MchukiaUonevu
JF-Expert Member
- Feb 17, 2012
- 207
- 79
Kimsingi fao la kujitoa liachwe kuwa hiari kwa anayetaka kuacha michango(fedha) yake au anayetaka kuchukua haki yake aruhusiwe kufanya hivyo. Kwa kuwa terms za ajira hutofautiana kati ya mwajiriwa mmoja na mwingine,basi pia hata strategy au style ya kuweka akiba hutofautiana pia. Kwa mfano kuna watu wengi tu kutokana na mishahara yao na majukumu, 10% inayochukuliwa na mfuko wa pensheni ndio savings yake,hiyo 90% inayobaki baada ya kukatwa pensheni hawawezi ku-save kutokana na hali ya maisha.(Na hawa ndio wengi).
Kwa mchanganuo huo ni wazi kwamba mtu atakapoacha ama kuachishwa kazi atategemea ile akiba ndio aanzie maisha kwa wakati husika,sasa kama mtu ana miaka 35,kusubiri miaka 20 ndio achukue haki yake,huu ni ukatili! Na kipindi chote hichi (miaka 20) kama hakuajiriwa tena huyu mtu ataendesha vipi maisha yake.? Hata hivyo,hata kama kutakuwa na interest kwa kipindi NSSF/PPF...wanapokaa na hela yako,sidhani kwa mfumo wa ukuaji wa uchumi wetu kama itaweza kushindana na inflation rate!
Kama tunataka watu wengi wawe na ajira,lazima tu encourage watu kuwa wajasiriamali. Mtu anapoacha kazi na kwenda kuanzisha project yake,kama ni kuku,mgahawa,duka,basi,kilimo,real estate n.k,ni nafasi nyeti ya kuwapa watanzania wengine ajira. Na pale alipoacha kazi pia ni nafasi ya Mtanzania mwingine kuajiriwa. Hizi ndio ajira zenyewe,na sio zile tunazodanganywa na wanasiasa,eti ntawapa vijana ajira,..liers!Sasa tukiweka mfumo huu ni kuwatisha watanzania wasithubutu au waogope kujiajiri na badala yake wajishike kwenye ajira miaka nenda rudi hata kama ajira hiyo haibadilishi maisha yake. Watu waachwe wachukue haki yao mara tu wanapoacha au kuachishwa kazi bila kujali kama ataajiriwa tena au la! Wanaotaka kuendelea kubaki kwenye hii mifuko nao rukhsa.