Mgomo wa madaktari - Updates


Jana nimesoma jinsi dawa za meno zenye madini ya Fluoride kama vile Colgate zinavyosababisha matatizo makubwa sana ya kiafya ikiwemo ugonjwa wa moyo, cancer na kisukari. nakaona pia jinsi nchi nyigi za ulaya zilivyopiga marufuku dawa hizi tangu mwaka 2006.

Nikasoma pia jinsi dawa za uzazi wa mpango maarufu kama njiti zilivyo balaa kuubwa katika afya ya mama na jinsi dawa hizo zilivyozuiliwa kuuzwa katika masoko ya ulaya na marekani

Sasa nikatafakari jinsi vitu hivi vinavyoshamiri ndani ya nchi yetu na jinsi ambavyo matatizo yake yanavyoongezeka kila kukicha. Nikagundua hatuna viongozi nchi hii kwani wanajua hili na wanafumbia macho.

Nilikua naongezea tu hoja yako kwa kifupi ili mlengwa aelewe zaidi
 
Madaktari msijione kuwa nyie mmesoma sana kuliko wengine au fani yenu ni ya muhimu sana kuliko zingine. Fani zote ni muhimu kulingangana na mahitaji ya muda huo. Msitake kuiyumbisha nchi. Tumieni uzalendo kwa Taifa lenu!

Utatumiaje uzalendo kwa viongozi wasio wazalendo. Ndugu usiwe unakurupuka.
 

na kwa hili ilitakiwa pinda ajiuzulu kwa kwenda kinyume na bosi wake. Makinda ajiuzulu kwa ishu ya posho, piinda ajiuzulu kwa ishu ya posho na arusha ila kwakuwa hakua uwajibikaji wataendelea kudunda tu
 
wewe ndiye kilazawa kwanza kwa sababu hujui umuhimu wa mawaziri kuondolewa unavyoinfluence muafaka wa madaktari

kama mawazo yako ndio hayo.....wewe ni kilaza...........


Mazee.......hii tabia ya ku-copy na kupaste ndio UKILAZA wenyewe........samahani sana..........hebu fungua box kidogo....ndio utaelewa..........


Mkuu Riwa......siku zote naheshimu sana maandiko yako........are you really serious.........hebu chukua mawazo yako hayo yaweke katika picha iliyo kubwa kidogo......toka nje ya madaktari kidogo...........please

..............Kwa hiyo wewe una akili nyingi kuliko madaktari wakiwekwa pamoja? Usilolijuwa ni sawa na usiku wa giza. Ina maana hata kama wewe ungekuwa kwenye nafasi ya Mponda ungegoma kujiuzuru kwa kuwa huoni mantiki?

yaani na wewe ndio unajiona umeona mantiki...........mantiki my foot.........na wewe ni Kilaza tu.......


Asante sana Bob............heshima mbele


Unajua nini Bob.......watu wanajisahau na kutekwa na ushabiki zaidi ya kufikiri.......Asante Mkuu..........
 
Kuna mtu aliandika kwenye blog ya michuzi kwamba mwajiriwa hawezi na hana haki ya kumlazimisha mwajiri amfukuze mwajiriwa mwenzake. kama hivyo ndivyo madaktari wanapata wapi hiyo nguvu ya kumlazimisha mwajiri atende kinyume na sheria za ajira?

Nijuavyo mie Waziri si mwajiriwa wa Serikali. Angekuwa mwajiriwa taratibu zake zipo tofauti lakini kwa kuwa si mwajiriwa ndio sababu hana 'tenure' ya kukaa ndani ya huo utumishi wa umma.
 
 
Wakuu,

Nilishaandika siku chache zilizopita kuwa Mungu amewapofusha macho na kufisha akili za viongozi wa CCM ili kila wakifanyacho kiharibike na hatimaye watoke madarakani ili tunusurike.
Kwa wanaofuatilia mambo ndani ya ccm watakubaliana nami kuwa hakuna lenye mwelekeo linalofanyika likafaa kwa wao wenyewe kwanza (ndani ya chama) na kwetu wananchi. Mungu amewafitinisha kila mmoja anaongea lugha yake. Kama kungekuwa na serikali makini (hasa Rais),leo hii viongozi wa wizara ya afya wangekuwa wamebaki na uwakilishi wa wananchi wao pekee. Akili ya kawaida inakataa Rais kuwang'ang'ania labda wanamsaidia kufanya uganga wa kienyeji!

Ushauri
Wananchi tuungane na madaktari kugoma ili hawa ccm waondoke nchi irudi kwenye mwelekeo.

Nawasilisha
 

Ni wapi wewe ulipopewa Moral Authority kwamba unachoandika wewe au mtazamo wako wewe ndio sahihi na wengine hawako sawa!?
Haya ndio madhara ya nchi kukubali kuhifadhi mpaka masokwe mahali patakatifu.
 
...suala la kuunganisha mgomo na kutaka kujiuzulu kwa Mawaziri............wagome kwa sababu zingine....sawa sio hii ya kutaka Mawaziri wajiuzulu........

kuunganisha suala la kugoma na kujiuzulu kwa Mawziri ni UKILAZA USIO NA KIFANI..............

Hawa madaktari wamelewa sifa baada ya kuwaunga mkono kwenye mgomo wao wa kwanza, wamekuwa juu ya haki ya maisha hasa baada ya kuingiza mambo yaliyo nje na matakwa yao kwenye mgomo wao. Wamelewa sifa na wawajibike, they have to be responsible for their actions.


Kuna fani muhimu zaidi ya udaktari i.e bila walimu (kama nao wangeamua kugoma uso kikomo) wengi wao wasingekuwa madaktari hivi leo.
 
Mimi naona tufute bunge na madiwani na pesa zinazotumika huko kwa sasa zielekezwe katika kuimarisha sekta ya afya nchini. Nadhani nchi hii inahitaji zaidi madaktari na manesi kuliko inavyohitaji wabunge na madiwani.
 

Siku mgomo wa kwanza ulipoisha maDkatari wakati wanatoa kauli ya kurudi kazini waliweka wazi kinachofuata...waliweka wazi kuwa watendaji waliobaki wa Wizara ya Afya (Waziri na Naibu wake) wajiuzulu au kutimuliwa, jukumu ambalo WM Pinda alimtwisha Rais...Madaktari waliweka wazi kuwa tarehe 3 march watakutana kujadili progress ya mchakato utakaojumuisha madai yaliyokuwa pending. Tarehe 3 March maDaktari walikutana na wakatoa tamko kuwa wanaelewa kuwa serikali iko katika mchakato wa kuangalia jinsi ya kuboresha maslahi ya watunishi wa afya na mazingira ya kazi, ila kuna jambo ambalo halihitaji mchakato....Mawaziri kujiuzulu! Na walitoa tamko nini kitakachofuatia iwapo hawatajiuzulu!

Badala yake Mawaziri hawakujiuzulu na serikali kutangaza ubabe na kuwakingia kifua....NANI ANATAKA SIFA HAPO?

Let me tell you...with or without public support, we reached the point of no return! Kurudi kazini ni iwapo tu Mawaziri watajiuzulu kupisha watu wengine tutakaowaamini kuwa wana nia ya dhati ya kuboresha maslahi na ubora wa huduma za afya, then tutarudi mezani...hata kama will take years, atleast tuwe kwenye mchakato na watu tunaojiaminisha wana nia ya dhati!
 


Tatizo letu ni mnapogoma 'eti kwa vile waziri na naibu wake hawajajiuzulu' .... mtarudi mezani baada ya waziri na naibu mpya kuteuliwa au mnataka hiyo wizara muindendeshe wenyewe?

Kiasi cha kusema with or without public support mko kwenye point of no return, ni kiburi, jeuri ukatili na uasaliti kwa wananchi. We better live without dr than kuwa na madrs wa kaliba yenu, wauaji.
 
Naogopa sana, kuwachokoza zaidi Madaktari. Nahisi mlipuko wa mgomo mkubwa zaidi. Hasa kama provocation itatumika, hapo busara inahitajika zaidi. We should learn to hit the route cause rather than scape goat (Wazee wa ilala na mdaktari wapi na wapi, hayo ni mambo yakizamani.)
 
Pleaseeeee................
...baada ya kuwaunga mkono?
hebu tueleze ulivyowaunga mkono!
 
Madaktari msijione kuwa nyie mmesoma sana kuliko wengine au fani yenu ni ya muhimu sana kuliko zingine. Fani zote ni muhimu kulingangana na mahitaji ya muda huo. Msitake kuiyumbisha nchi. Tumieni uzalendo kwa Taifa lenu!

Hayo siyo madai ya madaktari bali ni mawazo yako binafsi!!!
 
Mgomo utapita kama ilivyopita mingine, na huu sio wa kwanza wala wa mwisho.
 

Hilo litakuwa ni dai jipya ambalo wewe ndio umeliongezea...madai yetu yako clear, na mpaka sasa unayafahamu!

Kiburi, jeuri, ukatili na usaliti kwa wananchi (wakiwemo maDaktari) walianza serikali wenyewe, na ndio maana leo tumefikia hapa...wewe kama Freema ulichonga chochote kuhusu mapungufu hayo ya serikali? au serikali inaweza fanya hayo..ila kwa maDaktari ni nongwa?!

Tangu mwanzo wa mgomo serikali pamoja na wananchi malimbukeni kama wewe mnaongelea kuhusu wajibu wa maDaktari tu kwa wananchi..na kwa serikali....nini wajibu wa mwananchi kwa Daktari wake? nini wajibu wa serikali kwa maDaktari wake? wewe kama mwananchi unadai niwajibike kwako, wewe umetimiza wajibu wako kwangu? serikali imetizimiza wajibu wake kwangu? kama kuua hata serikali ni wauwaji kwa kutotimiza wajibu wao, na wananchi pia ni wauaji kwa kutotimiza wajibu wao..

Pengine wananchi wenyewe wangedai maboresho ya huduma za afya wanazotoa maDaktari ikiwemu vifaa, madawa na mazingira bora ya kazi labda mimi kama Daktari nisingehitaji kugoma! Sasa kila kitu shaghala baghala, na tatizo linaonekana dhahiri wapi lilipo, au nani anazuia mchakato wa maboresho...maDaktari wanagoma kwa benefit ya wote wewe unawabeza na kuwaita majina ya ajabu! Wewe mpata huduma mwenyewe ndio unakuwa wa kwanza kunikatisha tamaa kukupa huduma bora ninazoamini unastahili..sababu tu ya ushabiki wa kipuuzi!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…