Mh. Mnyika kwa hili umepotoka!...

Mh. Mnyika kwa hili umepotoka!...

Hili la life expectancy nakuunga mkono 100%
Kwamba mifuko HAIKUWA na fao la kujitoa, si KWELI kabisa. LAPF wanalo katika sheria yao. Tembelea website yao utaona moja ya mafao wanayotoa ni lile la kujitoa. NSSF wanatoa ingawa sikuwahi kuona kama ni moja ya mafao yao
Kama mwajiri ni Serikali basi michango huwa ni 15% mwajiri, 5% mwajiriwa
Kama mwajiri ni sector binafsi basi michango huwa ni sawa yaani 10% each.
Lakini nachelea sana kukufahamisha na kimsingi kukuelimisha namna ambavyo unapotoka na kujaribu kuwahadaa watanzania. Kama hutajali, kama ulivyosema mwenyewe tujadili kwa hoja bila kejeli na matusi, niambie TOFAUTI KATI YA SOCIAL SECURITY NA PENSION. Nitarudi ukinipa hiyo tofauti
 
nachoona hapa ni matunda ya multiple ID,mwanzinsha mada na baadhi ya wanaomuunga mkono naamini ni mtu moja anapigia upatu huu wizi wa magamba,tunasema hivi hizo pesa ni akiba zetu na tutazichukua tunapozihitaji! Kama unabisha subiri bunge likatae kurekebisha hiyo sheria uone tutakachofanya...kwa hili tupo tayari kwa lolote hata mvue nguo hatutakubali.nimemaliza...
 
Heshima kwako Mzee wa Lula ulichokielezea ndicho kilivyo;haiwezekani mimi nimeacha kazi nina 35yrs nisubiri baada ya 20 ijayo;sasa nitaishije ?maana ile akiba ndio ninayoitegemea niweje kujiweka sawa na kupambana na maisha;na kumbuka labda nisingependa kuajiriwa tena ningependa nikiwa na nguvu nijiajiri na kupambana na maisha nikiwa kijana na nguvu!!

Matakwa yao ya kuendesha mashirika yetu haya kisiasa ndio kosa lake hilo ,watawala hawataki kufanya home work yao,wanaenda kuchota tu kirahisi:

Wafanyakazi wote tuwe pamoja na tuangalie wabunge fuata upepo wote ambao hawatasaidia kurudisha ile window pale,tuhakikishe hawarudi bungeni,wafanyakazi tuna mtandao mkubwa sana kwa ndugu na jamaa wanaotutegemea moja kwa moja na extended family,piga kura yako kwa chama kingine tupate mabadiliko!

Na pia hao wakuu wa mashirika wasichaguliwe kirafiki na kidini kwa matakwa ya Rais ili akikwama aweze kuichota tu!!wapitishwe kwa interview na wakaidhinishwe na Bunge kwa kura pale!wasihusishwe na Rais kabisa!!!
 
  • Thanks
Reactions: MTK
Mnyika ange raise hii concern yake wakati hii sheria ikipitishwa. Nashangaa hakufanya hivyo. Sijui anataka ijadiliwe tena upya kwa mantiki ipi.

Naye pia tumweke kwenye hilo kundi la BENDERA FUATA UPEPO!!

Kwa upande wako sishangai sababu hoja ameileta 'MNYIKA' ingekuwa imetolewa na mtu kutoka ule upande mwingine ungeshawishika kuipima hoja,lakini kwa sababu hoja imeletwa na flani basi!
 
Mkuu mimi nitajadili hayo niliyoweka red.
Mkuu upo nchi gani? nakuuliza hivyo kwa sababu pengine hujui au labda unapotosha kwa makusudi kabisa.
Mfanyakazi hukatwa 10% ya mshahara wake na mwajiri wake hukatwa 10% ya huo mshahara ukipiga mahesabu jumla ya mchango wa mwajiriwa(jumlisha na ule anotoa mwajiri) ni 20% ya mshara wake wa kila mwezi na sio 5% kama ulivyosema.
Pili hiyo michango mwajiriwa ambayo anakuja kuchukua(fao la kujitoa) ni malimbikizo ya kipindi chote alichokuwa akifanya kazi so unavyojaribu kulinganisha malimbikizo na mshahara wa mwezi mmoja kunakuwa hakuna uwiano wowote.

pili ningependa kukuelimisha jambo moja.
Pensheni ni kitu tofauti kabisa na fao lakujitoa.
Kwa Serikali makini hutoa pensheni kwa wazee bila hata kujali kama (huyo mzee) katika ujana alaiajiriwa au la.
Pension inatakiwa iwe ni grant kwa mwananchi mzee.
Fao la kujitoa ni pesa za mwajiriwa ambazo alikuwa akizihifadhi ili zimsaidie kuendesha maisha yake pindi ambapo hatokuwa na ajira tena.(iwe ni kwa kuacha, kufukuzwa kazi au kutokuwa na nguvu za kufanya kazi tena)

Nakuunga mkono katika hili.
 
kuhusu swala la mafao wanatakiwa wazungumze watu wamgodini, wewe unayejifanya unaleta hoja za kuchambua usichokijijua utaleta shida.

Watu wamelipia hela wewe unataka kuleta hoja ya kipuzi ambayo itafanya baadhi ya wanachama kunyimwa mafao yao?

Kwanini wasingepitisha iyo sheria kwa ALPF? Nyie leteni soga mtajuta na drama mnazozitengeneza.
 
Mnyika ange raise hii concern yake wakati hii sheria ikipitishwa. Nashangaa hakufanya hivyo. Sijui anataka ijadiliwe tena upya kwa mantiki ipi.

Naye pia tumweke kwenye hilo kundi la BENDERA FUATA UPEPO!!

Nikuulize,
Wewe hii sheria wakati inapitishwa bungeni uliiona? Waweza kunitajia kifungu kilichoipitisha hii sheria?

Kukusaidia tu, Sheria inapotungwa kunaweza kukawa na "supporting regulations" ambazo si lazima zipite bungeni, ndio uhuni uliofanyika hapa!!

So hata kama Mnyika (usisahau na wabunge wako wa Magamba pia) walikuwepo, basi serikali iliwapiga "chenga ya mwili"
 
Umeelezea vizuri sana na analysis yako nimeipenda. But kuna vitu tunatofautiana kidogo.

Kwanza kumbuka kuwa nia ya compulsory pension scheme ni kwa ajili ya kukusaidia wakati wa uzee au kipindi ambacho huna uwezo wa kufanya kazi. Kufanya withdrawal ni kinyume na maana ya scheme yenyewe. Tungekuwa na voluntary/supplimentary schemes, ndio mtu ungeruhusiwa kutoa mafao yako muda wowote na pension yako ingetegemea na performance ya hiyo scheme.

Kuhusu formula, kila mfuko umeanzishwa na sheria yake na kila moja wakati wa kuanzisha walifanya analysis ya kutosha wakaona formula inayofaa ni ipi. Ukiangalia mifuko yetu, formula inayoumiza ni ya NSSF ambayo ni ya muda mrefu, ikufuatiwa na PPF ambayo ikikuja baada ya NSSF. PSPF na LAPF formula zao ni nzuri kwasabu mifuko ya hivi karibuni. Nafikiri hili suala SSRA wameshaliona na mifuko husika inarevise formula zao.

Sikubaliani na wewe kuwa actorial valuations zinaonyesha kuwa mifuko inakaribia kufa. Ukiangalia mifuko mingi inaidai serikali yetu kiasi kikubwa cha fedha. Ukijumlisha deni la serikali kwenye hesabu za haya mashirika unaona bao haya mashrika going concern yake ipo vizuri.

Kuhusu kuwekeza kwenye projects ambazo payback period yake ni ya muda mrefu, kumbuka kuwa pension fund zinawekeza kwa ajili ya kufulfil long term obligations. Wanachofanya ni matching ya cashflows zao na obligations zao. Nafikiri wanafanya vizuri kwenye portfolio zao na mixture of short term na long term assets ndio maana hatuwahi kusikia mfuko wowote umesuffer liquidity problems.

Acha kujitoa ufahamu kwa ajili ya kutetea mafisadi na matumbo yenu,report ya CAG imesema live hii mifuko ipo mbioni kufilisika na fedha za wanachama kupotea,mbona unapotosha umma? Wewe ndio CAG?
 
Hili la life expectancy nakuunga mkono 100%
Kwamba mifuko HAIKUWA na fao la kujitoa, si KWELI kabisa. LAPF wanalo katika sheria yao. Tembelea website yao utaona moja ya mafao wanayotoa ni lile la kujitoa. NSSF wanatoa ingawa sikuwahi kuona kama ni moja ya mafao yao
Kama mwajiri ni Serikali basi michango huwa ni 15% mwajiri, 5% mwajiriwa
Kama mwajiri ni sector binafsi basi michango huwa ni sawa yaani 10% each.
Lakini nachelea sana kukufahamisha na kimsingi kukuelimisha namna ambavyo unapotoka na kujaribu kuwahadaa watanzania. Kama hutajali, kama ulivyosema mwenyewe tujadili kwa hoja bila kejeli na matusi, niambie TOFAUTI KATI YA SOCIAL SECURITY NA PENSION. Nitarudi ukinipa hiyo tofauti

so·cial se·cu·ri·ty
Noun:
Any government system that provides monetary assistance to people with an inadequate or no income
(in the US) A federal insurance program that provides benefits to retired persons, the unemployed, and the disabled

Pen·sion/ˈpenSHən/
Noun:
A regular payment made during a person's retirement from an investment fund to which that person or their employer has contributed...
A boardinghouse in France and other European countries, providing full or partial board at a fixed rate
Verb:
Dismiss someone from employment, typically because of age or ill health, and pay them a pension
 
Hicho unachokisema ndiyo exactly kilichonistua.

Tumezoea kuona wanasiasa wakikimbizana kusaka cheap popularity, lakini siku zote Mnyika ameonesha umakini wa hali ya juu kwa kufanya homework yake vizuri na kujiridhisha.

Lakini kwa nilichokiona leo kimeonyesha kukurupuka kwa hali ya juu, kusikozingatia maslahi mapana ya nchi kwa siku za usoni. Yeye anaongelea kusaka sahihi wakati hajawa hata na kikao kimoja cha wataalam na wadau wengine ili kuona basis ya hoja yake.

Alichofanya ni kuwa carried away na bandwagon ya popularity contest, at the expense ya future generations... Kwa kifupi
anaanza kuonesha dalili za kuwa kama wale wa NDIIIYOOOOO...... siku za usoni.

Pamoja sana.

me sijaona hoja hapa...ngoja nipite tu....iko agenda nyuma ya pazia
 
Mnyika ange raise hii concern yake wakati hii sheria ikipitishwa. Nashangaa hakufanya hivyo. Sijui anataka ijadiliwe tena upya kwa mantiki ipi.

Naye pia tumweke kwenye hilo kundi la BENDERA FUATA UPEPO!!
Mkuu ziwa nyasa limechukuliwa na Yule mwanamke wa shoka huyu wa kwetu amebakia akikenua meno tu na kutesa wakina ulimboka
 
Umeelezea vizuri sana na analysis yako nimeipenda. But kuna vitu tunatofautiana kidogo.

Kwanza kumbuka kuwa nia ya compulsory pension scheme ni kwa ajili ya kukusaidia wakati wa uzee au kipindi ambacho huna uwezo wa kufanya kazi. Kufanya withdrawal ni kinyume na maana ya scheme yenyewe. Tungekuwa na voluntary/supplimentary schemes, ndio mtu ungeruhusiwa kutoa mafao yako muda wowote na pension yako ingetegemea na performance ya hiyo scheme.

Kuhusu formula, kila mfuko umeanzishwa na sheria yake na kila moja wakati wa kuanzisha walifanya analysis ya kutosha wakaona formula inayofaa ni ipi. Ukiangalia mifuko yetu, formula inayoumiza ni ya NSSF ambayo ni ya muda mrefu, ikufuatiwa na PPF ambayo ikikuja baada ya NSSF. PSPF na LAPF formula zao ni nzuri kwasabu mifuko ya hivi karibuni. Nafikiri hili suala SSRA wameshaliona na mifuko husika inarevise formula zao.

Sikubaliani na wewe kuwa actorial valuations zinaonyesha kuwa mifuko inakaribia kufa. Ukiangalia mifuko mingi inaidai serikali yetu kiasi kikubwa cha fedha. Ukijumlisha deni la serikali kwenye hesabu za haya mashirika unaona bao haya mashrika going concern yake ipo vizuri.

Kuhusu kuwekeza kwenye projects ambazo payback period yake ni ya muda mrefu, kumbuka kuwa pension fund zinawekeza kwa ajili ya kufulfil long term obligations. Wanachofanya ni matching ya cashflows zao na obligations zao. Nafikiri wanafanya vizuri kwenye portfolio zao na mixture of short term na long term assets ndio maana hatuwahi kusikia mfuko wowote umesuffer liquidity problems.

Nashukuru kwa majibu yako though hujajibu maeneo yote niliyopenda watanzania wapate majibu kwa mashaka ya fedha zao katika mashirika ya pendion.

Sheria hii unasema imejadiliwa April 2012 kwa nini haiku fanyiwa enough advocacy kwa wadau kabla ya kupelekwa bungeni kujadiliwa na kupitishwa? Vyama huru vya wafanyakazi vimekanusha kushirikishwa on behalf of employees. Lakini napata mashaka ya maelezo yako ktk hili, umesema pia kuwa katika sheria ya pension hapakuwepo clause ya withdrwal, je ipi ilijadiliwa April 12?

Act no 8 ya pension schemes iliyoiokoa PPF baada ya privatization ya parastotal organizations, sheria hii ilitangazwa sana na PPF kws sababu ilikuwa inawapa uhai wa kuishi wakati NSSF wakiipinga sababu ilikuwa inawanyima wanachama, kwa sababu walitegemea watumishi kutoka katika mashirika ya umma kuhamisha michango yao kwenda NSSF. Tunachojiuliza mbona hii haikufanyika kuelimisha wanachama mapema?

Katika mkutano wa mwaka 2006/2007 uliofanyika Golden Tulip organized by World Bank na ILO kutaka kutaka kuyaunganisha mashirika ya pension Tanzania baada ya kuwa utitiri wa mifuko yenye calculation tofauti, idea ya wafadhiri ktk mpango huu ni kutaka kuboresha pension system Tanzania, je hii imefikia wapi au imehujumiwa na mafisadi wansofadika na uwepo wa utitiri wa mifuko unaosababisha pension kuwa duni?

Katika majibu yako on investment policy esp on long term, the matching concept, ni sahihi, lakini je hizo fedha za wanachama mnazokopesha serikali za hazirudi kwa mujibu wa maelezo yako, je loan policy kwa govt inasemaje? Mnakopesha out of the policy or within the policy? Kama kuna loan policy je si wanakuwa na collateral ln the loan ambayo we can recover our money on default?
On the same, how do we project ufisadi and misuse of funds, is it part of our plans?
 
Go mnyika go intelligent peoplez mp, i cant blv kwamba haka ka pension kangu ambako nilitaka baada ya miaka mitatu ya kazi kanitoe kununua kiwanja na mtaji wa biashara nitakasubiri hadi miaka 28 ijayo.! Haki vile naapa, ikilazimika kuandamana nitakuwa mstali wa mbele ,huu ni wizi wa waziwazi, jk na wezi wenzie wamechota zote hazina kumekauka wana taka wahamie kwenye pension funds ..tusikubali
 
Sober Kadiri nilivyosikia toka vyombo vya habari, baadhi ya waliohojiwa kama Tucta, walisema wao walishirikishwa lakini kipengele hicho hakikuwepo.Walichomeka baadae.Mimi nadhani kama kilikuwepo toka awali basi waliopitisha hawakujua madhara yake.

Naamini kama angekuwepo Dr Slaa bungeni angeshatuhabarisha mapema kabla ya sheria hiyo kupitishwa.Chukua mfano wa sheria ya uchaguzi iliyopitishwa kwa mbwembwe na kusainiwa ikulu. Kuna kipengele ambacho hakikujadiliwa bungeni lakini serikali ilichomeka.Tukaambiwa hicho kipengele hakikuwepo.Nadhani wote tunakumbuka.

Hapa wenzetu walikosa umakini.
 
Last edited by a moderator:
Hivi Mnyika alikuwa wapi wakati mswada unapitishwa bungeni?

Ukiuliza swali hili kuelekea kwa mbunge wa upinzani utakuwa hauko makini! Hoja zote walizopinga zilipitishwa na jani la gomba. Hili linahusika pia.
 
Mtoa mada tengenezeni mfumo mzuri wa ajira na hakikisheni watu wanafaidi mafao sio wazee wanapata sh 30000/= kwa mwezi. Lakini waambie waliokutuma watoe acturial report ya hiyo mifuko ili tuhue kuwa hakuna liquidity stress. Mimi kama mwanachama nina haki gani juu ya matumizi ya fund yangu huko ilipo.
 
Mh. Mnyika siku zote nimekua namuona ni mbunge makini sana na anayejishughulisha kujua mambo.

Lakini kwa hili la kutaka sheria ipitiwe upya na kurudisha mafao ya kujitoa naona amepotoka sana. Nashawishika kuamini kuwa nayeye kwenye hili ameingia kwenye mkumbo wa kusaka cheap popularity kwenye mambo ya kitaalamu zaidi. Najua nitashambuliwa kwa mtizamo huu ila nieleze sababu za mtizamo huu wangu......

Huu ni ujinga unaofanywa na tuliowapa mamlaka ya kutawa.wanatumia pesa za wanachama kuinvest kwenye miradi ambayo haikufanyiwa upembuzi yakinifu matokeo yake wanapata hasara mf.machinga complex n the like.

Logic ya alichokisema CAG ni ikitokea leo wanachama wakataka kuchukua michango yao mifuko chali.Lakini wakipitisha hii sheria yao wanauhakika wa kuzungusha kwa hicho kipindi chote.
 
Sio kampuni zote zzinadumu kwa muda mrefu, na suala la pension ni la mtu binafsi. Huu ni upuuzi tu. mtu anaweza kustaafu mapema zaidi. au kuhama kabisa shirika la hifadhi. Kwanza hawa ni wezi, hawalipi equivalent value ya pesa unazotoa. Kuna mambo mengi ya kurekebisha katika hii sheria.
 
Umeelezea vizuri sana na analysis yako nimeipenda. But kuna vitu tunatofautiana kidogo.

Kwanza kumbuka kuwa nia ya compulsory pension scheme ni kwa ajili ya kukusaidia wakati wa uzee au kipindi ambacho huna uwezo wa kufanya kazi. Kufanya withdrawal ni kinyume na maana ya scheme yenyewe. Tungekuwa na voluntary/supplimentary schemes, ndio mtu ungeruhusiwa kutoa mafao yako muda wowote na pension yako ingetegemea na performance ya hiyo scheme.......

Hapo kwenye red colour, angalia sana usije ukawa umenasa kwenya ntego wa unafiki wa hali ya juu sana.
Kabla ya kuandika hayo hapo kwenye red colour, ulitakiwa kufanya utafiti uone kama kweli katika nchi hii ya Tanzania jambo hili linafanyika, au ni theory tu inayotumika ili kunyonya wafanyakazi.

Kifupi hali katika Tanzania yetu hii iko hivi:-

  • pension schemes sio kwa ajili ya kukusaidia utakapo kuwa mzee, ila ni kwa ajili ya kukusanya pesa kwa ajili ya matumizi ya serikali, mfano, wafanyakazi wa iliyokuwa jumuiya ya afrika mashariki, wote sasa ni wazee, hebu niambie wanalipwa pension kiasi gani ???
  • je?, unajua pension wanayolipwa wastaafu kwa sasa ??? mfano, aliyewahi kuwa mkuu wa majeshi Tanzania, kwa sasa ni mstaafu anayelipwa Tzs. 50,000 (Tzs. elfu hamsini tu) kwa mwezi. Hii inamsaidiaje yeye kama mzee mstaafu.

Angalizo kwa wote:
Kabla ya kutoa maoni kwenye mada nzito kama hii ya maswala ya pension, fanya utafiti kwanza, vinginevyo, wewe ni mnafiki tu, au wewe pia ni mmoja wa wanaofaidika na udhalimu huu wa kunyima wafanyakazi haki yao ya mafao.
 
Back
Top Bottom