Mh. Wenje umenitukania baba yangu

Mh. Wenje umenitukania baba yangu

We mbulula kweli sio wajumbe wote 201 wamekula rushwa ni baba yako na wenzake tu wachache.Msosi wa kuzamia mtamu kuliko anaopika bimkubwa wako nyumbani.Upo?
 
Siasa zitakupandisha presha! Acha hivyo hivyo as far as babako hakucomment nafikiri limekuta wengi siyo yeye peke yake
 
Wenje amefanya unafiki na kutaka kujionesha kwamba ana msimamo mkali kwenye tv. Mimi nimeishi na waheshimiwa hawa hapo site ii area D Dodoma na nilichojifunza ni kwamba wabunge bila kujali vyama vyao wenyewe ni marafiki wakubwa, wanakula, kunywa pamoja. Je yeye Wenje hajawahi kukirimiwana mbunge wa CCM au mbunge wa chadema kumkirimu wa CCM. Je hii nayi ni rushwa Wenje. Acha kuwakashifu wenzio kuwafanya wana njaa sana wakati kuna wajumbe wana ukwasi zaidi yako.
 
Angesema wamepewa kila mmoja shs. 10m ungelalamika? Ubwabwa umemponza baba yako. Aibuuuuuuu
 
Ushahidi gani unaohitaji hukuona jana Wenje anavyowadhalilisha wajumbe wa 201?

Hakuna cha kudhalilisha aliwapa walichostahili, wao ni wawakilishi wa wananchi wanakwenda nyumbani kwa waziri usiku hadi saa saba? Kama siyo kwenda kufundishwa cha kusema ni nini? Tunamshukuru sana mh Wenje kwa kuwaumbua hao machumia tumbo.
 
Kwanini umedhani babaako ndo alikua mlengwa? Kuna ukweli hapo
 
Wenje amefanya unafiki na kutaka kujionesha kwamba ana msimamo mkali kwenye tv. Mimi nimeishi na waheshimiwa hawa hapo site ii area D Dodoma na nilichojifunza ni kwamba wabunge bila kujali vyama vyao wenyewe ni marafiki wakubwa, wanakula, kunywa pamoja. Je yeye Wenje hajawahi kukirimiwana mbunge wa CCM au mbunge wa chadema kumkirimu wa CCM. Je hii nayi ni rushwa Wenje. Acha kuwakashifu wenzio kuwafanya wana njaa sana wakati kuna wajumbe wana ukwasi zaidi yako.

Hiyo ipo kwani siasa siyo vita na uhasama, lakini wenje mazungumzia ktk hali kama hii ya katiba kwani inahitajika kila upande kuwa na mtaji wa wapiga kura, na lazima ujue hao wajumbe ni kwanini wamepelekwa hapo bungeni! Siyo unaangalia mbele tu mzee.mimi nipo hapa dodoma naona hali ilivyo.
 
hivi mipaka ya rushwa ni ipi? hizo laki tatu si mtego huo huo na wote wamo!!
 
Sikupenda ule ushabiki wa hoja aliounyesha Wenje, jinsi alivyofoka na kufurahia hisia za unyonge waliopata baadhi ya wabunge wateule. Sikupenda, LAKINI Wenje alikuwa na ujumbe MZITO SANA.

Madai ya Wenje ni uwepo wa vikao haramu vikiongozwa na viongozi wa serikali ambao wamekuwa wakiwapiga msasa hawa wabunge! Hii ndio tatizo. Dr Kawambwa - alitaka kulia huyu- alivyokuwa anajieleza kwamba yeye hakuwaita bali watu wale kutoka kwenye taasisi za elimu waliomba kukutana naye. Inawezekana huyu rafiki yangu anasema kweli, lakini Shukuru amekuwa anatumiwa- yeye sio mwanasiasa- lakini kutokujua kusema HAPANA ndio kunamtesa. Inawezakana sana baadhi ya haya mapandikizi ndani ya kundi la 201 ndio wamemponza kwa kuhamasisha wenzao waende kwa waziri naye akawakubalia. Agenda za huko nyumbani kwa mawaziri hawa ndio alizokuwa anazilenga Wenje.

Kwa nini makundi kama haya yasikutane kwenye uwazi na mchana, maana kazi za Bunge ni aidha jioni kuanzia saa 10 au saa 4 had 7. Kama agenda ni za wazi wangekutana ndani ya majengo ya bunge tuseme saa 2-4, au 8-10. Mbona inawezekana. Lakini pongezi Prof Jumanne -- yeye alikiri kukaribisha na kuwakarimu! Yote ni mamoja tu, ni jinsi ya kuchochea fikira. Na ndugu zangu wengine kina Dr Michael Francis- ni muhimu wakaelewa wametumwa na taasisi zao na wala sio kwenda kufanya makundi kwa kujikusanya kwa wanasiasa! Mtachafuliwa.

Nilimsikitikia sana yule Mama wa Kimasai maana hakujua kinachoendelea. Ulikwenda kupigwa msasa Mama na umeshapigika na kwa kuwa hukuwa na shida na vijisent vyao kwa sababu una vyakula na mifugu ya kutosha, walikufaidi kikweli kweli. Umekuwa mfuasi wao kwa gharama ndogo sana. Kwa lugha nyingine UMEJIUZA! Wenje alikuwa sahihi lakini lugha ndio shida hasa kwa ndugu zangu wa kipande kile cha Wenje
 
hivi mipaka ya rushwa ni ipi? hizo laki tatu si ndio mpango huo huo na wote wamo ndani!!!
 
Kwako muheshimiwa Wenje tafadhali niombe radhi.
Nimekusikia jana ukieleza bungeni kwamba wale wajumbe 201 wa bunge maalum la katiba wamepewa rushwa ya chakula na vinywaji.
Baba yangu nae miongoni mwao. Kweli baba yangu mzazi kabisa adanganyike na kitu kidogo kama chakula?
Kwangu hili tusi kwa mzazi wangu.

Mh,WENJE kauli zako zinaudhi

Kwahiyo baba yako anaweza kudanganyika na kitu gani kama unaona kwa hadhi yake hawezi kudanganyika na kitu kidogo kama chakula? Unajuaje kama baada ya chakula aliondoka na bahasha yake nzuri tu ambayo muda si mrefu utaona mabadilko hapo nyumbani ya ukarabati au kagari kapya au na hata akipendezwa akakuongezea mama mdogo? Wewe mwambie babako kama ni msosi asiuache na bahasha achukue kama kawaida lakini atakachoambiwa achanganye na za kwake kama yule Kong'ota wa JK
 
Baba yangu namtambua vyema ni miongoni mwa wazalendo wachache waliobaki ktk nchi hii.
Siamini kama chukula chaweza kumfanya abadili misimamo yake.

Na wewe inaonyesha ukipewa rushwa unatoa.........
 
Kwako muheshimiwa Wenje tafadhali niombe radhi.
Nimekusikia jana ukieleza bungeni kwamba wale wajumbe 201 wa bunge maalum la katiba wamepewa rushwa ya chakula na vinywaji.
Baba yangu nae miongoni mwao. Kweli baba yangu mzazi kabisa adanganyike na kitu kidogo kama chakula?
Kwangu hili tusi kwa mzazi wangu.

Mh,WENJE kauli zako zinaudhi

Kwahiyo Mshua wako alikula? nauliza bcoz mwenyeji amekubali hadharani kua kawalisha na pia amewakarimia kama ilivyo desturi yetu waTZ. mbona hujiulizi kabla Baba yako kwenda huko bungeni alishaitwa na nani kwa ukarimu tu ktk chakula?? na je ni watanzania wangapi ata random tunaitwa kwa chakula na mawaziri tu kwa ukarimu. I am sorry to say inawezekana baba yako ndo anayetutukana WaTZ kwa kushiriki milo isyo kua na faida kwa waTZ.
Hongera Wenje kwa kutufungua macho. Hua tunalalamika watu vijijini wandanganywa kwa pilau kumbe hata watu walioteuliwa kutuwakilisha wanaweza danganywa kwa pilau. This is extremely low for those who ate.....very low ...very very low lower than I thoght was possible. Binafsi wameniangusha sana.

Nota bene: Rushwa haimanishi kumpa mtu kitu ambacho yeye hawezi kukipata, kama huyo aliyedai ana ngombe 3000, ila unaweza ukawa na uroho wapilau au chips samaki wakati huo ngombe zako zipo arusha hazikusaiidi kukata kiu ya samaki.:A S 13:😛izza:😛izza:😛izza:😛izza::tape:
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom