punguzeni ushabiki acha kuamini uzushi. Siasa ni mchezo mchafu.
 
Hata kusoma lugha ya picha huwezi?

Utakuwa umekosea jukwaa mkuu,

Zitto wa buzwagi si Zitto wa leo.

Najua mshabiki wa simba hawezi kuhamia yanga hata ishuke daraja and that's the worst thing about being a fun. One day utakuja kujua ukweli
 
Tunachukia viongozi wazuri sababu ya vyama na vyama hivi hivi ndiyo vinatufanya kushabikia viongozi hata wasiostahili.
 
Huyu anafaaa kwa maonesho kama twiga vile na simba porini, sio siasa tena. MSALITI WA UKOMBOZI hawezi kuwa hazina
 
Kiukweli Zitto is a political genius, chini ya jua hakuna binadamu hata mmoja asiye na mapungufu, mapungufu ya Zitto ni machache sana kuliko mazuri yake. Tatizo ni kwamba watanzania wengi wamezoea siasa za kinafiki kama ni nyeusi wanataka waambiwe ni nyeupe. Kama kuna mtu mwenye hoja ya kumponda Zitto hapa amuweke mwanasiasa yeyote wa nchi hii na awafanyie comparative analysis kupima mazuri na mabaya ya Zitto na wanasiasa wengine tuone. Zitto ni muhanga tu wa siasa chafu za washindani wake kisiasa wanaoutambua uwezo, nguvu na ushawishi alionao. Zitto ni mfano bora wa kuigwa na wanasiasa wa vyama vyote kwa kuendesha siasa za kiungwana na kistaarabu.
 
hakuna ubishi katika vijana wanaotegemewa na taifa hili zito ni mmojawapo anajiamini, anajua kujenga hoja thabiti japo ana mapungufu km mwanadamu lkn ni kijana ambaye anaweza kusimama popote duniani akazungumza na kuiletea sifa Tanzania.
 
kuna wakati ukijifanya mkombozi wa watanzania unaweza kukimbia kichaa......unaowakomboa wanakugeuka; sijuia zitto akiamua kuendelea na maisha yake ana hasara gani??
 
Prof. Lipumba akerwa na
Zitto Mtwara.
Prof. Lipumba ambaye ni
wenyekiti wa chama cha
wananchi Cuf amekerwa na
tabia isiyo ya kinidhamu
wala staha iliyofanywa na
mbunge wa kigoma
kasikazini Bwana Zitto
Kabwe,
Katika kikao cha dharula
alichokiitisha usiku ule wa
mkutano baada ya
kumaliza kuhutubia,
alitufokea viongozi wa
Mtwara kuhusu alichokiona
katika mkutano, alisema
aliwaona wanachama wa
ACT-Tanzania wakiwa na
mavazi yao na bendera zao
akahoji kwanini tuliwaalika
wakaja wakiwa na bendera
zao na kuzichomeka
hewani?
Mmoja wetu aliinuka na
kujibu vizuri kuwa wale
vijana tuliwakamata baada
ya kuwaona na bendera
hizo katika viwanja vyetu,
tulipotaka kuwapeleka
polisi mmoja wao
aliyejitambulisha kwa jina
la Kaila alisema yeye ni
afsa habari wa chama
chao taifa,
Akadai kuwa walialikwa na
zitto kuhudhuria mkutano
ule,na wamekuja kwa gari
lake alilowapatia waje
nalo, ‘’Mh Mwenyekiti
tunakuomba radhi sana
kwa uliyoyaona pale
uwanjani, wale vijana
hatukuwaita sie,
aliyewaleta toka dar es
salaam ni swahiba wako
uliyeongozana nae Zitto
Kabwe, hata gari
walilokuja nalo ni lake
kawapatia’’
Lakini pia prof. lipumba
alidai kuwa ‘’zitto hana
heshima hata kidogo kwa
sababu tumemwalika sisi
katika jukwaa la chama
chetu, amekosa jukwaa la
kuhutubia siku nyingi, leo
tumempa fadhila lakini
ametufanyia vitimbi,
amekodi mpaka waandishi
wa habri wake bila hata
kuniambia, kumbe hata
wafuasi wake
amewagharamikia waje
wakiwa na bendera na
mavazi ya chama kingine
katika mkutano wetu”?
alihoji Prof. Lipumba
‘Mbona asitumie jukwaa la
hicho chama cha wapambe
wake? ikiwa ana unafiki wa
namana hii basi hafai
kupewa hifadhi kabisa’
alimalizia Prof. Lipumba
Tarehe 31/12/2014 chama
cha wananchi cuf kilifanya
mkutano wake katika
viwanja vya mashujaa hapa
mjini Mtwara ambapo zitto
kabwe alikuwa mgeni
mwalikwa, pia watu
wanaodaiwa kuwa wafuasi
wa zitto walivamia
mkutano huo wakiwa na
bendera na mashati yenye
chama kingine ambacho
hakikuwa na makubaliano
ya kufanya mkutano
pamoja na cuf..
 
Zitto ni mbunge kupitia chadema, amefanyiwa fitina ya kutaka kuvuliwa uanachama akaenda mahakamani kwenye haki. Lakini alishasema hadharani kwamba atakuwa wa mwisho kuondoka chadema. Ni muumini wa demokrasia ya kweli, ya ukweli na siasa safi. Unataka msimamo gani zaidi ya huo? punguzeni ushabiki acha kuamini uzushi. Siasa ni mchezo mchafu.

Kweli kabisa mkuu ZZK ana msimamo na ni mzalendo.....maadui wake wa siasa ndo wanamchafua
 
Back
Top Bottom