Mh. Godbless Lema aonja joto la jiwe!

Mh. Godbless Lema aonja joto la jiwe!

picha ndo muhimu,labda huyo mwandishi hana vifaa kutuweza kupata picha u karne ya simu za upepo!
 
kama ni kweli basi watakuwa wamewalipa vijana na kwa kuwa vijana wa ccm wanamawazo finyu kama alivyo sema chitanda..

jibu muulizeni mbunge wa Tarime atakupa jibu kwa kipondo chake sasa magazeth yameandika kinyume
 
Hii ni habari ya kutunga. Godbless kule tarime anakubalika kupita kiasi. Kwani siku walipompopoa kwa mawe mbunge wao, walimsahau Godbless Lema? Si alikuwepo kule kule? Propaganda.
 
Hii ndo serikali ya kiswahili(kikwere,kizaramo,matumbi,wadigo etc) bwana! Inaridhika na chapati na chai basi. Hakuna seriousness hata kidogo, issue sensitive zinachukuliwa kiswahiliswahili tu!
Hata yale ambayo hayajatoka sehemu hizi za kiswahiliswahili bado na menyewe eti yanajibu hoja kama hadija kopa! Nchi hii hatuna serikali kwa sasa period.

Hii serikali inazidi kujichimbia kaburi kila inapojaribu kujibu mapigo ya chadema. Nilishawaambia Nyerere aliwalaani hawa jamaa ila hawajijui. Sasa hivi wanatembea uchi kama kichaa lakini hawajui kama wako uchi. They will never amount to anything mpaka wanaingia kaburini 2015. CCM inawayawaya,imekuwa tambala bovu inaelekea kuzama.

Poleni mgeukieni Mungu ilimsalimike japo roho zenu.





Mungu atusiaidie maana mie
 
Kuna vyombo vya habari vimeamua kujitoa kabisa kwenye soko la habari, muda si mrefu magazeti yao yatakosa wasomaji kabisa, redio zao zitakosa wasikilizaji na tv zao kukosa watazamaji
 
UHURU ni gazeti linaloishi kwa kuuza uongo na kutegemea ruzuku toka CCM. Sijui baada ya 2015 litaishi vipi katika sekta ya magazeti maana CCM haitakuwa na ruzuku tena.
 
Madiwani waomba wadhibiti ukimwi kujengewa uwezo

MADIWANI katika halmashauri ya wilaya ya Bunda mkoani Mara wameiomba serikali kuzijengea uwezo kamati za kudhibiti Ukimwi za ngazi za vitongoji, vijiji na kata ili ziwe kutekeleza majukumu yake ipasavyo. Wakitoa maoni yao kwenye warsha ya siku
Soma Zaidi | Maoni | HabariPicha
slices_04.gif
slices_05.gif
slices_01.gif
slices_02.gif
HABARI ZAIDICUF kizimbani kwa 'ubabe'
Walimu 40 waenda likizo kwa kukosa mishahara
Trafiki waja na mbinu mpya kuwabana madereva
Mfungwa ajiua kwa kujitosa majini
Madiwani Dodoma wasomewa madudu ya Halmashauri

Kama habari hizo ni kutoka habari leo la Jumapili basi batu tunazisubiri, lakini kama ni toleo la Jumamosi habari kama hizo hazipo.
Pili tukio kama hilo vyombo vingine vya habari visipate habari kama radio na TV, na iwe tu uhuru na habari leo ni jambo la kutatanisha.

Kama mtoa mada ametunga nadhani adhabu yake ni kufungia Jamii forums.
 
UHURU ni gazeti linaloishi kwa kuuza uongo na kutegemea ruzuku toka CCM. Sijui baada ya 2015 litaishi vipi katika sekta ya magazeti maana CCM haitakuwa na ruzuku tena.

Halafu halina soko ndio maana wanakuwa na habari za kutunga ili kupata wateja wanaciciem, vinginevyo ni gharama za uendeshaji tu zinaigharibu CCM
 
Wanajiridhisha kwa vile wa kile cha Magamba alipopolewa basi ndo formula na huyu Elibariki (Godbless) lazima atakuwa amepopolewa - Wanaota wanatembea mchana kweupe... Poleni wa Magamba!
 
Hapo hakuna umbeya si kamuulizia hali tu kama kajifungua tupate kumpa hongera zake

Si utamaduni wa kiafrika na hasa niseme wa Kitanzania kwa mwanaume kumuuliza mwanamke asiyekuwa na uhusiano wowote kuhusu ujauzito wake eti kwa kutaka kujua kama amejifungua ili ampe hongera!. Kwa hakika tuna utaratibu kwa kupashana habari kama hizi ndani ya jamii yetu ya kitanzania. Kizazi cha nyoka kinatumaliza!
 
Kwa hiyo tusiwe na tunaamini pia habari kutoka gazeti la Bilicanas na mwanahalisi??
 
Na bado, Lema ni mfano wa generation next ya leaders wa nchi hii, mtazusha mtavumisha cha moto mtakiona!
 
Maiti waliosuswa Tarime waharibika
Imeandikwa na Samson Chacha, Tarime; Tarehe: 21st May 2011​
UTATA wa mazishi ya watu wanne kati ya watano waliouawa baada ya tukio la kuvamia Mgodi wa North Mara wilayani hapa Mei 16 umeendelea, baada ya ndugu wa marehemu kuendelea kususa miili huku ikiendelea kuharibika katika chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali ya wilaya. Hadi Mei 21, ni mwili mmoja tu uliochukuliwa, huku mingine minne ikibaki mochari, kwa maelezo kwamba, ndugu wa marehemu wanamsubiri mganga wao na wanasheria ambao ni viongozi wa Chadema, Mabere Marando na Tundu Lissu.

Habari za uhakika ambazo gazeti hili linazo zinasema, wanandugu hao wamekataa kuchukua miili hiyo mpaka itakapochunguzwa, huku uchunguzi ukishuhudiwa na Marando na Lissu. Miili ambayo mpaka jana ilikuwa haijachukuliwa ni ya mwanafunzi Emmanuel Magige wa
Nyakunguru, Chacha Ngoka mkazi wa Kewanja Nyamongo na waliokuwa wakazi wa Mugumu, wilayani Serengeti, Mwikwabe Marwa na Chawali Bhoke. Mwili pekee uliochukuliwa na kuzikwa ni wa Chacha Mwasi wa Bisarwi Komaswa. Kutokana na kususia maiti, Kamishna wa Jeshi la Polisi anayeshughulia masuala ya Operesheni, Paul Chagonja, amesema jeshi lake linasikitishwa na baadhi ya wanasiasa kuingilia matatizo ya Makosa ya Jinai kwa kushawishi wafiwa kususia miili ya ndugu zao wakati inazidi kuharibika hospitali. “Hakuna polisi aliyemfuata mtu yeyote aliyeshambulia askari wetu kwa mawe na silaha za jadi, pia hatujakataa kuwa waliouawa hawakupigwa risasi na polisi, sasa huyo mganga anayesubiriwa anatarajia kuja kuandika kuwa wameuawa na nini, kama si siasa kavu ya kusumbua ndugu za marehemu?” alihoji.

Chagonja alisema baadhi ya ndugu wa marehemu walitaka kuchukua miili ya ndugu zao, lakini baadaye wakasema wanasubiri daktari wao na wanasheria Marando na Lissu wafike kushuhudia, lakini tangu Jumatano zimekuwa zikitolewa ahadi za uongo huku miili ya marehemu hao ikiharibika. Aliongeza kwamba, tayari Polisi ina taarifa kuwa, wafiwa wamehifadhiwa nyumbani kwa Diwani wa Chadema Mjini hapa (jina tunalo) na kuna ndugu vijijini wameshindwa kufanya shughuli zao za kujipatia kipato wakisubiri kuzika kwa sababu ya kukwamishwa na wanasiasa.

Kamishna Chagonja alisisitiza kwamba, Polisi inafanya uchunguzi wa mauaji hayo na kama itabainika kuwa askari walioua walifanya makusudi, sheria itafuata mkondo wake na hawezi kutoa hukumu kwa kuangalia upande mmoja. Alisema kuna askari zaidi ya saba waliojeruhiwa kwa mawe akiwamo Mrakibu Simon Mrashani na Mrakibu Msaidizi Hassan Maya na wenzao watano. Aidha, magari ya Jeshi yaliharibiwa kwenye mapambano hayo kati ya polisi na watu zaidi ya 800 waliovamia mgodi kutaka kupora mawe ya dhahabu. Wakati ikiwa haijafahamika siku ambayo wanandugu hao wataridhia kuchukua miili ya ndugu zao, Mkuu wa Wilaya, John Henjewele, ameonya kwamba endapo ndugu wa marehemu hao watashindwa kuchukua miili hiyo na kuizika, Serikali itazika. Aidha, aliwaonya wanasiasa, hususani wa Chadema wanaotajwa kujiingiza na kuligeuza tukio hilo kuwa la kisiasa, akiapa kwamba Serikali haitafumbia macho wanaochochea uhalifu.

Mei 20 Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema (Chadema), alirushiwa mawe na kundi la watu katika mji mdogo wa Sirari aliposhawishi vijana wa mji huo kujiunga na maandamano ya chama hicho Mei 21, wakati wa kuchukua miili ya watu wanne, ambayo bado iko mochari.
Tukio hilo lilitokea siku chache baada ya Mbunge wa Tarime, Nyambari Nyangwine na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya hiyo kupitia CCM, Amos Sagara, kupigwa mawe walipokwenda Nyamongo kuwapa pole wafiwa.

Sirari ni ngome ya Sagara ambaye pia ni Diwani wa Sirari, hivyo kutimuliwa kwa mawe kwa Lema kulitafsiriwa kuwa ni kulipa kisasi baada ya vijana wa eneo hilo kuchukizwa na kitendo cha Diwani wao kupigwa Nyamongo na wafuasi wa Chadema.
Habari Leo
​
 
Tunasoburi source nyingine za habari na walio karibu na Mbunge Lema watupe habari kamili, maana taarifa za sasa hazijathibitishwa.
 
Hii ndo serikali ya kiswahili(kikwere,kizaramo,matumbi,wadigo etc) bwana! Inaridhika na chapati na chai basi. Hakuna seriousness hata kidogo, issue sensitive zinachukuliwa kiswahiliswahili tu!
Hata yale ambayo hayajatoka sehemu hizi za kiswahiliswahili bado na menyewe eti yanajibu hoja kama hadija kopa! Nchi hii hatuna serikali kwa sasa period.
Hii serikali inazidi kujichimbia kaburi kila inapojaribu kujibu mapigo ya chadema. Nilishawaambia Nyerere aliwalaani hawa jamaa ila hawajijui. Sasa hivi wanatembea uchi kama kichaa lakini hawajui kama wako uchi. They will never amount to anything mpaka wanaingia kaburini 2015. CCM inawayawaya,imekuwa tambala bovu inaelekea kuzama
Poleni mgeukieni Mungu ilimsalimike japo roho zenu.

Mungu atusiaidie maana mie
Wewe mshamba kabisa unayedhani kuwa kabila fulani au dini fulani ni bora. Hayo ni mawazo mgando tena yanaonyesha una utumwa wa akili'
 
Hii ndo serikali ya kiswahili(kikwere,kizaramo,matumbi,wadigo etc) bwana! Inaridhika na chapati na chai basi. Hakuna seriousness hata kidogo, issue sensitive zinachukuliwa kiswahiliswahili tu!
Hata yale ambayo hayajatoka sehemu hizi za kiswahiliswahili bado na menyewe eti yanajibu hoja kama hadija kopa! Nchi hii hatuna serikali kwa sasa period.

Hii serikali inazidi kujichimbia kaburi kila inapojaribu kujibu mapigo ya chadema. Nilishawaambia Nyerere aliwalaani hawa jamaa ila hawajijui. Sasa hivi wanatembea uchi kama kichaa lakini hawajui kama wako uchi. They will never amount to anything mpaka wanaingia kaburini 2015. CCM inawayawaya,imekuwa tambala bovu inaelekea kuzama.

Poleni mgeukieni Mungu ilimsalimike japo roho zenu.





Mungu atusiaidie maana mie

Hilo kabila lako unaliona bora zaidi ya hayo uliyoyataja hapo juu. Huu ni ujinga na upumbavu usio na kipimo. Binadamu wote ni sawa pale unapoondoa mapungufu ya mtu mmoja mmoja. Wewe naona una akili za Ki CCm CCm (Uchaga na Chadema while CCM knows wanajua fika wana Wabunge uchagani). Hatutaki akili mgando zenye kudharau, kudhalilisha na ubaguzi wa utu wa Mtanzania.
 
Umesahau kwamba lema anavuta ile kitu mbaya kwa kizazi.cha sasa

Sijasahau na wala sijui kabisa tena sijawahi kusikia kuwa anavuta. Ila wewe ndugu Makupa ndo nasikiasikia unavuta hiyo sigara kubwa, ama labda source yangu siyo reliable!!!!! :focus:
 
Back
Top Bottom