MAAGIZO YA VIJANA WA TANZANIA KWA KAMANDA LEMA:
KWA KUSHIRIKIANA NA 'WASHIRI-CHADEMA' NENDA ARUMERU MASHARIKI KUWAFIKISHIA SALAAM ZA KUPIGANIA KUREJESHWA KWA 'HAKI, HESHIMA NA UTU WA KILA MTANZANIA'
Hakika Vijana wote nchini Tanzania nawapeni HEKO SANAAAAAAAAAAAAAAAA kwa kumfanya kijana mwenzetu Mhe Kamanda Gobless Lema, Mbunge wa Arusha Mjini, kwa kumfanya huyu mwenzetu awe ni mtu wa kukinyima usingizi kila kiongozi wa MAGAMBA pamoja na maafisa wa serikali ma-kada kama Yohana Tendwa.
Kimsingi, huyu kijana mwezetu wala hatumheshimu kwa kitu pesa alizo nazo mfukoni maana kiukweli fedha bado hana; na wala vijana hatujachagua kumheshimu huyu kijana mwenzetu kwa kuwa na cheo tu cha ki-bunge maana wapo wengi tu wenye vyeo vikubwa zaidi ya hiyo tena wanaolipwa Tshs 20,000,000/- na miposho zaidi juu (Kafulila et al).
Naam, nasema Machalii wote Tanzania hatujachagua kumheshimu na kumpa ufuasi uliotukuka Kamanda Lema shauri ya usomi wowote maana kama ni usomi tu tunao Ma-Profesa kibao nchini lakini wanajificha mbele ya dhuluma tunaofanyiwa wanyonge wa nchi hii huku wao wakiendelea kuvuta kuku kwa mrija hata bila ya kujali vijana wa nchi hii hali yetu ikoe.
Hakika, kuna kitu cha kipekee mno kile kinachomfanya Kamanda Lema nyota yake ang'ae mpaka kuwatikisa Ma-Washiri CCM huko AruMeru, kila alichonacho huyu kijana mwenzetu ambacho Mamilionea wenye fedha za kukwapua kama Lowassa hawana.
Ndio, nasema kuna kitu kikubwa sana chenye upekee kinachomfanya wanyonge wa nchi hii wamkubali Kamanda Lema na kumkataa Msomi kama Dokta Bana anayeonekana kuwa ni mfano hai wa wasomi wanaokubaliana na wadhulumishi wa nchi hii kwa kila kitu ilmradi tu mkono uende kinywani mwakwe.
Wala sio siri tena kwamba kwetu sisi vijana kumtii kule huyu kijana mwenzetu maneno yake na kumpuuza Waziri Ngeleja yoooote haya yanatokana na kitu kidogo sana lakini chenye upekee mno katika uhai na mustakabali mzima wa taifa letu leo na kesho.
Ni kweli, kwake huyu Kamanda Lema kwamba vijana tunatambua kitu lulu, kuaminika, kutegemeka na thamani kubwa iliomo ndani ya KILE ANACHOSIMAMIA NA KUIAMINI KWANIABA NA FAIDA YA WANYONGE kutufariji wakati wote wa shida na dhuluma zisizoisha kote nchini
Kwake yeye Kamanda Lema, bila kitu KUJIKWEZA, vijana wenzake tunatambua dhahabu ya ajabu mno katika ule ujasiri wake wa kutete Maslahi ya Umma kwa kuzingatia misingi ya ile falsafa ya KUREJESHWA KWA HESHMA, HAKI NA UTU WA MTANZANIA.
Hadi hapo sasa, Kamanda Lema, kwa maagizo yetu sisi vijana wa nchi hii tunaodhulumiwa sana, tunaoporwa sana rasilmali zetu na vile vile kila mara KUPOKONYWA HAKI ZETU ZA KUJICHAGULIA VIONGOZI TUNAOWAPENDA SISI WENYEWE, hivi sasa tunakuagiza kupitia chama chetu makini CHADEMA uongozi timu ya kukata na shoka kwenda AruMeru Mashariki kusaidiana na Wapiganaji wenzetu wakazi wa pale kuendesha kampeni ya kufa mtu, chumba hadi chumba hadi kiongozi wa kweli wa wananchi kupatikana bila rushwa!!
Kazi iendelee na utetezi wa haki za sisi wanyonge iwe mbeeeeeeeeele kama tai!!