Mh. Wenje umenitukania baba yangu

Mh. Wenje umenitukania baba yangu

Baba yangu namtambua vyema ni miongoni mwa wazalendo wachache waliobaki ktk nchi hii.
Siamini kama chukula chaweza kumfanya abadili misimamo yake.

Baba ako kanunuliwa kwa ubwabwa atetee kura ya wazi.
 
kweli wale wenye njaa tu ndio wanalalamika. mbona prof safari, mahalu, lipumba, mtatiro, mtikila na wengine hawajalalamika?
ni baadhi ya wajumbe wachache wenye njaa za ubwabwa kama baba ako ndio wanalalamika
 
nadhani ungemlaumu babako kwa kukubali mwaliko na kula ubwabwa. wenje hajakosea maana kasema ukweli. sana mwite babako aje kulalamika yeye kama kaonewaaaa
 
Sikupenda ule ushabiki wa hoja aliounyesha Wenje, jinsi alivyofoka na kufurahia hisia za unyonge waliopata baadhi ya wabunge wateule. Sikupenda, LAKINI Wenje alikuwa na ujumbe MZITO SANA.

Madai ya Wenje ni uwepo wa vikao haramu vikiongozwa na viongozi wa serikali ambao wamekuwa wakiwapiga msasa hawa wabunge! Hii ndio tatizo. Dr Kawambwa - alitaka kulia huyu- alivyokuwa anajieleza kwamba yeye hakuwaita bali watu wale kutoka kwenye taasisi za elimu waliomba kukutana naye. Inawezekana huyu rafiki yangu anasema kweli, lakini Shukuru amekuwa anatumiwa- yeye sio mwanasiasa- lakini kutokujua kusema HAPANA ndio kunamtesa. Inawezakana sana baadhi ya haya mapandikizi ndani ya kundi la 201 ndio wamemponza kwa kuhamasisha wenzao waende kwa waziri naye akawakubalia. Agenda za huko nyumbani kwa mawaziri hawa ndio alizokuwa anazilenga Wenje.

Kwa nini makundi kama haya yasikutane kwenye uwazi na mchana, maana kazi za Bunge ni aidha jioni kuanzia saa 10 au saa 4 had 7. Kama agenda ni za wazi wangekutana ndani ya majengo ya bunge tuseme saa 2-4, au 8-10. Mbona inawezekana. Lakini pongezi Prof Jumanne -- yeye alikiri kukaribisha na kuwakarimu! Yote ni mamoja tu, ni jinsi ya kuchochea fikira. Na ndugu zangu wengine kina Dr Michael Francis- ni muhimu wakaelewa wametumwa na taasisi zao na wala sio kwenda kufanya makundi kwa kujikusanya kwa wanasiasa! Mtachafuliwa.

Nilimsikitikia sana yule Mama wa Kimasai maana hakujua kinachoendelea. Ulikwenda kupigwa msasa Mama na umeshapigika na kwa kuwa hukuwa na shida na vijisent vyao kwa sababu una vyakula na mifugu ya kutosha, walikufaidi kikweli kweli. Umekuwa mfuasi wao kwa gharama ndogo sana. Kwa lugha nyingine UMEJIUZA! Wenje alikuwa sahihi lakini lugha ndio shida hasa kwa ndugu zangu wa kipande kile cha Wenje
hebu ifike wakati beleshi liitwe beleshi na sio kijiko kikubwa (lets call a spade a spade, not a big spoon)
 
Suala la rushwa linaeleweka kabisa,jaman ubwabwa ni rushwa,,,wala hilo halina kificho,msimung'unye maneno hapa,
Kuna mtu mliwai kumripot hapa kuwa aligawa rushwa ya VITUMBUA KULE NZEGA,-NIMEMSAHAU JINA,,,,ila ile nayo ni rushwa
 
Huyu anasumbuliwa na "mtoto wa nje syndrome"...hajapata malezi ya kutosha ya wazazi na hasa upande wa baba..kwa hiyo hamuelewi vizuri babake...yeye anamwona booonge la baba...kumbe babake bei poa tuu sahani ya wali unampindua akili anaanza kufuata ya maboss wake.

Angalizo:- hujachelewa bado kumfahamu vizuri babako...omba ruhusa kwa mamako ukakae na babako muzidi kufahamiana vizuri na hasa tabia yake ya kurubuniwa kirahisi na vitu kama wali, pilau, vitumbua na hata nyama choma na bia.

Aibuuuuu...yani huyo mroho wa wali ni babako?....kweli mwanaume hasifiwi kula...babako anasifiwa kula tena wali saa 7 usiku?
 
Ushauri wangu kwako inabidi tu uandamane hadi bungeni no way out Makamee.
 
Last edited by a moderator:
Who cares, sipendi matusi yako kua mstaarabu ndugu yangu.
 
Kwako muheshimiwa Wenje tafadhali niombe radhi.

Nimekusikia jana ukieleza bungeni kwamba wale wajumbe 201 wa bunge maalum la katiba wamepewa rushwa ya chakula na vinywaji.

Baba yangu nae miongoni mwao. Kweli baba yangu mzazi kabisa adanganyike na kitu kidogo kama chakula?
Kwangu hili tusi kwa mzazi wangu.

Mh,WENJE kauli zako zinaudhi

tatizo baba yako kaiwekea njaa yake fence. Safi sana wenje mtukanane na huyu mwanafisadi...
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom