Mh. Mnyika kwa hili umepotoka!...

Hicho unachokisema ndiyo
exactly kilichonistua.

Tumezoea kuona wanasiasa wakikimbizana kusaka cheap popularity, lakini
siku zote Mnyika ameonesha umakini wa hali ya juu kwa kufanya homework
yake vizuri na kujiridhisha.

Lakini kwa nilichokiona leo kimeonyesha kukurupuka kwa hali ya juu,
kusikozingatia maslahi mapana ya nchi kwa siku za usoni. Yeye anaongelea
kusaka sahihi wakati hajawa hata na kikao kimoja cha wataalam na wadau
wengine ili kuona basis ya hoja yake.

Alichofanya ni kuwa carried away na bandwagon ya popularity contest, at
the expense ya future generations... Kwa kifupi
anaanza kuonesha dalili za kuwa kama wale wa NDIIIYOOOOO...... siku za
usoni.

Pamoja sana.

na wabunge kula pensheni kila baada ya miaka 5? za kwao zinatoka wapi? kwa nini na wao wasisubiri hadi wawe na 55 au 60? huu ubaguzi wa waziwazi ndio unachochea migomo ya wafanyakazi wa kada nyingine!
 
Magu
Umeelezea vizuri sana na analysis yako nimeipenda. But kuna vitu tunatofautiana kidogo.

Kwanza kumbuka kuwa nia ya compulsory pension scheme ni kwa ajili ya kukusaidia wakati wa uzee au kipindi ambacho huna uwezo wa kufanya kazi. Kufanya withdrawal ni kinyume na maana ya scheme yenyewe. Tungekuwa na voluntary/supplimentary schemes, ndio mtu ungeruhusiwa kutoa mafao yako muda wowote na pension yako ingetegemea na performance ya hiyo scheme.

Kuhusu formula, kila mfuko umeanzishwa na sheria yake na kila moja wakati wa kuanzisha walifanya analysis ya kutosha wakaona formula inayofaa ni ipi. Ukiangalia mifuko yetu, formula inayoumiza ni ya NSSF ambayo ni ya muda mrefu, ikufuatiwa na PPF ambayo ikikuja baada ya NSSF. PSPF na LAPF formula zao ni nzuri kwasabu mifuko ya hivi karibuni. Nafikiri hili suala SSRA wameshaliona na mifuko husika inarevise formula zao.

Sikubaliani na wewe kuwa actorial valuations zinaonyesha kuwa mifuko inakaribia kufa. Ukiangalia mifuko mingi inaidai serikali yetu kiasi kikubwa cha fedha. Ukijumlisha deni la serikali kwenye hesabu za haya mashirika unaona bao haya mashrika going concern yake ipo vizuri.

Kuhusu kuwekeza kwenye projects ambazo payback period yake ni ya muda mrefu, kumbuka kuwa pension fund zinawekeza kwa ajili ya kufulfil long term obligations. Wanachofanya ni matching ya cashflows zao na obligations zao. Nafikiri wanafanya vizuri kwenye portfolio zao na mixture of short term na long term assets ndio maana hatuwahi kusikia mfuko wowote umesuffer liquidity problems.
 
Last edited by a moderator:
Kweli dada irene umeamua kujitoa hadi huku unakuja ila kama mnekuwa mnasema nachukua baada ya miaka 55 na value ya hela inakuwa sawa lakini huu uzembe wa check ya buku kwa wazee wa EAC haukubaliki Sober
 
Last edited by a moderator:
Naunga mkono hoja, hasa kwasababu unaonyesha kuona mbali, kama kipengele chenyewe cha sheria kinachopingwa na wafanyakazi wengi kinavyoonekana. Ila naona pia umevuka mpaka kwa kusema kwamba Mnyika anatafuta "cheap popularity". The mere fact that he is against it does not necessarily make him a cheap popularity seeker.

Mkuu usione labda namsema mh. Mnyika out of nowhere. Kusema anatafuta cheap popularity maana yangu ilibase kwanye mambo makuu matatu.

1. Muswada huu wa mabadiliko ya sheria ulipitishwa bungeni mwaka huu, mwezi wa Aprili, hardly miezi minne mpaka leo. Najiuliza kwa mbunge makini kama Mh. Mnyika alikua wapi wakati wakiujadili mpaka leo ajitokeze kuonekana "mtetezi wa wafanyakazi?" What if wafanyakazi wasingeraise the alarm!

2. Hoja hii iliibuliwa na Mh. mbunge wa kisarawe kama jambo la dharura, na spika aliamuru Mtoa mada ailete hoja yake rasmi, lirudishwe kwenye kamati husika, kamati ikutane na wadau wote, halafu kamati imshauri spika on the way forward baada ya kukutana na wadau.

3. Mh. Mnyika mara nyingi kama sio zote, amekua ni mtu wa kufanya kazi kwa data za uhakika na huwa namkubali sana kwa kufanya homework. Ajabu kwenye hili, mara baada ya kikao kuahirishwa kakutana na waandishi wa habari na anaongelea kutafuta sahihi za wabunge!!!... Yani jambo la kitaaluma analitreat kisiasa. jambo litalo impact maisha ya maelfu ya wazee siku za usoni analichukulia kama masihara na kitu cha kushangiliwa kama umefunga goli.
 
Mkuu kwanza unaongea kitu ambacho haukifahamu.
naomba nipe link ya NSSF ianyosema mwanachama atachangia 5%. Mimi ni mwajiriwa na ni member wa NSSF na nilijaza mkataba from the first day naajiriwa. Kwenye fomu yao wameandika kabisa kuwa ninakatwa 10% ya mshahara wangu na mwajiri ananichangia 10% hakuna 5% wala 15%.
Bado nakukumbusha tena kuwa kuna tofauti kubwa sana kati ya mshahara wa kila mwezi na pesa ambazo ulikuwa ukizihifadhi kwa miaka mingi.
Kumbuka ni pesa hizo hizo ambazo unaziona ni ndogo ndizo serikali inazichota na kuzifanyia projects za kifisadina hatimaye inashindwa kuzirudisha.

Mkuu unachosema kina ukweli baada ya kufanya homework hapa. Ila kuna taarifa kuwa hata kwa NSSF na mifuko mingine wanayochangia asilimia 10%, kwa mabadiliko ya sheria hii, mifuko yote wataruhusiwa kuwa na flexible rates
yani either 5%/15% au 10/10%.

Kuhusu pesa kuwekezwa, lengo kuu la hii mifuko ni kulipa pensheni. Lazima tukumbuke ili mifuko iweze kulipa pensheni ambazo ni meaningful, ni lazima pesa inayokusanywa iwekezwe ili iweze kupata thamani kadri muda unavyoenda.
 
Mimi navyoelewa, neno potoka unapoli address kwa mtu maana yake ni kwamba when it comes to mawazo yake au mtazamo wake, Mnyika is very unusual, abnormal, very unconventional, yupo way off the accepted standards relative to you - wewe ukiwa kinyume na haya yote; Ina maana tayari umesha establish kwamba when it comes to suala hili, mtazamo na mawazo yako ndio kipimo cha what is normal, conventional, usual, and accepted as a standard;

Lakini nina amini haukuwa na maana mbaya; ila naomba kama kuna interest ambayo unaweza to declare juu ya suala la mafao, nadhani itasaidia kuchangamsha zaidi huu mjadala.

Mkuu wangu nimekupa na naomba nirudie upendekeze neno ambalo unaona linakufurahisha au litamfurahisha Mheshmiwa(sababu namheshimu) ili tusitoke nje ya mada namimi nitakua tayari kurekebisha heading ya uzi huu.

Kuhusu kuwa mawazo yangu tu kuwa ndiyo sahihi, sidhani kama nia yangu ilikua hiyo. Ila kwa kutazama miongozo ya ILO, International Social Security Association na hata bodies kama SSRA hapa nyumbani, na hata mashirika karibia yote ya pensheni, you can safely say the core ya hoja zangu ndiyo zinavyokubalika kimataifa.

Tumalize kuzunguka mbuyu kwa kukuomba tena upendekeze neno mbadala. NITAREKEBISHA!
 
ushauri kwa mtoa mada, jifunze maana ya social security! Pili, pension hutolewa kwa aliyechangia kwa miaka 15! (miezi 180). Tatu, wazee wetu wa iliyokuwa EA, wanadai nini? Nne, wangetoa taarifa mapema watu wajiandae. Hivi mi nimefanya kazi miaka 7 kwa lengo la kupata pesa ya kujisomesha au kufungua mradi, you spoil my long term plan? Just like that? Acha utani mkuu
 
ushauri kwa mtoa mada, jifunze maana ya social security! Pili, pension hutolewa kwa aliyechangia kwa miaka 15! (miezi 180). Tatu, wazee wetu wa iliyokuwa EA, wanadai nini? Nne, wangetoa taarifa mapema watu wajiandae. Hivi mi nimefanya kazi miaka 7 kwa lengo la kupata pesa ya kujisomesha au kufungua mradi, you spoil my long term plan? Just like that? Acha utani mkuu
Nikusahihishe tu, kuchangia kwa miezi 180 ndio kigezo cha kupata pensheni na siyo kwamba ukishachangia miezi 180 unaweza kuchukua pensheni yako. Miaka ya pensheni inabaki ilele ile 55 voluntary na 60 compulsury!

Pili, unategemea hela za withdrawal ndio ukaanzishie mradi?? Huu ni kama wendawazimu
 
Nadhani ile post humu kwamba mifuko inakaribia kufilisika ina ukweli. Kwanini mlione hili sasa wakati hii mifuko iko tangu enzi. Ina maana mlipoanzisha fao la kujitoa hamkuona taabu za uzeeni ndo mnaziona leo? Siku hizi ajira hasa binafsi hazitabiriki mtu anaweza fanya kazi miaka miwili mitatu wanakutema then unaniambia nisubiri uzeeni? Miduko hii inafilisika na wala siyo huruma kwe wazee wala nini.

Mkuu wangu labda nikurekebishe tu sehemu ndogo. Sheria za kuanzisha mifuko hii ya pensheni haikuwahi kuwa na kipengele cha mafao ya kujitoa.

Sema kwa vile asili ya mifuko mingi ya pensheni hapa Tanzania ilianzia kwenye mifuko ya akiba(provident), kwa maana inakuwekea akiba pesa zako mpaka mwisho wa ajira, ndiyo maana kulikua na utaratibu huu wa kujitoa for so many years.

Sheria nyingi zilizobadili Provident Fund kwenda kwenye PENSION fund, ziliondoa(kwenye sheria) utaratibu wa kujitoa. Sababu ilikua lazima uanze na Provident fund ili ujijengee uwezo wa kuwa pension fund pale mfuko ukikomaa.

SSRA walichofanya ni kusimamia sheria ambazo zilikua zimefumbiwa macho kwa kitambo. Hii ni baada ya wataalam mbalimbali wa mifumo hii ya mifuko ya pensheni kushauri kwamba kama taifa tunaelekea pabaya sana kwa kutokua na safety net kwa wazee wetu pindi watakapostaafu.

Hii mifuko ina mapesa ya kutosha na si ya kutetereka leo wala kesho.

Tafuta RAIA MWEMA la wiki hii kuna makala nzuri ya Mwandishi Lula Mwananzila kuhusu vipi hizi vurugu zingeweza kuepushwa kitambo.
 
na wabunge kula pensheni kila baada ya miaka 5? za kwao zinatoka wapi? kwa nini na wao wasisubiri hadi wawe na 55 au 60? huu ubaguzi wa waziwazi ndio unachochea migomo ya wafanyakazi wa kada nyingine!

Mkuu wangu,
Wabunge wetu wengi ni watu wa kuonewa huruma, kwa sababu ukiachilia wachache ambao wana pensheni, wengi wao wanadhani pensheni haiwahusu kwa wao ni waheshmiwa. Mwisho miaka mitano wanavuta cheque wanapeleka kwenye elections(Kosa kubwa!!).

Wako wabunge wengi ambao ukiwaona leo hii walivyopigika na walikuwepo bungeni mpaka 2005 au 2010, hautoamini!. Yote hii ni kukosa uelewa wa nini maana halisi ya pensheni.

Wabunge nao wanapaswa kuwa ndiyo mfano kwa wananchi wanaowaongoza kwa kuwa wa kwanza kujiandikisha kwenye mifuko ya pensheni. Hasa wabunge vijana aina ya Mh. mnyika. Lakini kwa wabunge ambao walishastaafu(miaka 55 au 60), hawatalalizimika tena kujiunga na mifuko hii kwa mujibu wa sheria.
 
mleta mada Sober msome Ndibalema na Magu ukiweza kujibu hoja zao nianza kuchangia zaidi vinginevyo wewe ndiyo unatafuta ujinko tena wa kijinga..

Mkuu, fuatilia majibu niliotoa kwa Ndibalema na majibu ya Rejao kwa Magu, kama una mengine tunaweza kuendelea na debate.

I know hii issue imewagusa wengi, ila ili tujenge taifa la kuheshimika ni lazima tufunge mikanda.
 
Wazo la awali lilikuwa zuri kama wafanyakazi wangekuwa na uhakika wa kudumu kwenye ajira mpaka muda wa kustaafu. Ikumbukwe waajiriwa wengi si wajasiliamali na kwa viwango vya mishahara yetu walio wengi hawana akiba ya kuweza kuwasaidia pindi wakikosa kazi ghafla kama kuachishwa kazi, ulemavu, n.k. Kwa wenzetu nadhani wana utaratibu wa kupewa pesa ya kujikimu kwa wale wasiokuwa na kazi tofauti na sisi.
 
Ccm wameifilisi hiyo mifuko sasa wanatafuta njia za kujihami kwa kuwazuia watu wasichukue pesa yao. Mi kama nimeajiriwa serikalini/mashirika halafu nikaanzisha biashara au kampuni yangu na kijiwe kikanichanganyia ikabidi niache kazi nikiwa na miaka 35 na sina tarajio la kuajiriwa tena, kwa nini nisubiri miaka 25 kuchukua pesa zangu? Haingii akilini.
 
Mkuu mimi nitajadili hayo niliyoweka red.
Mkuu upo nchi gani? nakuuliza hivyo kwa sababu pengine hujui au labda unapotosha kwa makusudi kabisa.
Mfanyakazi hukatwa 10% ya mshahara wake na mwajiri wake hukatwa 10% ya huo mshahara ukipiga mahesabu jumla ya mchango wa mwajiriwa(jumlisha na ule anotoa mwajiri) ni 20% ya mshara wake wa kila mwezi na sio 5% kama ulivyosema.
Pili hiyo michango mwajiriwa ambayo anakuja kuchukua(fao la kujitoa) ni malimbikizo ya kipindi chote alichokuwa akifanya kazi so unavyojaribu kulinganisha malimbikizo na mshahara wa mwezi mmoja kunakuwa hakuna uwiano wowote.

pili ningependa kukuelimisha jambo moja.
Pensheni ni kitu tofauti kabisa na fao lakujitoa.
Kwa Serikali makini hutoa pensheni kwa wazee bila hata kujali kama (huyo mzee) katika ujana alaiajiriwa au la.
Pension inatakiwa iwe ni grant kwa mwananchi mzee.
Fao la kujitoa ni pesa za mwajiriwa ambazo alikuwa akizihifadhi ili zimsaidie kuendesha maisha yake pindi ambapo hatokuwa na ajira tena.(iwe ni kwa kuacha, kufukuzwa kazi au kutokuwa na nguvu za kufanya kazi tena)

Achana naye huyo ni Irene,kasahau kwamba tunakatwa 30% paye na mikopo tuliyokopa 30%!!
 
Ukitaka kuharibu mjadala wako weka ushabiki na kejeli.
 
Hicho unachokisema ndiyo exactly kilichonistua.

Tumezoea kuona wanasiasa wakikimbizana kusaka cheap popularity, lakini siku zote Mnyika ameonesha umakini wa hali ya juu kwa kufanya homework yake vizuri na kujiridhisha.

Lakini kwa nilichokiona leo kimeonyesha kukurupuka kwa hali ya juu, kusikozingatia maslahi mapana ya nchi kwa siku za usoni. Yeye anaongelea kusaka sahihi wakati hajawa hata na kikao kimoja cha wataalam na wadau wengine ili kuona basis ya hoja yake.

Alichofanya ni kuwa carried away na bandwagon ya popularity contest, at the expense ya future generations... Kwa kifupi
anaanza kuonesha dalili za kuwa kama wale wa NDIIIYOOOOO...... siku za usoni.

Pamoja sana.
Tatizo ni hizi hoja za kutetea wanyonge zinapoletwa na upinzani bungeni,ingekuwa ccm hakuna neno,je unakumbuka hoja hii iliibuliwa na mbunge wa ccm na kuambiwa na spika kwenda kukusanya maoni? Je ulisikia malalamiko ya wale wafanyakazi wa migodi kwa yule mbunge wa ccm aliyekwenda kukusanya maoni? Iwapo hoja imeondolewa je malalamiko yao yatajadilliwa na nani? Sasa tumeanza kusikia wafanyakazi waliopo kwenye hiyo mifuko wamegoma na wengine wanafukuzwa kazi je kunafaida hapo? Kwa nini tanzania inaendeshwa kwa maandamano kila mahali bila shaka ni kutokana na maamuzi ya kibabe km haya
 
Sober Hebu tuondolee pumba zako hapa, nenda kapate supu naona bado upo sober tu!! Acha kutumika wewe ngeke,huna ushawishi wowote,mambo ya brella hauyajui kila mtu anafungua kampuni kwa lengo flan unajua deepgreen ilifungua kampuni ikapiga hela na ikafa hyo kampuni? Je unajua makampuni kama hayo and like ya kina muhando yapo mangapi?

Mnyika ni mfano wa kuigwa hana cha kutafuta popularity hata kidogo,wewe ndio unatumika kwa kuchumia tumbo
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom