Planner
JF-Expert Member
- Apr 5, 2011
- 348
- 148
Hapo kwenye red colour, angalia sana usije ukawa umenasa kwenya ntego wa unafiki wa hali ya juu sana.
Kabla ya kuandika hayo hapo kwenye red colour, ulitakiwa kufanya utafiti uone kama kweli katika nchi hii ya Tanzania jambo hili linafanyika, au ni theory tu inayotumika ili kunyonya wafanyakazi.
Kifupi hali katika Tanzania yetu hii iko hivi:-
- pension schemes sio kwa ajili ya kukusaidia utakapo kuwa mzee, ila ni kwa ajili ya kukusanya pesa kwa ajili ya matumizi ya serikali, mfano, wafanyakazi wa iliyokuwa jumuiya ya afrika mashariki, wote sasa ni wazee, hebu niambie wanalipwa pension kiasi gani ???
- je?, unajua pension wanayolipwa wastaafu kwa sasa ??? mfano, aliyewahi kuwa mkuu wa majeshi Tanzania, kwa sasa ni mstaafu anayelipwa Tzs. 50,000 (Tzs. elfu hamsini tu) kwa mwezi. Hii inamsaidiaje yeye kama mzee mstaafu.
Angalizo kwa wote:
Kabla ya kutoa maoni kwenye mada nzito kama hii ya maswala ya pension, fanya utafiti kwanza, vinginevyo, wewe ni mnafiki tu, au wewe pia ni mmoja wa wanaofaidika na udhalimu huu wa kunyima wafanyakazi haki yao ya mafao.
Be blessed, Naanza kuamini kuwa wananchi tumeshajua kuwa maisha yetu yako mikononi mwetu,no one cares for our future,labda hao SSRA wangetuambia vp thamani ya fedha uliyoweka kwa kipindi hicho itakuaje ukizingatia kuwa shilingi yetu inaporomoka kila uchao,pia kwa jinsi wastaafu wetu wanavyonyanyasika hadi sasa sijaona vivid example ya kujustify hicho kiini macho cha kuwa eti 'wanaamini hiyo pensheni itakusaidia',pia nataka suala la mfuko upi ujiunge nalo liwe kwa mtumishi manake mwajiri anakuamualia yeye na huna choice! wote wenye kudhani watatudanganya milele muda wao umekwisha, sema hapana kwa unafki na wizi wa jasho la wafanyakazi !