Bushmamy
JF-Expert Member
- Aug 18, 2019
- 8,848
- 15,252
Madereva wa Daladala Mkoani Arusha wamegoma leo Kwa kile wanachodai kuwa ni Bajaji kufanya Kazi kama daladala.
Idadi kubwa ya wanafunzi na watu wazima wamekuwa wakitembea kwa miguu na wengine wakiwa tu vituoni wakiwa hawajui cha kufanya.
Mamia ya wakazi wa jiji la Arusha wakiwemo wanafunzi wa shule,wamekumbwa na adha ya usafiri mara baada ya madereva wa daladala Mkoani hapa kugoma kwa kile wanachodai kuwa ni Bajaji kufanya Kazi kama daladala na hivyo kuwalazimu abilia kupanda Guta na kutembea kwa miguu.
Mgomo huo ambao umeanza mapema leo ,umewaathiri zaidi wanafunzi ambao wamefungua shule leo,ambao walionekana wakiwa kwenye vituo vya usafiri wakisubiri magari mbalimbali na wengine wakilazimika kudandia pikipiki za mizigo( guta )na wengine kutembea kwa mguu umbali mrefu.
Baadhi ya madereva wa daladala eneo la kwa Mirombo walionekana wakicheza mpira huku magari yao ya usafiri wakiwa wameyaficha maeneo mbalimbali wakiwa na madai kwamba hawatapeleka gari barabarani mpaka serikali itoe tamko juu ya utaratibu mpya kati yao na bajaji ambao hautaathiri mapato yao.
====
UPDATE;
Hali ilivyo katika Kituo Kikuu cha Daladala Kilombero Jijini Arusha ambapo daladala zipo katika mgomo wa kutoa huduma wakidai Bajaj zinaingilia njia zao na hivyo kuathiri mapato yao ya kila siku.
Hali ilivyo Kwa Morombo jijiji Arusha Kwenye mgomo wa Daladala usiokuwa na kikomo madereva wakilalamikia kuongezeka kwa Bajaji jijini Arusha na Kuwaingilia kwenye Ruti zao ambapo Wananchi wametumia usafiri wa Mguta leo kuingia mjini
Daladala za kutoka Morombo kwenda Mjini, daladala za kutoka Engo kuelekea Mjini.
Daladala za kutoka Uswahili kwenda Mjini. Ngusero kwenda Mjini
Ndani ya Kituo cha Daladala cha Kilombero hakuna daladala kabisa, Bajaj na bodaboda ndo zinafanya kazi tu na hazitoshelezi abiria ni wengi.
Bajaj zimepandisha bei kutoka Tsh. 500 hadi Tsh. 1,000.
Pia soma: Arusha: Usafiri wa daladala kurejea, madereva wamaliza mgomo