LATRA yasajili kwa muda daladala kuiongezea nguvu mwendokasi

Replica

JF-Expert Member
Aug 28, 2017
1,446
7,821
Mimi nashauri mradi wa mabasi ya kibluu ufe kwani wameshashindwa, daladala zitumie barabara ya mwendokasi. Kwakuwa hayatakuwa yanakaa foleni, yatabeba watu wengi kwa wakati mfupi, kuliko kwenda kituoni na kusubiri mwendokasi lisaa lizima.

Kimara wameshindwa, sasa watawezaje kuendesha njia mpya za Mbagala na Gongo la Mboto? Pia wakienda huko wasiue ruti ambazo mwendokasi haifiki.

AU

Liwe soko huru kwa wote, waache daladala na watu wachague daladala au mwendokasi.

Pia soma > Napinga Daladala kuingizwa kwenye BRT

========

Daladala.jpg

Ni kupunguza tatizo la usafiri kwa abiria wanautumia usafiri wa umma Barabara ya Morogoro.

Hivyo ndivyo unavyoweza kusema, baada ya Mamlaka ya Usafiri Ardhini (Latra), kukubali kusajili kwa muda daladala 15 kusafirisha abiria katika barabara hiyo ya Morogoro.

Daladala hizo ambazo zinatakiwa ziwe na uwezo wa kubeba abiria kuanzia 25, zitakuwa zikifanya safari zake Mbezi Luis kwenda Makumbusho kupitia Barabara ya Morogoro.

Ikumbukwe tangu mradi wa mabasi Yaendayo Haraka ‘mwendokasi’ uanze rasmi mwaka 2016, daladala ambazo zilikuwa zikifanya safari zake hadi Mbezi zilisitishwa.

Mwananchi
 
Daladala hizo ambazo zinatakiwa ziwe na uwezo wa kubeba abiria kuanzia 25, zitakuwa zikifanya safari zake Mbezi Luis kwenda Makumbusho kupitia Barabara ya Morogoro.
Wangeongeza sharti jingine ziwe ni safi, viti vizuri na hazina uchakavu wa mabodi maana zipo zingine ukikaa ndani unaona chini kote na mvua zikinyesha zinavuja mpaka basi
 
Hivi kuna mradi ambao kama nchi tumeweza kuusimamia na ukawa endelevu tangu tumepata uhuru? Isije ikawa tunalaumu bure mradi wa mwendokasi kusuasua kumbe ndiyo uwezo wetu kiusimamizi umeishia hapo.

Sent from my SM-A037F using JamiiForums mobile app
Sisi ni wepesi wa kuanzisha mambo mapya ili kupata 10%, thereafter hakuna anayejali, jifunze kutoka stand mpya ya Dodoma, Magufuli terminal, na hata ile ya Morogoro Masoko na hospitali mpya zilizojengwa, ukienda vyooni kupo hoi bin taabani, usafi tu unatushinda je maintenance tutaweza?

Haya nenda Chuo Kikuu cha Kunguni watu wameshindwa kupuliza dawa tu je matengenezo mengine wataweza?
 
Back
Top Bottom