Mgomo wa madaktari - Updates

Upinzani bongo haupo Simba na yanga pekee bali hata pinda na madaktari.
 
There is time for everthing done on this earth,

there time to cry and there is time to laugh

there time to plant and there is time to uproot

there time to dance and there is to be sad

(the bible)
there time to hold and there is time to let go

The minister and deputy are facing nothing short of a munity. Its dis heartening that the senior leaders have no sense of accountabity and are bent to hold on causing untold inconvinience and suffering to maltitude of the sick.

There time to hold and there is time to quit. Lucy and Mponda this is the time quit.
 

Hapo ndipo ninaposhangaa...nchi inaendeshwa kienyeji-enyeji, kijinga-jinga, kiusanii-sanii, kiwizi-wizi...na katika yote hayo ni wananchi ndio wanaolipia gharama kwa kutaabika. Nchi nzima tunajua hilo, tunalilalamikia kila siku/saa/dakika/sekunde...angalia vyombo vya habari vyote ikiwemo mtandaoni! Tunapiga-piga kelele tu...tumeshashushuliwa kelele za mlango (wananchi) hazimnyimi usingizi mwenye nyumba (wenyenchi), bado tu tupo-tupo kama mazuzu!

Leo hii madaktari wametuonyesha ya kuaddress sensitive issues kwa serikali hii 'kiziwi' na 'pofu'...na kwa kubanwa huko serikali inaanza angalau kusikia na kuona....watu wanaona wivu na kuwabeza! Eti kwa nini maDaktari!? waTanzania mnataka nini!? Kama mnamsubiri 'mesiya' aje kuondoa kilio chenu sisi waKwere tunasema 'kalagha baho', endeleeni kusubiri!
 
Sasa hivi kuanzia raisi, waziri mkuu na watendaji wake wote wakuu wapo either kwenye simu zao zenye internet au kwa komputa zao wanafuatilia kinachoendelea mitandaoni kuhusu mgomo, mpaka jioni watakuwa wanasubiri tu na itafika kipindi wataenda kulala, ikawa usiku ikawa mchana siku ya tatu ya mgomo!
 
Nawaunga mkono Madaktari, si kwa sababu wameacha kutibu wagonjwa, ila kwa sababu wameamua kurisk ajira zao, ili kupingana na udhalimu wa watawala.
Madaktari ni sehemu ndogo sana ya jamii ya Watanzania ambao wananyanyasika sana na huyu oppressor. Naamini damu ya watanzania inayomwamwagika ni SADAKA kubwa, na hatimaye dhalimu huyu atashindwa na kuachilia hatamu.

Tunasoma katika Bible kuwa Daudi, kijana mdogo kabisa alilishinda jitu kubwa pana na lenye nguvu -Goliath kwa kutumia silaha duni kabisa na ya kimasikini- kombeo.
Madaktari hawana hata silaha ya kupigana nayo zaidi ya taaluma zao kichwani. Ni namna ya upole na ya mwisho kabisa ya kushinikiza haki itendeke kwa manufaa ya Taifa zima , na wala si wao tu...mwenye akili atakuwa ameshalielewa hili tayari.

Ukitaka kujua serikali babaishi iliyokosa kauli basi chukua PINDA KAMA sample. Mtu huyu sijui hata akiwa nyumbani kwake anadiscuss nini na familia yake! Kama alilia Bungeni kwa kuona huruma kwa Albino, kinachomshinda sasa hivi kulilia Watanzania wengi ambao equally wanakufa kwa jeuri ya serikali yake, nini?

Naumia sana moyoni kwa madhila yanayotokea kwa ndugu zangu wagonjwa, lakini nashawishika kusema mgomo huu uendelee, hadi Ukombozi wa kweli utakapooneka...hata vita ya kukomboa nchi huandamana na damu za askari mashujaa!
 
Hivi hawa Mawaziri wanaotakiwa kuondolewa wao taaluma yao ni nini? Wote huwa nasikia wanaitwa Daktari, au sivyo? Wakiondolewa Madokta hawa tumpeleke nani pale? Wasira au Chenge? Maana kama Madakitari wote hawafai kuanzia Dr. Mtasiwa, Nkya na Mponda basi Baraza likivunjwa tuweke Mawaziri wenye taaluma tofauti. Kwa maoni yangu hii approach ya kutaka Waziri ajiuzuru eti kwa sababu alitamka maneno ambayo Madokta wameona yanawakera ni kuonyesha kutofahamu vyema dhana ya kuendesha Serikali. Kwani hawa ndio wameshindwa kununua vifaa vya mahospitali na madawa? Je, hawa ndio wanapanga mishahara ya Madaktari? Kwani mbona uongozi wa TUGHE una madaktari, kwanini wasingeanza na hao kwa kushindwa kuwatetea ili kuboresha hali zao? I am totally buffled by these senseless arguments. Kwani waliposhinikiza mwanzo na kupelekea Nyoni na Mtasiwa kuondolewa, kuna faida gani imepatikana? Sasa ni zamu ya Nkya na Mponda, kesho itakuwa ya Pinda na Bilali. Next itakuwa ya Kikwete na Mkuu serikali yake yote. Then we will leave at the mercy of Doctors! Come on Drs, go back to work and use lawful means to present your grievances!:A S embarassed:
 
hapo mkuu inabidi utafute contacts za Mzee Ali H. Mwnyi (sio Hussein) alikuwepo huko Shinyanga mpaka alazimike kujiuzulu!

Halafu hilo la pili ni kuwa hii nchi ina wakazi zaidi ya milioni 45 na sio lazima Mponda na Nkya pekee ndio waweze kushika hizo nafasi, pia muulize Mzee Tendwa anavyo vyama vingi amevisajili pale ofisini kwake hivyo sio lazima ccm daima!

 
kweli wanainchi tunateseka
ukiwaambia tubadilishe huu mfumo wa utawala na siasa,mnaaza kusema hakuna mbadala wa chama
tunahitaji sana kuwaelimisha wasiolewa kutowachagua washenzi wa siasa za maji taka ili tuwape akili
ona sasa vita ya panzi na kunguru tunaumie sie wanainchi!!

kwakweli nasikitika sana
 

Mkuu nafikiri watakuwa wametia akili sasa kuwa serekali haiko kwa ajili yao!
 
Serikali isikilize madai ya madaktari kepusha maafa yatakayotokea.Bila kufanya hivyo ni wao viongozi ndo watabeba lawama zoote.
 

ukimdiscuss sana pinda ni kumuonea, madaraka aliyo nayo hayawezi ni sawa na mtoto wa darasa la nne umpe mtihani wa chuo kikuu akifeli uanze kumgombeza Pinda hana uwezo na hata nafasi aliyopewa ni kama kuzima makundi baada ya kuanguka lowassa lakini hana uwezo,!
 
Mgomo huu unawaathiri wananchi wa kipato cha chini zaidi ya hauwagusi kabisa hao walioko madarakani. Sisi tunaopata haya madhara 2015 tutavaa: mashati ya kijani +kofia za njano na tutakula pilau + soda + kondoo pia musisahau tutakuwa tunasafiri kutoka sehemu moja ya kampeni hadi nyingine kwenye malori. OMBI: Captein Komba tunaomba utoe albam mpya mwaka huu. Hilo tu ndilo omb letu sisi wananchi
 
uwaue madaktari? halafu utawatibu wananchi kwa masaburi yako? sitashangaa ukini ndambia kuwa unafanay kazi ukulu. sishangai kabisa ndio type ya watu mnaoongoza nchi

Hapana, Ikulu ya leo haina udikteta. Mimi ni dikteta wa ndani ya damu. Anaegoma na kusababisha vifo vya wengine na kutoweka kwa amani, unamuua tu. No discussion. Kikwete anawachekea sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…