Mh Godbless Lema amjibu Tendwa

kinachozunguka kinarudi kilipotoka, na kipandacho hatimaye hushuka,
Hakuna cha wazee wa mila wale wazee wa boma, Arumeru ni Tanzania na mtanzania yeyote anaweza kwenda muda wowote.
Huyu Tendwa anazeeka vibaya na siasa za maji ya chooni.
 
  • Thanks
Reactions: FJM
watanzania tuelimike sasa, si chochote vurugu zote zinatoka CCM ona walivyojichora wakati wa kupendekeza wabunge katika vyama vyao kila kona kabla ya uchaguzi. wameshajulikana hao......kuchakachua kura ndio mbinu yao. then inashangaza unaongozaje watu wasiokutambua wala kukutaka.
wajue Kimya kingi kishindo kikuu.
Kuna Mtu alitegemea Ghadafi atakuja kuondolewa madarakani....ingwa siungi kifo chake na kuwekwa sokoni, ila aliondoka bila kupenda
 
Tendwa kweli ni JK( janga la kitaifa)Nakumbuka 2010 alipotoa hukumu kuhusu kukosa sifa kwa mgombea wa urais wa ccm alisema kila chama kimepewa hukumu hivyo yeyote anayetaka kujua wavione vyama husika. Ilishangaa sana hukumu gani hiyo ambayo haiwekwi wazi?Ila ninaamini muda wao wa kurelax unakaribia mwisho. Tunataka utaifa kwanza mengine yafuate.
 
Kama mambo ndiyo hivi kuna siku tutasikia Tendwa anatwambia mgombea fulani asifanye kampeni ktk jimbo fulani kwasababu wazee wa kimila wamesema amewakosea heshima kugombea kupitia upinzani!!
 
Kwa masikito kabisa naomba niseme mbegu inayopandikishwa kwenye siasa za Tanzania kwa sasa itazamisha hii nchi. Wazee hawa walitukwana lini? Na kwa nini hawachukuwa hatua wakati huo? Wanapata wapi mamlaka kisheria ya kusema mtanzania fulani harusiwi mahali fulani? Katiba inasema wazi juu ya uhuru wa raia ndani ya mipaka ya nchi, sasa hawa wazee wa Kimeru wanataka kutuambia mila zao ziko juu ya katiba ya nchi hii? Kwa nini wasiende mahakamani kama kweli Lema amewakwaza?

Hawa wazee wa Kimeru wamenifadhaisha sana. Hivi kweli tuna wazee mufilisi kama hao?
Lakini linalonisikitisha zaidi ni kauli za msajili wa vyama vya siasa hapa nchini. Tendwa anaona hatari ya kugawa watu kwa makabila au anajali mshahara wake? Leo hii wataanza wazee wa kimeru, kesho watakuja wamasai, keshokutwa watakuwa wagogo, mwishoni tutajikuta tunaugua ugonjwa wa Kenya. Na sasa wameanza makanisani.

Natamani vijana wa Arumeru wafanye kinyume kabisa na matwaka ya hawa wazee hatari! Wawashikishe adabu kwa kuchagua mtu ambaye wazee hawamtaki.
 
Mkuu WildCard,

Mkuu Mbowe ni mMachame kabila linalofanana lugha kwa karibu sana na kabila waMeru.waMeru na waMachame wanatengenishwa na uwanja wa ndege wa Kilimanjaro [KIA].WaMachame ni waChagga utashangaa hawasikilizani kabisa na waMarangu au waRombo toka mkoa wa Kilimanjaro lakini wanasilikizana baadhi ya matashi kwa kiasi kikubwa na waMeru toka mkoa wa Arusha.


Mbowe atakwenda kwenye kampeni hizi? Dr Slaa na Ukatoliki wake je? Siasa za AruMeru ni hasa. Tendwa naye anazidi kuwachafua CHADEMA.
 
Kwa masikito kabisa naomba niseme mbegu inayopandikishwa kwenye siasa za Tanzania kwa sasa itazamisha hii nchi. Wazee hawa walitukwana lini? Na kwa nini hawachukuwa hatua wakati huo? Wanapata wapi mamlaka kisheria ya kusema mtanzania fulani harusiwi mahali fulani? Katiba inasema wazi juu ya uhuru wa raia ndani ya mipaka ya nchi, sasa hawa wazee wa Kimeru wanataka kutuambia mila zao ziko juu ya katiba ya nchi hii? Kwa nini wasiende mahakamani kama kweli Lema amewakwaza?

Hawa wazee wa Kimeru wamefedhaisha sana. Hivi kweli tuna wazee mufilisi kama hao?
Lakini linalonisikitisha zaidi ni kauli za msajili wa vyama vya siasa hapa nchini. Tendwa anaona hatari ya kugawa watu kwa makabila au anajali mshahara wake? Leo hii wataanza wazee wa kimeru, kesho watakuja wamasai, keshokutwa watakuwa wagogo, mwishoni tutajikuta tunaugua ugonjwa wa Kenya. Na sasa wameanza makanisani.

Natamani vijana wa Arumeru wafanye kinyume kabisa na matwaka ya hawa wazee hatari! Wawashikishe adabu kwa kuchagua mtu ambaye wazee hawamtaki.
Hizi ndio huwa zinaitwa SIASA KATILI. Lowasa na washirika wake wa 1995-2005 wanazijua sana hizi. Kumbuka mambo aliyoundiwa SAS kwenye kinyang'anyiro cha Urais mwaka 2005. CHADEMA na sio mgombea wao, wajiandae kwa makombora ya aina hii toka kwa wapinzani wao. Piga ua mkwe wetu lazima awe Mbunge. Amrithi babae.
 
  • Thanks
Reactions: FJM
CCM ni chama cha waislam. Hakina tofauti na mzoga wa mbwa!

Kauli hii siyo nzuri kuhusisha dini na mzoga wa mbwa!!!! Kiukweli hata CCM haina la maana lakini usifikie kufanya conclusion kuwa ni chama cha waislamu!!!!! Madai yako hayana ushahidi wa moja kwa moja bali kama tetesi tu kuwa CCM ni chama cha kidini.
 
Wana JF kitendo cha Msajili wa vyama vya siasa Jonn Tendwa kazungumza na Waandishi wa habari na kusema kuwa katika tathimini yake katika uchaguzi wa Arumeru Wazee wa kimila wamemwambia kuwa wanamwonya Lema asiende kwenye kampeni eti watamuuwa kauli hii imenisikitisha kama si kunishangaza kuwa Tanzania kuna tatizo gani?.

Hii bila kumumunya maneneo ni makakati wa ndani wa CCM wa kuandaa mazingira ya vurugu ili ikionekena CCM inashindwa waanzishe vurugu katika kampeni ili watu waumizwe waogope kwenda kupiga kura.

Hili naomba CHADEMA wajiandae mapema . Haingii akilini mtu wa heshima kama msajili wa vyama kuongelea vitu vya vurugu kutoka kwa watu wa kimila waabudu mizimu na wasiomjua Mungu. Nasema hakika haya mnayofanya laana ya Mungu na damu zitakazo mwagika bila hatia itakuwa juu yako na familia yako na vizazi vyako.

Mimi nadhani wazee hawa ilikuwa ni wakati wa kujenga Tanzania yenye amani zaidi kwa kuweka mazingiza ya watu kushindana kwa hoja na kwa amani ili ichi yetu ambayo imepata heshima kubwa iendelee kuwa nchi ya amani.

Tuachane na mawazo mgando kuwa ni lazima nyie muendelee kutawala na kutumia mbinu hata zisizofaa jamani tuamke watu wa aina ya Tendwa ni ukoma kwa Taifa.
HAIKUBALIKI KAMWE KUTUMIA UKABILA KATIKA KAMPENI ZA ARUMERU MASHARIKI,NASEMA KWA SABABU WAPO WATANZANIA AMBAO WAKO TAYARI KUFA KUPINGA HILI JAMBO AMBALO LINAPIGIWA DEBE NA KIONGOZI WA KITAIFA KAMA JT,NAWAITA WATZ WOTE TUANDAMANE HUMU JAMVINI KUMPINGA YEYE NA WOTE WENYE KUTUMIA KAMPENI ZA UKABILA.WATANZANIA TUNAANZA KUJUANA KWA MAKABILA? JE WAZEE WA KABILA FULANI HAWANA TOFAUTI YA ITIKADI ZA KICHAMA YAANI WOTE NI CCM? NANI KAWATUMA NA KUWALENGESHA KWA MSAJILI WA VYAMA? Sasa G.LEMA NENDA ARUMERI TUONE KATIBA ITACHEZEWA NA NANI NA KUTATOKEA JAMBO AMBALO NI HATARI KAMA UKABILA UTARUHUSIWA KWENYE KAMPENI HIZO. Mwisho nashauri wazee wa busara na hekima waingilie kati kupiga vita wazee wa kikabila kuacha kutishia raia wa nchi yao.PIA VYOMBO VYA HABARI NA MSAJILI WAWE TAYARI KUPELEKWA THE 'HAGUE' KAMA MAUAJI
 
  • Thanks
Reactions: FJM
CCM ni chama cha waislam. Hakina tofauti na mzoga wa mbwa!

Mkuu, acha kutoa kauli za aina hii unless una concrete evidence kuthibitisha hayo madai yako. Ubaguzi wa kidini ni hatari sana kwa usalama wa nchi yetu.
Tuwachambueni ccm kwa kuangalia udhaifu wao wa kisera, kiutendaji, na mambo mengine yanayoendana na siasa, lakini siyo kwa kutazama dini zao.
 
Tendwa Janga la Taifa,sijuwi huyu mzee kwanza anawatoto wanaakili timamu.Mimi ningekua hata ni jirani yangu huko kwetu ningemshauri kitu kimaoja ,aachane na kazi hii ,awe mshauri wa sheria katika kampuni za uwakili siamesoma na Jaji mstaafu,huyu mzee anakokwenda ni kubaya,watu watampinga mimi nakwambieni hayo mambo anayodai ni zamani kwelikweli,wewe na usomi wako huo huwezi kuzungumuzia habari za kishirikiana mbele ya kamera/TV ,aise ndo maana nasikia viongozi wengi wanatembea na mabodyguard wawili,wa kwanza ni ulinzi wa macho ,mwingine wa kiroho,--hiyo ni kubali ni kweli ,ref mwanza wewe angalia tu kiongozi wetu akiwa ameenda sehemu hakubariki,utaona huko nyuma yake kuna walizi wamesimama wawili,wote wanakazi mbili,then kunamutindo siku hizi wa pete ,ref,mtoto wa mkulima mbona zamani alikuwa hana pete leo hii ndo kafanikiwa ndo anavaa pete?

Kaka, ungemshauri awe mshauri wa kampuni za kisheria wakati hapo kwenye kikao cha hao anaowaita wazee wa kimeru ameshindwa kuwaambia kuwa hilo wanalo taka kulifanya ni jinai? huko kwenye hizo kampuni si ndo atakuwa Hazard kabisa, huwa najiulizaga hivi hawa watu wa magamba vyuo walivyo soma ndo hivi hivi tunavyo vifahamu au mara baada ya hizo shule walikwenda kwenye shule zingine zinazo fundisha kwa Mtaala wa Kimagamba?

Anyway, ndo maana huwa wanaingia mikataba ya kuangamiza taifa then hao hao wanaenda mahakamani kushitaki wanashindwa na serikali inaaingia kwenye wakati mgumu zaidi, shame on him.
 
Source: Habari leo.Ingawa chanzo cha habari ni tata lakini ninavyowajuwa Wameru ni watu wa vurugu mtindo mmoja CCM wanaweza kutumia nafasi hiyo kupenyeza sumu ya uasi mara wakigundua maji yako shingoni.Ni vyema CDM wakamwondoa G Lema katika kampeni za Meru vinginevyo watajuta na uenda ukawa mwanzo mbaya wa CDM katika siasa za kanda ya kaskazini.

Ikumbukwe Laigwanani Elowassa atapenda kuonyesha bado ni mwanasiasa muhimu katika eneo la Arusha na Manyara ili ndoto zake za urais mwaka 2015 zizidi kung'aa.Sijui Lema alitamka maneno gani ila ninachojua ni mmoja wa wanasiasa wachovu kupindukia wasiojua ABC ya siasa ni bahati mbaya sana nilitoa taadhari mapema lakini hakuna aliyetaka kusikia au kuamini nilichosema.

G Lema asiende Arumeru kama hawajui wameru angewauliza Rais wa awamu ya pili A H Mwinyi,A L Mrema na Askofu Dr Thomas Laiser na Askofu Dr Erasto Kweka katika mgogoro wa KKKT kanda ya kaskazini.Wameru ni rahisi sana kutumika hasa katika zama hizi ambazo vijana hawana ajira.

Huishi kufiki kinyume kwenye suala linalomgusa Lema? Kama katenda kosa la jinai si wamfungulie mshitaka?
 
Kweli Nchi Inaelekea Pabaya sana, sasa nimeamini katika Nchi hii Ukiwa Upande wa Chama Cha Mapinduzi hata Umtukane Rais wewe Utapeta tu, Hata utishie Kuua Mtu maadam unafanya hivyo kwa Maslahi ya Chama wewe Utapeta, Na ninaamini hata uue Mtu maadam unafanya hivyo kwa Maslahi ya Chama UTAPETA tu

Naanza kwa Kwa Kuwauliza Wafuatao

1. Kamanda Saidi Mwema Umeyasikia ya ARUMERU?
2. Andengenye Umeyasikia ya Arumeru?
3. Kikwete ( Mwenyekiti wa CCM na Amiri Jeshi Mkuu) Umeyasikia ya Arumeru?

Kwamba CCM kupitia Wazee wake wa Arumeru wamemwomba Kiongozi Mwandamizi wa Serikali Ndg John Tendwa ( Ambaye ni Msajili na Mlezi wa Vyama vya Siasa) amfikishie Ujumbe Mbunge wa Arusha Mjini Ndg Gobless Lema kwamba Akifika Arumeru tu DAMU YAKE HALALI YAO.

Nikiwa kama Mtanzania na Mpenda Amani nimesikitishwa sana na Kiwango cha U.puu.zi alichoonesha Ndg John Tendwa kukubali kuwa Messeger wa Wauwaji.

Nilitegemea baada ya Wazee hao ambao Bila shaka wanafahamika kumtakia Maneno hayo Mpuuzi Tendwa ( Naomba nimwite Mpuuzi) badala ya Kuita Vyombo vya Habari na Kumfikishia Ujumbe huo Mh Gobless Lema angepeleka Taarifa katika Jeshi la Polisi ili Hao Wanaojiita Wazee wa Arumeru Wakamatwe na Kuchukuliwa hatua Stahiki ( Naamini kutoa ahadi ya kuua mtu, tena Mbele ya Kiongozi wa Serikali ni Kosa la Jinai)

Sitashangaa sana kesho hao Wazee hao Wauaji wa Arumeru wakitimiza Ahadi yao waliyoitoa Mbele ya Ndugu Tendwa Serikali na ikitoka na Kusema kwamba " Tulishamuonya Lema kupitia kwa Tendwa lakini hakusikia". Moderators itabidi mnisamehe kwa kweli ila sina Jina la Kumpa KUWADI WA MAUAJI TENDWA zaidi ya MPUUZI, ALIYELEWA UGIMBI WA MADARAKA.

Nasema Tendwa ni Kuwadi wa Mauaji, anapaswa kukamatwa na kueleza Mengine ambayo ameelezwa na Wauaji Hao, hatuwezi Jua inawezekana hata Silaha itakayomuua Lema anaifahamu

Natoa Mwito kwa Saidi Mwema, Kiwete, Naohodha na Vyombo vya Usalama kwa Ujumla kuwakamata Hao Wazee Wauaji wa CCM na Kuwadi wao Tendwa akawe Shahidi Nambari Moja. Tumeona yaliyotokea Songea kwa Sababu tu ya Watu waliolewa Ugimbi wa Madaraka kupuuzia Vilio vya Wananchi juu ya Kauli kama Hizi Zilizotolewa na Wazee wa CCM Arumeru ambazo hata ahzihitaji Ushahidi Maana zimetolewa Mbele ya Kiongozi wa Serikali

Mods Tafadhali Msiunganishe hii
 
kumtenganisha tenga na ccm ni kazi bora tu ungefanya kazi hii hapa chini
:eyebrows::eyebrows::photo:
Utaishia :crutch: kama sio :washing: ama :hatari:

AZHQlyXv3PIKAAAAAElFTkSuQmCC
 
Vipi mbona mapovu yanakutoka umesoma post nzima ukaona utoke hivi mijitu mingine hovyo kabisa.

Huishi kufiki kinyume kwenye suala linalomgusa Lema? Kama katenda kosa la jinai si wamfungulie mshitaka?
 
Back
Top Bottom