....Mimi nafkiri, badala ya kutaka kifungu cha mafao ya kujitoa kirudishwe na hivyo kujihakikishia kuona vurugu za wazee mitaani kama wale wa jumuiya ya afrika mashariki siku za usoni. Ni bora tukaacha sheria ibaki kama ilivyo(kwa maana ya kuzuia mafao ya kujitoa) ILA iongeze kifungu kitakachomtaka mwajiri awe na scheme ya kuchangia wafanyakazi ambayo ni over and above the basic pension scheme, ambayo mtu ataweza kuacess fedha zake pale atakapoacha kazi....
Niishie hapo, naomba tujadili bila matusi.
Nina uhakika utakuwa umetumwa ww si bure, na ufie mbali na upuuzi wako! Mfano mzuri umeutoa ww mwenyewe na bado unatetea upuuzi huo, je Wazee wa Africa Mashariki wanahangaikia fao la kujitoa au pension? na je wanachokiadai kitawasaidia kuwa na maisha bora kwenye umri wao kwa sasa?
Ndio maana nakuambia wewe ni mpuuzi usiyestahili kupuuzwa! Pamoja na point ulizoelezwa huko juu na kujifanya mbishi jaribu kufuatilia yafuatayo pia;
1. Fahamu kwamba sifa ya kupata pension si kufikisha miaka 55 pekee bali kuna sharti ya idadi ya michango ie NSSF ni lazima angalau uchangie michango 180 (miaka 15), je unafahamu kwamba ni chini ya asilimia 20 tu ya watanzania wanaweza kudumu kwenye ajira kwa muda wote huo (hasa sekta ya madini) kwa sababu mbali mbali km vile kampuni kufirisika (maana mdororo wa uchumi ukitokea sekta ya madini ndio ya kwanza kuathirika), madini yenyewe kuisha na mgodi kufungwa, kufukuzwa kazi (kuna sababu nyingi sana huku za kufukuzwa kazi mfano kuangusha gari kama ajali), kupata magonjwa sugu (silicosis, magonjwa ya mapafu kwa watu wa underground, ukimwi nk) na kuwa declared unfit, na mengineyo mengi tu. Na kumbuka ukifukuzwa kazi wana mtandao wao wa kuwasiliana ili usipate kazi kwingine kokote ndani ya tanzania, hili serikali na watu wenye akiri finyu kama wewe hamjawahi kuliona mnafikiri naendekeza mambo ya serikali ya Kuiba mabilioni ya fedha na unahamishwa kituo tu.
2. Kwa kutumia mfano wako huo huo; naweza nikafanya kazi miaka 8 (nikiwa na umri wa miaka 35) nikaachishwa kazi baada ya kukosa nguvu ya kazi kwa sababu ya maradhi, nitalazimika kusubiri kwa muda wa miaka 15 ijayo ndo niweze kupewa michango yangu (maana sina sifa ya kulipwa pension kwa sababu sijafikisha miaka 15), kama nitajikongoja nifike huo umri (maana wengi watakufa kabla ya kufikia umri huo) nitaenda nikapewe vimchango vyangu ambvyo kwa wakati huo vitakuwa havina msaada mkubwa kwangu kwa wakati huo maana mfumuko wa bei utakuwa umetafuna samani yake kwa asilimia kubwa sana.(Mfano ni mzee wa East Africa aliyesafiri kutoka Mwanza hadi Dar kwa gharama ya 35,000/= nauli na alipofika akalipwa penseni ya 1,500)
Naomba niishie hapo maana nadzidi kupata hasira na watu kama ww ambao mnafikiri dunia ya leo bado ni ya wajinga mnaoweza kuwaibia pesa zao mnavyotaka; mmeiba twiga, mmeiba matrilioni ya shilingi na kuweka kwenye mabenki ya nje, mmeiba EPA na mengine mengi bado mnakutaka hata vya mifukoni mwetu...............huo upuuzi hatuutaki Mnyika bravo