Mh. Mnyika kwa hili umepotoka!... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mh. Mnyika kwa hili umepotoka!...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Sober, Aug 4, 2012.

 1. Sober

  Sober JF-Expert Member

  #1
  Aug 4, 2012
  Joined: Jun 6, 2008
  Messages: 289
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Mh. Mnyika siku zote nimekua namuona ni mbunge makini sana na anayejishughulisha kujua mambo.

  Lakini kwa hili la kutaka sheria ipitiwe upya na kurudisha mafao ya kujitoa naona amepotoka sana. Nashawishika kuamini kuwa nayeye kwenye hili ameingia kwenye mkumbo wa kusaka cheap popularity kwenye mambo ya kitaalamu zaidi. Najua nitashambuliwa kwa mtizamo huu ila nieleze sababu za mtizamo huu wangu.

  Kwanza, katika nchi zote za Afrika kusini mwa Jangwa la Sahara, hakuna kitu kinaitwa mafao ya kujitoa kwa mfuko wowote wa pensheni. Hiki kituko kipo hapa Tanzania tu na chanzo chake ni wanasiasa wa aina za mh. Mnyika wanaokua tayari kuweka maisha ya maelfu ya wazee wa miaka ijayo kwenye maisha ya dhiki na hivyo kufa mapema baada ya kustaafu kwa ajili ya umaarufu wao(wanasiasa) wa mpito.

  Pili, ukiondoa PPF na NSSF, Tanzania ina mifuko mingine pia, nayo ni LAPF, PSPF na ZSSF, huko kote hakuna hilo fao la kujitoa na halikuwahi kutolewa. Mtu ukiacha kazi hata baada ya miaka 15 ukapata kazi kwenye private sector, utatakiwa kurudi kwa ajili ya mafao yako pale tu umri wako utakapofika miaka 55 au 60.

  Tatu hili jambo la kutumia "ujinga" wa watu(nikimaanisha kutojua sekta hii vizuri) ili kujitengezea umaarufu wa mpito ndio jambo ambalo kizazi hiki kilianza kuonekana kuchoshwa nacho, lakini Mh. Mnyika anaonekana kurudia kosa lilelile la kutumia "ujinga" wa watu kujinufaisha. Kumwambia mtu ajitoe at 46yrs ni kumhakikishia uzee usiokua na uhakika wa staha. Mheshmiwa hebu pita BRELLA wakupe data za biashara zinazofunguliwa kwa mwaka, halafuna baada ya miaka mitano asilimia ngapi ya hizo biashara bado zinakuwepo sokoni. Nakuhakikishia utaweza kuanguka kwa mshtuko! Kuna data inaongelea 67% ya biashara mpya zitapotea sokoni ndani ya miaka mitano. Hivyo kusema watu watajifungulia biashara ni wishful thinking ambazo kila mtu yupo entitled kuwa nazo, ila we need a reality check hapa. Huwezi kuwa mwajiriwa miaka nenda rudi halafu siku ukapewa bulungutu, bila kuwa na basic entrepreneurial skills ukategema kusurvive sokoni.

  Nne, hii hadithi ya kupotosha ya Life Expectancy ya mtanzania ni miaka 53. Ni kweli Life expectancy ni miaka 53, ila ukokotaoji wake unapatikana kwa average ya vifo vyote nchini kwa mwaka. sasa kwa nchi kama yetu ambapo kuna vifo vingi sana vya watoto chini ya umri wa miaka mitano, si ajabu vikashusha life expectancy at birth. Lakini kama life expectancy ingetazamwa wakati wa umri wa kuanza kazi, say 20yrs, utakuta watanzania wengi wanafika miaka 65 na kuendelea... Hivyo si sahihi kusema watu wanakufa at 53 halafu mafao yatatolewa at 55yrs( hapa naona kuna gap kubwa mno ya uelewa wa hii concept).

  Hivi mh. Mnyika anajua kuwa kwa kung'ang'ania kurudishwa kwa mafao ya kujitoa ni kuwaumiza wafanyakazi kuliko kama wangesubiri pensheni? Chukulia mfano, mtu aliyeanza kazi na miaka 25, akatumika kwa miaka 20. Atakuja kulipwa mafao ya kujitoa kwa kutizama kilichopo kwenye account yake kama kilivyo!!!... inawezekana kabisa huyu mtu kipato chake kilipanda sana ndani ya miaka mitano ya mwisho kutokana na experience, lakini kitakacholipwa ni kilichopo kwenye account yake kama kilivyo. Hapa utakuta kuna miaka ile 15 ya mishahara midogo akiwa bado junior officer ndio atakayojumlishiwa kama ilivyo na hii miaka mitano ya mishahara mikubwa. Wakati kama angekuwa ni wa kupokea pensheni angelipwa kufuatana na mishahara yake ya miaka ya mwisho kabla hajastaafu, ambayo mara nyingi ndiyo mikubwazaidi katika career ya mtu. Sijui mheshmiwa unalisemeaje hili...

  Ukiwa kijana na nguvu zako, siku zote unaona kama kuwa mzee na kikongwe ni kitu cha mbali sana na kwamba unaweza kujipanga vizuri ili usizeeke kwa dhiki. Lakini ni muhimu tujiulize mh. Mnyika, kama ukiwa na nguvu na mshahara wako unachukuliwa asilimia 5% kwa ajili ya akiba ya uzeeni. Kwanini basi ushindwe kujipangilia maisha kwa hiyo asilimia 95% unayobakiwa nayo? Jamani tusipende cheap popularity, tuwawaingiza watanzania wenzetu kwenye dimbwi la dhiki wakati wa uzee, ambapo hata nguvu za kujishughulisha zimekwisha.

  Hivyo ni vyema Mh. Ukakaa na wataalam wa kwenye hii mifuko, na hasa wataalamu wenye kufanya tathmini za mifuko ya pensheni na ujue kiundani nini hasa maana ya mifuko ya pensheni. Malengo na madhumuni yake. Ni vizuri na huwa nafarijika sana ninapoona mwanasiasa kijana akijishughulisha kutaka kujua mambo yanayokua ya kitaalam kwa kukaa na kujifunza kwa wataalam badala ya kuzunguka kusaka saini za wanasiasa wenzake ili kurudisha nyuma juhudi za muda mrefu za wataalam, wenye nia safi ya kuweka safety net kwa ajili ya wazee wa kitanzania na vizazi vyao.

  Mimi nafkiri, badala ya kutaka kifungu cha mafao ya kujitoa kirudishwe na hivyo kujihakikishia kuona vurugu za wazee mitaani kama wale wa jumuiya ya afrika mashariki siku za usoni. Ni bora tukaacha sheria ibaki kama ilivyo(kwa maana ya kuzuia mafao ya kujitoa) ILA iongeze kifungu kitakachomtaka mwajiri awe na scheme ya kuchangia wafanyakazi ambayo ni over and above the basic pension scheme, ambayo mtu ataweza kuacess fedha zake pale atakapoacha kazi.

  Bottom Line, pensheni ni muhimu muhimu sana... Kila siku ukienda kwenye fukwe za Zanzibar utakuta vizee vya kizungu vimejazana vinakula maisha. Na hii siyo rocket science. wenzetu waliona mbali, wakaamua kwa makusudi kufuta mafao ya kujitoa kama bado una nguvu zako. Ili unapozeeka uzeeke kwa heshma!

  Niishie hapo, naomba tujadili bila matusi.
   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  Aug 4, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Kama Ungekuwa Mkali kwa Wabunge wa CCM wanaozima UMEME kwa Wananchi kama ULIVYO kwa JOHN MNYIKA

  Kweli ningejua WANANCHI wanataka nchi yao; Lakini SIJAWAHI KUONA HOJA YOYOTE ya kumlaumu OLE SENDEKO na

  TIMU YAKE HUMU... WOTE WAMENYWEA... NI KULAUMU anayeonyesha anafanya kazi akiwa BUNGENI kuonyesha

  HAFAI... ni kweli ...............
  HAANGALIWI MTU USONI...
   
 3. Mchambuzi

  Mchambuzi JF-Expert Member

  #3
  Aug 4, 2012
  Joined: Aug 24, 2007
  Messages: 4,817
  Likes Received: 1,128
  Trophy Points: 280
  Una hoja za msingi lakini ilikuwa haina haja ya kumwambia Mnyika amepotoka. Ungemwambia tu kiustaarabu kwamba haukubaliani nae katika hilo kwa vigezo ulivyoainisha kwani ukimsoma vizuri mnyika, all he does ni kuwasilisha mawazo yake objectively na kwa maslahi ya watanzania kupitia nafasi yake.

  Dhana ya kutotumia matusi (kwani tusi is simply a rude expression), pia dhana ya kutotafuta cheap popularity kwa kuweka headings za kum degrade mhusika, nadhani wewe mwenyewe zote hizi umezi violate.

  Vinginevyo una mawazo mazuri, na binafsi kuna mengi nimejifunza.
   
 4. Sober

  Sober JF-Expert Member

  #4
  Aug 4, 2012
  Joined: Jun 6, 2008
  Messages: 289
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Hicho unachokisema ndiyo exactly kilichonistua.

  Tumezoea kuona wanasiasa wakikimbizana kusaka cheap popularity, lakini siku zote Mnyika ameonesha umakini wa hali ya juu kwa kufanya homework yake vizuri na kujiridhisha.

  Lakini kwa nilichokiona leo kimeonyesha kukurupuka kwa hali ya juu, kusikozingatia maslahi mapana ya nchi kwa siku za usoni. Yeye anaongelea kusaka sahihi wakati hajawa hata na kikao kimoja cha wataalam na wadau wengine ili kuona basis ya hoja yake.

  Alichofanya ni kuwa carried away na bandwagon ya popularity contest, at the expense ya future generations... Kwa kifupi
  anaanza kuonesha dalili za kuwa kama wale wa NDIIIYOOOOO...... siku za usoni.

  Pamoja sana.
   
 5. y

  ycam JF-Expert Member

  #5
  Aug 4, 2012
  Joined: Mar 17, 2012
  Messages: 755
  Likes Received: 739
  Trophy Points: 180
  Naunga mkono hoja, hasa kwasababu unaonyesha kuona mbali, kama kipengele chenyewe cha sheria kinachopingwa na wafanyakazi wengi kinavyoonekana. Ila naona pia umevuka mpaka kwa kusema kwamba Mnyika anatafuta "cheap popularity". The mere fact that he is against it does not necessarily make him a cheap popularity seeker.
   
 6. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #6
  Aug 4, 2012
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Mkuu mimi nitajadili hayo niliyoweka red.
  Mkuu upo nchi gani? nakuuliza hivyo kwa sababu pengine hujui au labda unapotosha kwa makusudi kabisa.
  Mfanyakazi hukatwa 10% ya mshahara wake na mwajiri wake hukatwa 10% ya huo mshahara ukipiga mahesabu jumla ya mchango wa mwajiriwa(jumlisha na ule anotoa mwajiri) ni 20% ya mshara wake wa kila mwezi na sio 5% kama ulivyosema.
  Pili hiyo michango mwajiriwa ambayo anakuja kuchukua(fao la kujitoa) ni malimbikizo ya kipindi chote alichokuwa akifanya kazi so unavyojaribu kulinganisha malimbikizo na mshahara wa mwezi mmoja kunakuwa hakuna uwiano wowote.

  pili ningependa kukuelimisha jambo moja.
  Pensheni ni kitu tofauti kabisa na fao lakujitoa.
  Kwa Serikali makini hutoa pensheni kwa wazee bila hata kujali kama (huyo mzee) katika ujana alaiajiriwa au la.
  Pension inatakiwa iwe ni grant kwa mwananchi mzee.
  Fao la kujitoa ni pesa za mwajiriwa ambazo alikuwa akizihifadhi ili zimsaidie kuendesha maisha yake pindi ambapo hatokuwa na ajira tena.(iwe ni kwa kuacha, kufukuzwa kazi au kutokuwa na nguvu za kufanya kazi tena)
   
 7. k

  kundaseni meena Member

  #7
  Aug 4, 2012
  Joined: Apr 22, 2012
  Messages: 62
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  unachokisema ni sawa lakini bado unatoa ushauri ule ule ambao MNYIKA anataka kuufanyia kazi kwamba angalau mtu aweze kuaccess acount yake pale anapoacha/anapoachishwa kazi. una mawazo mazuri lakini nahisi wewe ndo umepotoka kwa kukosoa kile unachokipendekeza wewe mwenyewe.
   
 8. Sober

  Sober JF-Expert Member

  #8
  Aug 4, 2012
  Joined: Jun 6, 2008
  Messages: 289
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Mkuu haijalishi nipo wapi.

  Ila ukiingia kwenye website ya PPF utaona sehemu inayosema mwanachama atachangia asilimia 5% ya mshahara na mwajiri atachangia asilimia 15% ya mshahara, ukijumlisha unapata hiyo 20% uliyoongelea. Na hata NSSF wanaweza kuchangiwa kwa uwiano huo huo kama mwajiri akiona inafaa. hivyo hoja ya kuwa kila mwezi unabakiwa na asilimia 95% ya mshahara tena bado ukiwa na nguvu zako inasimama.

  Pensheni kwa wazee wote nchini ni wazo zuri sana, na hakika ni ndoto ya kila mtu. Ila kiukweli halitekelezeki ndani ya miaka 50 ijayo kwa ukuaji huu wa uchumi. Kwa Fertility rate yetu ya 5.4% na GDP Growth rate 7.5% itakua ni kujidanganya kuanza kuota kuwa sasa serikali itaweza kuwalipa pensheni ya kukidhi wazee wote.

  Nadhani bado unakumbukumbu ya mgomo wa juzi wa madaktari na baadae waalimu. Serikali imeshasema ingawa nia ya kuwaboreshea mishahara wanayo lakini uwezo hauruhusu. Hili la pensheni kwa wazee wote litakua far fetched kweli.
   
 9. Sober

  Sober JF-Expert Member

  #9
  Aug 4, 2012
  Joined: Jun 6, 2008
  Messages: 289
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Sijui mwenzangu unalielewaje neno KUPOTOKA!

  Lakini kwa vile hapa sio mashindano ya semantics, naomba upendekeze neno ambalo litakufurahisha wewe pamoja na wengine waliolichukulia negatively hilo neno.

  Nami nitarekebisha title ya uzi huu.
   
 10. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #10
  Aug 4, 2012
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Mkuu kwanza unaongea kitu ambacho haukifahamu.
  naomba nipe link ya NSSF ianyosema mwanachama atachangia 5%. Mimi ni mwajiriwa na ni member wa NSSF na nilijaza mkataba from the first day naajiriwa. Kwenye fomu yao wameandika kabisa kuwa ninakatwa 10% ya mshahara wangu na mwajiri ananichangia 10% hakuna 5% wala 15%.
  Bado nakukumbusha tena kuwa kuna tofauti kubwa sana kati ya mshahara wa kila mwezi na pesa ambazo ulikuwa ukizihifadhi kwa miaka mingi.
  Kumbuka ni pesa hizo hizo ambazo unaziona ni ndogo ndizo serikali inazichota na kuzifanyia projects za kifisadina hatimaye inashindwa kuzirudisha.
   
 11. Mchambuzi

  Mchambuzi JF-Expert Member

  #11
  Aug 4, 2012
  Joined: Aug 24, 2007
  Messages: 4,817
  Likes Received: 1,128
  Trophy Points: 280
  Mimi navyoelewa, neno potoka unapoli address kwa mtu maana yake ni kwamba when it comes to mawazo yake au mtazamo wake, Mnyika is very unusual, abnormal, very unconventional, yupo way off the accepted standards relative to you - wewe ukiwa kinyume na haya yote; Ina maana tayari umesha establish kwamba when it comes to suala hili, mtazamo na mawazo yako ndio kipimo cha what is normal, conventional, usual, and accepted as a standard;

  Lakini nina amini haukuwa na maana mbaya; ila naomba kama kuna interest ambayo unaweza to declare juu ya suala la mafao, nadhani itasaidia kuchangamsha zaidi huu mjadala.
   
 12. George Kahangwa

  George Kahangwa Verified User

  #12
  Aug 4, 2012
  Joined: Oct 18, 2007
  Messages: 539
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Wakuu,

  Mashirika yanatofautiana, mengine ni 15% mwajiri kwa 5% mwajiriwa (mfano PSPF), na Mengine 10 kwa 10 (kv. NSSF).

  NB
  Nimepata kufika ofisi ya NSSF pale Ubungo mara kadhaa, nilikutana na watu wengi ambao walifika pale kuchukuwa mafao yao, si kwa kuwa ni wazee bali ajira zao zimekoma na hawatarajii kuajiriwa tena. Kama sheria itaendelea kusimama hivyo, basi atakayeacha kazi leo akiwa na miaka 25 atasubiri kwa miaka 30 kuchukua pesa yake.

  Mtoa Mada
  , kwa maana hiyo hicho unachodai kwamba huongezeka miaka ya baadaye hakitakuwepo. Aidha, nadhani hata suala la kushuka kwa thamani ya fedha linaweza likawa na athari hasi kwa huyu atakayesubirishwa kwa miongo mitatu.
   
 13. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #13
  Aug 4, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145

  Yaani Mnyika anatafuta CHEAP Popularity? Kama Mnyika anatafuta Cheap Popularity kwahiyo Hatuna WABUNGE

  Wote Ni BENDERA FUATA UPEPO basi... HUKO BUNGENI hawatungi tena Sheria ni kula na kufisadi; yaani atakuwa ndiyo

  kama wa CCM?
   
 14. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #14
  Aug 4, 2012
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,588
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Hivi Mnyika alikuwa wapi wakati mswada unapitishwa bungeni?
   
 15. cooper

  cooper JF-Expert Member

  #15
  Aug 4, 2012
  Joined: Nov 24, 2011
  Messages: 394
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 45
  Nadhani ile post humu kwamba mifuko inakaribia kufilisika ina ukweli. Kwanini mlione hili sasa wakati hii mifuko iko tangu enzi. Ina maana mlipoanzisha fao la kujitoa hamkuona taabu za uzeeni ndo mnaziona leo? Siku hizi ajira hasa binafsi hazitabiriki mtu anaweza fanya kazi miaka miwili mitatu wanakutema then unaniambia nisubiri uzeeni? Miduko hii inafilisika na wala siyo huruma kwe wazee wala nini.
   
 16. TabletFellow

  TabletFellow JF-Expert Member

  #16
  Aug 4, 2012
  Joined: May 17, 2011
  Messages: 928
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  sober una point.... nimependa your analysis, ila umaharibu kwa kuongea kishabiki

  you are better and wiser.. use your wisdom better
   
 17. Rejao

  Rejao JF-Expert Member

  #17
  Aug 4, 2012
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 9,239
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Mnyika ange raise hii concern yake wakati hii sheria ikipitishwa. Nashangaa hakufanya hivyo. Sijui anataka ijadiliwe tena upya kwa mantiki ipi.

  Naye pia tumweke kwenye hilo kundi la BENDERA FUATA UPEPO!!
   
 18. Magu

  Magu Senior Member

  #18
  Aug 4, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 158
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Mh. hoja yako ya lawama zako kwa Mnyika haijazingatia mambo mengi ambayo watu wanataka kujua na yanawapa mashaka ya fedha zao. Maswali ambayo sheria hii haijajibu ni kamaifuatavyo,

  1. Je ni lazima mtu aajiliwe katika formal sector baada ya ajira yake ya kwanza kuisha? Ukizingatia kuwa ajira nyingi ni contractual na pia focus kubwa ni kutaka watu wajiajiri? Think in a long run and not in a short run.

  2. Kumekuwepo na utofauti wa mafao ya pension tofauti kwa mashirika yanayo operate ndani ya nchi moja, kwa maana ya calculation za pension na utoaji wa mkupuo wa kwanza na pension na baadae monthly pension, je hii huoni pia ni tatizo?

  3. Formula ya pension ni kandamizi kwa mwanachama, kama wewe ni mtu unayejua angalau hesabu ndogo tu, je inaweza ingia akilini mwako kupata the little sum mwanachama anapata kama pension na angeweza kuwa na mifumo mingine ya kuhifadhi fedha yake ambayo angepata gawiwo mfn ya kunumua share za mashirika na kuwekeza katika amana mbalimbsli na mabenki pia, je umewahi tafuta tofauti ya ruturns za option zote hizo?

  3. Siyo kweli kuwa LAPF hawakuwa na fao la withdrawal! Hebu tembelea tena act yao usidanganye watanzania amvao leo wanaelewa kinachoendelea duniani kote.

  4. Mashirika yetu ya pension hasa yale giant kama NSSF, PPF, PSPF semeni ukweli! Yawezeka acturial valuation report zenu zinaonyesha mashirika kuelekea kushindwa kujiendesha kwa sababu mbali mbali ndiyo mana mmefanya lobbing kwa regulatory authority kuyanusuru mashirika yasishindwe kulipa wanachama wanaostaafu na kujitoa. Sababu ya report kuonyesha kushindwa kujiendesha ktk kulips mafao ni kama ifustavyo;
  A. Mashirika yamewezeka katika miradi mikubwa ambayo payback period ni mda mrefu mfano wa uwekezaji UDOM, Daraja la Kigamboni, majengo makubwa, mradi wa kuzalisha na kufua umeme NSSF, etc, miradi hii haijaanza kuleta matunda kwa mashirika hivyo na changamoti. Hesabu walizopiga za returns from investment hazikuwa realistic due to poor investmement policy na pia udhaifu wa wataalamu katika mashirika, ndo maana sasa wanataka watu wasijitoe ili madhirika ya survive.

  B. Changamoto ya mashirika mengi hasa ya madini kutaka kufungwa pia imeonekana italeta matatizo kwa mashirika yetu, kwa sababu makampuni ya madini kama kahama, buzwagi, Nzega, Geita etc wafanyakazi wake wanafedha zao nyingi katika mashirika haya, na life span ya mashirika haya haizidi miaka 5 ijayo, na average age ya watumishi katika mashirika ya madini inaweza kuwa 40 yrs, hivyo serikali inafanya maamuzi kuyakinga mashirika haya.

  C. Mashirika yanakabiliwa na changamoto ya mortality rate, ambayo inafanya walipe fedha nyingi kwa watumishi wanafao fariki kwa warithi wao, hivyo they restrict other withdrawal to safeguard thier compnies.

  D. Mashirika mengi ya pension yamekuwa yanalaumiwa sana kwa matumizi mabaya ya fedha za wanachama, katika ufisadi katika manunuzi, wizi wa fedha, pia kukopesha au kutoa ruzuku kwa vyama vya siasa. Wote tutakuwa shahidi kuna nyuzi ngapi hapa JF za mismanagement ya fedha PPF ambazo tumeletewa? Hii yote ndo inafanya pension iwe ndogo na ifanye watu kytokuwa na hamu ya kusubiri hiyo pension ndogoo na tena baada ya miaka 55!

  Mwisho napenda kuyashauri mashirika ya pension waache hii lobbying waliofanya mana itaua wazee wetu wengi, mpaka mda huu tu wastaafu wengi wanakufa sababu ya pension kwa sababu anachosubiri katika miaka 55 siyo anachopata, hivyo pressure due demand ya maisha inamuua. Pia kwa nini kama hii miradi inajengwa kwa fedha za wanachama mwisho wa siku zusitolewe share za kuimiriki hiyo miradi kwa wanachama, nadhani hii itawafanya watu wasiwaze kutoka maana watakuwa ni sehemu ya umiliki wa miradi na mashirika kwa ujumla.
   
 19. Mzee wa Rula

  Mzee wa Rula JF-Expert Member

  #19
  Aug 4, 2012
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 8,177
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Nimepitia maoni ya wengi naona hitilafu ni ndogo,

  1.0 Kwanza kuna mifuko ambayo wanachangia watumishi wa umma kama GEPF, PSPF. Katika hiyo inategemeana lakini kama mtumishi anachangia GEPF atakuwa anakatwa 10% na mwajiri 10% hali kadhalika kama yeye anachangia 5% basi mwajiri 15%.

  Na hii ni hata kwa mifuko mingine kama NSSF, LAP n.k. Lakini hiyo kwangu siyo hoja ya msingi.

  2.0 Hoja ya msingi ni hii, mtu anapoaacha kazi ama kwa kufukuzwa, kuachishwa au vyovyote vile ana mambo mawili:-
  (a) Aendelee kutafuta ajira nyingine au
  (b) Ajiajiri.

  Kutokana na wafanyakazi wengi wa kitanzania kuwa na mishahara midogo isipokuwa wachache wengi hujikuta ha save na kutegemea hicho ambacho ni haki yake.

  Kumwambia mtu huyu ambaye ameshindwa kusave akiwa na aidha 90% au 95% ya mshahara ni kumnyima nafasi hata ya kuweza kujikimu au kuanza maisha mapya.

  Labda hiyo point nitakuwa nibase kwa mtu aliyefukuzwa lakini vipi kwa yule ambaye nae kwa hiari yake ameamua kuacha aidha amechoka kazi toka kwa muajiri huyo.

  Naye utamnyima nafasi ya haki yake ambaye angepaswa kuipata na kuitumia inavyofaa kuliko kumsubirisha mpaka miaka 50 - 60%.

  3.0 Hoja hii imekuja wakati ambapo tunaambiwa NSSF na mifuko mingine ipo katika hali mbaya ya kifedha kutokana na serikali kuweka kukopa sana na kushindwa kurudisha kwa wakati. Hili nalo linaongeza mkanganyiko.

  Binfsi nataka mtu akiacha kazi apewe chake akafie mbele ya safari. Nyingine ni longo longo.
   
 20. rweyy

  rweyy Senior Member

  #20
  Aug 4, 2012
  Joined: Aug 5, 2011
  Messages: 160
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 45
  hapa aliye potoka ni wewe mtoa mada kuna mambo unayoyasema ni ya vitabuni.jiulize ni wafanyakazi wangapi akiachishwa kazi leo ana huakika wa kupata ajila tena.kinacholeta utata hapa ni ni thamani ya fedha leo mimi nadai sh. 3m baada ya miaka 25 ijayo fedha hiyo itakuwa na thamani gani? wewe usione sisi wajinga tuna jua liba itakuwa ni ndogo sana kulinganisha na thamani ya fedha.unapo sema wazee wanaangaika fikilia ukinipa fedha hiyo nikiwa na umuri wa miaka 55 ni kweli nitafika nayo kwenye umuri wa miaka 70?
   
Loading...