Mh. Godbless Lema aonja joto la jiwe!

Ccm inabidi mjue nyie (hata kama mlichakachua kula) inabidi mjue nyie ndio wenye dhamana na hii nchi, ushabiki wenu wa kijinga kushabikia fujo sijui mmetoa wapi?

Naona sasa mmepoteza dira hamjui hata mlivyokuwa mnachakachua kura mlitaka kuwafanyia nini wadanganyika? Sasa badala ya kufanya chochote kuwasaidia wadanganyika mmebaki kuingia kwenye malumbano na wapinzani.

Waacheni wapinzani wafanye kazi yao ya kuhamasisha wananchi, mwenye uwezo wa kuchambua mbivu na mbichi ni wananchi wenyewe sasa nyie mna 5 years ahead kuongoza chapeni kazi acheni bla bla.
 
Ccm bana...inanikumbusha karimjee walipoleta vitoto ili vizomee kisa jana yake tambwe kazomewa..kwanza ingekuwa kwel TBC wasitangaze kwel?

wangetangaza kwa nguvu zao zote na kwa sura ya tabasamu.
Tuwaombee kwa Mungu tu hawa wenzetu wanaonyenyekea mikate kwa kuliabudu tumbo, akili zao huwezi kuzitofautisha na watoto we enzi za Tsh. 20, ambao walikua wanaikataa Tsh.100 na kuililia Tsh.20 kwa sababu ilikua kubwa in size than Tsh.100.
USIPOTEZE MUDA WAKO KUBISHANA NA MTU ANAYETUMIA REFERENCE TOFAUTI NA YAKO KULITAZAMA JAMBO.
 
Chadema sio watu wa kukurupuka, Maandamano yao always huwa na Mantiki. Mh Lema yupo Arusha!
 
Mkuu, unayosema ni ukweli mtupu

Mkuu huyu lema asipoacha hicho hicho kitu anachovuta mpaka kinamfanya kama chizi naamini hatamaliza kipindi chake cha ubunge kabla hajachanganyikiwa moja kwa moja na kwa umri alionao tiba inakuwa inakuwa ni ngumu sana labda kama anazo kama akina MARADONA
 
Hizi habari za kweli kabisa kuna jamaa yangu alikuwa huko ndio kaniambia, kweli Lema kapondwa jiwe, huyu jamaa ni pumba sana sijui huo ubunge alipataje, yaani ni mtu wa fujo

Kumbe uliambiwa na jamaa yako!! Wewe na jamaa yako wote wapuuzi kwa kueneza uongo hapa.
 
Mkuu huyu lema asipoacha hicho hicho kitu anachovuta mpaka kinamfanya kama chizi naamini hatamaliza kipindi chake cha ubunge kabla hajachanganyikiwa moja kwa moja na kwa umri alionao tiba inakuwa inakuwa ni ngumu sana labda kama anazo kama akina MARADONA

hii ccm ya sasa bila kupiga ile kitu kazi haiendi kamanda lema usiingie jukwaani bila kupiga maana hata obama ilimtoa.
 
hii ccm ya sasa bila kupiga ile kitu kazi haiendi kamanda lema usiingie jukwaani bila kupiga maana hata obama ilimtoa.

beerobama-300x246.jpg

bila hii kitu mambo hayaendi
 
Cdm msipomthibiti huyu lema atakiua chama kama si akili punguani watu wanaomboleza yeye anaenda kuhamasisha maandamano shame on you uongozi wote wa cdm
Ni kweli cdm wasipomdhibiti Lema ataua chama cha magamba ccm, wajinga wakubwa nyie mnaotetea upuuzi wa polisi kuua raia wema kwa kisingizio kwamba ni majambazi kama walikua ni majambazi kwanini polisi wanataka kuwapa pesa ili wazike tangu lini polisi wanatoa pesa kuwalipa waharifu? kama Lema ndie aliyeenda kuhamasisha fujo je Lema huyo huyo ndie aliyehamasisha polisi kupiga raia risasi kwa kisingizio kwamba ni majambazi? lakini pia Lema amekuja hapa tarime tarehe 19 raia wameuwawa tarehe 16 hamuwezi kuona huo utofauti? shame on you polisi na huyo mbunge kilaza aseme tu kwamba hakubaliki kama anafikiri kwamba wananchi wamechochewa kumpiga basi hakubaliki, mtu akija kwako akachochea familia yako wakakupiga basi maana yake ni kwamba ana ushawishi nyumbani kwako kuliko wewe aibu, kama nyambari anaweza aende jimboni kwa Lema nae akachochee wampige tuone asituletee propaganda za kijinga za tbc,uhuru jambo leo na habari leo,
 
Mkuu huyu lema asipoacha hicho hicho kitu anachovuta mpaka kinamfanya kama chizi naamini hatamaliza kipindi chake cha ubunge kabla hajachanganyikiwa moja kwa moja na kwa umri alionao tiba inakuwa inakuwa ni ngumu sana labda kama anazo kama akina MARADONA

Hizi habari za kweli kabisa kuna jamaa yangu alikuwa huko ndio kaniambia, kweli Lema kapondwa jiwe, huyu jamaa ni pumba sana sijui huo ubunge alipataje, yaani ni mtu wa fujo

Mama umeshajifungua? Achana na Lema kila mtu anajua kuwa Lema ni wicked crook! Inawezekana alifuata ule mmea huko Tarime

Hivi ili habari iwe ni ya ukweli inatakiwa iripotiwe katika chombo kipi cha habari? Kwa hali ilivyo sasa hivi ni kwamba habari ni habari pale inaporipotiwa katika magazeti fulani ambayo machoni mwa wateule fulani ni reliable!
Nimeipenda hii Signature ya Uncle Rukus naona ina ujumbe muhimu sana kwenu ila naona siku hizi mnazidi kupungua au ndio kujivua gamba.
:angry:Ni ujinga kukubali kutumiwa kama Condom:msela:, kwa raha na maslahi ya watu wengine
 
MBUNGE wa Arusha Mjini Kupitia Chadema, Godbless Lema, amerushiwa mawe na kundi la watu katika mji mdogo wa Sirari alipotaka kushawishi vijana katika mji huo kujiunga na maandamano ya chama hicho jana wakati wa kuchukua miili ya watu wanne ambao bado ipo mochari ya hospitali ya wilaya ya Tarime.

Kamanda Mkoa wa Tarime/Rorya, Costantine Massawe, jana alithibitisha tukio hilo la kurushiwa mawe lililofanyika saa 11 jioni wakati Mbunge huyo alipokwenda Sirari akiwa na gari lake na wafuasi wa Chadema waliokuwa na sare za chama hicho waliposhuka kutoka ndani ya gari hilo huku wakisema nguvu ya umma hadi kieleweke, na kuanza kuwakusanya vijana kwa nia ya kuwashawishi wajiunge na maandamano ya chama hicho mjini Tarime na Nyamongo.

Kamanda Massawe alisema Jeshi lake lilipata taarifa kuwapo na mkusanyiko usio halali uliokuwa unafanywa na wafuasi wa chama hicho katika mji huo wa Sirari, ambapo msafara huo wa Lema ulikumbana na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya hiyo kupitia CCM, Amos Sagara.

Sagara ni Diwani wa kata hiyo ya Sirari na mmoja wa watu waliopigwa mawe katika msafara wa Mbunge wa Jimbo hilo, Nyambari Nyangwine, Nyamongo, ambapo vijana wa maeneo hayo ya Sirari walikasirishwa na kitendo cha Diwani wao na Mwenyekiti wa Halmashauri kupigwa Nyamongo na wafuasi wa Chadema, ambapo nao walitaka kulipiza kisasi.

Mbunge Lema na msafara wake walipanda ndani ya gari aina ya Toyota Land Cruiser haraka huku wengine wakining’inia mlango wa nyuma huku mvua ya mawe ikiwafuata nao wakipiga mayowe hadi kituo kidogo cha Polisi katika eneo la Forodha na msafara huo kuokolewa na polisi wa kituo hicho waliojihami kwa silaha kuzuia vijana hao waliokuwa na hasira na kisha kusindikizwa na polisi kuondoka katika maeneo ya mji huo.

Hali ya kisiasa wilayani hapa si shwari kutokana na vurugu za watu watano waliouawa walipovamia mgodi wa North Mara Barrick ambapo Chadema imekuwa ikiegemea kwa familia za marehemu na kuzishawishi kususa miili hiyo.

Mkuu wa Wilaya Tarime, John Henjewele, ameonya kwa wanachama wa vyama vya siasa wanaotaka kuleta vurugu kwa kutumia maafa hayo kisiasa, Serikali itawachukulia hatua kali. Hilo ni tukio la pili la kupigwa mawe wabunge ambapo Mei 18, Nyangwine na msafara wake walishambuliwa Nyamongo walipokwenda kuwapa pole wafiwa.

Source: Habari Leo

my take:
Hili gazeti naona limegeuka kuwa la udaku, muda wanaousema wa saa 11 jioni Mh. Lema alikuwa Arusha na aliwahutubia wananchi maeneo ya hospitali ya St. Thomas.
Gazeti la habari leo, uhuru pamoja mwananchi linaandikiwa na kilaza mmoja anaitwa samson chacha pia huyu jamaa alikua mwenyekiti wa kijiji kupitia ccm. huyu jamaa ni muongo sana akipewa hela anaweza kuandika chochote huku Tarime tunamuiita nyoka sababu ya uzushi wake ccm hawana uwezo wakumpiga Lema sababu wako wachache sana hapa tarime nyoka kafie mbali na uzushi wako kama lema alipigwa weka picha tuone
 
magazeti yanayopokea habari za kupikwa za akina ridhiwani, amos makala, maregesi wa epa na mafisadi wengine ambao kila kukicha wanatumia magazeti kutafuta njia ya kuwachafua wabunge na viongozi wa CDM. Hayana lolote hayo na uzur ni kuwa hata wananchi siku hizi wamewastukia na magazeti hayo yanasomwa na wale wanaotafuta tender serikalini na kwenye chama (chama cha magamba).
 
Wandugu JF members hivi huyu anaitwa Shibuda yuko wapi mbona haonekani katika harakati za peoples power? Au ndio tuseme nini juu yake.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom