Mgomo wa Daladala Kigamboni

Bayebe

Senior Member
Jan 31, 2014
152
198
Leo Tar 20 May 2021 kuanzia Majira ya Asbuhi Magari ya Abiria maarufu kama Daladala Yaendayo Kigamboni Kupitia Daraja kuu la Kigamboni (Mwl.Nyerere) Yamegoma kufanya Safari zake kutoka Kigamboni hadi Karume Ilala kupitia Kilwa Road.

Sababu ni Kupinga kuhamishwa kwa Kituo kikuu cha Mabasi hayo kutoka Ferry Kivukoni hadi Kata ya Tungi. Abiria /Wananchi wengi wanapata Tabu sana muda huu.

Pia njia ya Mji Mwema kuelekea PembaMnazi wamegoma.

1621505124309.png
 
Watendaji na wapangaji wa haya mambo sijui huwa wanafikiria vitu gani au kwa sababu wao hawatumii huu usafiri wa uma ndio maana hawazingatii athari kwa walaji.

Pale kivukoni ndio center kubwa ambayo watu kutoka viunga vyote vya kigamboni huletwa na mabasi kisha baada ya hapo wavuke kwenda mjini au wapande hizo machinga kupitia darajani, sasa leo unapohamisha basi za machinga na kuzipeleka ndani ya mji wakati bado kituo kikuu cha hizi basi nyingine kinabaki kuwa kivukoni hapo unakua unawalazimisha abiria wanaotaka kuvuka kupitia darajani wapande bajaj (Tsh 500) ili kuzifata hizo machinga huko Tungi na baadae alipe tena kiasi hicho hicho anapokua anarudi.

Kwa mtu wa kipato cha chini nyongeza hii ktk gharama ya usafiri ni kubwa, mamlaka husika inabidi walitazame vizuri ili maboresho wanayofanya yasiumize watumiaji wa huduma husika.
 
Halmashauri wanatakiwa watafute eneo la stendi pale ferry - sasa kuwapeleka Tungi wakati abilia wako ferry wapi na wapi..
 
Leo Tar 20 May 2021 kuanzia Majira ya Asbuhi Magari ya Abiria maarufu kama Daladala Yaendayo Kigamboni Kupitia Daraja kuu la Kigamboni (Mwl.Nyerere) Yamegoma kufanya Safari zake kutoka Kigamboni hadi Karume Ilala kupitia Kilwa Road.

Sababu ni Kupinga kuhamishwa kwa Kituo kikuu cha Mabasi hayo kutoka Ferry Kivukoni hadi Kata ya Tungi.

Abiria /Wananchi wengi wanapata Tabu sana muda huu.

Pia njia ya Mji Mwema kuelekea PembaMnazi wamegoma
CCM oyee
 
Watendaji na wapangaji wa haya mambo sijui huwa wanafikiria vitu gani au kwa sababu wao hawatumii huu usafiri wa uma ndio maana hawazingatii athari kwa walaji.

Pale kivukoni ndio center kubwa ambayo watu kutoka viunga vyote vya kigamboni huletwa na mabasi kisha baada ya hapo wavuke kwenda mjini au wapande hizo machinga kupitia darajani, sasa leo unapohamisha basi za machinga na kuzipeleka ndani ya mji wakati bado kituo kikuu cha hizi basi nyingine kinabaki kuwa kivukoni hapo unakua unawalazimisha abiria wanaotaka kuvuka kupitia darajani wapande bajaj (Tsh 500) ili kuzifata hizo machinga huko Tungi na baadae alipe tena kiasi hicho hicho anapokua anarudi. Kwa mtu wa kipato cha chini nyongeza hii ktk gharama ya usafiri ni kubwa, mamlaka husika inabidi walitazame vizuri ili maboresho wanayofanya yasiumize watumiaji wa huduma husika.
Sijui kwanini wakati wa kupanga huwa hawashiriki watu muhimu kama hao?
 
Back
Top Bottom