Mh Godbless Lema amjibu Tendwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mh Godbless Lema amjibu Tendwa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Joblube, Feb 23, 2012.

  1. J

    Joblube JF-Expert Member

    #1
    Feb 23, 2012
    Joined: Mar 4, 2011
    Messages: 367
    Likes Received: 2
    Trophy Points: 35
    Wana JF kitendo cha Msajili wa vyama vya siasa Jonn Tendwa kazungumza na Waandishi wa habari na kusema kuwa katika tathimini yake katika uchaguzi wa Arumeru Wazee wa kimila wamemwambia kuwa wanamwonya Lema asiende kwenye kampeni eti watamuuwa kauli hii imenisikitisha kama si kunishangaza kuwa Tanzania kuna tatizo gani?.

    Hii bila kumumunya maneneo ni makakati wa ndani wa CCM wa kuandaa mazingira ya vurugu ili ikionekena CCM inashindwa waanzishe vurugu katika kampeni ili watu waumizwe waogope kwenda kupiga kura.

    Hili naomba CHADEMA wajiandae mapema . Haingii akilini mtu wa heshima kama msajili wa vyama kuongelea vitu vya vurugu kutoka kwa watu wa kimila waabudu mizimu na wasiomjua Mungu. Nasema hakika haya mnayofanya laana ya Mungu na damu zitakazo mwagika bila hatia itakuwa juu yako na familia yako na vizazi vyako.

    Mimi nadhani wazee hawa ilikuwa ni wakati wa kujenga Tanzania yenye amani zaidi kwa kuweka mazingiza ya watu kushindana kwa hoja na kwa amani ili ichi yetu ambayo imepata heshima kubwa iendelee kuwa nchi ya amani.

    Tuachane na mawazo mgando kuwa ni lazima nyie muendelee kutawala na kutumia mbinu hata zisizofaa jamani tuamke watu wa aina ya Tendwa ni ukoma kwa Taifa.
     
  2. Mwita Maranya

    Mwita Maranya JF-Expert Member

    #2
    Feb 23, 2012
    Joined: Jul 1, 2008
    Messages: 10,569
    Likes Received: 104
    Trophy Points: 145
    Pamoja na Tendwa kuwa msajili wa vyama vya siasa, na kwa mantiki hiyo yeye ndiye mlezi wa vyama vyote vya siasa nchini kisheria, lakini kiuhalisia Tendwa amekuwa ni mlezi wa ccm na amekuwa akifanya mambo mengi ya kijinga ili kuisaidia ccm.

    Tendwa huyu ndiye alikurupuka na kutaka kuhalalisha raisi kikwete kuzidisha muda wa kampeni mwaka 2010 wakati wagombea wengine wakishushwa na polisi toka majukwaani, ama kuzuiliwa kupanda majukwaani hadi pale NEC ilipokuja kumkana.

    Tendwa huyu ndiye alishiriki kikamilifu kukihujumu chama cha CCJ kisipate usajili wa kudumu ili kuinusuru ccm na hofu ya wanachama wake kadhaa kujimega na kutimkia huko.

    Tendwa huyu ndiye alifumbia macho na ameendelea kufumbia macho matumizi makubwa ya fedha yaliyofanywa na ccm katika kampeni za uchaguzi mkuu mwaka 2010 na katika chaguzi ndogo wakati amepewa uwezo na mamlaka kisheria, kwa mujibu wa sheria ya gharama za uchaguzi ya 2010.

    Mambo ya hovyo yanayofanywa na Tendwa ni mengi sana kuyaeleza, lakini itoshe kusema kwamba kama kuna mtu amekuwa akifikiria kwamba Tendwa hayuko bias basi alikuwa anakosea sana na amtazame Tendwa kwa uangalifu mkubvwa atamuona jinsi anavyotumia ofisi yake kukisaidia chama chake cha ccm.
     
  3. GeniusBrain

    GeniusBrain JF-Expert Member

    #3
    Feb 23, 2012
    Joined: Nov 3, 2010
    Messages: 4,321
    Likes Received: 18
    Trophy Points: 135
    Napata wasiwasi na uwezo wako wakuchambua mambo, ni mdogo mno kuzidi hata punje ya mchanga !

     
  4. Wambandwa

    Wambandwa JF-Expert Member

    #4
    Feb 23, 2012
    Joined: Dec 3, 2006
    Messages: 2,240
    Likes Received: 337
    Trophy Points: 180
    Huyu Tendwa umri unamtupa mkono, ajabu badala ya kuwa na hekima na busara anakuwa na akili kama ya mtu taahira. Kama kweli wazee wa kimeru walimwambia maneno hayo kweli kwa nini asikae nao na ku resolve tatizo hili?

    Kuzungumza na waandishi wa habari jambo hili ili iweje, Lema asiende kufanya kampeni wakti ukifika? Mh. Lema hawezi kukubali, na huko CCM kazi wanayo ndo watajua kuwa kwa kumweka mkwewe EL wamepotea njia. Ngoja tusubiri tuone, kule si Igunga watu wa Meru wanakula na kushiba wanakunywa maziwa badala ya chai hivyo njaa iliyotengenezwa na CCM kule hakuna, hawaongeki au tuseme hawauzi kura yao.
     
  5. Bhbm

    Bhbm JF-Expert Member

    #5
    Feb 23, 2012
    Joined: Oct 31, 2009
    Messages: 716
    Likes Received: 17
    Trophy Points: 35
    Sasa wewe mwenye brain nyingi si uonyeshe uwezo wako hapa kwa kumwaga point za maana....mtu mzima hovyooooo
     
  6. KirilOriginal

    KirilOriginal JF-Expert Member

    #6
    Feb 23, 2012
    Joined: Feb 13, 2012
    Messages: 1,921
    Likes Received: 444
    Trophy Points: 180
    Magamba wameanza, wameru tunawafahamu vzr, sasa hili la Tendwa ni janja ya ccm kujisogeza karibu na watu wa arumeru, magamba ndo zao wanalia kukanyagana wamezoea kuwadanganya watanzania kila kona ya nchi ref Igunga. Mzee Tendwa usiwasaidie magamba kupenya arumeru acha ngoma iwe faire play
     
  7. Ileje

    Ileje JF-Expert Member

    #7
    Feb 23, 2012
    Joined: Dec 20, 2011
    Messages: 3,872
    Likes Received: 1,658
    Trophy Points: 280
    Kilichotakiwa na Tendwa ni kuwaonya wazee wasijiingize katika uvunjifu wa amani na pia kuiomba serikali kuimarisha ulinzi ili kampeni zifanyike kwa haki na amani.
     
  8. B

    Bobuk JF-Expert Member

    #8
    Feb 23, 2012
    Joined: Oct 8, 2010
    Messages: 5,876
    Likes Received: 481
    Trophy Points: 180
    I have never ranked Tendwa high! Mimi ninajiuliza hata huo U-JUDGE aliupataje? au ndiyo ainadhirisha ule msemo kwamba CCM is a mental disease? Once you're a CCM zealot your thinking and reasoning capacity approaches ZERO!!.

    Yaani "Wazee" wanapanga kufanya JINAI, tena JINAI ya kutoa ROHO ya mtu, mbele ya Kiongozi Mkubwa, Msajili wa vyama vya SIASA, tena mwenye Cheo cha U-JUDGE (Kama kweli ni judge, maana wajita kila mtu ni JUDGE), badala ya kwenda kutoa report POLICE ili kuzuia hiyo JINAI isitendeke JUDGE mzima na k.o.r.o.n.d.a.n.i zake anakwenda kuropoka kwenye vyombo vya habari? Hivi kweli huyu anayejiita JUDGE alipass hata hiyo LLB 101? Au ndiyo wale ma-JUDGE wa Kijita?! YEGO JAJI
    Kama ma-Judge tulionao nchi hii ni wa aina ya akina Tendwa no wonder mahakama zetu zimeshindwa kutenda HAKI. Huyu Tendwa kama angeletewa kesi yaina I suspect angetoa SUMMARY DISMISSAL kwamba Lema ameuawa kwa KIHEREHERE chake kwasababu alionywa hakusikia.

    Ruling za aina hii is ONLY POSSIBLE IN TANZANIA.
     
  9. DOUGLAS SALLU

    DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

    #9
    Feb 23, 2012
    Joined: Nov 13, 2009
    Messages: 11,591
    Likes Received: 4,702
    Trophy Points: 280
    Kama kuna mtu anastahili kuuwawa basi ni yeye Tendwa,mnafiki mkubwa huyu mzee bishoo wa kubana bana pua.
     
  10. only83

    only83 JF-Expert Member

    #10
    Feb 23, 2012
    Joined: Oct 15, 2010
    Messages: 5,252
    Likes Received: 445
    Trophy Points: 180
    Msameheni huyu mzee,nadhani anapaswa kuwa ICU akitibiwa matatizo ya kufikiri..na ndio matatizo ya kuendelea kung'ang'ani kwenye ofisi wakati uwezo wa kuongoza umepungua.
     
  11. K

    KIROJO Senior Member

    #11
    Feb 23, 2012
    Joined: Dec 7, 2011
    Messages: 169
    Likes Received: 0
    Trophy Points: 0
    Tendwa Janga la Taifa,sijuwi huyu mzee kwanza anawatoto wanaakili timamu.Mimi ningekua hata ni jirani yangu huko kwetu ningemshauri kitu kimaoja ,aachane na kazi hii ,awe mshauri wa sheria katika kampuni za uwakili siamesoma na Jaji mstaafu,huyu mzee anakokwenda ni kubaya,watu watampinga mimi nakwambieni hayo mambo anayodai ni zamani kwelikweli,wewe na usomi wako huo huwezi kuzungumuzia habari za kishirikiana mbele ya kamera/TV ,aise ndo maana nasikia viongozi wengi wanatembea na mabodyguard wawili,wa kwanza ni ulinzi wa macho ,mwingine wa kiroho,--hiyo ni kubali ni kweli ,ref mwanza wewe angalia tu kiongozi wetu akiwa ameenda sehemu hakubariki,utaona huko nyuma yake kuna walizi wamesimama wawili,wote wanakazi mbili,then kunamutindo siku hizi wa pete ,ref,mtoto wa mkulima mbona zamani alikuwa hana pete leo hii ndo kafanikiwa ndo anavaa pete?
     
  12. Gagurito

    Gagurito JF-Expert Member

    #12
    Feb 23, 2012
    Joined: Feb 11, 2011
    Messages: 5,610
    Likes Received: 25
    Trophy Points: 135
    Tendwa yupo kikazi zaidi. Anatetea maslahi ya magamba!
     
  13. only83

    only83 JF-Expert Member

    #13
    Feb 23, 2012
    Joined: Oct 15, 2010
    Messages: 5,252
    Likes Received: 445
    Trophy Points: 180

    Napata wasiwasi na uwezo wako wa kufikiri na kutoa hoja,inaonekana ubongo wako hauna uwezo wala aibu ya kudandia mambo.Hivi wewe uoni kauli ya Tendwa ni janga kwa Taifa?
     
  14. k

    kizazi kipya JF-Expert Member

    #14
    Feb 23, 2012
    Joined: Jul 21, 2010
    Messages: 329
    Likes Received: 5
    Trophy Points: 35
    hata mimi napata waswasi na uwezo wako wa kuchambua mambo ukiwa kama independent person(bila kutumwa)
     
  15. Kigogo

    Kigogo JF-Expert Member

    #15
    Feb 23, 2012
    Joined: Dec 14, 2007
    Messages: 20,498
    Likes Received: 1,453
    Trophy Points: 280
    tutamsokomeza vijiti kama gadafi wala hatuna haraka naye ....
     
  16. K

    Kintiku JF-Expert Member

    #16
    Feb 23, 2012
    Joined: Feb 3, 2011
    Messages: 611
    Likes Received: 72
    Trophy Points: 45
    TZ hakuna tofauti kati ya aliyesoma na Ngumbalu linapokuja suala la kuongea. Tendwa aibu hii ni kubwa sana kwa familia yako hasa kama una watoto wa kiume, wanajisikiaje unavyotoa kauli kama hizi za kujitongozesha kwa CCM?
     
  17. M

    Massenberg JF-Expert Member

    #17
    Feb 23, 2012
    Joined: Jun 4, 2011
    Messages: 1,173
    Likes Received: 1,061
    Trophy Points: 280
    Wewe mwenye uwezo mkubwa unaandika ID yako GeniusBrain badala ya Genius Brain, wewe una unafuu gani?
     
  18. Ulukolokwitanga

    Ulukolokwitanga JF-Expert Member

    #18
    Feb 23, 2012
    Joined: Sep 18, 2010
    Messages: 8,418
    Likes Received: 3,905
    Trophy Points: 280
    Hao wazee ni matokeo ya kazi ya kisiri siri ya Edward Lowassa kuweka himaya yake hapa nchini kwa kumtanguliza mkwewe. Nashangaa hata Nape anacheza hiyo hiyo ngoma na Membe yuko kwa David Cameron kuwajadili wasomali na huku Mzee Six yuko busy na Kanumba. Janja ya Lowassa kiboko yake ni CDM tu. Nassary alipata zaidi ya kura 30,000 (Baada ya kuchakachuliwa) 2010 bila hata Lema kwenda kule. CCM wao tishio lao kubwa ni Lema tu wanasahau kuwa CDM sio one man army. Lwaigwanani wenye njaa na waliohongwa na EL wazuie CDM yote kama wanaweza
     
  19. Kakulwa P

    Kakulwa P JF-Expert Member

    #19
    Feb 23, 2012
    Joined: Feb 8, 2012
    Messages: 200
    Likes Received: 1
    Trophy Points: 0
    Kama MZEE TENDWA kama anasema ukweli kuwa wazee wa kimila WASHIRI wamekaa kwenye kikao wakatamka maneno ya kudhamiria KUMUUA GODBLESS LEMA MH basi jeshi la polisi liwakamate wafunguliwe mashtaka ili wachukuliwe hatua za kisheria kwa kuwa tayari shahidi kwenye kesi hiyo yupo.
    Kama Mzee Tendwa katumwa na chama chake kusema maneno hayo na siyo ya wazee wa kimila, afunguliwe mashtaka ya uchochezi na wazee hao wa kimila WASHIRI maana watakuwa mashahidi ktk kesi hiyo kwa kuwa hawakusema maneno hayo.
    Kama hakuna hatua zitakazochukuliwa dhidi ya Mzee Tendwa na Washiri. wananchi wa jimbo la Arumeru Mashariki waamue kuwa na kiongozi makini ambaye hatokani na urithi wa kifamilia ifikapo tarehe 01.04.2012. Kura yao ya kuwakomboa ni muhimu sana.
     
  20. K

    KAMANDA HANGA Senior Member

    #20
    Feb 23, 2012
    Joined: Sep 22, 2011
    Messages: 158
    Likes Received: 0
    Trophy Points: 0
    Baada ya msajiri wa vyama vya siasa John Tendwa kuwasemea wale aliowaita wazee wa Arumeru, kundi jipya limeibuka na kudai Tendwa kalisemea kundi la wazee wa CCM nao wanakuja kama wazee wa UPINZANI kusema yafuatayo:-
    1. Neno la kutishia kuua tayari ni kuua na hawakutarajia mtu makini kama Tendwa kuendelea kulisisitiza hadharani kama sio kuchochea vurugu.
    2. Lema hakumtukana mtu hata kama alionyesha vidole viwili kwani yeye mda wote anatetea maslahi ya chama chake. Walitaka atamke kidumu chama cha mapinduzi ndo waridhike?
    3. Wanadai kila mmoja anaweza kuua na wote pande zote mbili ni wakazi na wana Arumeru hawana haja ya kutishana kwani wanatumia siraha sawa na mbinu sawa.
    4. Wanamwambia Lema karibu Arumeru hata leo waone nani anakuwa wa kwanza kumfunga paka kengere.
    5. Mwisho wanamwambia Tendwa awe tayari kujibu mbele za watanzani juu ya madhara yoyote yatakayojitokeza kutokana na vurugu anazozichochea kwa wanameru yeye akishirikiana na CCM.
    Wazee hao nao wanajipanga kuitisha mkuta na waandishi wa habari mda wowote.
    Source: Dr mmoja hospitali ya Tengeru ambaye ni Mmeru mkazi wa Sing'si.
     
Loading...